Mr. SADC_TZ
Senior Member
- Nov 7, 2014
- 105
- 22
-Ujio wa mshambuliaji mpya wa Simba SC, Daniel Sserunkuma unaibua maswali mengi kweli.Kutokana na Taswira ya ushindani ktk ligi yetu...je ataweza kuhimili changamoto za VPL.
-Kama Ushindani ktk ligi.
-Presha kutoka kwa mashabiki ya kumtaka afunge goli kila mechi.
-Sifa kutoka kwa Magazeti ya Udaku.
-Au tutegemee kama yaliyomkuta Mwenzake Hamisi Tambwe.
Msimu wa kwanza tu ..kawa Top scorer.... kashiba sifa kutoka kwa mashabiki na magazeti...sifa zikazidi..basi ndio kiwango kimeporomoka...!na hatimaye baada ya msimu mmoja arudi Gor Mahia.
-Kama Ushindani ktk ligi.
-Presha kutoka kwa mashabiki ya kumtaka afunge goli kila mechi.
-Sifa kutoka kwa Magazeti ya Udaku.
-Au tutegemee kama yaliyomkuta Mwenzake Hamisi Tambwe.
Msimu wa kwanza tu ..kawa Top scorer.... kashiba sifa kutoka kwa mashabiki na magazeti...sifa zikazidi..basi ndio kiwango kimeporomoka...!na hatimaye baada ya msimu mmoja arudi Gor Mahia.
![]()
Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania Simba SC.
Raia huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.
''Nimefurahia miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.
Mchezaji huyo wa kimataifa katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini Daresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi ya Tanzania.
Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.
Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.
BBC Swahili