Spika aongezewa ulinzi

Spika aongezewa ulinzi

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Posts
3,007
Reaction score
2,462
x9F+kX5QowbGgAAAABJRU5ErkJggg==
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameongezewa ulinzi pamoja na kubadilishiwa namba za gari analotumia kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa simu.

Taarifa ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Chadema kutoa namba za Spika na kuzigawa kwa wafuasi wake waliofika kwenye mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam hivi karibuni ili wamtumie ujumbe mfupi wa simu.

Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.

Taarifa zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa vitisho ambavyo inaonyesha kuwa wananchi wana hasira naye na ndiyo maana ameongezewa ulinzi.

Vyanzo vyetu vya habari vimeeleza kuwa gari la Spika Makinda limebadilishwa namba kwa kuondolewa herufi S ambayo humaanisha Spika na kuwekwa namba nyingine ambazo bado hazijajulikana.

"Watu wanaomtumia ‘meseji' wana hasira, wanaweza kumdhuru na ndiyo maana ameongezewa ulinzi. Hata magari yake aliyokuwa akitumia yamebadilishwa na kupewa mengine tofauti," kilieleza chanzo chetu cha habari.

Spika Makinda mwenyewe alipopigiwa simu ili kueleza kuhusu suala hilo la kuongezewa walinzi simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah naye simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.Tangu Chadema wagawe namba hiyo baada ya kumtuhumu Spika pamoja na msaidizi wake, Job Ndugai kuwa amekuwa akipindisha kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.

Taarifa zilieleza kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na kutumiwa ujumbe za vitisho.Wakati hayo yakitokea, tayari Ofisi ya Bunge imesema itawachukulia hatua kali wale wote waliotumia lugha chafu kwa ujumbe mfupi ama kupiga moja kwa moja kwa Spika na Naibu wake.

Katibu Mkuu wa Bunge, Dk Kashililah juzi alisema kuwa kutoa namba si tatizo, bali kuzitumia namba hizo kinyume na taratibu ndiyo haitakiwi, jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.

"Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria. Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake," alionya Kashililah.

"Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali.

"Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; "Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu."
 
wakati ukilaumu wengine kwa vitisho wakati huo huo wewe mwenyewe Dr.kashillah(wa kichina)unatoa vitisho kwa wengine Ebu waache wananchi waendelee kutoa maoni bila kujaribu kuwatisha kwani wanalipia hizo simu waache watoe mawazo yao
 
Hawa watu wapuuzi sasa; kwani namba za Spika zilikuwa hazijulikani? MBona ni public information? Namba za Rais zinajulikana, namba za Waziri Mkuu zinajulikana; imekuwa namba za Spika? Chadema hawakutoa namba za Spika hadharani; namba hizo alizotoa yeye mwenyewe, CDM wao walizirudia tu kwenye mkutano wa hadhara; wangeweza kumwelekeza mtu aende kwenye tovuti ya Bunge au kuzitafuta kwa namna nyingine.

Kosa la wale viongozi waliotaja jamba za Spika na Naibu wake hawakuwa na ujumbe Specific wa kumwambia Spika. They should have a standard message - short, clear and pointed.
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.
 
acha ujinga unalopoka tu kwa yale unayoyajua japo unataka kudanganya umma kuwa hujui,wananchi hao ndio waajiri wa maspk hao wanayohaki ya kuwakaripia hao unaowaona ni waungu watu,tunataka viongoz wa nchi hii wanapotaka kufanya maamzi yeyote yasyo na tija kwa wananchi wajue maamzi hayo yatawagharimu.
 
Watanzania ni mabingwa katika kumalizia hasira zao kwenye keyboard and keypad, kwa njia hii kila aina ya maneno machafu wanayajua. Inapokuja kwenye physical confrontation na ukichukulia hata kanuni za bunge wengi hawazijui, thubutu, huwezi kuwaona.

