Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Barabara iliyofungwa kwa Makinda haijafunguliwa
Spika wa Bunge, Anna Makinda
Na Joseph Zablon, Mwananchi (email the author)
Posted Jumatatu,Marchi11 2013 saa 16:24 PM
Manispaa ya Kinondoni imeshindwa kuifungua barabara inayowaunganisha wakazi wa Kijitonyama na Sinza iliyofungwa wiki 52 zilizopita ili kuruhusu ukarabati wa nyumba iliyoko katika kiwanja namba 630.
Nyumba hiyo inamilikiwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Aprili 14, mwaka huu Spika Makinda kupitia Kampuni ya ujenzi ya Conctrete System Ltd, aliomba kibali cha kuweka uzio na kuifunga barabara hiyo iliyoko jirani na nyumba yake, kwa ajili ya usalama wa vifaa vya ujenzi na wapitanjia.
Ombi liliridhiwa na Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Athanas Uriyo Mei 10, mwaka 2011.
Hata hivyo ombi hilo lilitumwa kwa mhandisi, siku moja baada ya gazeti hili toleo la Aprili 14, mwaka 2011, kuandika habari za kufungwa kwa barabara hiyo bila maelezo.
Kitendo hicho kililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kupitia kwa Diwani wao, Ulole Ulole Juma.
Ulole aliliambia Mwananchi kuwa siku za kufungwa kwa barabara hiyo zimemalizika na yeye hakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kufuatilia suala hilo.
Alisema hata hivyo sasa anamsihi Spika Makinda kuifungua barabara hiyo, ili kuwawezesha wananchi kuitumia.
Ulole alisema kulingana na barua hiyo, wiki 52 zilizokuwa zimetolewa na Manispaa ya Kinondoni, zimemalizika tangu Julai mwaka jana, lakini inashangaza kuona barabara bado imefungwa.
"Mbaya zaidi kumesimikwa kibanda cha mlinzi huku kukiwa hakuna dalili za barabara hiyo kufunguliwa," alisema.
Mhandisi wa Uriyo mara kadhaa alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kufafanua suala hilo, aliomba apewe muda na kuahidi kutoa maelezo baadaye lakini hata alipotafutwa tena alisisitiza kupewa muda zaidi kwa madai kuwa ama yupo safari au katika semina.
Hii ni aibu kubwa kwa Bunge, nchi na dhihaka kwa sheria zetu.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1717276/-/1284xb3/-/index.html