Special Thread: CECAFA Senior Challenge Cup 2013

Special Thread: CECAFA Senior Challenge Cup 2013

Rwanda katolewa rasmi ktk mashindano!!! kapigwa 1 na Sudan..Now Uganda v Eritrea. Okwi, kiiza ndani.

Mchezaji bora wa mwanaspoti kashindwa kuisaidia timu yake ya Taifa?
 
Mchezaji bora wa mwanaspoti kashindwa kuisaidia timu yake ya Taifa?

Hata George Opong Weah alikuwa mchezaji bora wa dunia huku timu yake ya Liberia ikishindwa kufurukuta hata mbele ya Taifa Stars; Sembuse Niyonzima! Mkuu Masuke huu ukweli unaufahamu, kinachokusumbua ni usimbasimba tu.
 
Last edited by a moderator:
Dk 35

Emmanuel Okwi anaipatia Uganda bao la tatu...

Eritrea 0 - 3 Uganda
 
Dk 45 HT

Eritrea 0 - 3 Uganda
 
Hata George Opong Weah alikuwa mchezaji bora wa dunia huku timu yake ya Liberia ikishindwa kufurukuta hata mbele ya Taifa Stars; Sembuse Niyonzima! Mkuu Masuke huu ukweli unaufahamu, kinachokusumbua ni usimbasimba tu.
Mkuu mimi nilikuwa nauliza tu, lakini angalau George Weah unaweza sema kwamba aliokuwa anacheza nao kwenye klabu angalau walipokuwa kwenye timu zao za Taifa walikuwa wanafanya vizuri pia lakini huyu mchezaji bora wa mwanaspoti hata wale anaocheza nao kwenye klabu yake wawapo timu ya Taifa wanambwelambwela tu hadi Somalia kawatoa jasho, hapo lazima kuwe na maswali kwa nini wakikutana kwenye klabu wanaonekana ni bora hadi mwanaspoti anawatuza.

Kuna mawili ama Tanzania ligi yetu ni dhaifu kama nilivyowahi kusema mwezi mmoja uliopita au bahasha hutembea ili timu yao ya klabu inufaike na hatimaye wachezaji wake kuonekana ni wazuri hadi huchaguliwa timu zao za Taifa lakini ubora wao unashindwa kuonekana.
 
Last edited by a moderator:
Dk 55

Eritrea 0 - 3 Uganda
 
Mkuu Masuke tatizo la TZ ni strikers hebu angalia timu iliyocheza na Somalia nani alikuwa Ace Striker? Hakuna pale mbele waliwekwa viungo akina Kiemba na Ngassa, hivyo timu inapocheza bila strikers unategemea magoli yatoke wapi? Niyonzima naye ni kiungo siyo striker, unategemea afanye nini? Yanga hakuna rushwa; Simba na Azam ndio zao.
 
Last edited by a moderator:
Dk 72

Eritrea 0 - 3 Uganda
 
Hivi yule ngongoti wa Simba toka Uganda mbona hadakii Cranes na Amisi Mapenati mbona haonekani katika timu ya Intamba Murugamba? Masuke, tiririka Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Dk 80

Eritrea 0 - 3 Uganda
 
Dk 90 FT

Eritrea 0 - 3 Uganda
 
Mkuu Masuke tatizo la TZ ni strikers hebu angalia timu iliyocheza na Somalia nani alikuwa Ace Striker? Hakuna pale mbele waliwekwa viungo akina Kiemba na Ngassa, hivyo timu inapocheza bila strikers unategemea magoli yatoke wapi? Niyonzima naye ni kiungo siyo striker, unategemea afanye nini? Yanga hakuna rushwa; Simba na Azam ndio zao.

Utetezi wako wa kwamba tatizo la timu ya Tanzania ni striker hauna nguvu sana kwa sababu kikosi kilichoko Kenya kina Elias Maguli ambaye nadhani ana magoli tisa kwenye ligi, kuna yule bwana mdogo wa Mtibwa Luizio naye ana magoli zaidi ya sita kwenye ligi, kuna Mrisho Ngasa ambaye kwenye timu yake huchezeshwa kama second striker ana magoli matano kwenye ligi sasa wote hao hakuna anayefulukuta kule, anyway labda mfumo wa mwalimu ni tofauti na kwenye vilabu.

Tarehe moja Novemba nilitoa angalizo lakini watu wakaniona naendekeza Usimba wangu.
Masuke commented on Yanga Vs JKT Ruvu said:
Kwa kweli Tanzania hatuna timu za maana (Yanga pamoja na kuongoza magoli matatu wanabutua butua tu na wengi wako timu ya Taifa halafu wanawakilisha nchi kwenye ligi ya mabingwa) sasa najua kwa nini Taifa star haifanyi vizuri na hata mashindano ya CAF vilabu vyetu havifanyi vizuri, Asante Azam TV kutuonyesha uozo wa ligi yetu.
 
Hivi yule ngongoti wa Simba toka Uganda mbona hadakii Cranes na Amisi Mapenati mbona haonekani katika timu ya Intamba Murugamba? Masuke, tiririka Mkuu.

Kuhusu Ngongoti nadhani atakuwa ameachwa ila kuhusu Amisi Tambwe Mapenati hajaitwa kwa sababu Burundi wanataka watumie wachezaji wao wa ndani ili kujiandaa na mashindano ya CHAN ndo maana hata mshambuliaji wenu hajaitwa.
 
Back
Top Bottom