Spika Ndugai: Lissu alishambuliwa kwa risasi 28-32 lakini zilimpata tano, awataka wabunge kuchangia nusu ya posho zao

hakika kwa hili bunge limeungana bila kuonesha tofauti za kiitikadi... ni mfano mzuri wa kuigwa na jamii nzima.. hata huku mitaani wenzetu wanapopatwa na majanga hatupaswi kuchekana na kudharauliana bali kusimama pamoja kwa nguvu moja kama walivyofanya wabunge leo hii.

Mungu awabariki sana wabunge
 
Nahisi waliopanga kumuua tundu lissu saizi watakuwa wanajilaumu sana wanaposikia tundu lissu bado yupo hai.
 
Muda huu sote tunasikitika!

Mungu akitaka kukunusuru Hakuna wa kukudhuru, nmetazama lile Gari na maeneo lilipopigwa risasi kwa kweli Mwenyezimungu ni Mwingi wa Rehma!

Warusha risasi nao wanasikitika Pengine wanalaumiana kwa kutokuwa 'wafanis kazini'!

Kama bado wako hai watakua wanakunywa konyagi tu sasa hivi uku nafsi zao zikiwauma.
 
umoja na mshikamano ndio ngao pekee itakayotupeleka tunapoenda na kufika salama, mambo ya kubaguana na kuzomeana watu wazima haileti picha nzuri
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema Bungeni kuwa gari ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu lilishambuliwa kwa jumla ya risasi 28 hadi 32 lakini zilizompata na kumjeruhi Tundu Lissu ni tano tu.

Ndugai amesema kwa hesabu alizofanya cha Wabunge waliopo leo, kiwango cha mchango wa wabunge kitakua Tshs Milioni Arobaini na tatu (Tsh 43,000,000/=) kutoka kwenye nusu ya posho yao ya siku ya leo.
Alijuaje.alikuwa anaziesabu akiwa wapi
 
Angetuambia na hao waliomshambulia walikuwa wangapi...
Atueleze na walinzi wa bunge walikuwa wapi wakati wa tukio.
Inashangaza sana wakati huu wa vikao kuwa na ulinzi mkubwa Dodoma lakini hili jambo likatokea, najiuliza huo ulinzi uliopo ni wa nini..?
Ilitokea wakati fulani walinzi wa bunge walizubaa kidogo kutii amri ya spika walipoambiwa wamtoe Mnyika bungeni na spika akawawajibisha, lakini tukio hili ambalo ni kubwa zaidi sidhani kama walinzi watawajibishwa!
 
Muda huu sote tunasikitika!

Mungu akitaka kukunusuru Hakuna wa kukudhuru, nmetazama lile Gari na maeneo lilipopigwa risasi kwa kweli Mwenyezimungu ni Mwingi wa Rehma!

Warusha risasi nao wanasikitika Pengine wanalaumiana kwa kutokuwa 'wafanis kazini'!
Dunia hii ni ya ajabu sana.
Kilichopo katika fikra za mtu mwingine ni tishio mno, usishangae hata pale hospital walikuwepo kuhakikisha kama lengo limetimia!
 
Back
Top Bottom