Spika Sitta Ampiga Mweleka Tido Muhando | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta Ampiga Mweleka Tido Muhando

Discussion in 'Sports' started by Brooklyn, Jun 15, 2010.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Katika hali ya kushangaza jana TBC1 ilionyesha mechi live kati ya Cameroon na Japan pamoja na Holland vs Denmark. Wengi tulishtuka kwani ni juzi tu baada ya mechi kati ya German na Australia tulitangaziwa na TBC kwamba wasingeonyesha kupitia TBC1 mechi za mchana na jioni kutokana na wao kurusha matangazo ya Bunge linaloendelea mjini Dodoma.

  Wakati naangalia taarifa ya habari ya TBC1 saa 2 usiku, ndipo nikang'amua kwamba Spika wa Bunge Mh. Samwel Sitta alikuwa amewaagiza TBC1 wasikatize matangazo ya Kombe la Dunia kupitia TBC1 na amewashauri warekodi vipindi vya bunge na kurusha baadae baada ya mechi za kila siku kuisha.

  Katika maelezo yake Mh. Spika "mzee wa kasi na viwango" alieleza kwa ufasaha umuhimu wa Kombe hili la Dunia na kwa jinsi watanzania wengi wanavyolifuatilia kwa ukaribu ikiwemo "Mh. Rais na wabunge wenyewe" na hivyo kukatiza matangazo hayo ni kuwanyima mamilioni ya watanzania kufuatilia michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika.

  Binafsi nakupongeza sana Spika Sitta kwa kuliona hilo.................naamini TBC wameshauza ving'amuzi vya kutosha ku break even katika mradi wao wa TBC 2 na sasa watuachie watanzania tufaidi uhondo wa WOZA 2010.

  Naamini Spika Sitta ambaye ni member hapa jamvini alipitia link hiyo hapo chini na kuelewa kilio cha wananchi na hivyo kushauriana na TBC1 kutengua uamuzi wa awali.


  https://www.jamiiforums.com/sports-and-entertainment-forum/63797-mkurugenzi-wa-tbc-bw-tido-mhando-umechemka-big-time.html
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hon Speaker, I beg your pardon. Is world cup a nation's priority?
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  mi nilikuwa nimeshatune mozambique tv narud badae tbc naikuta gem ipo

  nikajisema moyoni bongo tambaraleeeeeeee, maana hata wabunge kinao wanafatilia mashindano hayo kupitia simu zao wakiwa mjengoni
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kuangalia Bunge check kupitia Star TV au hata kupitia radio. Binafsi na declare kabisa kwamba sitoangalia kabisa bunge mpaka world cup iishe.......kwanza sioni kipya zaidi ya wabunge kusimama dakika tisa kuponda mswada wa bajeti na kutumia dakika ya kumi kuunga hoja na kumpongeza waziri husika kwa hotuba nzuri.

  WOZA 2010
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  another evidence kwamba national priorities hazipo kabisaaaaaaaa, yaani tuangalie WC ambayo hata ndugu zetu kenya hawapo!!!

  Siajabu yule mkenya aliyesema sisi ni party animals anamaana ya kweli!!
   
 6. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nafikiri kuna kitu watu mna miss hapa, issue si kwamba kati ya WC na Bunge kipi cha muhimu, hapa issue ni kwamba WC inaonyeshwa na TV moja tu hapa nchini ambayo ni TBC wakati bunge linaonyeshwa na TV zingine mfano Star TV na ITV.

  Binafsi sioni logic kwa nini tung'ang'anie TV zote tatu yaani Star TV, ITV na TBC zionyeshe bunge wakati tunaweza tukaacha hizo mbili zioneshe bunge na TBC ituonyeshe mpira.

  Ili 'wazalendo' mnaoona mnastahili kuangalia bunge mwendelee na siye tunaoona soka kwa sasa ndio kiburudisho cha msingi tuendelee.

  Ni mtizamo tu!!!
   
