Special Thread: Hivi Mungu hakuwa na njia nyingine ya kutuondoa duniani zaidi ya kifo?

Ni hivi, wewe ni kiumbe wake, kabla haujafikiri au kupata utambuzi tayari yeye anajua kipi kitakachotokea, sasa wewe unabahatisha haujui hatma yako, yeye anajua nini kilichopo mbele kwa uhakika. Sasa katika mazingira hayo unashauri nini? embu jitafakari
Kama tayari anajua kitakachotokea hata nikiomba hakibadilishi kitu, kuna tofauti gani na asiyeomba.
 
Kama tayari anajua kitakachotokea hata nikiomba hakibadilishi kitu, kuna tofauti gani na asiyeomba.
Mkuu sisi ni viumbe dhaifu sana, tuna limitations kwenye tambuzi, fahamu na uwezo wetu, ukishajua hilo usitake kufikiria mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Ni hivi hapa duniani tukiishi sana ni miaka 100-110 kwanini hatuwezi kwenda 200?

Kuna mtu aliyetuumba ameamua hivyo na hatuna uwezo, mpaka sasa kwenda beyond that pamoja na sayansi na technology yote iliyopo. Ni limitation tu.

Nije kwenye hoja yako, ni kweli anajua hatma zetu, je kwanini uombe au usiombe? hilo linabaki kwenye utashi wako, haulazimishwi. Wapo watu waliomba wakafanikiwa na wapo walioomba hawakufanikiwa, Mungu ndiye muweza wa yote, anatupa tunachostahili na siyo tunachohitaji.
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.
Mwanadamu ni mavumbi na mavumbini atarudi.
Kuna ulimwengu wa roho na huu Wa mwili ili kuonyesha kuwa ukifa hauendi sayari yoyote bali lazima urudi kwenye chanzo cha uhai wako na kile chanzo cha mwili wako yaani pumzi ya uhai irudi kwa Mungu(ulimwengu Wa roho) ili afanye maamuzi kuwa roho yako ikae salama au la!
Na mwili kurudia chanzo chake yaani mavumbini
 
Mimi naamini kwamba mungu yupo ila tatizo Ni kwamba yawezekana habar zake zimepindishwa Kama ilivopindishwa habari ya idd Amin dada na yule jamaa wa zanzibar(okello)
 
Mungu Hayupo
Mbingu Haipo
Kuzimu Hakupo

Kila kitu ni Maada
Na kifo ni Mfumo wa Asili,Unao hakikisha kuwa Kiumbe pekee kinachoweza kumudu mazingira yake ndio kinachopaswa kuishi

Pale tu Mfumo wako wa Mwili unapoanza kupata hitilafu na Kushindwa Kumudu Mazingira yanayokuzunguka Mfumo huu unakuondoa

Wasayansi wanauita Natural selection
"Survival for the fitness"

So next time mtu anakataa roho,jua Mfumo huu umemuondoa cause hawezi Tena Kimudu Mazingira yake
 
Hakuna njia nyngne zaidi ya hayo.ndyo mana alimtuma mwanae pekee kuikomboa dunia.john 3;14.
 
kabla hujaomba option hiyo ya kutoruhusu kuzaliana kwa watu ili kumaintain populationn basi unatakiwa kufahamu kuwa wewe ni product ya kizazi kilichopewa nafasi ya kuzaliana na kama option unayoitaka ingekuwepo basi kizazi kilichokuzaa kingekuwa na nafasi ya kuishi milele bila ujio wako kufikilika na nafsi yako haingekuwepo tena ..

So the universe offers life kwa njia ambayo inaruhusu kila soul tofauti tofauti ziweze kusavaivu na kupita from one era to another...

kama ungekuwepo uchaguzi wa kutozaa basi wewe uliyeandika hii thread usingekuwepo...

