Spika aikataa kambi ya Hamad na Kafulila

Mi nafikiri CHADEMA wawakubali hao NCCR,TLP,CUF,wakileta ujinga kuna vifungu vinaruhusu kuwaondoa kama ilivyokuwa kwa John Cheyo,tatizo ni kuwa hivi vyama haviaminiki,watu wana hila zao za kisiasa,i can understand CHADEMA hesitation to work with this guys but it worth trying working together.


Ndugu kama huna uhakika wa jambo ni bora ukanyamaza usionekane mpumbavu au mwenye mapenzi na watu wa aina fulani. Nchi hii haitaendeshwa kwa mapenzi ya vyama zaidi ya uzalendo kutoka katika mioyo yetu. CUF 2005 - 2010 walikuwa na wabunge wenye kukidhi kuunda kambi ya upinzani peke yao sasa kwa mampenzi yako kwa CDM yanakutia upofu ukasema maneno usiyo yajua
HAMAD ni mtu hatari kwa bara.CUF haijawai kuipa CDM ofa bali walibanwa na kanuni, walimpa ofa UDP in 1995-2000 if am not mistakeni
Kama magreat thinkers hatuwezi kuwashutumu viongozi wawe wa CDM, CCM, PPT na vyama vingene eti watu wa hatari sana maneno haya hata CCM wanapenda sana kuyatumia hata CUF na vyama vya upinzani lakini tusikubali kumeza uchafu huo. Tukisema Hamad ni mtu hatari basi tuwe tunakumbusha tukio fulani mfano "alisababisha watu waandamane wakauwawa 2001" sioni ajabu watu wakasema hivyo au labda mtu hatari alipokuwa waziri kwenye serikali ya Mwl Nyerere alitumia madaraka vibaya. We are great thinkers tusiwashutumu watu shutuma zisizo na "mashiko"

Wenye kumbukumbu nzuri wataungana na mimi vyama vya CDM na CUF ndio vyama vya kwanza Tanzania vilivyokubaliana kufanya kazi pamoja na kusimamisha mgombea mmoja wa Urais 2000 CDM hawakumsimamisha mgombea Urais na waligawana kwenye majimbo vyama husika vilipokuwa na nguvu CDM haikusimamisha mgombea na CUF hawakufanya hivyo. Lakini ushirika ule ulikoma 2005.
 
Marytina,nakubaliana na wewe bora kuwa na watu wachache wazalendo, ila si vibaya wakawapa nafasi,wakiharibu watolewe.

Kuhusu suala la pili, Chama chenye wabunge wengi katika upinzani ndo huunda kambi ya upinzani,baada ya uchaguzi ndo hali imebadilika,miaka iliyopita CUF ndo walikuwa wengi na chini ya Uongozi wa Hamad Rashid kama mwenyekiti wa kambi ya Upinzani,CHADEMA walishirikishwa na si UDP tu kama ulivyosema,walishirikiana vizuri navyofikiri.

kuwa na msimamo wa mawazo hapo juu unaonekana kukubali hapa unapinga hueleweki
 
Mkuu,

Ni chama gani au vyama gani vimeunda serikali ya muungano?
Kama una jibu la suali hili basi vyama ambavyo havijaunda serikali ni vyama vya upinzani.

Ukirudi na hoja ,ya "ndoa" ya CCM na CUF Zanzibar, Zanzibar hawana bunge wana kitu kinaitwa baraza la wawakilishi na wanaoingia humo ni wawakilishi sio wabunge.

Tunachanganya sana mambo haya na kuufanya upinzani uwe dhaifu. Kama upinzani wataungana ,at least, wataipeleka puta CCM lakini kwa chama kimoja tu, tutegemee nyundo ya CCM itatumaliza au itatutia kilema.

hawa cuf na nccr nafikiri mwanzo(baada ya matokeo) nakumbuka mbowe alizungumza nao wakatia ngumu sasa sijui nini wanachotaka?
 
hata chadema wakiungana na Cuf na Nccr bado kwa idadi sisi em wataongoza. Kwa hiyo kuwakumbatia Cuf na Nccr haitawapa ushindi wa hoja kupita! Plus yaliyooneshwa na Cuf na Nccr ktk uchaguzi, siku ya walkout et al yanatupa true colors za hawa jamaa bila kusahau yale majadiliano ya Mbowe na Rashid!

