Je, mwitikio mdogo wa wananchi kwenye ziara za viongozi wakuu CCM unaponywa na vikao vya chama vya dharura?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Kuna tatizo la mapokezi ya viongozi wa chama limejitokeza Manyara na Singida. Kuna mgawanyiko mkubwa umejitokeza jambo lililopelekea Nyalandu na Kabudi kurejeshwa jukwaani wakisaidiwa na askofu wa KKKT.

Mwenyekiti ameona wazi kwamba safu iliyopo kwenye chama haijafanya kazi iliyokusudiwa kwa ufanisi. Wenyeviti na makatibu wakuu wa chama kwenye mikoa wameshindwa kushawishi umma.

Kimeitishwa kikao cha dharura ambapo tunategemea kuna watu wataondoka kwenye mfumo wa dola, serikali na chama kupisha wapya.

Je, mabadiliko ya rasilimali watu yataleta toka? Au tutazidi kupeana ulaji? Tulijiaandaa kukataliwa?

Kwanini tusingekeza nguvu kupambana na rushwa na kuimiza haki? Nisrati kuvaa nguo za CCM huku tukijua hana mvuto kunawafundisha nini waliopo kwenye chama?

Lini tutawathamini wana CCM na kuachana na kuwapa promo wanaotoka upinzani? Mpinzani amepewa nafasi kubwa sana ndani ya CCM kuliko mwanaccm kindakindaki na hii inatokana na kuwanunua binadamu badala yakuwatengeneza viongozi.

Tujitafakari, chuki ndani ya CCM inaletwa na kukataliwa kwao.....tunakwenda kumtafuta mjomba wake Lissu for what...tusimame wenyewe tunaweza bila kutegemea nguvu na ushawishi wa ndugu waliopo uponzani
 
Kuna tatizo la mapokezi ya viongozi wa chama limejitokeza Manyara na Singida...
Mbona hiyo ni kawaida sana siku hizi?

Suluhisho lake ni kulipa watu pesa na kuwasomba kwa ma-fuso kutoka mikoa mingine kuja kuhudhuria, na pia kuhakikisha wanafunzi na walimu wa shule za msingi na sekondari zilizo jirani wanahudhuria kwa shuruti.

Pia, kukiwa na wasanii kadhaa wa Bongo fleva inasaidia kuvutia ma-jobless kuja kusikiliza mziki kwenye mkutano😁
 
Back
Top Bottom