Special thread ya visa,mikasa na matukio ambayo hatutasahau.

Special thread ya visa,mikasa na matukio ambayo hatutasahau.

1gb

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
2,395
Reaction score
3,298
Habari wana jf.
Lengo kuu la thread hii ni kusimuliana Visa,mikasa na Matukio ya KWELI KABISA,Ambayo hutakuja kuyasahau kwa kipindi cha maisha yako yalio salia.haijalishi story yako ni ndefu/fupi na pia unaweza ukaiandika kwa kirefu au kwa kifupi.Dhumuni ni kujifunza kutoka kwa wenzetu kuwa alipokosea yeye basi na wewe usikosee kupitia somo utakalo lielewa kulingana na Utashi wako.Haya karibuni Kumbuka story iwe kweli imekutokea wewe/ndugu,jamaa na marafiki lakini unauhakika ilimtokea na sio ulisimuliwa
Nitaanza na mimi.
Sitasahau siku ambayo dada yangu,alipo nusurika kifo,baada ya kunywa sumu alipo gundulika anatembea na mume wa Dada ake yaani shemeji yake.
Ni story ya kweli ambayo dada yangu aliisababishia familiya yetu aibu ya miaka kadhaa na kuonekana familia yetu ya ajabu kwelikweli.Dada yangu huyu ni mtoto wa 8 katika familia ya watoto 9.Anaitwa Stela(sii jina halisi) ndiye aliye niachia ziwa,yaani baada ya yeye kuzaliwa ndo nikafuaata mimi.
Kipindi hicho mimi nilikuwa na miaka 14 nikiwa darasa la 6.Mama yangu mzazi alisafiri na kwenda kumtembelea kaka yetu ambae alikuwa anaishi Tabora,na baba yetu akahama nyumbani na kwenda kuishi kwa mama mwingine(nyumba ndogo) ambae walizaa nae miaka kumi 16 iliyopita,Mara tuu mama alipokwenda kwa kaka yetu baba nae akatoweka nyumbani,Hapo ndipo vimbwanga vilpo anzia.Pale nyumabni tukabaki Huru kabisa.Tulibaki watatu tuu ndani ya nyumba.nikiwemo Mimi,Stela na mtoto wa ma mdogo kipindi hicho akiwa na miaka 8.dada na Kakazangu wakiwa na maisha yao majumbani mwao, Stela kwa kipindi hicho alikuwa msichana mzuri,sista duu kweli kweli tena alikuwa single.Shemeji yangu ntamwita Kitombii(sii jina halisi) alikuwa anaishi mbali na sisi. Alikuwa anaishi na dada yangu ambae ni watano kuzaliwa anaitwa Enea(sio jina halisi).
Kitombii na Enea walikuwa wanaishi kwa ndoa halali na walikuwa na watoto wawili.
Kitombii na Enea walikuwa wanakaa mbali kidogo na sisi,naweza kufananisha (sisi Kawe,Dar na wao(kitombii&Enea)walikuwa wanaishi Kibaha,Pwani)
Kitombii alikuwa na biashara zake huku kawe kwa hivyo safari zake zilikuwa ni za mara kwa mara,ilikuwa haipiti siku tatu bila kuja kutujulia hali na kufuata masuala yake ya biashara na jioni kurudi Kibaha.
Basi maisha yaliendele vizuri,ghafla Stela akaanza kuplan biashara na ndoo kwanza alikuwa amemaliza form four akiwa na miaka 19,mwishowe akapata muafaka wa kufungua biashara ya Restaurant.Kiukweli binafsi nilifurahia biashara aliyokuwa anaifanya dada angu,kwa furaha kubwa kila nilipokuwa nikitoka shule hata chumbani kwangu siingii,napitia kwa Stela Restaurant,napata chochote na kurudi nyumbani,Safari za kitombii sasa ikawa haziishi kuja Nyumbani,na kwenda kumwona Stela kazini kwake(Stela Restaurant)kitombii ikafika wakati akawa harudi kuiona familia yake Kibaha,Stela akazidi kupendeza,akanawili vyema,wataalamu wa mambo watu wazima wakaanza kuhisi jambo,Nikiwa mwanafunzi,sielewi kitu na akili haijakomaa nilikuwa sielewi mambo ya wakubwa,Ndipo siku moja tukakorofishana na mwanafunzi mwenzangu (msichana) nikampiga sana,kama ilivyo kawaida ya wasichana matusi,basi nikatukanwa mfululu mpaka nikapatwa na aibu na neno baya nililolinasa kupitia matusi yale ni kuwa 'malaya sana nyie,na ndoo maana dadaako anatembea na mme wa dada aake(yaani Stela natembea na Kitombii).Kiukweli nilipatwa na aibu na ubabe woote ukaniisha,nikabaki mkimya,Siku nzima sikuwa na furaha kabisa. Sasa ENDELEA......
Siku hiyo nilirudi nyumbani nikiwa mnyonge,na sikutaka kumuhusisha/kuumuuliza mtu yeyote kuhusiana na habari nilizipata shuleni,siku,wiki zilipita ndipo siku moja nikiwa najianda kuamka ili niende shule,mida ya saa 11 ndipo nikasikia mlango wa sebuleni ukigongwa,Sikutaka kuamka na kwenda kumfungulia huyu mgeni badelea kuskizliendelea kuskiza kinachoendelea hapo sebuleni,niliskia mlango wa Chumbani kwa Stela ukifunguliwa,ndpo nilipoweza kuifahamu sauti ya mgenia aliyekuwa akigonga,Hakuwa mwingine bali ni rafiki yake Kitombii aitwae Mapinduzi,Mapinduzi alimuuliza Stela kama kitombii alilala hapa nyumbani kwetu?Stela alikanusha katakata kuwa kitombiii hakufika tangu jana usiku walipo achana pale resturant na wala hajalala kwetu.Mapinduzi aliondoka,nikiwa nimetega maskio alfajiri hiyo,kwa mara ya kwanza niliweza kupatwa na mshangao baada ya kuskia minong'ono ya Esta akimweleza Kitombii alikuwa anatafutwa na mapinduzi,Sikuweza kuelewa upande wapili unasema nini kutokana na sauti ya kitombii kuwa nzito yenye kukoroma na ya chini sana kwahivyo sikuweza kumwelewa lkn nilitambuwa kuwa ni sauti ya Kitombii,kwa kweli nilijisikia Vibaya sana,nilipatwa na hasira na hapohapo nikakumbuka kauli ya yule msichana tuliekorofishana nae wiki chache zilizopita.Nikiwa bado natafakari yaliyotokea punde,Nikaskia mlango ukigongwa kwa mara nyingine tena..Itaendelea.Mwana jf kama umelipenda wazo langu na hii thread ibaki kuwa endelevu,basi Changia lolote/gonga like tulisongeshe.
 
