Spora Liana: RC Arusha aliniomba hongo ya Millioni 100

Spora Liana: RC Arusha aliniomba hongo ya Millioni 100

Kazi ipo kama waziri wa tamisemi anaingiaga huku ataona hiyo na ifanyiwe kazi.Mbona watu wameanza kubadilika?hii hata mwigulu akiikuta atifanyia kazi na huyo rc wanayemsemea ni nani?waziri mkuu mrudishe huyu mama arusha kwa faida ya serikali na nchi yetu alikaa pale tukaona mapato yameongezeka sana na hili halina ubishi

Hivi unafikiri kama Mkuu wa Wilaya/mkoa anaomba 100, unategemea nini kwa Waziri?
 
Katika viongozi wachache WAADILIFU ambao nchi hii imebakiza basi ni pamoja na huyu Mama Liana Spora.

Lakini kwa kuwa RUSHWA ni mfumo wa kitaasisi unaolindwa na serikali ya CCM I'm afraid she is fighting losing war.

Mamalaka inayotakiwa kumuwajibisha huyo RC wa Arusha aliyeomba RUSHWA ya TShs. 100 milioni, ndiyo kinara wa rushwa (kesi ya ngendere kula mahindi kumpelekea tumbili).

The writting is already on the wall, finally mama Liana Spora atakufukuzwa kazi na huyo RC aliyeomba rushwa atatanukiwa cheo! Yangu macho!

Ndicho kitakachotokea. Inasikitisha sana. Huyu Mkuu wa Mkoa wa Arusha anaweza kuwa ndiye amemtengenezea Mama Sipora hii kesi ya mambo yaliyotokea akiwa Mkuranga katika jitihada za kummaliza. Kama jamii, lazima tuwe na taratibu za kuwatambua na kuwaenzi watu aina ya Mama Sipora. Tukiendelea na tabia ya kusifia wezi na watu ambao hawatekelezi majukumu yao kwa uadilifu, hatutafika popote. Kama wakimfukuza kazi, natumaini kwa uwezo alio nao atapata kazi nyingine nzuri.
 
Kwa nyakati hizi huyu mama anaonekana hana akili nzuri ,kama mtu hupendi rushwa unaonekana MWENDAWAZIMU na baadaye utachekwa na kudhauriwa pale ukija kuwa nje ya mfumo na maisha yako kuwa ya kawaida.Kwa rushwa ilivyo ota mizizi huyu mama atachukiwa kila sehemu atakayoenda na mwisho atapigwa zengwe tu aache kazi.
 
Aisee wewe humjui huyo mama anamisimamo kama mpemba,yaani haangalii cha uccm wala nini yeye ni kazi tu

Ndiyo maana nimesema huyu Spora Liana ndiye atakaye onja joto la jiwe.Maana amewazuia wenye shamba lao kujichotea.
 
Sitalipa kodi tena.....nchi ya wahuni hii...
 
Spora Liana is a performer sema tu serikali ya ccm haipendi kufanya kazi na performers.
 
Liana-Spora-October14-2014.jpg


Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana

Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana, amesema mwaka jana alivyokuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha aliingia katika mgogoro mkali na Mkuu wa Mkoa baada ya kugoma kutoa milioni 100. Mkurugenzi aliyasema hayo jana wakati akijitetea mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, dhidi ya madai ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo na Ushirika, Dk. Francis Mallya, wa Halmashauri ya Mkuranga.

Liana alitoa madai hayo bila kutaja jina la Mkuu wa Mkoa aliyeomba fedha hizo wala hakufafanua kwa undani kuhusiana na jinsi alivyoombwa fedha hizo wala lengo lake. Mkurugenzi huyo alikuwa akihojiwa na Mwanasheria wa mlalamikaji, Getrude Cyricus, ambaye alitaka aeleze kitu gani kilimfanya akaingia kwenye mgogoro alivyokuwa Mkurugenzi wa Jiji.

Mbele ya Mwenyektii wa Baraza hilo, Jaji Hamis Msumi, alidai kuwa "RC Arusha alitaka nitoe Sh milioni 100 nilivyokataa ndiyo chanzo cha mgogoro," alidai Liana. "Watumishi ambao hawanipendi ni wale ambao wanataka kutafuna fedha za umma au kujichotea watakavyo, nimesimamia hilo na ndiyo msimamo wangu na sitayumba," alisisitiza.

Alidai ulaji ndani ya Halmashauri una mtandao mrefu sana na unahusisha watu wengi na kwamba daima hakubaliani na watu wanaochota fedha ya umma kwa manufaa yao wenyewe. "Kila Halmashauri niliyopita nimeziba mianya ya ‘ulaji' wa fedha za umma, niliingia Mkuranga kukiwa na mapato ya milioni tatu kwa mwezi, lakini ndani ya muda mfupi nilipandisha hadi kufikia milioni 71, Jiji la Arusha niliweza kufikisha hadi zaidi ya bilioni moja, sikubaliani na ulaji, wizi na hapo ndipo napigwa vita sana kila ninapohamishiwa," alidai.

