Special kwa wana CDM na wana Igunga tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Special kwa wana CDM na wana Igunga tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Aug 16, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,035
  Trophy Points: 280
  Muhimu: Nani kati ya hawa unamwona anafaa kupeperusha bendera yetu Igunga toa pia sababu.

  1. Kajua Sebastiani 2. Marco Amos 3. Kahema John, 4. Buzinza Magego, 5. Dickson Samsoni, 6. Anwari Luhumbi, 7. Erasto Tumbo, 8. Joseph Mwandu, 9. Juma Katigula, 10.Frank Matto, 11.Joseph Mapalala 12.Juma Chaha.

  Pamoja Tutaweza, Nimerudi kuwashika............mapambano ndiyo yanaanza..... People's Power.

   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna hata mmoja kwani yeyote kati yao akisimamishwa akakutana na mgombea wa chama dume atashindwa vibaya
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna hata mmoja kwani yeyote atakae kutanishwa na chama dume atashindwa vibaya. Sidhani hata km 10% ya kura atapata
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mgombea wa kambi ya upinzani Igunga awe ni mmoja tu. Ni kivipi mgombea huyo apatikane; viongozi watusaidie kuratibu hilo.
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mkuu tunaomba utusaidie CV zao ili tuongeze uwanja wa kutoa maoni yetu!!
   
 6. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tulizoeya kusikia ccm wamejitokeza wagombea wengi sasa imekuwa na cdm kazi hipo.mpaka sasa 12ccm na 15cdm
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,080
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni ishara tosha kwamba Chama kinakua kwa kasi ya kutisha na wananchi wanakuwa na imani kubwa nacho. Ni dalili njema kwa upinzani na ukuaji wa demokrasia kwa ujumla japo ndio hivyo tena vikwazo havikosekani.
   
 8. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  CCM si chama dume tena kishakuwa dumejike!
   
 9. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hapa nafikiri atakuwa Erasto Tumbo ana uzoefu.
   
 10. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu,hujatueleza vema kama ndio waliochukua fomu ama wewe ndio unawapendekeza?
  Yote kwa yote tunaomba CV zao.
  Huyu Frank Matto, (kama ni yule yule ninayemfahamu wa Igunga)...ni mzaliwa wa pale,(wazazi wake wana asili ya Mkoa wa Mara, lakini wamefanya kazi miaka mingi sana hapo Igunga).Amesomea shule ya msingi hapo Igunga na masomo ya Sekondari (Kidato cha kwanza hadi cha nne) kafanyia Sekondari ya Umoja-Tabora. Kidato cha tano na sita kasoma Mpwapwa-Dodoma (huko ndiko nilipomfahamu). Alikuwa waziri wa Afya shuleni hapo. Na pia alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa wanafunzi wasabato shuleni hapo. Amefanya shahada ya kwanza ya elimu jamii (Sociology) na kuhitimu mwaka 2008-UDSM.Ni kijana wa miaka kati ya 27-31 hivi. Sikuwahi kusikia 'scandal' katika huo uongozi wake ambao nimeutaja.Kisiasa,sikuwahi kutambua yuko 'mrengo' gani haswa.Sifahamu kwa sasa anajishughulisha na nini.
   
 11. p

  plawala JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakiwezi kuzalisha wala kuzaa tena
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Umeambiwa hii ni kwa wana CDM tu na watu wa Igunga. You are none of the above. So split.
   
 13. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Hayo ndo mabadiliko na ukuaji wa democracy. Adui mkubwa kwa watanzania sasa ni kauli kama aliyoitoa Nchimbi juzi wakati akihitimisha bajeti ya wizara yake alisema eti UZALENDO NI KUIPENDA CCM! Hiyo ni kauli ya kuipiga vita kwani wananchi wanaweza danganyika kwa matamshi ya kijinga kama hayo.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Quinine,
  Labda nikupe Kiungo kikubwa cha kumpata mgombea mzuri kati ya hao.
  Kwanza waite wagombea wote kisha wape karatasi ambayo kila mmoja wao ataandika jina moja la mgombea ambalo kama siii yeye atachaguliwa basi anapendekeza jina hilo!.. Jina moja tu.. Nina hakika lipo jina litakalokuwa na kura nyingi hivyo wagombea wenyewe wanampitisha.

  Hilo kwanza pili, ni muhimu sana kumpata mtu ambaye nin mwenyeji Aluwatan na mwenye kufahamika kwa vijana wa kizazi kipya na anaweza kuwakilisha hoja nzito za wana Igunga. Hii njia ya pili ni kwenda Igunga kwenyewe mapema na kuuza majina haya kabla.. Hapo ni rahisi sana kusikia vijiweni nani anauzika kwa sababu Hapa JF woote kina sisi tunaishi mbali na Igunga wengine hata hawajui Igunga iko wapi mkoani Tabora.

