PreGE2025 Spika Dkt. Tulia: Huwezi kusema mtu katekwa kama hukuona

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,992
Reaction score
5,660
Majibu fikirishi kutoka kwa Mh Tulia Ackson kuhusiana na kupotea kwa Mh Mdude Nyangal, mwanachama wa CHADEMA

Your browser is not able to display this video.

Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Tulia Ackson akifafanua hoja ya Bunge kutotoa maelekezo kuhusu uwepo wa matukio ya Watu kudaiwa kutekwa na wengine kupotea Nchini, amesema hiyo inahitaji ushahidi na isiwe suala la kusikia.

Amezungumza hayo wakati akihojiwa na Wasafi FM, Mei 9, 2025, Mtangazaji Charles Williams alimuuliza “Kumekuwa na vitendo vinavyoitwa vya Utekaji, hata Ripoti ya LHRC imeeleza hilo, hapa Mbeya amepotea Mdude (Nyangali), CHADEMA na Serikali wametangaza dau kwa atakayefanikisha kupatikana kwake.”

Akaongoza “Je, vitendo vya Watu kupotea au kutekwa vinaonekana vimeshamiri au vimerejea kwa kasi, Watu wanadhani Bunge lina sababu ya kusimamisha kusimamisha shughuli zake na kulijadili kwa kina suala hilo, wewe unasemaje?"
 
Muongo mkubwa, anafumbia macho kwakuwa ye ni moja ya wanufaika!
Mdude ametekwa kwasabb ya misimamo yake dhidi ya watawala wasiopenda kukosolewa...na uzuri Mdude alishasema hapa ikitokea amepotezwa mhusika atakuwa ni sa100!.

Uongo mwingine wa Tulia, mke wa Mdude aliyekuwepo wakati wa ukamataji amethibitisha kwamba mmewe amechukuliwa na mapolisi...tena kwa kumpiga sana hadi kutokwa damu nyingi...Tulia anatuzuga hapa na mifano yake yakijinga!
 
Kwenda misikitini na makanisani ni kutafuta kukubalika kwenye jamii. Ni kama mila tu. Haina uhusiano na uadilifu na kupenda haki kwetu.

Uovu tunaofanyiana ni uthibitisho.
 
Kipindi kile Cha mauaji ya albino, bunge lilipojadili hiyo hoja ya dharura, je walikuwa na ushahidi wa nani anawateka au kuwaua maalbino?

Anasema hivyo Kwa sababu yeye ni spika aliwekwa hapo kimikakati, hivyo pamoja na uelewa na ubobevu wale mkubwa, bado kwenye issues kama hizi atajifanya kuwa bunge halina Cha kuazimia. Ila la kuongea mechi ya Simba na Yanga hilo wanalo la kuazimia na Wala siyo hali tete ya usalama nchini.
 
Hivi watanzania tunategemea miujiza? Tumeambiwa upelelezi wa shambulio la Lisu umekwama kwa sababu aliyeshambuliwa yuko nje ya nchi. Hivi anapouawa mtu upelelezi unafanyikaje?
 
mwanasheria anapokuwa mwanasiasa. shithole.

watu walimwona mzee Ali Kibao akitekwa kwa kushushwa kwenye basi na baadaye anakutwa ameuawa

mke wa Mdude ameona Mdude akitekwa, sasa sijui anaongea nini huyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…