Spika Tulia adai watu watafute majibu ya hoja zao kwa kuwauliza viongozi wao na si kwenda barabarani kuandamana

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Tulia Ackson ametoa wito kwa watanzania kutafuta majibu ya hoja walizonazo kwa kufuata utaratibu na njia sahihi lakini sio kwa njia za kwenda barabarani.

Dkt,Tulia ameeleza hayo wilayani Makete mkoani Njombe wakati akizungumza na wanaCCM kwenye mkutano mkuu wa jimbo wa wilaya hiyo uliokuwa maalum kwa ajili ya uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2020 - 2023 chini ya Mbunge wa jimbo hilo Festo Sanga.

"Mwananchi mwenzangu usikubali mtu anayetaka kuchochea vurugu tutaathrika sote kama liko jambo halieleweki kwenye jamii,serikali imeweka viongozi hadi kwenye ngazi ya kitongoji nenda ukaulize huko kama hupati majibu muwakilishi wako yuko hapa kama kwa mbunge ni mbali nenda kwa diwani,hujamuona nenda hata kwa mtendaji tafuta majibu ya hoja zako sio barabarani"amesema Tulia

Kauli ya Spika imekuja muda mchache baada Kamanda wa Polisi Tanzania,IGP Camilius Wambura kuwataka wanaondaa maandaamano nchi nzima ili kuiangusha serikali kusitisha mara moja kwa kuwa jambo hilo ni uhaini.
 
Watuambie nawakili mwambusi nawenzake waliokamatwa check point morogoro mikumi wamepelekwa wapi maana kamanda mkuu wamkoa keshasema hajapata taalifa zao
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Tulia Ackson ametoa wito kwa watanzania kutafuta majibu ya hoja walizonazo kwa kufuata utaratibu na njia sahihi lakini sio kwa njia za kwenda barabarani.

Dkt,Tulia ameeleza hayo wilayani Makete mkoani Njombe wakati akizungumza na wanaCCM kwenye mkutano mkuu wa jimbo wa wilaya hiyo uliokuwa maalum kwa ajili ya uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2020 - 2023 chini ya Mbunge wa jimbo hilo Festo Sanga.

"Mwananchi mwenzangu usikubali mtu anayetaka kuchochea vurugu tutaathrika sote kama liko jambo halieleweki kwenye jamii,serikali imeweka viongozi hadi kwenye ngazi ya kitongoji nenda ukaulize huko kama hupati majibu muwakilishi wako yuko hapa kama kwa mbunge ni mbali nenda kwa diwani,hujamuona nenda hata kwa mtendaji tafuta majibu ya hoja zako sio barabarani"amesema Tulia

Kauli ya Spika imekuja muda mchache baada Kamanda wa Polisi Tanzania,IGP Camilius Wambura kuwataka wanaondaa maandaamano nchi nzima ili kuiangusha serikali kusitisha mara moja kwa kuwa jambo hilo ni uhaini.
Hawezi kuwapangia watu namna ya kudai haki zao as long as wako within the law
 
Tulia wewe ni mtu ulipewa nafasi uliyonayo haustahili wala huna sifa za kuwa spika basi tu nchi hii ukiwa na uwezo wa kuwa msifia wakuu unapewa ule...Hujawahi kusimamia maslahi ya wananchi huna historia hiyo.Nikuambie tu wamekuepo Ma Spika wanaishi mionyoni mwa watu Akina Samwil Sitta..Wewe hutakumbukwa kwa lolote na hicho kiti kama vile alivyokalia Ndugai akaondoka kwa aibu utaondoka kwa aibu.Aibu sana na utashangaa..sisi tunatulia tunaaangalia shobo zako na kukuhurumia tu you wont stay there forever mkidharau watu na kujiona mna akili nyie na nchi ni yenu nyie .Hii nchi sio yenu ni ya wote.
 
Huyo naye, viongozi wanahoja gani. Wote wanatetea ugali wao.
 
Back
Top Bottom