Special Thread: Hivi Mungu hakuwa na njia nyingine ya kutuondoa duniani zaidi ya kifo?

Hiyo ndiyo njia nyingine ya kwenda sayari nyingine.

Binadamu hawezi kuhamishwa akiwa anajitambua maana ni mbishi sana.

Fikiria leo dude linakuja kuwa upande uende sehemu nyingine utoke duniani uache chura, pombe, mali na vinginevyo utaenda kweli.

Acha tuhame bila usumbufu.
na akihamishwa huku anajitambua anaweza akatumia mbinu zake kutoroka na kurudi duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimesema Mungu hayupo,hii ni "Default position" kwa Mtu yoyote anayepinga uwepo wa kitu chochote
Lazima aseme hicho kitu "Hakipo" kwa sababu haoni namna yoyote ya hicho kitu kuwepo

Sasa wewe unayesema kitu fulani kipo,bila Shaka utakua unajua ni namna gani hichi kitu kinaweza thibitishika kuwa kipo

Kwahio wewe ndie unaepaswa kuthibitisha Kuwa Mungu yupo

Nithibitishie kuwa Mungu yupo?
Kisichokuwepo hakipo kwa muktadha gani?
 
Hapo ndipo utagundua kama mungu hayupo maana kila kilochokuwa na mwanzo kina mwisho

Hiyo ni sheria ya ulimwengu na kama mungu yupo nae ameshakufa hakuna kinachobaki milele
 
Mtoa mada unatuuliza sisi kwani sisi mungu ?? au huku JF kuna mungu atakujibu ??

Ok anyway , hata kama hauna akili basi jitahidi kujifanya una akili angalau .... Sio kuongea ongea pumba tu hapa .
 
Inabidi tuvumilie tu, maana kama kamtoa mwanawe pekee kufa msalabani kwa mateso, sisi ni nani, ila Yesu akiwa ndani yako kifo unakifurahia tu, maana unaenda kwa muumba wako, tatizo lipo kwa sisi wenye kuogelea kwenye maovu mara kuteka, kuua au kupoteza watu, utajiri w kafara, yaani kila siku unamuuzi Mungu na binadamu wenzako unafiri kifo utakionaje, na ndio yule jamaa alikuwa haendi kwenye misiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yesu ndo kifurugobe gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.

mkuu Muumba wetu anamakusudi yake hawezi kuruhusu mambo flani kwa sababu flani. mfano we unataka walio fariki waendelee na mawasiliano na walio hai,huoni itakua hatari zaidi sababu mchawi au gaidi waengendeleza uovu wao .nadhani leo kuna watu wangekuwa wa nawasiliana na osama awafundi ugadi...
 
Waislam nao wanafuata mpango wa biblia? umeamini vipi mpango wa biblia ndio bora kuliko mingine, tunarudi kule kule dini ni imani tu hazina uhakika wowote hata mapokeo yake ni imani tu, walioandika vitabu vya dini ni watu kama wewe.
nani kakwambia kama waislam wanafuata mpango wa biblia na wakati sisi tuna kitabu chetu kilichosheheni maono yenye ukweli na busara na ata tukifuata sisi hatuitambui kama ni biblia sisi tunaitambua kua ni injili ya mtume wa mungu issa a.s
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.
Nani anakuambia sisi tunakufa, Mwili ndio unakufa, kama vile unavyotupa nguo iliyochakaa ndio unavyovua mwili ulioshindwa kuishi na wewe. Ni ujinga kudhani sisi ni mwili, mwili huanzishwa na mbegu ya baba na yai la mama, Roho ambayo imeumbwa kwa mfano wa mungu ambayo ndio wewe inaingia mwilini. Roho kama alivyo mungu haionekani, lakini ndio inayoupa uhai mwili wako, kwa maana hiyo wewe ndio unajukumu la kuujenga na kuutunza mwili wako. Roho inahitaji kitu fulani Duniani, lakini hisia 10 zilizo mwilini zinapumbaza Roho na kujisahau, na kujazwa ujinga (Ignorant) inashindwa kujitambua kuwa inapaswa kuutumia kuutumia mwili kufikia malengo yake, badala yake inatekeleza malengo kwa mahitaji ya Mwili na Akiri, kwani inajiona iko tofauti na viumbe wengine, kwa nafasi na wakati iliopo, inajenga ubinafsi, uchoyo unayozaa chuki, inakuwa na tamaa ya kumiliki mali, vitu, na watu wengine. Siku ya kuachana na mwili yaani siku mwili unapokufa, Roho inajua ukweli ni nini ilikuwa madhumuni ya Roho kwenye ule mwili inaotengana nao, inajikuta tumepoteza muda adimu sana na hivyo inajuta. Kifo ni shift of conciousness from physical level of conciousness to higher level where there is no forms, apart of internal guilt concious ambayo inakulazimu kutafuta mwili kwenye huu ulimwengu wa birth control. Dhambi ni tendo lolote ulifanyalo kinyume na kufanikisha madhumuni ya uwepo wako mwilini, hata ukitoa sadaka iliuweze kuneemeka zaidi na maisha duniani utakuwa unafanya dhambi tuu like wise unaweza fanya ukatili lakini if saves the purpose of life ni thawabu. So ili ujue unatenda thawabu au dhambi ni lazima kujua why you in your body? To do what?.
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.

Vipi kuhusu njia ya namna tunavyozaliwa, je yenyewe hauna tatizo nayo?
 
Watu wangejaa huko sayari nyingine na kudondoka kurud tena dunia kungekua na mvua ya watu kwa msimu kama wangejaa huko sayarini
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.
Mila zingine ni sherehe.
 
Back
Top Bottom