Awali, Dk. Mallya alilieleza Baraza hilo kuwa kusimamishwa kazi kwa kipindi cha wiki 17 na wiki tatu kumemuathiri kisaikolojia, kiuchumi na hakutendewa haki kwa kuwa kanuni, sheria na taratibu hazikufuatwa na hivyo jamii kumuona asiyefaa. Alidai katika kumsimamisha kazi Liana alitumia ubabe kwa kuwa kwa kipindi chote aliwekewa zuio la kutotoka nje ya wilaya bila kibali na bila kamati ya uchunguzi ikikutana kwa siku moja kwa saa moja na kutoa uamuzi.

Alidai kwa wakati huo mama yake alikuwa mgonjwa alihitaji kupelekwa India kwa matibabu, alikosa ruhusa kwa madai kuwa ni mtuhumiwa huku akikataa asipandishwe daraja, hivyo kuathirika kiuchumi kwa kubaki kwenye daraja la mshahara wa TGSD J huku waliokuwa naye kazini wakiwa mbali. Akijibu madai hayo, Liana alisema Dk. Mallya alisimamishwa majukumu yake kutokana na mwenendo wa utendaji kazi zake na wizi wa fedha za umma kwa kushirikiana na Mkaguzi wa Ndani, Mwenyekiti wa halmashauri, Afisa Utumishi na watumishi wengine.

"Baada ya kuhamishiwa pale Agosti 2008, Septemba kulikuwa na ukaguzi maalum wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyotaja watumishi 68 na Mwenyekiti wa Halmashauri kuhusika kwenye ubadhilifu na kutakiwa kurudisha fedha hizo…niliwaandikia barua wote akiwemo Mwenyekiti," alidai.

Alidai ndani ya muda huo alipata safari ya kikazi na kumkabidhi ofisi Dk. Mallya, ambaye hakuwa na maelekezo ya kushughulikia ripoti ya CAG, lakini kwa kipindi kifupi aliitisha Bazara la Madiwani kwa ajili ya kuazimia kumfukuza kazi (Liana). Alidai katika ripoti hiyo Mwenyekiti wa halmashauri alikuwa anawekewa mafuta na halmashauri kila siku kwenye magari yake mawili na teksi yake na kutokana na urafiki wa Dk. Mallya na Mwenyekiti, walimuondoa na kumuweka yeye (Mallya) kama Kaimu DED.

Alisema Mkuu wa Wilaya, Clemence Urawia, alimtaka Dk. Mallya kuomuonyesha mashamba darasa yaliyotajwa kwenye ripoti ya CAG, lakini alimzungusha na yeye (Liana) aliomba ampeleke akampa msaidizi wake ambaye baada ya kusafiri kilomita tano alimueleza ukweli kuwa hakuna miradi kama hiyo. Kulikuwa na miradi hewa kama ya barabara, joshu, na bwawa ikiwamo kuweka katika ripoti iliyokwenda kwenye Kamati ya CCM wilaya mazao ambayo hayalimwi kwenye eneo husika.

"RC na DC waliniagiza kumfukuza kazi, lakini nilimwandikia barua ajieleze, lakini hakufanya hivyo…Dk. Mallya kwa kushirikiana na wengine alikuwa anafanya hujuma nyingi, lakini nilimsamehe na wakati mwingine kumtaka ajieleze na kuomba ushauri kabla ya kumchukulia hatua," alieleza. Liana alieleza kuwa kuna wakati hakuwapo ofisini fedha za uwekezaji zilitolewa na kuelekezwa kwenye ujenzi wa ofisi ya Mallya huku akijua fedha hizo zinapaswa kutekeleza miradi pekee badala ya matumizi mengine na kwamba kuna wakati faili la barua lilitoweka katika mazingira tatanishi.

Alisema fedha za wakulima wa korosho Shilingi milioni 65 zilitaka kuliwa, lakini kutokana na jitihada zake zililipwa kwa wakulima baada ya suala hilo kufika mbele ya kamati ya ulinzi na usalama. Alidai kuwa Dk. Mallya alikuwa anashirikiana na baadhi ya viongozi wa mkoa kumkwamisha na kula fedha za halmashauri na hata alipounda kamati ya uchunguzi hakupata ushirikiano stahili badala yake alipigwa vita ili akate tamaa, lakini hakurudi nyuma katika kusimamia fedha ya umma.

"Baada ya Dk. Mallya kusimamishwa mambo yalianza kwenda kwa kuwa nina taaluma ya kilimo, nilisimamia uanzishwaji wa mashamba darasa matano na kupata fedha nyingine za utekelezaji wa miradi 44 ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), ambazo zililiwa," alidai. "Kwa ujumla mazingira ya utendaji kazi kwangu yalikuwa magumu sana kwa kuwa yalitengenezwa na Dk. Mallya na wenzake waliotaka kutafuna fedha," alidai. Shauri hilo linatarajiwa kuendelea kesho kwa DED kuleta mashahidi zaidi ambao ni Mwansheria wa Halmashauri, Mkuu wa wilaya na Mkuu wa mkoa wa Pwani.

