Viongozi wa Serikali Mkoa wa Mwanza ebu angalieni Afya na utu wa wananchi wenu. Hivi kweli Wilaya ya Nyamagana tena Jiji kabisa mmekosa sehemu nzuri ya kuwaweka wafanyabiashara wadogo wadogo na machinga wa Buhongwa, hadi mkaamua kuwapeleka kwenye dampo la kumwaga uchafu na taka mlilojenga Buhongwa ??
Hili jambo linashangaza sana kuona binadamu wenzenu wanatafuta riziki yao kwenye eneo ambalo upande mmoja panamwagwa taka taka na kipande kingine ndani ya fensi moja ni shughuli za biashara!!.
Viongozi, ebu angalieni hata hayo mabanda ya hao wafanyabiashara ambayo wamejengwa bila usimamizi na mpangilio, mabanda yanachafua pia taswira ya jiji kwani yamejengwa kwa bati chakavu na kuezekwa kwa magunia! Hivi kweli tunasubili majanga ya moto yatokee ndio tuchukue hatua ?
Kwa kuwa mbunge Stanslausi Mabula wa jimbo la Nyamagana ameshindwa kuwasemea na kuwatetea wananchi wake na Halmashauri ya Jiji la Nyamagana Meya na Mkurugenzi wapo kimya, basi tunaomba Mkuu wa Mkoa Said Mtanda na Waziri TAMISEMI muingilie kati suala hili kwani halijakaa vizuri kabisa na madhara yake ni makubwa mno.
Mamlaka ebu amueni kati ya dampo na soko ni kipi kitoke na kingine kibaki, na kama litabaki soko basi watengenezee wafanyabiashara hao Mazingira mazuri ya biashara ili Serikali pia iweze kuingiza mapato na wao waweze kunufaika na biashara zao wanazofanya.