Spika Ndugai: Huku Mtu akishakuwa Polisi anaona kuweka Watu ndani ni raha. Watu wanarundikwa tu mahabusu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Spika wa Bunge la Tanzania amesema Polisi wanakamata Watu hovyo wengine wenye heshima zao na wanajulikana wanakoishi lakini wanarundikwa tu Rumande bila ulazima wowote.

Ndugai amesema "inatakiwa tujifunze kwa Nchi za wengine ambapo Mtu huwa anaitwa kituoni na kufanyiwa mahojiano kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kwasababu anafahamika na hawezi kukimbia. Huku ukishakuwa Askari tunaona kuweka Watu ndani ni raha".

Ameongeza "Hiki kitu binafsi kinaniuma sana. Mtu anawekwa ndani wiki nzima au mwezi halafu baadae anakuja anaachiwa wakati shughuli zake nyingi zimeshasimama. Sheria nazo hata ukitoka huwezi kudai chochote, Waafrika hatuthaminiani".

1620134410215.png
 
Ndugai amelaaniwa, lema amesema bado ndugai naona laana imeanza kumpata.

Hivi ndugai si ndio anabariki na kupitisha masheria ya hovyo ya kuweka watu ndani bila dhamana leo analalamika,akiambiwa spika na bunge ni dhaifu anan'gaka,pumbav kabisa huyu.
 
Mh mwaaa, Ndugai walonga mswano😃😃mh KWA kauli yoko tukipata sheria ya fidia kwa alielundikwa na askari then akagundulika Hana kosa itasaidia Sana tena alipe askari aliekamata, tumia kiti vizuri sasa.
 
Back
Top Bottom