Spika Tulia awakemea Watanzania wanaoishi nje ya Nchi Wanaomuongelea Rais Samia kwa Lugha isiyofaa au kumtusi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,127
Spika wa Bunge Dr Tulia amewataka Watanzania na wale waliokwisha badili uraia wanaoishi nje ya Nchi waache kumuongelea Rais Samia kwa Lugha isiyofaa au kumtusi

Spika Tulia amesema Dr Samia ni Rais wa JMT hivyo ni lazima aheshimiwe

Spika amesema utovu huo wa Nidhamu wa baadhi ya Watanzania walioko nje hauwasaidii lolote na wakumbuke kuwa wao ni Watanzania hata huko waliko

Source: TBC
 
Suala la uraia pacha ni pana sana ,kuna wengine wanataka uraia pacha ili waweze kutukana viongozi ili uraia mwingine uwalinde. Kabla ya kulikubali panabidi pawepo na mjadala mpana wenye kubeba maslahi mapana ya Taifa na kulinda ngao za Taifa letu.
 
Hahaha hapa amelengwa Mange tu...

Spika si angemfuata tu DM huko huko insta wachanane...maana Rais mwenyewe anayenangwa wala hana hata muda na hao wanaomnanga...
Muda anao mwingi sana ndio maana aliwahi kukisifia kifua cha Harmonize!
Usijidanganye kwa hilo!
 
Rais angekua anaelewa hata kinachozungumzwa tungeanza kuwa na hisia tofauti.

Ila haelewi na hana muda huo.

Yeye analetewa tu mikataba anasaini hata iwe mia kwa wakati mmoja alimradi ameshabiwa hao ni wawekezaji na nchi itafunguka.
 
Hahahh
Mange alimchana Supika kwamba amekakamaa kama amemwagiwa maji ya ndimu
Halafu Sa100 akamsema kama Kimama kifupi kinene kinarembulia mafisadi
 
  • Kicheko
Reactions: rr3
Suala la uraia pacha ni pana sana ,kuna wengine wanataka uraia pacha ili waweze kutukana viongozi ili uraia mwingine uwalinde. Kabla ya kulikubali panabidi pawepo na mjadala mpana wenye kubeba maslahi mapana ya Taifa na kulinda ngao za Taifa letu.
Kwa mfano wewe mtu akikutukana ama kukunanga inakupunguzia nini? Utendaji kazi ? Ama inakuzuia ku excute duties zako?

Tulionya humu na nyuzi zimo kile kitendo cha kwenda mbele na kupiga piga nae mapicha picha huku ni mtu aliyekuwa anatukana Magogoni, na aliyekuwa anamtukana ni boss wako mkuu and still you entertain ujuha huo
 
Sijawahi ku entertain huo ujingq wa huyo mwanadada hata siku moja, namuona ni mjinga fulani aliyeenda shule lakini hajaelemika.
 
Back
Top Bottom