Spika Ndugai aishangaa serikali kusitisha ujenzi Bandari Bagamoyo

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Spika amesema kitendo cha serikali kuanza ujenzi wa reli ya umeme kiwango cha SGR badala ya mradi wa Bandari Bagamoyo ni sawa na kugeuza mkokoteni kuvuta Ng'ombe badala ya Ng'ombe kuvuta mkokoteni.

=====

Dodoma. Kusuasua kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) mkoani Pwani, kumewaunganisha wabunge pamoja na Spika Job Ndugai kuibana Serikaliwakiitaka kutoa maelezo ya kina kwa nini hautekelezwi.
Wabunge hao wamesema mradi huo una tija kubwa ukikamilika sambamba na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao kukamilika kwake hakutakuwa na manufaa makubwa iwapo bandari ya kisasa haitakuwepo.

Mradi huo unaohusisha maeneo kadhaa ya viwanda, mji wa kisasa wa makazi unaoendana na mahitaji ya karne ya 21, kituo cha usafirishaji wenye thamani ya zaidi ya Sh23 trilioni, mkataba wa makubaliano ulisainiwa mwaka 2012.

Jiwe la msingi la mradi liliwekwa Septemba 2015 na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambapo ulikuwa utekelezwe kwa ubia kati ya kampuni ya Merchant Holdings International Limited (CMHI) na State General Reserve Fund (SFRF) ya Oman.


Hata hivyo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Maawasiliano, Isack Kamwelwe akiwasilisha hotuba yake Mei 9, alisema majadiliano na wawekezaji hao yamesitishwa baada ya kuweka masharti yasiyokuwa na masilahi kwa Taifa.

“Masharti hayo ni pamoja na wawekezaji kudai kuachiwa jukumu la kupanga viwango vya tozo na kutoruhusu wawekezaji wengine katika eneo la kati ya Bagamoyo na Tanga,” alisema Kamwelwe.

“Majadiliano hayo yanaweza kuendelea iwapo wawekezaji hao wataondoa masharti yasiyo na masilahi kwa Taifa.”

Jana Spika Ndugai na wabunge waliibana Serikali kuhusu mradi huo wakitaka kujua kwa undani kipi kimesababisha kutotekelezwa licha ya manufaa ambayo nchi itakapata utakapokamilika.

“Sifahamu kipi kimekwamisha mradi wa Bagamoyo. Waziri (Kamwelwe) ukipata muda unaweza kutufafanulia vizuri,” alisema Spika Ndugai huku wabunge wakishangilia.
Alisema aliwahi kwenda China kwenye jiji la Shenzhen na kuitembelea kampuni hiyo akiwa na baadhi ya wabunge ambapo walielezwa jinsi utakavyokuwa na kubaini kuwa una manufaa zaidi ukijengwa kwa wakati.

“Waliokuwa wakitaka kujega Bandari ya Bagamoyo walitufanyia uwasilishaji wa mradi huo jinsi utakavyokuwa, ukisikiliza huwezi kuacha kuunga mkono, Wachina walitueleza sijui kwa nini Watanzania mnapofikia jambo kubwa kama hili mnavuta miguu hamuamui,” alisema.
“Huu si mradi wa kuacha chondechonde na wote wanaofanya uamuzi wafanye, bandari itakuwa kubwa, viwanda, yaani...halafu hela karibu zote wanatoa wao. Tuache mambo mengine yote tukafungue uchumi.”

Ndugai alisema uwekezaji mkubwa wa karibu Sh23 trilioni haukupaswa kubezwa na kama timu ya makubaliano iliona hivyo basi kuna kazi ya kufanya.

“Lakini kampuni ya Kichina ni kampuni ya Serikali si ya kibabaishaji,” alisema.

Wabunge walivyochangia
Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Salehe alisema kama Bunge wanafanya makosa kuachia miradi mikubwa kama hiyo kufutwa bila majadiliano na Serikali.

Mbunge wa Hanang (CCM), Dk Mary Nagu alisema, “tulifanya hivyo (kuanzisha mradi) kwa kuwa tuliona sehemu ya kuweka ni Bagamoyo na mimi nilisaini mradi huo nikiwa waziri wa Uwekezaji (katika utawala uliopita).”

Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara ambaye ni mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage alisema mradi huo ungewezesha kujengwa viwanda 1,000 na kuzalisha ajira 500.

Wengine waliochangia ni mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu; Dk Shukuru Kawambwa (Bagamoyo-CCM); wa Buchosa (CCM), Dk Charles Tizeba; wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa; wa Ilala (CCM), Mussa Zungu na wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia.

Chanzo: Mwananchi
 
Spika amesema kitendo cha serikali kuanza ujenzi wa reli ya umeme kiwango cha SGR badala ya mradi wa Bandari Bagamoyo ni sawa na kugeuza mkokoteni kuvuta Ng'ombe badala ya Ng'ombe kuvuta mkokoteni.https://youtu.be/U_sLJOKbTsw
Siku zote tunasema hapa bunge ni muhuri wa serikali alikuwa haelewi tuna maana gani?, kweli huyu ni spika dhaifu
 
Kumbe ni maoni na mawazo ya wachina yeye anawakilisha kile wachina walichokisema na yuko makini sana ktk uongeaji wake huku akisisitiza "wao wanasema" ili kesho na kesho kutwa akiulizwa apate pa kutokea.

Anyway atleast amepata hata ujasiri wa kulisema hilo sasa sijui litakuwa na mwendelezo au ndo lishaisha hapo.

Maana nasikia wabunge hadi waziri mwenye dhamana wanapiga makofi najiuliza wanashangilia kitu gani?
 
Kumekuwepo na madai mara nyingi kuwa hii iliyopo iko - under utilized sasa kama ni hivyo wachumi wetu wangefanyaje? AMA madai kuwa iko under utilized ni ya uongo?
 
187A86E4-0DB4-4FC5-B849-FF8555E86918.jpeg


SPIKA ASHANGAZWA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO KUSIMAMA. ATAKA SERIKALI KUFAFANUA

Spika Job Ndugai ameitaka Serikali itakapo kuwa inahitimisha mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, kueleza kwa nini ujenzi wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani haufanyiki licha ya mzabuni kupatikana kutoka nchini China.

Amehoji hivyo, leo Bungeni baada ya Wabunge mbalimbali kuhoji mradi huo wa bandari kukwama wakati wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya mwaka 2019/20.

Amesema kuna wakati alitembelea China na walisema ujenzi wa bandari hiyo ukikamilika utakuwa na tija kubwa kwa nchi kuliko ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway - SGR) unaojengwa, na kushangaa kuwa ujenzi wa reli umeanza badala ya bandari.

Amefafanua kuwa kukamilika kwa SGR bila kuwa na bandari ya kisasa kama hiyo ambayo ilikuwa ijengwe Bagamoyo ni kazi bure kwani mpaka sasa nchini hakuna bandari nzuri hivyo Serikali inapaswa kuliona hili.

Aidha, baadhi ya Wabunge waliohoji kuhusu suala hilo na kuhitaji ufafanuzi ni Hussein Bashe(Nzega Mjini-CCM), Lucy Magereli(Viti Maalum-CHADEMA), Ally Salehe(Malindi-CUF), Charles Tizeba (Buchosa-CCM) na Dkt. Shukuru Kawambwa(Bagamoyo-CCM).
 
Wajenge vyote kwa pamoja,kwa vile Bagamoyo ndo ilianza waendelee nayo si ilikuwa na budget yake tayari???SGR nayo ina budget yake. Sasa kwa nini wameanza kucompare the incomparable???? .Jengeni vyote kwa kuwa havitegemeani budget. Na vyote ni maendeleo kwa nchi yetu.
 
Spika amesema kitendo cha serikali kuanza ujenzi wa reli ya umeme kiwango cha SGR badala ya mradi wa Bandari Bagamoyo ni sawa na kugeuza mkokoteni kuvuta Ng'ombe badala ya Ng'ombe kuvuta mkokoteni.https://youtu.be/U_sLJOKbTsw
Siku ya mwisho kila goti litapigwa
 
Back
Top Bottom