Spika wa Bunge Makinda Amegoma kufungua Barabara Ipitiayo Nyumbanikwake?

Status
Not open for further replies.

Kubwajinga

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,194
297
Barabara iliyofungwa kwa Makinda haijafunguliwa



makinda.jpg

Spika wa Bunge, Anna Makinda
Na Joseph Zablon, Mwananchi (email the author)
Posted Jumatatu,Marchi11 2013 saa 16:24 PM


Manispaa ya Kinondoni imeshindwa kuifungua barabara inayowaunganisha wakazi wa Kijitonyama na Sinza iliyofungwa wiki 52 zilizopita ili kuruhusu ukarabati wa nyumba iliyoko katika kiwanja namba 630.
Nyumba hiyo inamilikiwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Aprili 14, mwaka huu Spika Makinda kupitia Kampuni ya ujenzi ya Conctrete System Ltd, aliomba kibali cha kuweka uzio na kuifunga barabara hiyo iliyoko jirani na nyumba yake, kwa ajili ya usalama wa vifaa vya ujenzi na wapitanjia.

Ombi liliridhiwa na Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Athanas Uriyo Mei 10, mwaka 2011.
Hata hivyo ombi hilo lilitumwa kwa mhandisi, siku moja baada ya gazeti hili toleo la Aprili 14, mwaka 2011, kuandika habari za kufungwa kwa barabara hiyo bila maelezo.

Kitendo hicho kililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kupitia kwa Diwani wao, Ulole Ulole Juma.
Ulole aliliambia Mwananchi kuwa siku za kufungwa kwa barabara hiyo zimemalizika na yeye hakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kufuatilia suala hilo.

Alisema hata hivyo sasa anamsihi Spika Makinda kuifungua barabara hiyo, ili kuwawezesha wananchi kuitumia.

Ulole alisema kulingana na barua hiyo, wiki 52 zilizokuwa zimetolewa na Manispaa ya Kinondoni, zimemalizika tangu Julai mwaka jana, lakini inashangaza kuona barabara bado imefungwa.

"Mbaya zaidi kumesimikwa kibanda cha mlinzi huku kukiwa hakuna dalili za barabara hiyo kufunguliwa," alisema.

Mhandisi wa Uriyo mara kadhaa alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kufafanua suala hilo, aliomba apewe muda na kuahidi kutoa maelezo baadaye lakini hata alipotafutwa tena alisisitiza kupewa muda zaidi kwa madai kuwa ama yupo safari au katika semina.




Hii ni aibu kubwa kwa Bunge, nchi na dhihaka kwa sheria zetu.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1717276/-/1284xb3/-/index.html
 
Hivi angekuwa rais ingekuwaje? Maana hapo ni spika tu, naona zile msg kamaliza kuzisoma ngoja namimi leo nimtumie yangu
 
Nchi hii bwana ukiwa na madaraka unaweza ukafanya chochote unachopenda huyu ni spika tu hipo siku ataamua kuwachapa bakora wakazi wote wa kijitonyama kwa mwendo huu dah!hivi kwanini tunashindwa kuwa kama watu wa hapo kenya tu maana nikisema misri itakuwa mbali sana
 
Makinda Amelewa madaraka! Anafanya kile ambacho serikali yake hufanya na chama chake hufanya. Hakuna justification ya kufunga barabara inayotumiwa na wananchi kwa ajili ya mkubwa eti kulinda usalama wake. si ahame eneo hilo ili anede kwenye maeneo wakubwa wenzake walipo? Aibu inazidi kila kukicha kwa viongozi wetu wa chama tawala
 
mna uhakika ile njia kafunga yeye mhe. anna makinda??? the truth is ile njia imefungwa na TISS kwa sababu 'wanazozijua' wao hao TISS.
 
unashangaa?mbona arusha isdori shirima alifunga inayopita nyumbani kwake baada ya mkewe kumshauri kuwa inamtimulia vumbi nyumbani.mpaka leo wakuu wote wa mikoa wanaokuja hawaifungui isijeikawatimulia vumbi.chezea viongozi wa sisiem wewe.
 
.. tumuulize kwani kanuni za bunge zinasemaje juu ya hilo.kanuni.. ibara ya 51 personal life, uzuiaji wa raia kuona nyumba ndogo ya spika kwa maslahi ya bunge.
 
mtamwibia, watanzania kila kitu ni dili tu hata vipande vya tofali, mbao na nondo. piteni barabara zingine si zipo bwana. lah nendeni mahakamani mkadai haki yenu.
 
Huyu mama ana matatizo sana! Ndo maana hana mume, she doesnt deserve to be married. Anafaa kuwa sanamu la kuvisha nguo maduka ya nguo. Kale katabasamu katafaa
 
Yeye hatii sheria harafu analazimisha wabunge wa Cdm wahojiwe. Tunaomba hao Wabunge wagome mpaka na yeye atii sheria bila shuruti
 
Silaha bora au niseme ulinzi madhubuti ni kuwa na mahusiano mazuri na watu, na hasa majirani zako. Makinda ungeishi kwa amani na kulala usingizi mnono kama ungekuwa na mahusiano mazuri na jamii iliyokuzunguka. Kufunga barabara maana yake unajua tayari wewe huna mahusiano mazuri na watu. Mbona Mzee Mwinyi anakaa kwenye barabara kubwa kabisa sembuse Spika?

Aliye juu mngoje chini!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom