mwikumwiku
Senior Member
- Jul 15, 2011
- 153
- 35
Ni kweli kabisa kwamba Umombo siyo Lugha yetu ya Taifa kwa kuwa Lugha yetu ya Taifa ni Kiswahili. Lakini tususaha kuwa tumekubali umombo siyo tu kuwa Lugha ya Kimataifa bali kuwa moja ya Lugha za mawasiliano rasmi ya kiofisi. Cha msingi zaidi tumeamua na tuanaendelea kusisitiza kuwa lugha ya kufundishia kwenye taasisi za elimu ya juu ni umombo!
Nimesoma kwa mshangao tangazo la Chuo Kikuu cha Mtakatifu John kwa Umma kuhusu kufunguliwa kwa Chuo hicho baada ya kufungwa kwa muda. Tangazo hilo linasomeka hivi: " REOPENING OF THE UNIVERSITY AFTER TEMPORARY CLOSER" shida yangu hapa ni neno "closer" nadhani neno sahihi lingetakiwa kuwa "CLOSURE".
Kuna makosa ambayo katika hali ya kawaida huwezi kutajia kufanywa hasa kwa kuzingatia kosa hilo limefanywa wapi na limefanywa na nani! Hili ni tangazo kwa Umma na limetangazwa na chuo kikuu! Mh! Kwa kweli umakini wa chuo hiki unatia shaka! Sipendi kuamini kwamba kosa hili limefanywa na mhariri kwa kuwa yeye hufanya kazi ya kulibandika kama lilivyoandaliwa japokuwa kwa mhariri makini asingetakiwa kuruhusu makosa kama haya. Angekuwa mwanafunzi tungesema "mbumbu" je chuo hiki tukiiteje?