Stanbic bank kurejesha pesa zote za Tegeta escrow account

John Okello

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
459
207
Tarehe 26/11/2014 ni siku ambayo umma wa tanzania na wapenda haki wote walielekeza macho na masikio kufuatilia ripoti ya kamati ya bunge ya kudumu ya hesabu za mashirika ya umma (PAC) katika sakata zima la TEGETA ESCROW ACCOUNT, dunia ilisimama na wanyonge wote waliunga bila kujali itikadi za Imani zao za kidini au kisiasa na kuangalia mustakabali wa taifa letu.

Okello nilitafari haya mambo kwa kina na kuangalia kwa jicho la tatu namna mchozo huu haramu wa utakatishaji fedha haramu kuingiza katika mzunguko wa uchumi wa nchi , wakiongozwa na viongozi wakubwa na waandamizi wa serikali kutakatisha fedha chafu ili ziingie katika matumbo yao binafsi bila huruma.

Kubwa katika ripoti ile ilio somwa na Mh. Zito Zuberi kabwe (mb) mwenyekiti kamati ya PAC na makamu wake Mh. Deo Filikunjombe na kutoa mapendekezo kutokana na ushahidi wa vielezo uliotolewa kwa PAC na Mkurugenzi wa TAKUKURU kupitia BOT kuitangaza Stanbic Bank na Mkombozi Bank kuwa nitaasisi za kifedha za utakatishaji wa fedha haramu hapa nchini.

Okello maslahi yangu mapana kwa nchi ni namna pesa za umma kurejeshwa na si kujiuzuru tu kwa watu, njia moja wapo na ya kiweledi ya kurejesha pesa hizi ni kufuta njia sahihi za kisheria yaani( financial regulation on prevation of money laundering) za BOT , nathubutu kusema kuwa Stanbic Bank kwanza inapaswa kubanwa na kurejesha pesa hizi kwani ina uwezo kwa muainisho huu.

Kama tunavyojua kuwa Stanbic Bank ni tawi la banki kubwa Afrika inayo fahamika kwa jina la Standard Bank ambayo ina matawi UGANDA,KENYA, ZAMBIA ,ZIMBABWE, AFRIKA YA KUSINI na nchi nyinginezo nyingi Afrika ikiwa na mtaji wa takribani Zaidi ya USD 1 Trilion na hapa hoja si mtaji ila haiingii akilini hata kidogo kushindwa kufuata taratibu za kukinga na kuzuia utakatishaji fedha haramu katika mzunguko wa fedha na kuhusika kwakwe katika madudu haya kama ilivyo wahi kutokea HSBC ya Uingereza ilipo banwa na naibu mwanasheria mkuu wa Marekani (A.AG) Mr Larry Breuer ilipo patikana na hatia za utakatishaji fedha za madawa ya kulevya ya watuhumiwa toka Mexico na kulipa jumla ya kiasi cha dola za kimarekani $ 1.92 billion tareh 11 december 2012.

Malipo haya kwa serikali ya Tanzania kutoka Stanbic Bank yanatokana na kukutwa na hatia za kutofuata taratibu za kibenk na kamati ya PAC katika sakata la TEGETA ESCROW hivyo inapaswa kulipa kwanza panalti, fine na riba (interest) si tu kama walivyo fanya HSBC na Retures iliripoti "It is not a $ 1.9 billion fines for laundering money, it was a $ 1.9 billion fine for not following financial regulation about how to monitor and prevent money laundering", bali hata Baclays bank ilipo kutwa na hatia mwezi june 2012 ililipa kiasi cha euro 290 million.

Hivyo sasa ni wajibu wa serikali bila hofu yeyote na kwa kuwa wamejiridhisha kupitia ripoti ya uchunguzi wa takukuru na ni wakati muafaka kuiamuru Stanbic Bank kuirejesha pesa yote ya kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kulipa penalty na riba zote zitokanazo na makosa haya ( financial crimes) . Hili litakuwa fundisho kwa mashirika mengine ya kifedha ambayo sasa yanakuza tabia ya kudhani kuwa hii nchi haina utawala wa sheria kama ilivyo adabishwa Standard Chattered ilipo lipa kiasi cha $ 670 kwa serikali ya Uingereza.

Mapendekezo ya PAC si ya kubezwa hata kidogo na hii pia iwaangukie Mkombozi Bank bila kujali ni benki ya ndani ili iwe njia itakayo rudisha Imani kwa Watanzania kuliko siku zote ambapo taasisi au mtu binafsi anapokutwa na hatia na kukimbilia kukatisha mkataba au kumwajibisha kwa kujiuzuru huku nchi ikiwa imepata hasara mfano hapa katika hili uchumiwa nchi umeathirika katika kuongezeka kwa ufalifu wa kifedha na rushwa( increase of crimes and corruption),kuathirika kwa hadhi ya nchi kimataifa (damage of reputation and international consequences), kudhohofisha taasisi za fedha (weakened financial institution ), kudhofisha juhudi sekta binafsi ya uwekezaji uekezaji ( damage privatization effort).