Ukikaa ukifikilia utangua kuwa ili wewe uwepo hapa duniani na uanticipate maisha ni lazima kuna watu wamerisk maisha kwa ujio wako...

nafsi yako kuwepo hai ni kwa sababu baba na mama wa babu na bibi wa baba na mama yako walipewa option ya kufanya hivo unless unsingekuwepo...so we are the product of the allowed species to interbreed unless we re nothing at ol...ukiambiwa kuwa pumzi yako ipo mikononi mwa watu usikatae coz ujio wako ni maamuzi ya watu ambao waliamua wewe utokee...

So we die to signify that you were brought here by other's opinion to undergone multiplicity of their souls...

Na kudhihilisha hilo kuwa your presence ni kwa ajili ya mapendekezo ya wengine you have to die and perish away kukuonesha kuwa uhai wako umetokana na matakwa ya watu fulani na sio wewe...

Death is mandatory...

Sent using Nokia 8 Plus
 
1. Hiyo Dunia nyingine anakotupeleka, huu mwili hautakiwi, kifo ni njia muafaka wa kuuacha huu mwili ambao haudumu milele.
2. Kifo sio kibaya ni kizuri sana, sema kwa mtu aliye bado na nguvu kifo ni kibaya, na mara nyingi kifo kinakuja ktk umri huo kwa bahati mbaya tu, yaani binadamu kukosa marifa ya kuepusha kifo cha ujanani, mfano vifo vya ajari.
3. Kifo ni kizuri sana kwa binadamu mzee sana na aliyeishiwa nguvu. Kifo humpeleka kwenye maisha mengine yenye nguvu imara kabisa.
Hivyo njia ya kutuondoa hapa duniani kwa Kifo, ni njia bora sana kupita nyingine.
Henoko pekee ndiye aliyeweza kiondoka duniani kwa kutwaliwa akiwa bado ana nguvu zake imara.
Ila ukiambiwa na wewe utwaliwe leo kama Henoko utakataa katakata na kusema bado unataka kuishi duniani.
Hivyo tusubiri tufe wakati wa uzee na kama itakuwa bahati mbaya basi tunaweza ondoka mda wowote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo huwa ni maneno ya kujifariji tu, hata biblia yenyewe imeandikwa hivyo farijianeni, ila hakuna mwenye uhakika mtu akifa anakuwa na hali gani.

Kila dini na mpango wake waislam, wabudha hawatumii mipango ya Yesu.
Hakuna mpango mwingine nje ya Bibilia unaoweza kumsaidia mwanadamu na maisha yake.Mpango wa Yesu ndio mwisho. kufarijiana haimaanishi hakuna uhakika. hiyo ni tafsiri yako duni.
 
Varangati lake Mkuu acha kabisa! Hebu fikiria mpendwa kama Baba wa Taifa jinsi Watanzania tungepambana nalo hadi kulishinda! Acha kabisa Mkuu.

Hiyo ndiyo njia nyingine ya kwenda sayari nyingine.

Binadamu hawezi kuhamishwa akiwa anajitambua maana ni mbishi sana.

Fikiria leo dude linakuja kuwa upande uende sehemu nyingine utoke duniani uache chura, pombe, mali na vinginevyo utaenda kweli.

Acha tuhame bila usumbufu.
 
Nimefikiria sana mateso wanayopata wafiwa pindi wapenzi wao wanapofariki, hubaki na majonzi kwa muda mrefu wakikumbuka enzi za uhai wake, kuna baadhi kutokana na ukaribu waliokuwa na marehemu nao humfuata baada ya muda mfupi.

Sipingi wala sikosoi mipango ya Mungu lkn, najiuliza hivi hakuwa na njia nyingine mbadala ya kutuondoa bila kuacha alama na kutuacha na majonzi kiasi hiki.

Kwa mfano, badala ya kufa na kuonekana unazikwa angetuhamisha na kutupeleka sayari nyingine aliyowaandalia 'wafu' (siyo mbinguni) lkn tukabaki tunawasiliana nao kwa njia yeyote ile, tukacheka nao wakatushauri tuliobaki, labda tu angetuwekea kikomo fulani cha mawasiliano tofauti na wakati walipokuwa bado hai.

