Spika wa bunge (Anne Makinda) akiri posho kuongezwa!

Kwa walimu kutimiza miaka 50 ya uhuru kwa kushushwa madaraja, lazima sisi binafsi tuiandalie serikali hii zawadi maalum ya kuikataa kwa nguvu 2015 make najua chama chetu kimeshatekwa nyara na ccm! Na huko madarasani tuendeleze kumwaga sumu ya kuikataa ccm, ndiyo mchango bora zaidi tunaweza kutoa kwa sasa.
 
Ifikapo kwenye masilahi nilishasema wabunge wote ni wabinafsi. Rejea post zetu za nyuma kuhusu mjadala wa kuboresha mishahara ya wabunge.

Kujua nasema ukweli; kama si gazeti kuandika wabunge wote walikaa kimya na kuendelea kula posho zao. Alafu wakiulizwa wengine wanajifanya kushangaa "Eti kama wameongeza mimi sijui"!

Shame on you MPs!
 
Wezi utawajua tuu kwa kauli zao!spika na katibu wanakauli tofauti huenda hizo posho wanalipwa wabunge wachache zingine wana sign na kuiba
 
At least presha imeshuka huyu Kashililah alinichanganya sana.....nilikuwa najiuliza nitaiambia nini nyumba ndogo niliyokwisha i-promise.

Itabidi tubadilishane sasa haya maisha nanyie mpigike uswazi.
 
Sababu aliyoitoa ya kuhalalisha kupanda gharama za maisha haina mashiko. Kama gharama za maisha zimepanda, basi zimepanda kwa watanzania wote na siyo kwa wabunge tu.

Kama kilichoandikwa na magazeti ni sahihi, kwamba sitting allowance imepanda kutoka Sh. 70,000/= mpaka Sh. 200,000/=, huu unaweza kuwa ni mtego kwa CHADEMA ambao wamekuwa wakiikataa hii posho ya vikao.

Dr. Kashilila alisema ni wabunge walipendekeza, ajabu ni kwamba ni Wabunge gani? Mbona wabunge wa upinzani [CHADEMA] na wao wanashangaa? Mbona Januari Makamba anasema hilo halijui? Hii inaweza kuwa ni strategy ya CCM kuua hoja ya CHADEMA kugomea posho na imewekwa kama mtego. So, wabunge wa CHADEMA hicho ni chambo cha hoja yenu. Kazi kwenu, kusuka au kunyoa!
 
Zitto ameshauri watanzania wawanunie viongozi wanaoshabikia posho akiwemo spika makinda kuonesha kwamba haturidhiki na mtindo wa kujilimbikizia. Wewe unadhani kununa kutawapa ujumbe kwamba watanzania hawawaungi mkono?

Source: Zitto twitter account
 
Yaani nchi hii kila mmoja anaesema lake angalia swala la kenya kuwashambulia Al-shabaab Kikwete kawaunga mkono Kenya waziri wake Membe anawalaani.....kuhusu kulipwa Dowans Waziri alisema tunawalipa baada ya siku chache raisi akagoma...haya ya bunge katibu anasema posho haijaongezwa spika anasema imeongezwa....yaani hii serikali ni masaburi fulllllllllllllllll

Ngoja nitoe nauri, konda ananidai, dereva anasema mi staff. Hawa nao wanapingana.
 
What a lame excuse,eti nyumba zimepanda bei dodoma hii nchi ndio maana vijana tunajuta kuzaliwa tz
 
Hivi kwanini hawatumii wingi na umuhimu wao effectively? Say wagome for a month!

By the way hivi wabunge wakigoma kuna hasara yoyote?
 
eti bei ya vyumba hotel imeongezeka!jee waalimu wasio na mahali pa kuishi kabisa?
 
Wabunge ni wakatili na washenzi! Hawana huruma hata kidogo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
 
Spika wa Bunge Anne Makinda amesema ni kweli posho za wabunge zimeongezwa kutoka shilingi 70 elfu hadi laki tatu kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu mkoani Dodoma. Suala la msingi ni je maisha magumu ni kwa wabunge peke yao? Watumishi wengine wa Serikali na wananchi kwa ujumla waichukuliaje hali hii?
 
Walimu wa sekondari wawafundishe uraia wanafunzi, wawashauri wagome. Na wao wenyewe walimu wagome kwa kama mwezi au miwili. Kama kuandamana watapigwa na alshabaab basi wagome wakiwa majumbani mwao
 
Kabonga upupu gani kama hataki kusema imepanda mpa sh. ngapi? au nae anataka kutudanganya hajui ni ngapi imeongezwa
 
Back
Top Bottom