Spika tusaidie kujua CCM ilifanya vikao lini kumfukuza Nyalandu

Ndugai siku hizi kawa muongo sana !!! Jana alisema hana taarifa kama Nyalandu kajiuzuru ubunge.. Leo analeta story ya Ccm kumvua ubunge.... Wao wanachukua madiwani .. Chadema wanachukua wabunge...
Albadir mkuu

Swissme
 
Amenukuliwa PolePole akitamka kwa niaba ya CCM kuwa Ndugu Nyalandu amejivua nafasi zake na uanachama mwenyewe kwa kushindwa kasi ya JPM. Akipingana na kauli hiyo, Spika katika barua yake akikisemea chama cha CCM anakiri kupokea barua ya chama ikimuarifu kumvua uanachama Ndugu Nyalandu.

Kwa bahati nzuri ubayana huo wa matamko umetufanya tukumbuke misimamo ya CCM kupitia Ndugu Polepole kuhusu kufuata taratibu hasa vikao halali vya chama. Mwenendo huu unanipa binafsi mashaka na nina imani Spika anaweza kuwa na siri nyingi za CCM, sina shaka anazo taarifa za lini CCM walikaa kikao kumvua Ndugu Nyalandu uanachama.

Kwa kuwa si suala la chama tena na kwa mujibu wa barua ya Spika ni dhahiri kuwa suala la mahusiano ya wabunge ni la Bunge ningefurahi uwazi aliouonesha Spika uendelee kuwa bayana katika kuarifu tarehe na ni kikao gani kilichofanya maamuzi hayo.

Sina mashaka kuwa CCM ilifanya maamuzi kupitia vikao halali ikiwa barua ya Spika ni barua halali. Sina shaka wajumbe wa vikao hivyo wote walihudhuria kikao husika. Sina shaka kikao hicho kilifanyikia ndani ya Nchi. Sina shaka barua ya kuvuliwa uanachama na nafasi za Ndugu Nyalandu alizokuwa akishika ndani ya chama alikabidhiwa na chama.

Mashaka yangu yatabaki kuwa mashaka ikiwa utaratibu wa kuvua watu uanachama utatiliwa shaka na wasio na mashaka ndani ya CCM.

Albadir imefanyà kazi hawa mafisadi wa kijani wanajichanganya kichizi
 
Yaani masisiem yanajikanyaga vibaya sana. Wamesahau kuwa hawana kumbukumbu ili wawe makini!

Juzi tu polepole kasema jamaa kajivua uanachama mwenyewe. Leo nimesikia 'mtukufu' magogoni wezi wamehamia chadema (timing ya kauli ikinifanya nidhani alikuwa akiwataja wote waliohamia chadema akiwemo Nyalandu).

Sasa huyu speaker wa bunge LA jamhuri ya 'bomoa bomoa' naye anakuja na mengine! Dah, jamani! Mi nafikiri mratibu wao wa mauongo atafakari nafasi yake vizuri maana ni kama vile kazi inamshinda!
 
cha kisikitisha huwa hawaweki kumbukumbu wakiongozwa na mwenyekiti wao wa taifa, leo anasema hili, akiamka kesho anaongea kinyume chake tena na macho makavu utafikiri sio yeye.

kinachonishangaza ccm ndio wanaongoza dola, lakini kaz yao kulalamika kwamba mafisadi yapo chadema, sasa nini kinawazuia kuwawajibisha hao mafisadi walio ndani ya chadema.
 
Amenukuliwa PolePole akitamka kwa niaba ya CCM kuwa Ndugu Nyalandu amejivua nafasi zake na uanachama mwenyewe kwa kushindwa kasi ya JPM. Akipingana na kauli hiyo, Spika katika barua yake akikisemea chama cha CCM anakiri kupokea barua ya chama ikimuarifu kumvua uanachama Ndugu Nyalandu.

Kwa bahati nzuri ubayana huo wa matamko umetufanya tukumbuke misimamo ya CCM kupitia Ndugu Polepole kuhusu kufuata taratibu hasa vikao halali vya chama. Mwenendo huu unanipa binafsi mashaka na nina imani Spika anaweza kuwa na siri nyingi za CCM, sina shaka anazo taarifa za lini CCM walikaa kikao kumvua Ndugu Nyalandu uanachama.

Kwa kuwa si suala la chama tena na kwa mujibu wa barua ya Spika ni dhahiri kuwa suala la mahusiano ya wabunge ni la Bunge ningefurahi uwazi aliouonesha Spika uendelee kuwa bayana katika kuarifu tarehe na ni kikao gani kilichofanya maamuzi hayo.

Sina mashaka kuwa CCM ilifanya maamuzi kupitia vikao halali ikiwa barua ya Spika ni barua halali. Sina shaka wajumbe wa vikao hivyo wote walihudhuria kikao husika. Sina shaka kikao hicho kilifanyikia ndani ya Nchi. Sina shaka barua ya kuvuliwa uanachama na nafasi za Ndugu Nyalandu alizokuwa akishika ndani ya chama alikabidhiwa na chama.

Mashaka yangu yatabaki kuwa mashaka ikiwa utaratibu wa kuvua watu uanachama utatiliwa shaka na wasio na mashaka ndani ya CCM.
Huu ni msigano rasmi kitaarifa baina ya Mhusika katika CHAMA na MHUSIKA katika BUNGE hili linaonesha namna gani watu wetu tunaowaamini katika dhamana za utumishi WANAVYOTUMIKA hali hii ikiwa kiongozi wa mhimili mmojawapo yuko hivi je watendaji wa mihimili mingine watakuwa na hali gani?

Sote tunakumbuka kwa kina mama Sophia Simba na wenzake ilikuwaje!! Tena wanavyoogopa uchaguzi wanathubutuje kumfukuza mbunge labda sio fisiemu tunaowajua!!
 
Back
Top Bottom