 7. senator

  senator JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  TBC kama inavyojulikana ndio TV ya taifa na Ndio wenye Haki pekee yakuonesha WC kwa TZ, Spika sitta kwa kuwa nae ni Mnazi wa Futbol akaona ni vyema na haki kuwa wa TZ wapenda michezo ambao na yeye amekiri kuwa wameongezekana kutokana na kuwa rais wetu mpenda michezo wapate kuangalia Live mpira huo na kipindi cha Bunge kuwa recorded( wamekionesha leo asubuh saa2 mpaka).Naamini kabisa kwa mfano Ukiwepo mpira wa Brazil na IvoryCoast afu at the same time kuwe na Rais anatoa hotuba ..majority ya watu wa TZ watakuwa wapo kwenye upande wa Mpira.Spika Jana Kasema DUNIA KWA SASA IMESIMAMA WATU WAPO KWENYE SOKA!
   
 8. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,473
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  SS kazi nzuri la sivyo hawa TBC wangetesa sana waTZ na ving'amuzi vyao
   
 9. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  TBC walijua world cup itacoincide na bunge, kwa nini walibid.

  Unawasemea wapenda michezo kupata pleasure kwa mwezi mmoja, vipi prioroties za Taifa ni za muda gani?
   
 10. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hongera Spika Sitta..........wanaopenda kuangalia Bunge bado wana nafasi ya kuangalia vituo vingine.Vingamuzi vya TBC ni maji marefu kwa abongo wengi...BIG UP
   
 11. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mfano leo saa 11 jioni mambo ni kama hivi;

  Dodoma: Bunge la bajeti

  Nelson Mandela Bay: Ivory Coast Vs Ureno

  Je watanzania wengi watakuwa wanaangalia nini wakati vyote vinaenda hewani muda mmoja?

  Mh. Sitta amejibu......"wengi watakuwa wanaangalia mpira.."
   
 12. senator

  senator JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hivi Bongo tunapriority kweli?? Juzi wamekuja Brazili kwa 3Bil..leo bajeti yetu ina nakisi ya 5Tril sasa sijui vipaumbele vipi unavyosema ww!.
  kwa Bongo tunakwenda mzobemzobe tu..Bajeti ya bongo inasema vipaumbele ni kwenye miundombinu..Afya..Elimu nk.hizi zote ni blah Blah ambazo tumekuwa tukiimbiwa toka mkuu wa kaya aingie madarakani so sioni Jipya!!..Bunge hili nadhani nilakuzima moto tu wabunge wapo busy majimboni ndo mana hakuna full house kwa Mjengo.
  FIFA ilitoa vipaumbele kwa TV za taifa za nchi kuonesha na sio kwa gharama ya kutisha sanaa..otherwise ITV na Channel10 wangeweza kuungana na kurusha Matangazo ya WC.
   
 13. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Sema usiogope sema sisi wabongo tumezidi unafiki semaaaa
   
 14. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mweee! kazi ipo! No wonder tutaendelea kuwa masikini.Simwamini mtu kwa sasa.Najiamini mwenyewe tu.

  I AM TIRED OF ILLUSIONS!
   
 15. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Nadhani ilikuwa ni bizness startegy yaa kuuzia hivyo vi Decoder
   
 16. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kama hatuna priority basi tuendelee kushangilia hiyo hali?

  Ni Tanzania pekee ambapo speaker wa bunge anaona world cup ni muhimu kuliko kikao cha Bunge. Sitashangaa pale ataapoahirisha Bunge ili kucheki moja ya game anazozipenda, au pale wabunge watakapoacha kufuatilia kikao na kuangalia mechi kwenye simu zao.

  Watanzania tutaamka lini?
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na wameviuza kweli si mchezo ati.Strategy yao imewini.
   
 18. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tatizo tunashindwa hata kuwa na uelewa hata kwenye mambo makini.Mfano hata BBC pamoja na umuhimu wa WC hata siku moja hawawezi kuahirisha mambo ya maana kwa kuonyesha mpira hata kama ENGLAND wanacheza.Nandio maana kunakuwa na TV station nyingi na za michezo kama supersport ili kutochanganya habari.
  Walichotakiwa kukifanya TBC wangepromote hiyo TB2 iwe kama Channel ya michezo kama ndio wanaona michezo ina maana kuliko Bajeti ya serikali.
   
 19. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  You spot
   
 20. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ideal vs Reality
   
Loading...