Spika Makinda ama amechoka au ana hasira?

Spika Makinda ama amechoka au ana hasira?

Africa one

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
244
Reaction score
111
Spika wa JMT Mh. Annie Makinda leo naona analiingiza Bunge letu tukufu katika majaribu moja ya jaribu ni pale Mbunge anapoomba maelezo ya serikali lakini matokeo yake spika yeye anaingia kuhoji wanao kubali waseme ndio na wasiokubali waseme sio.

Kwa utaratibu huu spika wetu ama amechoka au ana hasira?
 
Muongozoooooooooooooooo!!

Wamesikika wabunge wa upinzani na spika kuahirisha bunge wakati waziri wa nishati na madini akisoma muswada wake.

Kwa nini hii miswada inalazimishwa kwa nguvu????

Job true true
 
Ina masilahi kwa wachache hasa mi ccm.UKAWA is doing better.
 
Spika wa JMT mh.Annie Makinda leo naona analiingiza Bunge letu tukufu ktk majaribu moja ya jaribu ni pale Mbunge anapoomba maelezo ya serikali lkn matokeo yake spika yeye anaingia kuhoji wanao kubali waseme ndio na wasiokubali waseme sio.
Kwa utaratibu huu spika wetu ama amechoka au anahasira?

Shida yake kubwa ni mashahidi watakaoandaa baada ya uchaguzi wa 2015. KAma unakumbuka yale ya kwenye kesi ya Tundu Lisu na ubunge wake! Wanajua wanachokifanya na wanafanya kwa makusudi ya mabavu!
 
Kwa kweli kama sheria zitaendelea kutungwa kama kinachifanyika sasa kule bungeni hizo hazitakuwa sheria. Naona umuhimu wa sheria hizo zitakazopitishwa kwa hati ya dharura kupingwa mahakamani. Wabunge wa CCM wamekuwa ni rubber stamps all the time wakati sheria zinawahusu watu wote.
 
Muongozoooooooooooooooo!!

Wamesikika wabunge wa upinzani na spika kuahirisha bunge wakati waziri wa nishati na madini akisoma muswada wake.

Kwa nini hii miswada inalazimishwa kwa nguvu????

Bora na iwe hivyo na huo wakifika nao awaulize wanaosema ndiyo waafiki! Huyu mama ni kweli kinda!
 
Limehailishwa naona wangetumia hekima sasa wana lazimisha tu kwann kuna nn hapa kwenye gesi kama wanazamira njema na rasilimali za nchi kwann wanalazimisha.
 
Huyo hakuwa na sifa na sifa za kuwa Spika in the first place. Wapo akina mama wengi tu wenye sifa kama suala lilikuwa awe mwanamke. Tunalipa gharama za ujanja wa kumwengua Sitta ulioongozwa na Kingunge kumbe alikuwa na yake.
 
wanalazimisha muswada wa sheria wa mafuta na gesi kwanni na ukawa hasa chadema wameomba mwongozo tundulisu spika kakaa kimya huku waziri wa nishati na madini akiendelea kusoma makelele yakaanza na ikabidi aseme wabunge wafuatao wamefanya fujo bungeni mnyika,machali,tundulisu,msigwa na wengine.
 
Kawataja wabunge Lissu,Mnyika,Machari,Gekul,Silinde,Masoud,na wengine kwamba ndo wamevuruga mkutano kwa kutoheshimu ukumbi.Spika kashindwa kbs kuliongoza bunge,anaibeba serikali,ila inaonekana ana jazba na akina LISSU na MNYIKA,tangu jana.
 
Kuna ulazima gani wa kuharakisha hii miswada kwa hati ya dharura...?
 
Back
Top Bottom