Spika Ndugai: Huku Mtu akishakuwa Polisi anaona kuweka Watu ndani ni raha. Watu wanarundikwa tu mahabusu

Huyu jamaa akili zake utafikiri mtandao wa Airtel, kuna wakati zinapotea, kuna wakati zinarudi. Haeleweki hata kidogo!
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Polisi wanakamata Watu hovyo wengine wenye heshima zao na wanajulikana wanakoishi lakini wanarundikwa tu Rumande bila ulazima wowote.

Ndugai amesema "inatakiwa tujifunze kwa Nchi za wengine ambapo Mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka Watu ndani ni raha".

Ameongeza "Hiki kitu binafsi kinaniuma sana. Mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote, Waafrika hatuthaminiani".

Unafiki mtupu. Yeye mbona alimpiga mpinzani wake wa uchaguzi fimbo mpaka akazirai. Anajifanya ana uchungu sana?
 
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Polisi wanakamata Watu hovyo wengine wenye heshima zao na wanajulikana wanakoishi lakini wanarundikwa tu Rumande bila ulazima wowote.

Ndugai amesema "inatakiwa tujifunze kwa Nchi za wengine ambapo Mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka Watu ndani ni raha".

Ameongeza "Hiki kitu binafsi kinaniuma sana. Mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote, Waafrika hatuthaminiani".

Walifanya kosa sana siku ile alimtandika mwenzie rungu la kichwa ilitakiwa akalale huko kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom