swagazetu
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 4,251
- 1,467
Waajf kuna mambo yanachefua ukiyadikia na kuyaona,hivi ninavyoandika tangazo lililopo ni shughuli zote za stand kwa maana ya usafirishaji na huduma za jamii kuhamishwa eneo la stand kwenda eneo la kiwana cha shule ya msingi jirani kupisha uboreshaji wa stand kuu hiyo kwa mda wa miaka miwili.Eneo lililotengwa limebanana kwa karibu na shule ya m/nyegezi na nyabulogoya na pia sekondari ya Nyabulogoya.hii ina maaa watoto hawataweza kutumia kiwanja kwa miaka miwili hiyo.
Pia athari ambazo kila mmoja anazifahamu ni madhara yatokanayo na shughuli za stand,aina ya watu wa stand na vurugu za stand.
Bado ukiangalia hili eneo halina barabara bora kumudu magari ya kuingia na kutoka barabara zilizopo ni vumbi na finyu sana lakini pia tutegemee ajali na watoto wetu kugongwa na mabasi yaendayo safari hasa kwa watoto wanaojidamka kuwahi namba shuleni.Eneo lenyewe halifai kwa shughuli hiyo.
Sababu ya mimi kuhoji ni kwa manufaa ya nani ni hii:
Mosi,Eneo la Buhongwa kilomita km tano kutoka stand hiyo kuna eneo la Dampo lenye takribani heka 40 na kwa sasa linajengwa dampo la kisasa hakuna harufu wala uchafu wa kunuka(ikumbukwe hata hapo nyegezi lilikuwa dampo kuu zamani hata stand ilipokuwepo lilihamishwa hivi karibuni),ukiangalia eneo la dampo barabarani kuna eneo la wazi kama heka tano zaidi halitumiwi km dampo lipo wazi tu japo kwa sasa limewekewa fensi.
Pili,Jirani na dampo hilo jirani na shule za Musabe kuna eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya Standa ya magari ya mizigo lipo wazi hakuna shughuli yyote inayofanyika pale lakini limeachwa tu badala yake wameenda kubanana na shule za watoto wetu.
Je ni kwa maslahi ya nani?