Mama Spika wala usiwe na wasiwasi, haya ni maneno ya debe tupu. hakuna mtu atakaye kudhuru kwa sababu ya kanuni ambazo wachache sana wanazijua. kilichofanyika ni mob mentality kuchagizwa na waheshimiwa ambayo imewasukuma watu kutenda deindividuation.

Huu ni upepo tu na utapita.
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.

tutakutananaye mahakamani, anielezee namna msj zangu zilivyomuathiri. Mahakama si chombo cha huruma, ni chombo cha haki.
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.

Chanzo cha matusi ni kupindisha kanuni za bunge na si mkutano wa Mwembeyanga..
 
Watanzania ni mabingwa katika kumalizia hasira zao kwenye keyboard and keypad, kwa njia hii kila aina ya maneno machafu wanayajua. Inapokuja kwenye physical confrontation na ukichukulia hata kanuni za bunge wengi hawazijui, thubutu, huwezi kuwaona.

Mama Spika wala usiwe na wasiwasi, haya ni maneno ya debe tupu. hakuna mtu atakaye kudhuru kwa sababu ya kanuni ambazo wachache sana wanazijua. kilichofanyika ni mob mentality kuchagizwa na waheshimiwa ambayo imewasukuma watu kutenda deindividuation.

Huu ni upepo na utapita.
Dumila, Geita nayenyewe yalikuwa ni upepo tu lakini mwisho wake umeuona? bado tunasonga mbele mpaka kieleweke
 
Hivi habari ya gesi Mtwara imefikia wapi..!??Serikali inalishughulikiaje hadi sasa!? Mwenye kujua tafadhali..
 
Watanzania ni mabingwa katika kumalizia hasira zao kwenye keyboard and keypad, kwa njia hii kila aina ya maneno machafu wanayajua. Inapokuja kwenye physical confrontation na ukichukulia hata kanuni za bunge wengi hawazijui, thubutu, huwezi kuwaona.

Mama Spika wala usiwe na wasiwasi, haya ni maneno ya debe tupu. hakuna mtu atakaye kudhuru kwa sababu ya kanuni ambazo wachache sana wanazijua. kilichofanyika ni mob mentality kuchagizwa na waheshimiwa ambayo imewasukuma watu kutenda deindividuation

Huu ni upepo tu na utapita.

..........

Mbona kikao kilichopita kanuni ilielekeza wazi wazi wabunge wanapaswa kujadili mpango wa maendeleo wa Taifa...ikiwamo miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo inamgusa Mtanzania Moja kwa moja.....kanuni hiyo ilikiukwa na ofisi ya spika ilitaarifiwa juu ya hilo.

Ni wazi kuwa spika ndiye anayepindisha kanuni...na ni vyema utaratibu wa kuulizana wazi wazi utumike kupitia wananchi maana wingi wao bungeni unaminya mianya ya haki kupatikana kwa wengine.
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.
na wewe acha unazi. Punguza kuwatetea magamba.
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.

Kwa hiyo kusisitiza kumtumia ujumbe spika maana yake kwa akili yako ni kumwambia kamtukane spika?!
Mkuu ushabiki hupofusha fikra huru!
 
Itabidi aongezewe na wale jamaa wa GG walau mmoja tu kumlinda.
 
Pana watu humu wanatutafutia ban kwa nguvu.
 
Kosa la wale viongozi waliotaja jamba za Spika na Naibu wake hawakuwa na ujumbe Specific wa kumwambia Spika. They should have a standard message - short, clear and pointed.

Ndio kosa la wanasiasa wetu wengi;
Huwaacha wananchi katika limbwi kubwa la sitofahamu;
Matokeo yake ujumbe uliokusudiwa haufiki;
Bali inakuwa fujo naam mchafugoke.
Tubadilike na Tujisahihishe.

Bazazi!
 
Tena tuna hasira nae kweli kweli hatuwezi kuvumilia upuuzi huu wa kudharau unma wa watanzania na kuyatetea mafisadi ili uende choo,hivyo vitisho vya kashindilia akamwambie kova amtafute rama ili ajibu mashtaka ya kum'mabwepande Dr.Uli....
 
Back
Top Bottom