All I can say is, Chadema walivyo wanatosha kupambana peke yao, na wana watu makini tu. Kama Cuf au Nccr au wabunge wengine hawataunga mkono hoja za Chadema zenye maslahi kwa nchi simply kwa kuwa wamewanyima nafasi then sisi tutawaadhibu kwa kuwanyima kura kwa kuwa watakuwa hawajatuwakilisha.

The bottom line, as I have always believe, ni kuwa Chadema kapiganeni vivyo mlivyo bungeni. Wananchi watajua tu kuwa wanahitaji kuongeza idadi ya wabung wa Chadema ili wajikomboe. Naomba msiingie mtego wa kuwakumbatia hawa jamaa wasaliti wenu. Kwanza hawajatubu kwa waliyowatendea!

Hapo kwenye bold sio CUF peke yao mkuu hata CDM kuna wabunge hawaku walk out au ndio ukipenda sana hata kama ana kasoro huzioni? Mwenzenu mie napenda sana lakini ukweli nauona nauvumilia nachukua kama ni changamoto kwani vyama vina ongozwa na watu wengi kila mmoja mwenye uono wake. Unachukia lakini unasonga mbele. Kikubwa hapa nadhani tuangalie jinsi gani ya kutatua matatizo yanayotukabili Umeme, Maji, Gas, Matibabu na Elimu sidhani kama haya mambo ya kambi ya upinzani yana tija kubwa sana kwetu na isitoshe kambi yenyewe kumbe sio "rasmi" yaani kwa kiswahili fasaha haitambuliki yanini tuumize vichwa vyetu yaani sisi hatujui maana ya isiyo RASMI??????????????????????????? Kweli?????????? Siamini haki ya Mungu!!!!
 
CCM ni kama shetani. Haina shikrani. Utamtumikia sana lakini mwisho wa siku badala akulipe , wewe ndio utakayemlipa! Tuone wataenda wapi sasa, na CDM wawe makini coz wakiwapokea 2, tumekwisha!
 
Nakumbuka vizuri sana kuwa msimamo wa CUF ni kuwa hawataungana na CHADEMA, hadi chadema wakutane na kupatana na viongozi wa NCCR-Mageuzi. CUF watuambie kuwa lini wamebadili msimamo, na kwa nini?
 
Michelle habari za asubuhi bibie.... naomba nikuulize mbona wao walikubaliwa kufanya kazi na CUF wakati huo Chadema walikuwa na viti vichache na CUF ilikuwa na uwezo wa kuunda kambi peke yao? Tuwe balance tuache ushabiki wa vyama vyetu jamani swali hivi hapa JF kungekalika kweli kama CUF wangekuwa wanafanya wanayoyafanya Chadema dhidi ya wenzao si ndio wangebezwa CCM B hao wameshanunuliwa hao na kadha wa kadha? Nafikiri haya mambo yanahitaji kuyatazama kwa jicho la tatu...

Mazingira ni tofauti na Bunge lililopita. Kwa sasa CUF ni sehemu ya Serikali na kama upinzani ukitaka kupinga kitu, Katibu Mkuu wa CUF atakuwa na ushawishi kwa wabunge wake waiunge mkono serikali
 
Nakumbuka vizuri sana kuwa msimamo wa CUF ni kuwa hawataungana na CHADEMA, hadi chadema wakutane na kupatana na viongozi wa NCCR-Mageuzi. CUF watuambie kuwa lini wamebadili msimamo, na kwa nini?

Unamaana CUF wanataka upinzani usahau yaliyopita wawe na solidarity?
 
Mazingira ni tofauti na Bunge lililopita. Kwa sasa CUF ni sehemu ya Serikali na kama upinzani ukitaka kupinga kitu, Katibu Mkuu wa CUF atakuwa na ushawishi kwa wabunge wake waiunge mkono serikali

Mkuu nakubaliana na wewe lakini sioni sababu ya watu kuumiza vichwa vyao eti wanajf hawajui tafsiri ya neno "kambi isiyo rasmi" ?????? Mie siamini kama hamjui labda mmetoka kuamka.
 
