Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Mada Maalum itakayozungumzia ziara nzima kwenye mchakato wa kampeni za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Agosti 27, 2025
Mwenyekiti wa INEC, Jaji Mstaafu Jacobs Mwambegele kwa mamlaka aliyopewa amemteua Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais kupitia CCM.
Pia soma > GE2025 - Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yawateua Samia na Nchimbi kugombea urais kwa tiketi ya CCM
Agosti 30, 2025, Dakawa, Mvomero, Morogoro
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema endapo Watanzania watakiunga mkono chama hicho, kitahakikisha kinaijenga Tanzania ambayo wananchi wanaitaka.
Dkt. Samia aliyasema haya wakati akizungumza na wakazi wa Mvomero katika Uwanja wa Dakawa Sokoine, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni za chama hicho.
"Jambo lingine tutajenga njia kubwa ya usafirishaji wa umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Morogoro kwenda Dumila, umeme ule utapita Mvomero na utawanufaisha Wanamvomero, uhakika wa umeme utakwenda kuwepo"
"Ndugu zangu, baada ya kusema hayo na mengine yatakayojitokeza tutakayoyatekeleza, niwaombe sasa tusimame pamoja na kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi ili tuendelee na kasi ya kuijenga Tanzania tunayoitaka,"
"Niwaombe sasa, tusimame pamoja na kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi ili tuendelee na kasi ya kuijenga Tanzania tunayoitaka. Tumesema ikifika 2050, Dira yetu inatuambia tuwe tumefika kwenye Tanzania tunayoitaka- Tanzania ya uchumi wa kipato cha kati lakini cha ngazi ya juu, Tanzania ambayo hakuna atakayelia na huduma za afya wala huduma za elimu wala atakayekosa maji bora na kukosa umeme wa kufanyia kazi zake na kumwangazia pahali alipo. Hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka, Tanzania ambayo uchumi wake utasimama na kujitegemea, Tanzania ambayo hatutaishi wala kufanya shughuli zetu za maendeleo kwa mikopo mikubwa, hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka, ifikapo mwaka 2050, safari yake inaanza miaka mitano inayokuja."
Kilosa
"Kwanza ninajua, bado kuna barabara ambazo zinataka kufanyiwa kazi, Barabara ya Kilosa- Ulaya-Mikumi, tumejenga sehemu, sehemu bado hatujajenga. Ninataka niwaambie miaka mitano ijayo tunakwenda kuifanyia kazi barabara hii. Lakini jingine ni kwamba kuna ushoroba ilikopita Reli ya SGR, ushoroba ule tunakwenda kuujenga viwanda na maghala ili uwe ushoroba wa biashara na kwa ilivyo bahati, ndani ya Wilaya ya Kilosa mna vituo viwili vya SGR kwahiyo jitayarisheni kwa fursa zilizoko kule, zile ni fursa za biashara na ninawaomba Wanakilosa mzitumie na msiwaache watu kutoka maeneo mengine kuja kuzitumia"