Spika awataka Freeman Mbowe na Halima Mdee wafike mbele ya Kamati ya Maadili. Matusi yawagharimu

Baada ya kipindi cha Maswali na Majibu Bungeni Dodoma leo Aprili 6, 2017, Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliomba muongozo wa hatua watakazochukuliwa Mbunge wa Hai, FREEMAN MBOWE na Mbunge wa Kawe, HALIMA MDEE kutokana na kupotomosha matusi Bungeni kwa kuwatukana viongozi wa Serikali na Spika wa Bunge. Freeman Mbowe amesikika akiwatukana Rais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge baada ya Wabunge wake Laurence Masha na Ezekiel Wenje kupigiwa kura za HAPANA kuwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Naye Mbunge wa Kawe, HALIMA MDEE Aprili 4, 2017 amenukuliwa akimtukana Spika wa Bunge Job Ndugai. Kutokana na Muongozo huo, Spika wa Bunge, JOB NDUGAI ameonesha masikitiko yake kwa jinsi Wabunge HALIMA MDEE na Mwenyekiti wake FREEMAN MBOWE walivyo na utovu wa Nidhamu. Spika amesema kuwa haiwezekani Bunge linawaita watu wa nje kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge wakati wabunge wenyewe wanakuwa na kiwango kikubwa cha Utovu wa Nidhamu.

Kutokana na hali hiyo ameagiza Mbunge wa Kawe, HALIMA MDEE kukamatwa popote alipo na kufikishwa kwenye mamlaka husika. Pia ameagiza FREEMAN MBOWE kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge na ameiagiza kamati hiyo kukutana haraka iwezekanavyo kushughulikia jambo hilo.

Wale mlioshangilia Paul Makonda kuhojiwa na Bunge, mshangilie pia Mbowe na Mdee kuwekwa kikaangoni.

Chanzo: TBC Taifa
You nailed it mkuu... sijui km watashangilia wale nyumbu
 
Nlitaka kushangaa, yaan mibunge bodus hawajui power ya spika..spika kwny circumstance mbal mbal hua ana power ya kuongoza nchi leo wabunge jingajinga wana personal problems wanamtukana spika..spika...so sad..huu uhuni 2 much
 
Ile juzi wakati wabunge walikuwa wapo kwenye mchakato wa kuchagua wabunge wa EALA wabunge wa upinzani pamoja na spika walipishana kwenye sheria za uchaguzo huo kukatokea na mabishano kipindi mabishano yanaendelea ikasikika sauti ya mdee ikimtukana spika kwamba we mpumbavu ........fala ndivyo ilivyokuwa kwa ufupi
asante sana ilinipita mbali. Sasa walijuaje kuwa alimlenga yeye kama hakutamka jina? anyway, labda tuone clip. Be it as it may, watamhukumu kumsimamisha bunge for long periods! Penye nia OVU itatekelezwa! Mbona yeye alimppiga mtu akazimia? Kuhoji kati ya Masha na Wenje nani mwanamke was it fair, lugha ya kistaarabu?
 
Mdee hapa umekosea sana dada angu hayo maneno si ya kiongozi hata kama ulikuwa umepanic nenda kaombe msamaha kwenye kamati we ni binaadam kama wengine kwa hiyo suala la kukosea ni kawaida sana.
 
Mbona huyu spika upinzan walimsifu sana inakuaje nae kaanza kutukanwa?sasa moto unaanza kua mkubwa maana kama spika nae anaanza kuonesha reactions zake yule DR tulia ndo balaa.yetu maskio
 
Sasa anayekuhoji kwenye maadili ndio huyo huyo mpinzan wako...bado safari ni ndefu
 
Je huyo spika aliposema kati ya masha na wenje nani mwanamke hilo sio tusi ni zawadi-eehh
Au ulikuwa huangalii TBC-by the way bungeni kuna kinga kama mtu kafanya kosa akiwa ndani ya bunge ni kamati tu inamuita na kumuonya sio kumpelekea polisi
Kma aliyeulizwa alijibu wote ni wanaume linakuwaje tusi?
 