Nakumbuka vizuri sana kuwa msimamo wa CUF ni kuwa hawataungana na CHADEMA, hadi chadema wakutane na kupatana na viongozi wa NCCR-Mageuzi. CUF watuambie kuwa lini wamebadili msimamo, na kwa nini?

yes na HR alitamka wazi wazi kuwa hawapo tayari kuungana na CDM katika kuunda kambi ya upinzani kwakuwa wao KAFU wana sera ya serikali ya umoja wa kitaifa na CDM haina sera hiyo...

that means..... justice has been convened and CDM should propose dialogue to include minority parties with MP's to form official opposition camp.... finished
 
hawa CUF si walizomea wakati CHADEMA wanatoka nje kumpinga KIKWETE ..by the way CUF si wana ndoa na CCM sasa wanakuwaje wapinzani??? iam confused
 
Mkuu,

Ni chama gani au vyama gani vimeunda serikali ya muungano?
Kama una jibu la suali hili basi vyama ambavyo havijaunda serikali ni vyama vya upinzani.

Ukirudi na hoja ,ya "ndoa" ya CCM na CUF Zanzibar, Zanzibar hawana bunge wana kitu kinaitwa baraza la wawakilishi na wanaoingia humo ni wawakilishi sio wabunge.

Tunachanganya sana mambo haya na kuufanya upinzani uwe dhaifu. Kama upinzani wataungana ,at least, wataipeleka puta CCM lakini kwa chama kimoja tu, tutegemee nyundo ya CCM itatumaliza au itatutia kilema.


Nooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!, ningefurahi sana kama Chadema wataendelea na msimamo wao wa kuwa na kambi yao bila kuwashirikisha hawa wengine.jamani ipo siri nzito hapo,ni nani asiyekumbuka kuwa NCCR iliyumika kuibomoa Chadema wakati wa campaign je tunajuaje kama hali hii imekwisha?,Ni nani asiyejua kuwa Kafulila ni ndumila kuwili anatumiwa na yeyote bora pesa? CUF tayari wanamuafaka,wao wenyewe ndani ya chama ni Tatizo,jana kuna mtu aliniambia Hata Lipumba anatamani kujihudhuru sababu ya kutokuwa na muelekeo thabiti katika utendaji.

Chadema, chonde chonde msikubari, hao ni mamruki wanatumika tu,kwani mwanzo si mliwashirikisha mambo lakini wakawagomea sasa nini tena.

Hamad najua umeyakosa marupurupu ya kuwa kiongozi wa upinzani ndiyo maana unatapatapa sasa,masanduku ya bia na soda sasa yamepungua etieeeeeeeeeeeeeeeeeee pole sana imekula kwako subiri 2015 mkiweza.
 
@mohammed shosi,
tofauti ya wabunge wa chadema ambao hawaku walk out na hawa Cuf na Nccr iko wazi! Wale ni wanachama wa Chadema na hawa si wanachama. Wale ni watoto wa nyumbani na kuna taratibu zilifuatwa kama ulikuwa unafatilia. Two problem fro two people of two different status are dealt differently!

Mimi binafsi sioni faida ya Chadema kujiunga na wasaliti wa wazi. Tuliyaona ya Rashid na Mbatia, what else do we need to see in order that we perceive? Sorry kama unawapenda Cuf but that is my stand, wasaliti!
 
Kabla Bunge halijaanza niliona CUF watakuwa watu wazurii sana kusaidiana na CHADEMA, lakin yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi wa Spika, Naibu Spika, Mwakilishi wa SADC, kauli ya Maalim Seif baada ya Chadema kutoka nje ya Bunge, na Hamad kukataa kukubaliana na ombi la Zitto achukue cheo cha Msaidizi wa Kambi ya Upinzani Bungeni utaona jinsi CUF walivyo hatari. Kwa sasa sioni haja ya CHADEMA kuungana na CUF & Co kwa sababu mambo mengi muhimu yameshapita na CUF hawakuonyesha ushirikiano wowote. CUF wanaangalia penye maslahi yao tu, sio wapiganaji wa kweli. Wanataka watumie mgongo wa CHADEMA kujiimarisha kisiasa baada ya kuona hakina sera zinazokubalika na wengi huku Bara
 
Mkuu nakubaliana na wewe lakini sioni sababu ya watu kuumiza vichwa vyao eti wanajf hawajui tafsiri ya neno "kambi isiyo rasmi" ?????? Mie siamini kama hamjui labda mmetoka kuamka.

