Sperm Bank in Bongo

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
Nimekaa nikiwaza hili. Inakuwaje kama wawili wameoana halafu hawakubahatika kupata mtoto? Yawezekana tatizo likawa kwamke au mume ila mara kama tatizo ni la mwanamke basi mwanaume huruhusiwa kutafuta mwanamke wa kuzaa neo huko nje. Vile vile Kama tatizo ni la mwanamke basi hutokea mifarakano na hatimaye mwanamke kufukuzwa. Kama tatizo ni la mwanaume, huyo mwanaume ni nadra sana kumruhusu mwanamke kutafuta mwanaume wa kuzaa nae.

Katika muktadha huu ndipo nilipofikiria ishu ya sperm bank hapa bongo. Ipo? Hii ingesaidia ndoa nyingi sana kuendelea kudumu pale ambapo mwanaume amepatwa na ugumba.
Nawasilisha.
 
Hakuna tofauti sana kati ya kutumia donated sperm kutoka sperm bank na mwanaume kubambikizwa mtoto.
 
Hatuzungumzii kubambikizwa hapa bali njia halali wanazoweeza kutumia wanandoa kupata mtoto kama mmoja hana uzazi
 
Kenya ipo ila hapa TZ bado, si unajua hosipitali zetu siasa ni nyingi kuliko utalaamu. Mshikaji wangu alikwenda hospitali Nairobi na sasa wa mtoto wa mwaka mmoja na ushee na hakuna tatizo lolote kwenye familia kwani mshikaji ndiye mwenye tatizo. Hata familia yao wanajua na wamekubaliana na hali halisi.
 
Mhhhh! Msije kuwekewa mbegu bomu badala ya kutoka mtoto wa kimatumbi anatoka mtoto wa kihindi/kichina au kizungu inakuwa kizungumkuti kingine tena.
 
Kenya ipo ila hapa TZ bado, si unajua hosipitali zetu siasa ni nyingi kuliko utalaamu. Mshikaji wangu alikwenda hospitali Nairobi na sasa wa mtoto wa mwaka mmoja na ushee na hakuna tatizo lolote kwenye familia kwani mshikaji ndiye mwenye tatizo. Hata familia yao wanajua na wamekubaliana na hali halisi.

hakuna sababu ya kuwaambia ndugu. Mnamaliza wenyewe. Halafu ikianza bongo sijui watatumia criteria zipi
 
Bado tupo nyuma sana kwa hilo kutokea..benki za damu tu zinatushinda leo hii tuanze habari za sperm
Watu wenyewe kwanza afya mbovu,tabia ya kwenda kuangalia afya tu ni tatizo...sasa hizo zitakua sperm au matope
 
Mkuu sfm unakosea. Mbona yanazaliwa makinda yenye afya tu huko mahospitalini? Suala la udhibiti mbovu ndio nitakuunga mkono
 
Kuna mwana saikolojia mmoja alishawahi kusema, nature ya mtu pia hufuatana na afya aliyokua nayo mzazi wake..mfano,unapomuona mtu mbishi ama mkorofi kupita kiasi,na matatizo mengine ambayo huathiri ubongo kwa namna moja ama nyingine
Sikatai watoto wengi huzaliwa na afya nzuri,lakini ninachozungumzia ni ile afya ya saikolojia!
 
hivi kuna watu walioathirika kisaikolojia kama wazungu? They live in hell. We just dont know. Bado naamini tungekuwa na sperm banks ingepatikana michango bora kabisa ya mbegu. Siamini kama hao wadhibiti wangealika mradi mtu tu kuchangia. Lazima wangeangalia afya ya mwili na akili, umbo, uelewa etc. Tena wagumba wangepata mbegu bora sana
 
Mmmmmhhhh, kama siamini vilee!!!
 
Mie ninazo zinanielemea, ila sitaki kutoa kwa benki nataka kuzimimina LIVE KWA MHUSIKA, KM kuna aliyetayari tuwasiliane maana atapata vyote - RAHA NA MTOTO:msela:
 
Back
Top Bottom