Mchaka Mchaka
JF-Expert Member
- Jul 20, 2010
- 4,516
- 1,404
Ila majimarefu sio kwamba amechanganyikiwa ila hachambi tu!
[h=3]Hii ndiyo hasara ya kuchagua waganga wa kienyeji na matapeli kuwa wabunge[/h]
Nani angeamini kuwa mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi angeshangilia uvunjaji sheria na haki za binadamu? Imetokea tena bungeni ambapo mbunge wa Korogwe Vijijini Steven Ngonyani aka Maji Marefu kusema eti kipigo alichopata mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka kilistahili. Laiti bunge letu lingekuwa ni bunge huyu alipaswa kuwajibishwa mara moja. Maana hii si kashfa ya kawaida.
katika mchango wake bungeni leo mbunge wa Korogwe kawatonesha madaktari kidonda! Kasema kama madaktari wamegoma kutibu watu kwa nini wanamtibu dr. Ulimboka? Madam Spika ikabidi amzuie kwamba swala liko mahakamani! Mi nadhani afya yake mgogoro angeishauri serikali yake
Uhuru wa mawazo ya kila mtu uheshimiwe, hata kama yako tofauti na ya kwako.
Mbunge wa Korogwe-CCM Stephen Ngonyani(Profesa Maji Marefu) amemshambulia vikali Dr Stephen Ulimboka na kuwataka madaktari wasimtibu.Spika Makinda ilibidi aingilie kati na kumuamuru Ngonyani kuacha mara moja kuzungumzia suala hilo ndani ya bunge kwa sababu liko mahakamani.Ngonyani akajitetea kuwa amechanganyikiwa kwa sababu aliumwa sana na watu wakamzushia kifo.Kabla ya kuwa Mbunge Ngonyani amewahi kuwa mganga wa kienyeji.Kauli hiyo ya Ngonyani ilionekana kushangiliwa sana na wabunge wenzake wa CCM.