Mkuu nataka unithibitishie kwa ushahid wa maandishi kwamba..DSTV wanalipa pesa nyingi sana kpl kuliko Ghana na Zambia.
1.Rwanda hawana Luigi yenye mvuto kuliko Tanzania .
2.Kama ni interest ya kuuza vifaa vyao basi wangeichukua ligi ya Tanzania yenye passionate and craziest fans.ambao wangekua ready to buy decoders to watch the league matches.
3.How come kpl is their biggest market.....wakati fans base ya kpl ni nusu ya Vpl.nani atakuwa Tatar ku-buy dstv decoder to watch kpl.
4.Ligi ya Tanzania ndiyo pekee east Africa yenye gate collection kubwa.
Hujaelewa kabisa, ukubwa wa soko la ving'amuzi hautokani na mvuto wa ligi bali ukubwa wa uchumi wa nchi husika. Uchumi wa Kenya upo juu ya Tanzania hivyo wananchi wake wengi zaidi wanaweza kununua ving'amuzi vya DSTV kuliko Tanzania na Rwanda zenye ligi zenye mvuto zaidi ya Kenya. Pia idadi ya watu inachangia, mfano ni Botswana, uchumi wao uko safi lakini idadi ya watu ni ndogo sana hivyo DSTV hana mpango wa kudhamini ligi yao.
Ghana na Kenya, zinakaribiana kiuchumi lakini Kenya ina idadi kubwa zaidi ya watu hivyo kupata udhamini mkubwa kuliko Ghana.
Ligi ya Nigeria haina mashabiki kabisa lakini ina udhamini mkubwa sana,
zaidi ya $8mn kwa mwaka kwa sababu wanaijeria ni wengi na wengi wao wana uwezo wa kununua ving'amuzi.
Kama sijakosea, nakumbuka udhamini wa DSTV kwa ligi ya Zambia unahusisha vilabu kupata milioni 60 tu kwa mwaka. Kenya vilabu hupata zaidi ya milioni mia kwa mwaka, DSTV wanamwaga around Ksh200mn ambazo ni zaidi ya Tsh3.5bn.
KPL being their market has nothing to do with football, it boils down to economy size, consumer purchasing power, middle class base where Kenya is way ahead of Tanzania. (Our middle class is reported at around 12% whereas Kenya at 44% and Uganda at 28% ndio maana DSTV wanadhamini Ligi za Kenya na Uganda ambazo hazina mashabiki na kuziacha Rwanda na Tanzania zenye mashabiki wengi zaidi).
Kwenye uchumi tunasema, uhitaji sio tu kupenda kitu bali sharti huambatane na uwezo yaani 'mfuko' (demand is all about willingness and ability of the consumer).
Kwa hiyo ni kweli kuwa Watanzania tunapenda mpira zaidi ya Wakenya na Waganda lakini uhitaji wa ving'amuzi vya DSTV ni mdogo kutokana uwezo wetu wa kiuchumi kulinganisha na Kenya na Uganda.