Tujadili.
.
Haya majonzi yametengenezwa na wanadamu wenyewe.

Unadhami waumini wa dini zinazofundisha juu ya Reincarnation - Wikipedia wanapata mateso haya?

Wapi?
 
Mkuu sisi ni viumbe dhaifu sana, tuna limitations kwenye tambuzi, fahamu na uwezo wetu, ukishajua hilo usitake kufikiria mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Ni hivi hapa duniani tukiishi sana ni miaka 100-110 kwanini hatuwezi kwenda 200?

Kuna mtu aliyetuumba ameamua hivyo na hatuna uwezo, mpaka sasa kwenda beyond that pamoja na sayansi na technology yote iliyopo. Ni limitation tu.

Nije kwenye hoja yako, ni kweli anajua hatma zetu, je kwanini uombe au usiombe? hilo linabaki kwenye utashi wako, haulazimishwi. Wapo watu waliomba wakafanikiwa na wapo walioomba hawakufanikiwa, Mungu ndiye muweza wa yote, anatupa tunachostahili na siyo tunachohitaji.
Kwa mujibu wa biblia Mungu anakujua hata kabla ya kuumbwa kwa dunia, ameshakupangia kila kitu huwezi kubadilisha mpango wake kwako kwa maombi.
 
Hakuna mpango mwingine nje ya Bibilia unaoweza kumsaidia mwanadamu na maisha yake.Mpango wa Yesu ndio mwisho. kufarijiana haimaanishi hakuna uhakika. hiyo ni tafsiri yako duni.
Waislam nao wanafuata mpango wa biblia? umeamini vipi mpango wa biblia ndio bora kuliko mingine, tunarudi kule kule dini ni imani tu hazina uhakika wowote hata mapokeo yake ni imani tu, walioandika vitabu vya dini ni watu kama wewe.
 
Inabidi tuvumilie tu, maana kama kamtoa mwanawe pekee kufa msalabani kwa mateso, sisi ni nani, ila Yesu akiwa ndani yako kifo unakifurahia tu, maana unaenda kwa muumba wako, tatizo lipo kwa sisi wenye kuogelea kwenye maovu mara kuteka, kuua au kupoteza watu, utajiri w kafara, yaani kila siku unamuuzi Mungu na binadamu wenzako unafiri kifo utakionaje, na ndio yule jamaa alikuwa haendi kwenye misiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila hivi vitu sometimes seems like mythical, sipingani na dini, ila kama Mungu aliamua kumtoa mwanawe wa pekee, kwanini huyo mtoto asingepambana na Shetani akapambana na dhambi, badala ya yeye kutundikwa msalabani, yeye angetumia uwezo wake wa kiungu kumtundika shetani msalabani akajifia apo, no shetani=no dhambi, kwisha habari.
 
Ndio hivyo kifo akiepukiki,inabidi tu kuwa mzalendo ili wadudu wa ardhini wapate chakula,kama sisi tunavyokula kuku,samaki,ng'ombe,mbuzi n.k na kuwasababishia majonzi hao wanyama.'Mla mwenziye naye uliwa'
 
Uthibitisho wako ni upi juu ya hiyo kauli yako?
Mimi nimesema Mungu hayupo,hii ni "Default position" kwa Mtu yoyote anayepinga uwepo wa kitu chochote
Lazima aseme hicho kitu "Hakipo" kwa sababu haoni namna yoyote ya hicho kitu kuwepo

Sasa wewe unayesema kitu fulani kipo,bila Shaka utakua unajua ni namna gani hichi kitu kinaweza thibitishika kuwa kipo

Kwahio wewe ndie unaepaswa kuthibitisha Kuwa Mungu yupo

Nithibitishie kuwa Mungu yupo?
 
Back
Top Bottom