Sserunkuma Atakuwa Kama Tambwe

Sserunkuma Atakuwa Kama Tambwe

141204121931_ssrenkuma_512x288_bbc.jpg

Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania Simba SC.

Raia huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.


''Nimefurahia miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.
Mchezaji huyo wa kimataifa katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini Daresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi ya Tanzania.

Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.

Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.

BBC Swahili
 
Watu wameanza kuharisha kabla hajaanza kucheza. Urefu wake ni 1.70m .Mmeanza kiwewe mapema.
 
Jaja alikuwa na mission moja tu kuwafunga lambalamba waitwao Azam FC. Kazi hiyo aliifanya na kuikamilisha vizuri sana, sasa amerudi kwao kupumzika.

Mawazo kama haya ndio yanafanya muhindi apigiwe magoti kila akitaka kuachia ngazi.Ujinga wa kupewa medali ya ujinga.
 
Mkuu huitaji kuonyesha mapovu yako ili tujue kwamba unakerwa na ukweli..!nikuulize vizuri! je ww ni mfuatiliaji wa soka...!
Baada ya kujibu swali hili ndio ufanye ku-reply to my comment.
Tusije tukawa tunabishana kumbe mwezangu si mtu wa soka.

Yaani hata kujua nani mfupi zaidi kati ya Ngassa na Ssrernkuma...inakusumbua!

Huna lolote...nenda kampigie magoti kanjibhai....subirini tar 13 mtamtambua ni nani
 
Mawazo kama haya ndio yanafanya muhindi apigiwe magoti kila akitaka kuachia ngazi.Ujinga wa kupewa medali ya ujinga.

Mjinga mwenyewe, unajiona una akili kumbe huna lolote! Shame on you Ngarna.
 
Last edited by a moderator:
hivi na mkongwe Danny Mrwanda wamemchukua tena au?

Ni kweli wamemsajili tena kwa dau dogo, si unajua Msongamanoni hawawezi ku-compete kwenye soko la kununua wachezaji bora na wenye gharama kubwa.
 
Serunkuma ni mmoja kati ya washambualiaji bora na hatari katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Ni mchezaji tegemeo pia wa timu ya taifa ya Uganda inayotajwa kuwa timu bora zaidi katika eneo hili, na pia yenye wachezaji wengi wenye ushindani wa namba.

Pamoja na ufupi wake, anatarajiwa kuleta chachu ya ufumaniaji nyavu ndani ya kikosi cha Simba kutokana na kasi, wepesi, akili, shabaha ya goli na nguvu pia. Tofauti na Tambwe ambaye anamudu zaidi kama mshambuliaji namba moja, Danny anatoa option nyingi katika mifumo mbalimbali kwa sababu anaweza kushambulia kutokea kushoto au kulia, kati kama lone striker na pia kama mshambulizi namba mbili. Lakini udhaifu wake mkubwa ni uwezo mdogo wa kucheza mpira ya kichwa.


Kama Tanzania itampa mazingira kama ya Kenya, timu nyingine za Ligi Kuu lazima ziwe concerned na huyu anayeitwa kidudu mtu maana ni ukweli ulio wazi kuwa jamaa anajua, na kwa mipira ya Tanzania ya kukimbizana anaweza kuwika zaidi.

Kwa upande mwingine, napenda kuipongeza Simba kwa kusajili mchezaji baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu badala ya kutumia usanii wa majaribio kumpa mtu mkataba. Nilitaka kusema imejifunza kutokana na makosa lakini kwa kuwa na majaribio ya huyo Mgabon naona inataka kurudi kulekule. Simba, Yanga na Azam ziache mara moja tabia ya kuwafanyia majaribio wachezaji wa kigeni na badala yake ziwe na maskauti watakaokuwa wanafuatilia mchezaji katika nchi za kigeni na anapokuja nchini apimwe tu afya na kupewa mkataba.
Mbona nasikia Azam ni bahari nyingine?
 