1gb umesomeka na kwangu Mi naunga hoja mkono.

Ngoja wadau wa jukwaa waje!
 
Last edited by a moderator:
Kisa kizuri,endelea nacho mkuu.
CC CHAI CHUNGU

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
ukimalizia nitakuja na yangu.cc liverpoolfc sikuiz unalinga na ka id kako et unaongoza lig ngoja ukutane na joseee
 
Sitakuja sahau siku ya leo nilipokua sokoine uwanja wa mpira mbeya mechi ya mbeya city na yanga,. Refa alipokataa goli halali la yanga na kunifanya niichukie sn soka la bongo,. Hajifi kutokanuaga tena viwanja vya mpira vya bongo
 
Sitakuja sahau siku ya leo nilipokua sokoine uwanja wa mpira mbeya mechi ya mbeya city na yanga,. Refa alipokataa goli halali la yanga na kunifanya niichukie sn soka la bongo,. Hajifi kutokanuaga tena viwanja vya mpira vya bongo
Safi sana wee ni mwelewa,manake umelielewa somo kikamilifu na ndoo maana hujaleta mbwembwe nyingi jukwaani.Pole kwa kulipenda soka la Bongo,ijapokuwa uzalendo ni muhimu.
 
Stak na siji liludia tena soka bongo unanaishaji tupu ila ntabaki kuipenda yanga
Safi sana wee ni mwelewa,manake umelielewa somo kikamilifu na ndoo maana hujaleta mbwembwe nyingi jukwaani.Pole kwa kulipenda soka la Bongo,ijapokuwa uzalendo ni muhimu.
 
Back
Top Bottom