Sababu aliyoitoa ya kuhalalisha kupanda gharama za maisha haina mashiko. Kama gharama za maisha zimepanda, basi zimepanda kwa watanzania wote na siyo kwa wabunge tu.
Kama kilichoandikwa na magazeti ni sahihi, kwamba sitting allowance imepanda kutoka Sh. 70,000/= mpaka Sh. 200,000/=, huu unaweza kuwa ni mtego kwa CHADEMA ambao wamekuwa wakiikataa hii posho ya vikao.
Dr. Kashilila alisema ni wabunge walipendekeza, ajabu ni kwamba ni Wabunge gani? Mbona wabunge wa upinzani [CHADEMA] na wao wanashangaa? Mbona Januari Makamba anasema hilo halijui? Hii inaweza kuwa ni strategy ya CCM kuua hoja ya CHADEMA kugomea posho na imewekwa kama mtego. So, wabunge wa CHADEMA hicho ni chambo cha hoja yenu. Kazi kwenu, kusuka au kunyoa!