Kwani kumwambia mtu unatembea kama "kobe" neno hilo si kumtusi mtu. Au ya mdee ndio matusi? Yote ni matusi wote wafikishwe kwenye kamati ya maadili
 
asante sana ilinipita mbali. Sasa walijuaje kuwa alimlenga yeye kama hakutamka jina? anyway, labda tuone clip. Be it as it may, watamhukumu kumsimamisha bunge for long periods! Penye nia OVU itatekelezwa! Mbona yeye alimppiga mtu akazimia? Kuhoji kati ya Masha na Wenje nani mwanamke was it fair, lugha ya kistaarabu?
Mkuu unajuwa hivi vyama vyetu tunavipenda sana mpaka inafikia hatua mwanachana akikosea tunashindwa kumkosoa kutokana na masilahi pamoja na mapenzi ya chama ndicho kinachofanyika kwenye vyama vyote .Hebu jaribu kufuatilia hiyo clip then utajaj
 
Anaonewa ndiyo kwani alipo mwambia akalishe manannii yake.alikuwa inamaana gani??

Au hizi Kamati za Maadili ni.kwa ajili.ya Upinzani tu?
wee pim..mbi unaongea ujinga gani, ulitaka Mbowe na huyo Muuza Papu..chi aachwe wao kina nan
 
Na huyohuyo spika , aliwaita wafanyakazi wa bungeni siku ivyo hiyo kuwa ,,,,

"wanatembea kama Kobe "

hapo ni wakati akiwagiza walete barua, kwa hiyo akaona kuwa wanatembea kama Kobe kweli ,inauma sana aisee.

Au yeye anaruhusa kutumia lugha yoyote ile.na kwa mtu yeyote?

Mimi siyo mfuasi wa vyama hivi vya siasa ila ; wakati mwingine viongozi hawa kama spika wanapaswa waache unafiki aiseee.
Endelea kusubiri uone kama hayo maneno yako yatakusadia mkanyeni mdee aache Bangi .
 
Unajua busara ni kitu cha Maana sana najua Halima alikosea lakini Spika alikosea zaidi majibu yake anavyowatreat wabunge ambao siyo wa CCM siyo wa staha! Kama kiongozi anapaswa kuona wote ni wabunge! Alivyokuwa anaongea na Mnyika hata na Tundu ilikuwa lugha ambayo siyo ya staha kabisa! Jiheshimu spika wabunge watakuheshimu na nanyi
Wabunge wa upinzani waheshimuni hao viongozi hata kama wanaonesha Chuki na dharau!
Mlimlilia yule binti kuwa ameshindwa kuliongoza bunge kuwa ana upendeleo, na maagizo kutoka kwa mkuu, leo Ndugai pia hafai? Mnamtaka nani sasa? Hamkosi vijisababu...
 
Ndugai anataka kujisafisha wakati ni yeye kama Kiongozi wa Bunge ndiye anayestahili adhabu.Hakutenda kwa hekima.Alikuwa anatukana hovyo hovyo.

Yaani amejionyesha ni kwa kiasi gani Ndugai Hafai.ni mpuuzi kabisa.
bora hata ya TULIA, et si ndo hivyo kamanda!!!!
 
ukidai haki yako nchini unaonekena mtomvu wa nidhamu,mbona hapo kabla hawakumpa 24hrs bashite asipojisalimisha polisi wamkamate?
 
Kwani kumwambia mtu unatembea kama "kobe" neno hilo si kumtusi mtu. Au ya mdee ndio matusi? Yote ni matusi wote wafikishwe kwenye kamati ya maadili
Eeeee!!!! mkuu umekatwa kichwa au ni mapenzi yako juu ya Halima M/vyama vya siasa, sina hakika kama hata hiyo akili uliyo nayo kidogo unaitumia vizuri!!!!

Hebu neenda youtube kama una nafasi ya kama dk 5 uangalie hiyo clip harafu urudi hapa utuambie kati ya kutembea kama kobe na spika acha ufala lipi ni tusi!!!!
 
Kiti cha Spika ndio muamuzi wa mwisho katika mtanziko wa mambo ndani ya jengo la bunge,anapaswa kuongoza kwa busara kuliko jazba na hisia za kichama.