Shossi mimi nimekuelewa vizuri! Lakin ukija ktk utekelezaji wake hakutakiwi iwepo, kwa maana ya kwamba wajiite hilo jina lakin asiwepo mtu wa kujiita MSEMAJI WA KAMBI ISIYO RASMI wala KATIBU WAKE. Kwa sababu wakishawepo hao watu maana yake ni KAMBI YA PILI YA UPINZANI hata wao waking'ang'ania watumie jina la KAMBI ISIYO RASMI. Tatizo la CUF ni kwamba hawataki kushuka kuwa chini ya CHADEMA kiuongozi ktk kambi ya upinzani, na isitoshe CUF priority ni maslahi yao zaidi, mengine ndo yanafuata baadae
 
Mohammedi Shossi, CUF haikuwa na akidi ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni peke yao kwenye bunge la 9. Wangeunganisha wabunge wengine wa upinzani nje ya Chadema bado akidi isingefika. They had no choice but work with Chadema.

Lakini sasa cuf imeolewa na ccm, ndoa ya kisheria na kiitikadi. Pia cuf imeshambulia Chadema waziwazi hadharani mara kadhaa.

Sasa hivi ombi la cuf kujiunga na Chadema bungeni ni la maslahi binafsi ya Hamadi Rashidi zaidi kuliko kulikomboa hili taifa. Ametoswa na chama chake. Wenzake wengi wamepewa ulaji serikalini yeye kabaki. Alizoea fungu la kambi ya upinzani bungeni sasa roho inamuuma.

Hivyo ni makosa kutumia reference za bunge lililopita kujenga hoja ya Chadema kukubali kufanya kazi na cuf
 
CUF wanataka waungane na CDM kwa masharti, kitu ambacho CDM hawakusema wakati CUF wana wabunge wengi. Waacheni CUF wabaki huko huko walipo, wakitaka kuungana na CDM yapaswa wawekewe masharti makali, maana tayari wameshaasi upinzani hadi ktk bunge la Muungano kwa kisingizio cha Serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Michelle habari za asubuhi bibie.... naomba nikuulize mbona wao walikubaliwa kufanya kazi na CUF wakati huo Chadema walikuwa na viti vichache na CUF ilikuwa na uwezo wa kuunda kambi peke yao? Tuwe balance tuache ushabiki wa vyama vyetu jamani swali hivi hapa JF kungekalika kweli kama CUF wangekuwa wanafanya wanayoyafanya Chadema dhidi ya wenzao si ndio wangebezwa CCM B hao wameshanunuliwa hao na kadha wa kadha? Nafikiri haya mambo yanahitaji kuyatazama kwa jicho la tatu...

Habari nzuri Shossi,naona umerudi salama!!

a)Nafikiri kuna tofauti zimejitokeza baina ya CHADEMA na CUF na NCCR na hata TLP kupelekea CHADEMA kuunda kambi yao wenyewe na hasa wakati na baada ya uchaguzi mkuu,pengine huko nyuma kulikuwa hamna grounds za CUF kuunda kambi yao wenyewe...

b) Jf pangekalika tu kama sababu zilizotolewa zinaridhisha wao kufanya hilo,ila ni kweli kabisa,yahitaji kuyaangalia haya mambo kwa jicho la tatu,hii ni siasa kaka,dirty game!
 
Hakuna sababu ya kuungana maana walionesha undumilakuwili tokea awali....wabadili kanuni kwa msaada wa mhisani wao ili watambulike km kambi rasmi! Vikao viwili tu vitatosha kutupa mwelekeo na lengo lao kwasasa
 
Back
Top Bottom