Spika aikataa kambi ya Hamad na Kafulila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika aikataa kambi ya Hamad na Kafulila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Jan 25, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,958
  Trophy Points: 280
  • Asema kanuni haziruhusu, awashauri waungane na Chadema


  SPIKA wa Bunge Anna Makinda amesema ni jambo lisilowezekana kuwepo na kambi zaidi ya moja ya upinzani bungeni.

  Makinda alisema hayo alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa gazeti hili aliyetaka kujua kanuni na sheria za Bunge kuhusu uundwaji wa kambi mbili za upinzani bungeni kama wanavyotaka kufanya wabunge wa Chama cha Wananchi wakishirikiana na wale wa NCCR-Mageuzi.

  Juzi aliyekuwa kiongozi wa Kambi ya Upinzani wakati wa Bunge la tisa Hamad Rashid (CUF) na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi), waliungana kuweka azimio la kutaka kuwepo na kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni kwa madai kuwa CHADEMA imejitenga nao.

  Akitoa ufafanuzi huo Dar es Salaam jana wakati wa semina ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Spika huyo alisema kambi ya upinzani inayotambuliwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge ni moja hivyo kuwa na kambi nyingine ni jambo lisilowezekana.

  Alisema utaratibu wa kuwa na kambi ya upinzani ni uwepo wa asilimia 12.5 ya wabunge wa upinzani bungeni ambao kwa mujibu wa kanuni za Bunge ndio wenye uwezo wa kuunda kambi hiyo.

  "Ni vizuri hivyo vyama wabunge wao wakakaa pamoja ili kuwa na kambi yenye nguvu kwa wapinzani wote… ili kuwa na kambi ya upinzani ni lazima upate asilimia 12.5 sasa CHADEMA wamefanikiwa katika hilo, kinachotakiwa ni kuridhia kwa jambo hilo," alisema Spika huyo.

  Aidha, alifafanua kwamba CHADEMA hawakukosea kuunda kambi ya upinzani lakini ni muhimu kuwa na kambi moja kama ilivyokuwa kwenye Bunge la tisa ambapo vyama vyote viliunda kambi moja yenye nguvu.

  "…Unajua kazi kubwa ya upinzani ni kuhakikisha wanaibana serikali katika utendaji hivyo kitendo cha kutokuwa na kambi moja kutawafanya wabunge wengine kushindwa kujua sehemu kuunga mkono hoja mbalimbali zinazowasilishwa bungeni," alisema.

  Wakati Spika Makinda akisema hayo, Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mrema alisema viongozi wa chama hicho walikuwa kwenye kikao jana kujadili suala hilo na kwamba watatoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari wakati wowote juma hili.

  "Kwa sasa hatuwezi kulizungumza jambo hilo maana siku nzima ya jana tulikuwa tukifanya kikao na kati ya tulichokuwa tukijadili ni pamoja na jambo hilo ambapo tunategemea kukutana na waandishi kwa ajili ya kueleza tulipofikia," alisema Mrema.

  My take: Kumbe Hamad alidokezwa juu ya jambo hili kuwa haiwezekani ndiyo maana sasa analazimisha kuungana na Chadema.
   
 2. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hamad mjanja mjanja sana huyu, si anatoka CCM eti? Waache wawakalibishe tu kuondoa mkanganyiko kwamba wametengwa ili wakiharibu wahalibu wao! Lakini CCM imekwisha watumia kwenye mambo muhimu sana kwenye ufunguzi wa bunge then sasa hivi inawatema, ikiwahitaji italikoroga tena sasa atakae linywa tunamtoa baruti
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Kwani CUF na NCCR Mageuzi ni vyama vya upinzani?mimi nakataa hivyo vyama ni CCM B
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Ni chama gani au vyama gani vimeunda serikali ya muungano?
  Kama una jibu la suali hili basi vyama ambavyo havijaunda serikali ni vyama vya upinzani.

  Ukirudi na hoja ,ya "ndoa" ya CCM na CUF Zanzibar, Zanzibar hawana bunge wana kitu kinaitwa baraza la wawakilishi na wanaoingia humo ni wawakilishi sio wabunge.

  Tunachanganya sana mambo haya na kuufanya upinzani uwe dhaifu. Kama upinzani wataungana ,at least, wataipeleka puta CCM lakini kwa chama kimoja tu, tutegemee nyundo ya CCM itatumaliza au itatutia kilema.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,958
  Trophy Points: 280
  Bora kilema cha nyundo kuliko kilema cha akili.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Kama CCM wangeona kuwa kuwa na kambi mbili bungeni kuna maslahi zaidi kwao, wangekimbilia kubadilisha kanuni kuruhusu hilo.

  CCM wanatumia huu msuguano na kutokuaminiana kwa vyama vya upinzani kama njia bora ya wao kukaa pembeni na kuchekelea upinzani wanavyohujumiana. Lakini pia wanajua kwa mazingira yaliyopo basi ni nafuu kwao kukishughulikia chama kimoja kimoja.
  Nafikiri upinzani walione hili.

  Makinda bila ya kujua pengine amewapa rai nzuri upinzani kuwa uungane ili nguvu yao iwe inaitoa serikali usingizini. Kwa CHADEMA kukataa ushauri huu basi watakuwa wamejiweka katika nafasi ya kukabiliana na CCM pekee na historia tokea 1995 inaonesha kuwa kila cha cha upinzani chenye nguvu kinapojitosa peke yake kupambana na CCM muhula unaofuata kinaibuka majeruhi.

