Spika Ndugai akitimiza azma yake ya kumvua Tundu Lissu ubunge wake kwa ubabe ndiyo atakuwa amejiharibia kabisa!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,160
Tumeisikia kwa masikitiko makubwa sana taarifa iliyotolewa na Spika Ndugai kuwa kwenye kikao kijacho cha Bunge, kinachotazamiwa kuanza tarehe 29 mwezi huu, kitajadili hatma ya ubunge wa Tundu Lissu, kwa madai kuwa ni mtoro na uongozi wa Bunge lake haujatoa baraka za shughuli anazofanya huko aliko

Kwa maana nyingine ni kuwa Tundu Lissu anahesabika na uongozi wa Bunge kama mtoro au kwa kiingereza tunaita kuwa ame-abscond!

Hivi kwa tabia hii inayoonyeshwa na Spika Ndugai hivi sisi wananchi tutakuwa na makosa tukisema kuwa uongozi wa Bunge unawajua "watu wasiojulikana" waliohusika na kumminia risasi zaidi ya 30 Tundu Lissu mwaka juzi??

Hivi kwa namna alivyoumizwa Tundu Lissu kwa risasi mfululizo zilizolengwa kwake kwa nia ya kumuua, ambapo dunia nzima "ina-sympathize" naye, iweje yeye Spika Ndugai afanye vice versa??

Hivi Spika Ndugai atawezaje kumwita mbunge Tundu Lissu kuwa ni mtoro wa vikao vya Bunge, wakati dunia nzima inajua kuwa Tundu Lissu amekuwa akiendelea na matibabu nchi za nje akiwa mahututi, baada ya kunusurika kuuawa baada ya kushambuliwa na "watu wasiojulikana" kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 30 kwenye gari yake??

Hivi inawezekanaje uongozi wa juu wote wa Bunge, akiwemo yeye Spika mwenyewe, Naibu wake, Tulia Ackson na Katibu wake wa Bunge, Kigaigai, wawe hawajakanyaga hata siku moja, katika hospitali ambazo anatibiwa Mbunge mwenzao Tundu Lissu zaidi ya mwaka hivi sasa, lakini leo wamwite mtoro??

Kama alivyosema Tundu Lissu mwenyewe na kumwambia Spika Ndugai kuwa asijaribu kumwaga petroli kwenye moto unaowaka kwa kuwa ni wazi kuwa utamlipua!
 
..toka Brussels Ubelgiji mpaka London Uingereza ni mwendo wa masaa mawili na nusu kwa treni ya mwendokasi.
Kile kipindi cha Hardtalk cha BBC alichoshiriki Tundu Lissu, ndicho kinachowafanya viongozi wa juu ya serikali hii ya awamu ya tano "waweseke" na kushindwa kuvilalia vitanda vyao......

Wenyewe watu wa serikali wanadai kuwa Tundu Lissu amepiga "fix" nyingi sana kwenye kipindi hicho, kuwa Tundu Lissu ameiongopea dunia, kwa kuwa kipindi hicho kinakadiriwa kuangaliwa na watu zaidi ya milioni 300 duniani kote.......

Mtangazaji Stephen Sackur anayeongoza kipindi hicho, ametoa mwaliko kwa Rais Magufuli ajitokeze kwenye Hardtalk nyingine ili ajibu mapigo......

Sasa mbona viongozi wa serikali mmeingia kihoro mno, wakati nafasi hiyo imetolewa na BBC ya kwenda kusawazisha hali ya hewa aliyoichafua Tundu Lissu??
 
Back
Top Bottom