Spika anapaswa kuamua kwa kufuata kanuni na taratibu za kibunge,pale ambapo kanuni zimekaa kimya,hapo "busara" za Spika hupaswa kutumika.Lakini Ndugai ameanza kutumia "busara za spika" hata katika maamuzi ambayo kanuni zipo wazi.Katika mazingira haya,kwanini watu wasikuone "fa***l**a?".

Leo kabetua kanuni,kaondoa kipindi cha maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu eti kisa "usomaji wa bajeti".Lakini inajulikana amemkimbiza PM asijibu maswali magumu juu ya serikali kuingilia uchaguzi wa EALA na Katibu wa bunge "kusajili" vyama viwili vya CUF,ile CUF A na CUF B wakati katika kumbukumbu ya vyama vilivyopo bungeni hakuna vyama hivyo.

Spika alimuuliza Mbowe juzi kwenye uchaguzi wa EALA,kati ya Masha na Wenje,nani ni mwanamke?haikuwa kauli nzuri na ya heshima kwa wenzake na wanaume wenye familia.Alivumiliwa kwa sbb yeye ndio mwenye kiti.

Serukamba aliwahi kutoa tusi kubwa sana lakini "alibebwa",Nkamia aliwahi mtukana Sugu kwa kumuita mbwa,ikapotezewa,Lusinde hutukana sana bungeni na wabunge hushangilia.

Ile sauti iliyosikika ni kama ya Halima Mdee,hakuna wa "kuthibitisha" kuwa ni ya Halima sbb hakuwa anaongea rasmi kama aliyepewa nafasi.Akikamatwa Mdee,akamatwe na yule aliyemwambia Mdee "kikalishe chini utulie".

Ndugai anaona makosa ya utovu wa nidhamu kwa wenzake tu,yeye mbona kwenye kura za maoni alimpiga mwenzake Chilongani na "sungururu" ya kichwa mpaka akazimia?Ule ulikuwa ni mfano mzuri?Tena naibu Spika na mbunge anayetetea nafasi yake?

Neno fala,linalingana na lile alilotamka Mkapa kuwa watu ni malofa,huyu naye alikuwa mfano mzuri kwa matamshi yale pale Jangwani?Lofa na kilaza ni maneno yenye uwiano,kilaza na fala yanashabihiana...Moja lilitamkwa na mkuu wa nchi,moja na Mkuu wa nchi mstaafu na moja ni la Mbunge wa Kawe.

Huu mfano wa lugha nzuri,uwe kwa viongozi wote,waliopo madarakani na waliotoka madarakani.Hii itajenga uhalali wa kukemea kila kiongozi anapovunja taratibu.

Hilo la Mbowe ni maagizo toka ule mhimili uliojichimbia kuliko mihimili mingine...

Mlinga aliyeomba muongozo anafahamika kwa lugha za kashfa na kuuzi,ndani ya bunge aliwahi kutamka kuwa wabunge wanawake wa UKAWA hawawezi kupata hizo nafasi bila "kuvua chu***p**".

Alishangiliwa na wabunge wote wa CCM,wake kwa waume,hata hao kina Stella Manyanya wanaojifanya wanaharakati wa jenda kwenye uchaguzi wa EALA hawakukemea kauli ile.

Katika kipindi ambacho Ndugai alipaswa kuacha vihasira vya kijinga na ajabu ajabu ni kipindi hiki.Miezi minne ya kukaa juu ya mashine India ilipaswa kubadili muelekeo wa maisha na mfumo wake wa kiuongozi.Lakini sbb madaraka hulevya,basi naye amelewa na kulewa!!Thawabu na malipo ya uhai ulioongezewa na Mungu,ni utumishi wenye haki na usawa kwa Watanzania na wabunge waliokupa nafasi ya kuwaongoza.Hii ndio nafasi nyingine uliyopewa na Mungu,itumie kuongeza marafiki na sifa njema itayakayobaki katika kumbukumbu na mioyo ya Watanzania.

Kila mtu alimtakia heri na afya njema,watu walimtumia meseji na kumpigia simu bila kujali itikadi zao.Watu walipenda arudi haraka ili kuja kuleta busara,mtangamano na ushirikiano katika bunge.Bahati mbaya na yeye amemezwa na "maagaizo" kutoka juu.
 
Back
Top Bottom