Spika Job Ndugai afunguka, aahidi kukaa chini na UKAWA

Spika Job Ndugai afunguka, aahidi kukaa chini na UKAWA

Unajua ukishaugua sana na ukapona,lazima dunia unaanza kuiangalia kwa mtizamo tofauti na kabla,kwasababu hujui mungu kakurudisha kwa malengo yapi,so you try to do the right thing...

Nothing worth like having your LIFE back! Atakua ilishachungulia kulee...akaona kila kitu duniani haina maana,ni ubatili mtupu!lazima ukipona uwe down to the earth.
 
Kwenye Bunge la Katiba Wapinzani walimpigia chapuo la Wazi wazi Mh. Samwel Sitta na kumtelekeza Mgombea wao Mh. Wakili Msomi Hashim Rungwe Spunda wakitegemea mteremko pindi akikamata wadhifa huo na baada ya kushinda Uchaguzi na kazi kuanza tulishuhudia Profesa Msomi Ibrahim Haruna Lipumba akaongoza wenzie kukimbia Bunge japo safari ile hawakuziba midomo na makaratasi.

Job Ndugai ni Mwana CCM na sku CCM ikimpokonya kadi ya Uanachama kama ilivyotaka kufanya hivyo kwa Samwel Sitta hatoweza tena kuwa Spik na Yeye analijua hilo!
Nadhani pia amajifunza kua haya mambo hata km unaipendelea serikali mwisho wake sio mzuri! Sitta saivi yupo wapi? Juzi apa jamaa wamemtoa kwy nyumba ya serikali kaenda mtaani kupanga sijui manzese etc so in the end you precisely get the opposite.
 
Yupo Live Azam Two.Anaongea kwa busara na lugha ya kutaka maridhiano.

Huyu ni Kiongozi
Ukitaka busara ugua, ukipona huwi ukimwengu huu, unakuwa unaishi kwa tumaini jipya maana hujui makusudi ya kuzidi kuwa hai
 
Subiri leo atapokea simu kutoka whitehouse kwa huo upuuzi alioongea kwenye media. Msimamo wetu ni kuhakikisha tunatawala wenyewe,hatutaki kukosolewa maana tunaharibiwa kwa wananchi.
 
Kwenye Bunge la Katiba Wapinzani walimpigia chapuo la Wazi wazi Mh. Samwel Sitta na kumtelekeza Mgombea wao Mh. Wakili Msomi Hashim Rungwe Spunda wakitegemea mteremko pindi akikamata wadhifa huo na baada ya kushinda Uchaguzi na kazi kuanza tulishuhudia Profesa Msomi Ibrahim Haruna Lipumba akaongoza wenzie kukimbia Bunge japo safari ile hawakuziba midomo na makaratasi.

Job Ndugai ni Mwana CCM na sku CCM ikimpokonya kadi ya Uanachama kama ilivyotaka kufanya hivyo kwa Samwel Sitta hatoweza tena kuwa Spik na Yeye analijua hilo!
Uwe unajaribu kuwa focused sometimes
 
Sioni uwezekano wa Job Ndugai kuamua yeye kama yeye kurejesha mahusiano mazuri ktk bunge kwa faida ya Taifa, hawezi kujituma labda km katumwa, kila amuzi awamu hii hutoka juu, hili nalo labda kama linatoka huko kupoza makali ya Ukuta, tutashuhudia mengi before sept mos.
 
Kifupi kanuni za bunge na taratibu zifuatwe mengine yoote ni kuzugana tu
Vinginevyo kanuni zinazoonekana zinamapungufu zibadilishe utapatanisha leo kesho yatarudia hayohayo wafuate kanuni
Kwani unafikiri shida kwa mteule ni kanuni au kibri?
 
Vijana wa ukuta muwe mnatoa habari za ukweli humu..si mnaona wabunge wenu wanatumia maandiko yenu kuropoka bungeni kwisha wanakosa ushahidi na kufungiwa kuhudhuria bunge
 
Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa Tanzania Job Ndugai, amesema anasikitishwa na Wabunge wa UKAWA na Tabia yao ya kutoka Nje. Japo ni haki yao kutoka nje lakini hivi karibuni imezidi. Japo itaendelea hivi tutakuwa hatujengi nchi amesema.

Ameahidi yeye mwenyekiti wa Bunge na naibu Spika watakaa na UKAWA wamalize hili tatizo kwani haipendezi spika unakaa mtu anatoka nje.

Amesema Sasa Nchi hii Migogoro, utengano umezidi, ni jukumu letu kama Viongozi kumaliza hii hali.

