johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,880
Spika wa Bunge la JMT Dr Tulia amewataka Mawaziri kusikiliza kwa makini hotuba za Rais wa JMT mh Samia ili wasiwe wanatofautiana
Dr Tulia aliyasema hayo baada ya Naibu waziri wa Nishati ndugu Byabato kuliambia Bunge kwamba mradi wa Bwawa la Umeme la Nyerere utakamilika October 2023
Baadae kidogo Byabato akatuma " kikaratasi" kwa Spika Tulia akisema alikosea kidogo Bwawa la Nyerere litakamilika June 2023
Ndipo Spika Tulia akamuuliza mara tatu kama ana uhakika na anachokisema. Byabato akasema ana uhakika kwa sababu ndivyo mkataba unavyosema.
Spika Tulia akamwambia mbona Rais amesema katika mkutano fulani kuwa Bwawa litaisha 2024? " Waheshimiwa Mawaziri muwe mnasikiliza kwa makini hotuba za Rais ili msitofautiane" alisisitiza Spika.
Chanzo: TBC