Ni Imani yangu Stanbic Bank wanalijua hili pia na wata fuata taratibu kurudisha mali hii ya umma kabla hali haijakuwa tete Zaidi na mamlaka husika ikiwemo wizara ya fedha watachukua hatua ya ufuatiliaji kabla wanachi atujawawajibisha kwa uzembe au ufisadi mwingine. Wabunge ni imani yangu mtaibana serikali kuiamrisha Stanbic Bank na Watanzania kama sasa ambavyo hatukujali imani za itikadi zetu kisiasa basi tuungane katika hili kuirejesha Mali hii ya UMMA.


Ahsante

Mzalendo John Okello.
 
Bado kuna sintofahamu nyingi sana, hakuna aliyeweza kuthibitisha kama zile hela ni mali ya UMA mpaka sasa.
 
Okello, Hela za Escrow zilikuwa laundered kivipi?

Kama hazikuwa luandering kwa nini uchukuwe hela na Semi Trailer.
Mimi ninafikiri sometime tutumie akili kidogo na kuacha kutumia masaburi katika kupambanua mambo.
 
Okello, Hela za Escrow zilikuwa laundered kivipi?

Mkuu zipo taratibu za kifedha zinazo simamiwa na BOT na kukiuka ni kuvunja sheria hizi ukifuatilia vielezo vya uchotaji wa fedha hizi toka BOTkwenda kwenye bank hizi mbili na jinsi per a single day transaction za amount kubwa zilizo kuwa zikifanywa ni dhahiri huu ulikuwa utakatishaji pesa haramu...
 
Kama hazikuwa luandering kwa nini uchukuwe hela na Semi Trailer.
Mimi ninafikiri sometime tutumie akili kidogo na kuacha kutumia masaburi katika kupambanua mambo.

ni sheria gani inazua mtu kubeba hela na semi Trailer?
 
Pana mangi mno kunako kadhia hini, sasa tutulie wavuane nguo wenyewe kisha nasi tutajafahamu nani mkweli na nani muongo ama mtumikia tumbole....!?
 
pamoja na yote mkuu haiwezekani TAKUKURU NA CAG wote kwa pamoja wajikanyage ikiwa bosi wao ni mmoja ... hapa kuna ufisadi wa wazi na stanbic imetakatisha fedha...

Jana nimemsikiliza Zitto mwanzo mpaka mwisho, report yao haijitoshelezi kusema kuna hela zilikuwa zinakuwa laundered, au kwamba ni mali ya UMA.
 
Last edited by a moderator:
Bado kuna sintofahamu nyingi sana, hakuna aliyeweza kuthibitisha kama zile hela ni mali ya UMA mpaka sasa.

Hata kama likibaki hivyo hivyo bado kuna gross negligence ya benki ya Stanbic katika hili suala la Money Laundering

Hawakufanya KYC ya kutosha kwa mteja wao PAP.

Akaunti ya PAP kupokea na kutoa hela nyingi kiasi kile in Cash ni red flag ya mondey laundering

Hata hivyo hairuhusiwi kwa vault ya benki yoyote ku hold such amount of cash (No insurer can handle it kwa sasa kwa hapa TZ to the best of my knowledge).

Pia huwezi kuihukumu Stanbic ukamuacha regulator BoT
 
Jana nimemsikiliza Zitto mwanzo mpaka mwisho, report yao haijitoshelezi kusema kuna hela zilikuwa zinakuwa laundered, au kwamba ni mali ya UMA.

basi kama akili yako ni finyu kias hicho sijui unaona kuna umuhimu gani wa kuish,

aibu kubwa kuwa na kichwa box kias hicho.
 
basi kama akili yako ni finyu kias hicho sijui unaona kuna umuhimu gani wa kuish,

aibu kubwa kuwa na kichwa box kias hicho.

Kilaza mkubwa wewe.
Zitto jana kasema moja ya uthibitisho kwamba zile hela ni za UMA ni kwamba kulikuwa kuna VAT component iliyopaswa kwenda TRA. Karani mkubwa wewe.

Wewe ukienda kununua kitu dukani ukapewa bei inclusive of VAT, huwa unapeleka VAT TRA au unampa hela yote mwenye duka.

mwana hizaya mkubwa wewe.

Pumbavu kabisa, kilaza wewe.
 
Mkuu labda viongozi wa serikali wa 2015 hawa wa sasa ndio wizi wenyewe.
Nawasifu Mkombozi bank kwa kutoa taarifa za usambazaji wa pesa hizo bila kusita.
Bado tunawataka wale waliochukua kwenye viroba
 
Back
Top Bottom