Dkt. Tulia aagiza hatua kwa waajiri wasiopeleka michango ya wafanyakazi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Sakata la mafao ya wastaafu limeibuka bungeni ambapo Spika Dkt. Tulia Ackson ameagiza Serikali kuwachukulia hatua waajiri wasiopeleka michango

Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson ameiagiza Serikali kuchukua hatua kwa waajiri wasiopeleka michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ili kuondoa usumbufu kwa wastaafu wakati wanapofuatilia stahiki zao.

Dk Tulia ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 19, 2023 wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni.
Agizo hilo lilitokana na majibu ya Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, (CCM) Angelina Malembeka.

Akijibu swali hilo, Katambi amesema wastaafu wengi wamekuwa wakipokea taarifa kupitia simu ya kiganjani na yeyote ambaye anakuwa amecheleweshewa kupata mafao yake wamekuwa wakichukua hatua.
“Hasa katika kuhakikisha kwamba tunapata nyaraka zao sahihi na kwa wakati, ili waweze kulipwa. Kwa hiyo wachache sana ambao wanapata changamoto hizo kwa sasa na ikitokea tuna dawati maalum la kupokea changamoto hizo,”amesema.

Amesema kama zipo changamoto hizo anamuomba mbunge awafikishie taarifa ikiwa ni pamoja na za ATCL.
Amesema taarifa tulizonazo ofisini wameshalipwa zaidi ya wafanyakazi 500 na wale wachache ambao wanachangamoto ilikuwa ni kuhusiana na taarifa sahihi kutowasilishwa ofisini ili walipwe.

Hatua hiyo, ilimuibua Dk Tulia ambaye alisema suala la ucheleweshaji wa stahiki za wastaafu ni changamoto kubwa kwa wapigakura.

“Mmelipunguza kwa sehemu kubwa lakini bado ni changamoto wanapokwenda huko (mifuko) badala ya kuwalipa fedha unawaambia akafuatilie mwajiri wake kule wakati kazi ya kufuatilia siyo ya mwajiriwa kwa sababu yeye hawezi kuuliza kama umepeleka au hujapeleka,”amesema

Amesema ni kazi ya yule mwenye mfuko ama ni kazi ya mfuko kufuatilia kwa yule ambaye halipi na kuwataka waendelee kulifuatilia upande wa mifuko iwapo waajiri wanapeleka michango.

“Kama hawapeleki ichukulieni hatua mifuko lakini huyu mwajiriwa asipate tabu anapostaafu alipwe pesa yake,”amesema.

Akijibu Katambi amesema mifuko ina sheria ambazo zinaanzishwa zinazoeleza kuwa ni kosa kwa mwajiri kutokuwasilisha michango kwa wakati katika mifuko hiyo kwa ajili ya wanachama.

Source: Mwananchi
 
Hatua gani kama si debe tupu , kuna hao TANESCO ndiyo kichefu chefu zaidi yaani muhitimu wa class ya 2022 anakuwa categorised kuwa Engineer wakati wa class ya 2021 anaendelea kusugua na utechnician wake . Nchi hii kuna UDINI na ukanda wa hali ya juu.
 
Ni jukumu la mifuko pia kufuatilia na kuwatoza faini mashirika yanayochelewesha. Tatizo kubwa ni kuwa uongozi wa mifuko wamebweteka kwa kutukutambua majukumu yao ambayo yamewekwa wazi kisheria
 
Ni jukumu la mifuko pia kufuatilia na kuwatoza faini mashirika yanayochelewesha. Tatizo kubwa ni kuwa uongozi wa mifuko wamebweteka kwa kutukutambua majukumu yao ambayo yamewekwa wazi kisheria
Una uhakika faini hazitozwi?
 
Back
Top Bottom