DC GAMBO ATUHUMIWA TUHUMA NZITO

Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Mrisho Gambo, alifika mbele ya Baraza hilo na Mkurugenzi wa Mji wa Korogwe kueleza jinsi anavyotukana na kudhalilisha watumishi wa halmashauri. Mkurugenzi wa mji huo, Lewis Kalinjuna, akiongozwa na mwanasheria Hassani Mayunga, alidai amefanyakazi kwenye halmashauri kwa miaka 27 na wakuu wa wilaya 14, lakini hajawahi kukutana na kiongozi mwenye lugha chafu na za kudhalilisha kama Gambo.

Alidai kuwa mara kwa mara amekuwa akiwaita watumishi kwenye vikao vya kamati ya ulinzi na usalama na kuwadhalilisha. Alidai DC Gambo amekuwa akitumia mikutano ya hadhara ya wananchi na watendaji kudhalilisha watendaji, ikiwa ni pamoja na kumtaka DED kutohudhuria vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ambavyo yeye (DC) ni Mwenyekiti.

Mkurugenzi huyo aliweka hadharani majina ya watumishi waliowahi kutukanwa na kudhalilishwa na kudai kuwa ana mashahidi juu ya malalamiko hayo. Alidai DC huyo amekuwa akilazimisha halmashauri kukiuka sheria za manunuzi, kuweka shinikizo watumishi kuchukuliwa hatua kinyume cha sheria. Kalinjuna alidai kuwa DC huyo alilazimisha kutumika kwa mafundi wa kawaida kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa huku fedha zilizotolewa zikiwa na masharti ya kutumia wakandarasi. Shauri hilo litaendelea kesho kwa mashahidi zaidi kutoa ushahidi wao.

Chanzo: Home
 
She is very very stupid....!!

What do you mean when you say the word stupid? You mean your mother? Your husband? Or something never existed? Come out clearly before we conclude stupidity on you, in its true meaning.
 
Inawezekana Muu wa Mkoa aliomba rushwa hiyo ya milioni 100.

Maswali ya kujiuliza

  • Tunauhakika gani kama huyu mkurugenzi naye ni janja yake ya kukwepa tuhuma ya kutumia vibaya madaraka yake?
  • Kwanini hakutoa tuhuma hizo mapema kwa mamlaka husika akiwa mkurugenzi katika kituo chake cha awali Arusha badala yake iwe sasa baada ya kuitwa na tume ya maadili kama mshtakiwa?

My take: This serves as one of examples, among many, of our corrupt authorities simply playing a business as usual game.As far as no one will be held responsible, presumably, it is a disease same as Ebola, thus should be cured even by importing the foreign medics. Just fed-up of Bongoland's "janjajanja". Kind of "ni upepo tu;utapita" style...
 
Hivi unafikiri kama Mkuu wa Wilaya/mkoa anaomba 100, unategemea nini kwa Waziri?

Ni viongozi wote wako hivyo. Wanaomba hata elfu moja. Si Umesikia Rais anapewa saa? Anajibalaguza lakini ndo walivyo na wanashindana kuiba pesa. Siku za nyuma huyo tunayeita Rais alipewa suti! Bado, baadaye watapewa hata chupi.
 
Inawezekana Muu wa Mkoa aliomba rushwa hiyo ya milioni 100.

Maswali ya kujiuliza

  • Tunauhakika gani kama huyu mkurugenzi naye ni janja yake ya kukwepa tuhuma ya kutumia vibaya madaraka yake?
  • Kwanini hakutoa tuhuma hizo mapema kwa mamlaka husika akiwa mkurugenzi katika kituo chake cha awali Arusha badala yake iwe sasa baada ya kuitwa na tume ya maadili kama mshtakiwa?

...


Na uwakika Waziri Mkuu anajaua, Na Raisi pia analijua hili, ila waliamua kulindana na kumtoa Arusha mama, ili jama waendele kutafuna.

Au wewe unafikiri kwanini walimtoa Arusha?
 
Na uwakika Waziri Mkuu anajaua, Na Raisi pia analijua hili, ila waliamua kulindana na kumtoa Arusha mama, ili jama waendele kutafuna.

Au wewe unafikiri kwanini walimtoa Arusha?

Mkuu una uhakika?

Kwanini sasa wakuu hao hawajamlinda mama asishughulikiwe na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma?

Yote yanawezekana:yeye kujihami au kweli aligusa maslahi ya wakubwa."Only in Tanzania...!"
 
Suala la RC Arusha kutaka rushwa kutoka kwa Sipora siyo siri, inasemekana hata takukuru walipewa taarifa ili wakamate RC , lakini serikali iliingilia kati kuzuia aibu isitokee. Nikusema kwamba manbo yanayoendelea maofisini ( ufisadi) yanabaraka ya serikali ya ccm. Ndiyo maana maDED huisaidia sana ccm wahati wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom