Spinning zinavyotugharimu

Tupo kwenye laiti traki. Tutembee vifua mbele. Tuwe wazalendo
 
Operation zifanyike kimya kimya kwa kumuogopa nani?
Kama mnataka misaada yao nendeni kwao mkafanye ushoga mpewe misaada maana naona inawauma sana.
NO USHOGA TANZANIA
Bora tule nyasi.

Msitake kujifichia kwenye ushoga, tatizo ni jiwe kwa kiburi cha madaraka. Kuchezea box la kura, kunyanyasa wapinzani, uhuru wa habari nk. Hilo la ushoga mnalichomekea ili mpate support ya watanzania wengi kuficha sababu hasa za kuchukuliwa hatua.
 
mambo yakiwa magumu Makonda ajiandae kwa kutolewa kafara, ndivyo watakavyo hao wapenda ushoga, jamaa akipigwa chini itabadili upepo...siungi mkono ushoga lkn ndivyo watakavyo hawa mabepari

Hili unalolipendekeza ni gumu sana. Apigwe chini apelekwe wapi? Kuna watu wasiostahili kuwa mbali na mwenye maamuzi. Huyu ni mmoja wapo, kama sio ndie mwenyewe mwenye funguo za makabati yote.

Unasahau pia msemo huu "Ukinilazimisha ndio unaharibu kabisa". Akifanya kama unavyopendekeza atadharauliwa!

Atolewe hapo labda asogezwe ndani zaidi kwenye giza ili atende bila kuonekana kwenye kamera kama ilivyo sasa.
 
Msitake kujifichia kwenye ushoga, tatizo ni jiwe kwa kiburi cha madaraka. Kuchezea box la kura, kunyanyasa wapinzani, uhuru wa habari nk. Hilo la ushoga mnalichomekea ili mpate support ya watanzania wengi kuficha sababu hasa za kuchukuliwa hatua.

Na hili la ushoga ndilo wanaloliweka mbele. Hawataki kabisa hayo mengine yawe sababu za kunyimwa misaada.

Lakini nami pia nawalaumu hawa wazungu kwa kiasi fulani. Tabia yao ni kupiga kelele nyingi linapojitokeza hili la mashoga. Wakati ukandamizaji unapofanyika kwa raia wa kawaida na wanasiasa, sauti zao huyu hafifu sana, na hazisikiki. Hii tabia yao hata mimi huniudhi.
 
Ushoga hautakiwi na watanzania walio wengi sana kwa sababu za kiutamaduni wetu.
Tatizo suala hili linashughulikiwa na mtu asiye na akili kabisa za kumtosha yeye mwenyewe, achilia mbali kuongoza mkoa.
Matokeo tunayaona live.
Mtu anaacha kushughlikia visima, barabara, kero za wananchi anarukia vilivyo juubya uwezo wake kufikiri na kutenda.
 


Ni hivi, baada ya kauli za Makonda, Serikali ilitoa msimamo na kupingana na Makonda. Lakini hawa DENMARK wameendelea kushikilia bango hata baada ya Statement ya serikali. Kwa akili ya kawaida, unaamini uamuzi wa Denmark ni kweli kutokana na mambo ya ushoga au kuna kitu wapigwa chini? TAFAKARI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…