  Vizuri juhudi zichukuliwe ku-heal majeraha na machungu ya uchaguzi na vyama vifanye kazi kwa kushirikiana. kwa uhalisia wa vyama vya upinzani TZ bado hakuna chama ambacho ni "king" mbele ya CCM.
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,958
  Trophy Points: 280
  Angekuwani spika wa Uingereza labda ningekubali kuwa ana nia nzuri na upinzani lakini huyuhuyu Makinda wa tanzania umesahau juzi alivyowabeza Chadema wakati anachaguliwa ndiye huyuhuyu anatoa ushauri, kwa mtu makini wala sihangaishi akili yangu kuelewa lengo lake.
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I hope chadema hawata fanya kosa katika kuwakubalia hawa watoto walio kataliwa
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Spika huyu mama nasubiri Bunge lianze nione atakavyokuwa mbabe
   
 10. M

  Marytina JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  spika makinda ameshazungumza na CUF+NCCR kuwa waende CDM ili waaribu na kuvujisha siri za kambi ya upinzani, hamna haja CDM kuungana na hao jamaa.
   
 11. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Itakuwa ngumu safari hii,manake huko upinzani watu sheria na kanuni wanazijua TF wanaweza mzidi experience anayojivunia......

  Mi nafikiri CHADEMA wawakubali hao NCCR,TLP,CUF,wakileta ujinga kuna vifungu vinaruhusu kuwaondoa kama ilivyokuwa kwa John Cheyo,tatizo ni kuwa hivi vyama haviaminiki,watu wana hila zao za kisiasa,i can understand CHADEMA hesitation to work with this guys but it worth trying working together.
   
 12. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hamad aache usanii hii nchi sasa hivi hakuna mtu mjinga,huwezi kuwa ndani ya serikali znz eti bara uwe mpinzani,huo ni uongo na unafiki
   
 13. M

  Marytina JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
   
 14. Taluma

  Taluma Senior Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ....Mike,

  Good point .....unafiki mtupu! Upande mmoja wa shilingi Hamad ni Serikali, upande wa pili anataka kuwa mpinzani wapi na wapi wandugu?
   
 15. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Hivi kunahitaji uwe na degree kuelewa maana ya " kambi ya upinzani isiyo rasmi" au mnataka tutumie nguvu nyingi kujadili mambo yasiyokuwa na tija wakati nchi inakabiliwa na matatizo lukuki??????? Waandishi wa habari wakibongo bwana!!! Agggrrrrr:disapointed:
   
 16. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160


  Marytina,nakubaliana na wewe bora kuwa na watu wachache wazalendo, ila si vibaya wakawapa nafasi,wakiharibu watolewe.

  Kuhusu suala la pili, Chama chenye wabunge wengi katika upinzani ndo huunda kambi ya upinzani,baada ya uchaguzi ndo hali imebadilika,miaka iliyopita CUF ndo walikuwa wengi na chini ya Uongozi wa Hamad Rashid kama mwenyekiti wa kambi ya Upinzani,CHADEMA walishirikishwa na si UDP tu kama ulivyosema,walishirikiana vizuri navyofikiri.
   
 17. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Michelle habari za asubuhi bibie.... naomba nikuulize mbona wao walikubaliwa kufanya kazi na CUF wakati huo Chadema walikuwa na viti vichache na CUF ilikuwa na uwezo wa kuunda kambi peke yao? Tuwe balance tuache ushabiki wa vyama vyetu jamani swali hivi hapa JF kungekalika kweli kama CUF wangekuwa wanafanya wanayoyafanya Chadema dhidi ya wenzao si ndio wangebezwa CCM B hao wameshanunuliwa hao na kadha wa kadha? Nafikiri haya mambo yanahitaji kuyatazama kwa jicho la tatu...
   
 18. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hata chadema wakiungana na Cuf na Nccr bado kwa idadi sisi em wataongoza. Kwa hiyo kuwakumbatia Cuf na Nccr haitawapa ushindi wa hoja kupita! Plus yaliyooneshwa na Cuf na Nccr ktk uchaguzi, siku ya walkout et al yanatupa true colors za hawa jamaa bila kusahau yale majadiliano ya Mbowe na Rashid!

  All I can say is, Chadema walivyo wanatosha kupambana peke yao, na wana watu makini tu. Kama Cuf au Nccr au wabunge wengine hawataunga mkono hoja za Chadema zenye maslahi kwa nchi simply kwa kuwa wamewanyima nafasi then sisi tutawaadhibu kwa kuwanyima kura kwa kuwa watakuwa hawajatuwakilisha.

  The bottom line, as I have always believe, ni kuwa Chadema kapiganeni vivyo mlivyo bungeni. Wananchi watajua tu kuwa wanahitaji kuongeza idadi ya wabung wa Chadema ili wajikomboe. Naomba msiingie mtego wa kuwakumbatia hawa jamaa wasaliti wenu. Kwanza hawajatubu kwa waliyowatendea!
   
 19. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Hamadi analilia fedha za kambi ya upinzani. Alinogewa
   
 20. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hiyo inaweza kua na ukweli.:kev::kev::kev::kev:
   
Loading...