Kwa nini nasema Spika Anne Makinda awaombe radhi wanaume?
Ni kwa sababu maana yake binafsi ya ufisadi. Sihangaiki sana na kujadili kauli yake mwaka juzi alivyoufahamu ufisadi maana imejadiliwa sana humu na wataalamu wameshtuonyesha nini kamusi zinavyosema kwamba fisadi ni mtu aliyekosa uadilifu (Bonyeza hapa).
Licha ya kamusi kuonyesha vile Anna makinda aliishia kuwasakama wanaume alipotumia neno fisadi.
Je, kama ufisadi ni aina ya ufusaka anaousema Makinda, kwa nini basi anaikwepesha jinsia ya kike kuwajibika kitendo kilekile cha kifisadi? Je, anataka kutuambia kwamba kuchaguliwa kwake mwanamke wa kwanza ngazi ile ni kusukuma uozo wote wa jamii kwenye jinsia ya kiume hata kama uozo ule unafanywa na jinsia ya kike pia?
Anne Makinda angekuwa muumini wa usawa wa jinsia walau angesema fisadi ni mhuni anayeingilia ndoa za watu. Japo si sahihi sana lakini walau kuna gender balance kidogo, jinsia zote zimeguswa.
Natoa wito kwamba spika huyu Anne Makinda aombe radhi kwa matumizi mabaya ya matamshi yake. Kwa sababu amedanganya umma kwa kujaribu kutunga maana mpya ya ufisadi wakati tukipekua dictionary na kamusi tunaona alichokisema ni aina mojawapo ya matumizi ya neno hilo bila msisitizo maalumu. Ufisadi ni kukosa uadilifu yaani corrupt person.
Hivyo hata mwanamke asiye na ndoa ni fisadi iwapo atachukua mwanaume mwenye ndoa waziwazi au kwa kujificha. Bila kujali mwanamke huyo ni mfagiaji barabarani, ni karani, ni sekretari. Pia bila kujali kuwa mwanamke huyo ni spika wa bunge la muungano.
Najua wapo wataotaka kupindisha mada kwamba wanaume sasa tunaanza kumashambulia spika kwa ajili ni mwanamke.
Wanaowaza kuleta madai hayo inabidi tuwanyamazishe mapema kwa kuwapa mfano wa yaliyompata spika mwenzake yaani Pius Msekwa mwaka 2003. Nakumbuka zilipigwa kelele nyingi kuhusu yeye kuwa Mwenyekiti wa board ya kampuni ya simu za mikononi yaani Vodacom wakati huohuo akiwa kama spika wa bunge.
Yeye alifafanua uenyekiti wake usivyoathiri uspka wake wa bunge. Na mwisho akatoa kauli kwamba wanaomsakama wanamuonea wivu. Alitumie neno "wana wivu wa kike"
Neno hili "wana wivu wa kike" wanaharakati wa kijinsia walilivalia njuga hadi kuipindisha mada ya msigi ya maslahi ya Msekwa, Vodacom na bunge. Mashambulizi ya wanaharakati hao yalimshinikiza spika Msekwa aseme kuwa hakujua kuwa neno "wana wivu wa kike" lingechukuliwa bango namna ile kwani ni neno la kawaida kwenye jamii.
Leo tuna spika mwangine. Si mwanaume tena, ni mwanamke, Anne Makinda. Wakati wa Msekwa kelele zilipigwa kwamba ni unyanyasaji wa kijinsia. Leo wale wanaharakati wote wako kimya kwa sababu Anne Makinda ni mwanamke mwenzao.
Kama Anne Makinda asipoomba radhi na ana baraka za ukimya wa wanaharakati wale sasa ndiyo tuone kuwa harakati za kijinsia zinamaanisha nini.
Tujihadhari.