Mimi naamini kwamba Sserunkuma, Tambwe, Jaja, na wengine wote ni wachezaji wazuri, ingawa sisemi kwamba timu zilizowachukua hazikukurupuka. Hilo sina hakika nalo. Tunalopaswa kuzingatia wakati tukiwatathmini wachezaji hao ni:
1. Mazingira ya ligi waliyoingia na waliyoihama: hata wachezaji wanaokubalika kuwa wazuri bila ya kutia chembe ya shaka, hutokea kutofanya vibaya mwanzoni au muda wote wa kuhamia ligi nyengine. Ballac, Shevchenko, Balotelli, Suarez, ni mifano michache. 2. Aina ya wachezaji kwenye timu aliyotoka ikilinganishwa na anakohamia: mara nyengine uwezo binafsi wa mchezaji anayen'gara huchangiwa ama kukuzwa na wachezaji/uchezaji wa timu aliyon'gara. Anapokosa wachezaji/uchezaji wa alikotoka, inamwia vigumu kuonesha ukali wake kwenye ligi mpya. 3. Uhusiano wake na benchi la ufundi na/au wachezaji wenzake: mchezaji anaweza kupendwa, kuaminiwa na kuvumiliwa na kocha mmoja lakini anapoangukia mikononi mwa kocha mwengine akakosa kuaminiwa kiasi hicho. Kaka na Mourinho ni mfano mmojawapo. Uhusiano kama huo kutoka kwa wachezaji wenzake pia unamwathiri 4.matarajio ya kupindukia kutoka kwa washabiki: wakati mwengine mchezaji anaweza kuwa hajafanya vibaya, ila kwa sababu matarajio ya wapenzi yalikuwa ni makubwa kwake, huonekana si lolote anaposhindwa kuyafikia. Jaja amefunga goli moja kwenye mechi saba za Ligi, amefunga mabao saba kwenye mechi kumi na moja. Si rekodi mbaya kwa mchezaji wa kawaida (fananisha na akina Diarra, Kipre, ngassa, na wengineo kwenye idadi hiyohiyo ya mechi za msimu huu). Lakini anaonekana garasa kwa sababu watu walitegemea mabao yote hayo aliyopata kwenye mechi 11 angeyafunga kwenye mechi moja tu. 5. Kuzidiwa na shinikizo la washabiki: Mchezaji anayetarajiwa kufanya vizuri akishindwa kuwaridhisha wanaomtarajia huwa anajikuta kwenye hofu ya kutofanya vizuri mechi inayofuata. Ndiyo yanayomsibu Balotelli licha ya utukutu wake. 6. Tofauti ya viwango vya ligi anayotoka na nayohamia: mchezaji aliyen'gara kwenye ligi ya kiwango kidogo anapohamia ligi ya kiwango kikubwa anaweza kuanzia kuwa mchezaji wa kawaida tu, mpaka atapokomaza uwezo wake kwenye ligi mpya. Hilo linaweza kuchukua muda. Hapa nakusudia ligi, siyo nchi. Mchezaji anaweza kutoka ligi ya chini ya nchi hiyohiyo na kun'gara, lakini anapohamia ligi ya juu yake uwezo wake usionekane haraka. Au mchezaji anaweza kutoka nchi yenye ligi ya kiwango kikubwa, lakini yeye alikuwa akicheza za madaraja ya chini zaidi ambayo ni dhaifu kushinda daraja la ligi anayohamia.
Yote kwa yote, tuwatathmini wachezaji wa kigeni kwa uhalisia huo, si kwa jinsi magazeti na blogu zinavowakuza au kuwananga kwa ushabiki wao.
 
Ni kweli wamemsajili tena kwa dau dogo, si unajua Msongamanoni hawawezi ku-compete kwenye soko la kununua wachezaji bora na wenye gharama kubwa.

Naona kila tasnia in ujanja wake, jamaa aliwahenyesha halafu baadae akajiongeza kuwa Vietnam wanamuhitaji tena, simba wakamtamani tena wakati walimwita kikongwe
 
It takes JUJU in order to survive katika ligi hii.....! si umemuona Tambwe sasa hivi...yaani utafikiri mke wa nyumba ndogo.hata kocha Phiri hamjali....!...naona sasa aondoke arudi burundi ampishe Andunje.
...katika hayo mambo ya JUJU waganda wako vzr sana mkuu...
 
Uongozi wa Aveva umeamua kutufanyia kituko kingine ndugu zangu...huu usajili wa haka kachezaji kafupi...sina uhakika nao..simply because kachezaji kaliongoza kwa magoli kwenye kaligi ka kenya sasa nao simba ndio wameona mlango wa kupitia...haka kachezaji ni kafupi kwelikweli...nilikaona pale msimbazi kalikuwa kanaingia ndani kumwaga wino.

Najiulizaga hivi kweli kataweza kuwakabili akina Canavaro na Yondani.

kusema kweli simba yangu ya nsimuu huu ni Ashki Majnuni.Ngoja niende kwa mtani Yanga (kwa mkopo)...hadi msimu huishe.

Tatizo pale Simba ni kuwa wachezaji hawasajiliwi na timu bali na viongozi. Mchezaji aweza kuchukiwa kwa sababu tu kasajiliwa na kiongozi fulani na kupendwa vilevile kisa ni aliyemsajili. Utashangaa muda huu Ivo au Tambwe hawana thamani kisa ni waliowasajili. Utashangaa wanamtafuta Kaseja ambaye hajaonekana uwanjani tangu ligi ianze ili wamteme Ivo. Wawaruhusu basi kina Tambwe na Chanogo waende Yanga na Azam ndipo waone majuto live. Uongozi huu wa Simba utakuwa majuto kwa wapenzi wa Simba mpaka watakapomaliza muda wao.
 
Mbona nasikia Azam ni bahari nyingine?


Hapana, Azam nao bado hawajajitofautisha sana na mababa zake Yanga na Simba. Wamesajili wachezaji wa kimataifa baada ya kumfanyia majaribio kama vile yule Mhaiti.

Japo hata huko majuu wachezaji wanafanyiwa majaribio, lkn yana tofauti sana na huku kwetu. Timu kama Azam inaweza kuchukua wachezaji bora tupu ktk nchi zinazotuzunguka na Afrika yote pia kama inavyofanya TP Mazembe kama walivyofanya kwa huyu Wawa.
 
Ni kweli wamemsajili tena kwa dau dogo, si unajua Msongamanoni hawawezi ku-compete kwenye soko la kununua wachezaji bora na wenye gharama kubwa.

Mchezaji bora kama emerson na jaja? au Ngassa na Tegete?
 
Tatizo pale Simba ni kuwa wachezaji hawasajiliwi na timu bali na viongozi. Mchezaji aweza kuchukiwa kwa sababu tu kasajiliwa na kiongozi fulani na kupendwa vilevile kisa ni aliyemsajili. Utashangaa muda huu Ivo au Tambwe hawana thamani kisa ni waliowasajili. Utashangaa wanamtafuta Kaseja ambaye hajaonekana uwanjani tangu ligi ianze ili wamteme Ivo. Wawaruhusu basi kina Tambwe na Chanogo waende Yanga na Azam ndipo waone majuto live. Uongozi huu wa Simba utakuwa majuto kwa wapenzi wa Simba mpaka watakapomaliza muda wao.

Katika jambo ambalo sitakaa niisapoti timu yangu ya Simba ni kumuacha Ivo na kumrudisha galasa kaseja.Ujinga mkubwa sana.
Nakubaliana na wewe pia simba na Yanga wanaosajili pale ni watu na sio timu...Sio simba sio Yanga akaunti zao zina shillingi sufuri.

Simba na Yanga hawachekani.Wote ni wababaishaji
 
Back
Top Bottom