Kasema Wabunge waliofungiwa ilitokana na matomeo ya sintofahamu. Kwani kabla ya kufungiwa tunaomba Mbunge afute kauli yake, arekebishe au alete ushahidi. Pale anapokaidi huitwa kutoa ushahidi lakini saa nyingine hukataa. Mfano kuna Mbunge alisema polisi wameleta Magari ya Washawasha 700. Tulipomwambia alete ushahidi akasema alisoma Kwenye JamiiForums. Kama bunge hatuwezi fanya kazi kwa kutengemea Mitandao

Anasema hii hali inayoendelea bungeni inachochea chuki na Migogoro. Ni bora sasa tukaa nchini kama taifa ili tumalize hii hali.

Anasema kama Spika hatavumilia vijembe na kejeli kuendelea Bungeni

Ni haki ya mbunge kutoka nje. Lakini wale waliobaki nao wanawashambulia waliotoka, hili nalo ni tatizo. Wabunge wakitoka nje mambo mengi huharibika. Inachafua hali ya hewa. Uchaguzi unapoisha, siasa huhamia Bungeni.

Tunachukulia Mbunge kama mtu mzima. Chama tawala na UKAWA na sisi tukae chini tuongelee hili swala.

Wabunge wamezoea kuona Spika na Naibu wake wakiwa wabunge wa kuchaguliwa, hii ya naibu Spika kuwa wa kuteuliwa wanahofu kwamba atakuwa anapokea maelekezo kutoka Sehemu Fulani. Naomba niwahakikishie kwamba, sisi hatupokei maelekezo kutoka sehemu yoyote bali tunatoa maamuzi yetu tunavyoona inafaa. Hivo watuamini.

Shida ya Ukawa ni Naibu spika aondoke kwenye kiti, huyu mama analishizwa chuki kwa Ukawa, hataki muongozo hataki chochote kutoka upinzani anapindisha kila kitu.
 
Akiongea kwa huruma nakumbuka siku anaongea kwa jazba baada ya tafsiri ya kambi rasmi ya Upinzani, alikuwa '' shetani '' kweli nashangaa leo kama '' malaikaaaaa ''
 
Mungu akubariki baba Spika.
Tumemchoka yule naibu jeuri.
 
Baada ya kuugua karud na busara..kachungulia kifo sa hv mpole anaongea point tu
 
Rudia kusoma tartiiiiibu utagundua kuwa mtoa mada hajakosea.
Dogo nadhani ugeni wako humu unakusumbua... Hiyo Heading mods pekee ndio wanaweza rekebisha..
So washafanya kazi yao.. Ila mtoa mada alidiliki kumuita job ndugai kuwa ni naibu spika. Nadhani hukuona mapema thread hii..sikutaka kuicopy ili uwe ushahidi sababu no need. Ila kwako wacha nikuwekee ukisearch Google haifutiki

Naibu Spika Job Ndugai afunguka, aahidi kukaa chini na UKAWA ...
www.jamiiforums.com › threads › naibu-...
Mobile-friendly - 3 hours ago - Akijibu Maswali yamoja kwa moja ya Mwandishi wa habari, Spika wa Tanzania Job ...
 
Hahaha leo hii UKAWA wanamshangilia Ndugai mwana CCM wakidhani atawatea hahaha kweli Simba akikosa chakula hula hata nyasi....ngoja tuone...hahahaha
 
Ndugai pamoja na mambo yake mengine ila huwa ana busara sana
 
Unaweza ukawa msomi wa juu na mbobevu ktk sheria na masuala ya utawala na uuonhoz lkn kama ulimi wako hauna uchaguzi wa nini cha kuongea na kama ufahamu wako haujajaa hekima, busara na maarifa kuongoza ni kugumu sana aisee.

Kwa wale wazazi wanalijua hili kuwa sheria na ukali wa wazazi kwa watoto huwa hakusaidii sana ktk malezi na maelekezi kwa watoto.Asilimia kubwa ya watoto wakaidi, sugu na walioshindikana ni wale ambao walibanwa na sheria hadi wamekuwa sugu.

Uongozi ni hekima,busara na maarifa. Kuna mahali ukiaply sheria panakataa unatakiwa utumie hekima na busara. Na ndio hata sala inayotumika kila asb kabla ya bunge letu kuanza.

Mhe Spika Job Ndugai heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Mungu akusaidie uwaweke watoto (wabunge) wako pamoja. Ni kweli una mitoto mingine mitundu kweli kweli mle ndani lkn baba mwenye hekima huwasahihisha,huwavumilia, huwakemea na wakati mwingine huwachapa bakora lakini yote haya ni kwa nia ya kuwarudi na kuwaweka pamoja.

Nakuombea Mungu ili akupe hekima na busara katika kuwaleta pamoja wanao hawa. Wewe ni baba wa wote Mungu akusaidie uwalete wanao pamoja
 
Back
Top Bottom