Spika Makinda ampiga Stop Stephen Ngonyani kumshambulia Dr Ulimboka

Hata hao waliomchagua mie sielewi vigezo walivyotumia! (Samahani simaanishi kuwatusi bali ninawasilisha unaive wangu katika hili maana niliamka tu na kusikia amekuwa Mbunge - Nadhani ninahitaji kuwa mwanafunzi mzuri wa siasa ya Tanzania)

Kila mahali penye mkusanyiko wa watu ni desturi kuwa na Daktari kwa ajili ya huduma ya kwanza na msaada wa dharura. ChiChieM wanalielewa hili na ndio maana wakamwingiza Maji marefu bungeni kwa ajili ya huduma ya kwanza na msaada wa dharura pale wanapokwama.
 
Duuh! Mhe. Ngonyani a.k.a maji marefu kaomba radhi kwa kauli yake ya jana bungeni dhidi ya Dr. Ulimboka. Jamaa kafunguka!
 
Kusema kweli mbunge huyu hakutumia akili kabisa japokuwa analopinga naweza kubaliana nalo.. Leo JF mtanichukia sana na madaktari mtanilaani.. Kama Madaktari wamefanya mgomo kutibu watu wote kwa nini huyu Ulimboka iwe tofauti? Brigedia Simba kalazwa mahtuti hajapewa huduma yoyote kwa sababu ya mgomo. Kuna jamaa yangu kaumizwa vibaya vilevile wakigombea sijui kiwanja huko Tegeta, kilichopo watu wanaomba Mungu tu rehma zake..Iweje mgonjwa mwingine awe na umuhimu zaidi wakati wa mgomo kushinda wagionjwa wengine?. Hapo ndipo unaweza jiuliza maswali kibao nje ya Ubinadamu na pengine kusema ujinga kama huu.
 
CCM wana akili za hovyo sana sasa walikuwa wanashangilia nini...wakiitwa dhaifu wanakasirika

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Viongozi wa kitanzania sometimes wako kama watoto...saa nyingine huwa nashangaa huwa wanafanya nini bungeni hija zao ni kama watoto wa kindergarten....Sasa mtu mzima na akili yake anashangilia statement ya Prof Maji Marefu...Really?.....
 
Back
Top Bottom