  Tatu, Ilani ya chama ktk uchaguzi huu mdogo lazima ukite penye donda!..Ardhi na Madini kama mtaji wa wananchi ni lazima ziwe sababu kubwa ya kampeni ktk kurudisha utajiri wa jimbo hilo mikononi mwa wananchi. Ardhi imeporwa na Kilimo cha kahawa kimekosa incentives kama zamani enzi za mwalimu ktk umwagiliaji na madawa..Ajira kwa wananchi iwe ndio mbiu ya chama. Kwa kila hoja nzito inayowakabiri wanaIgunga ndipo mnapotakiwa kugonga msumari kama ilani ya chama. Na bila shaka kwa Umaarufu wa CDM sasa hivi mtawapa mtihani mkubwa wana Igunga na pengine nasema tena PENGINE Chadema inaweza kushinda..
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  yeyote atakayepitishwa na cdm ndiye mbunge mteule wa igunga na baadae ataapishwa kuwa mbunge
   
 16. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,035
  Trophy Points: 280
  Shukrani mkuu Mkandara

  Njia yako ya pili ya kumpata mwenyeji ndiyo hasa ikifuatwa si tu na CDM bali na chama chochote inaweza kukipatia ushindi, kuhusu Ilani ni njia nzuri kwa watu walio na uelewa hasa kwa nchi zinazofuata utawala wa sheria kuwa distribution ya resources ni ya usawa hata kwa majimbo ya wapinzani, lakini kwa nchi zetu unaweza kuhubiri ilani hadi ukawapa na kopi lakini wakaona kama unakariri mashairi kumbe si hicho wanachokitaka. Ajira sidhani kama itauza kumbuka tunazungumzia jimbo la Igunga si Ubungo labda ardhi hasa kwenye kilimo mfano mbolea ya ruzuku hivyo vinaweza kuuzika. Asante mkuu ila hiyo njia ya kwanza sina uhakika nayo.
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,035
  Trophy Points: 280
  Mzee mabadiliko yanakuja ila kuna watu wanajifanya kutoyaona, tumeanza mbali sana nakumbuka kadi yangu ya kwanza nilikata mwaka 1992 United Movement for Democracy(UMD) cha Mzee Fundikira tulikwenda kwa kujificha ficha pale Magomeni Mapipa tukiogopa kuonekana na polisi.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Najua sana lakini hakuna wakati wa kuzungumzia Ajira kama wakati wa Njaa. Igunga umefika? hizi porojo za Rostam na ujenzi wa shule sijui Zahanati ni vitu ambavyo wana Igunga hawakuviomba na wala sii vitu ambavyo siku zote WanaIgunga wataisifia CCM..

  Siasa ni uwezo wa kuingia ndani ya vichwa vya watu ukajua kitu gani kinawakera zaidi halafu kaa Mpindani unakandamiza kwenye donda hilo. Amini maneno yangu mkuu wangu Tanzania ya leo Ujambazi, wizi na hata Ufisadi unakuja taratibu kutokana na kukosekana kwa ajira. Tunasukumwa ktk kona ya kimaisha hadi itafika siku tutafika mwisho wa Ukuta na hakuna kurudi nyuma tena isipokuwa kutokea mbele..

  Muda huo umekaribia na hakika Ajira ni kitu muhimu sana ktk uchumi unaloteteleka. Kilimo ni sehemu ya Ajira kama utawez akuboreshan kilimo cha Kahawa na chai Igunga wakati bei za mazao hayo zimepanda nadhani hili ni wazo zuri na la kile ktk kutatua matatizo ya wananchi kuliko kuwadanganya na khanga au baiskeli kama alivyocheza Rostam..

  Mimi nina hakika wananchi wameisha pata mwamko mpya, wana hasira na Ufisadi na wengine hawajui kabisa maendeleo zaidi ya upeo wa macho yao kwa hvyo ipo kila sababu kwanza kuboresha maisha yao kuliko kuwapa aghadi ya vitu ambavyo toka wazaliwe vilikuwa ni hadithi ama usafiri hadi Tabora au Dar..
  Chadema haishindi uchaguzi kutokana na jina la Mgombea, hapana ila mara nyingi ktk chaguzi nyingi duniani Chama tawala ndio mbunge wake hutokana na jina la mgombea if he/she can deliver..na upinzani it's always against the all idea (motion) kutetea haki ya wahusika..Kwa hiyo Chadema wanaweza shinda na mtu yeyote ilimradi tu wanachokipinga ni kile kinachowatia hasira wana Igunga na huyu mtu anaonyesha wazi atakuwa msitrari wa mbele kutetea haki yao...
   
 19. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ndio maana wanapatikana na wakufukuza baadaye, maana mamluki na wale wanaoitwa ma-opportunist lazima wajiunge CDM kwa malengo ya kupata nafasi chee za Ushindi kwa sababu Watanzania ugonjwa wao ni kutofiki na kutoelewa lolote zaidi ushabiki.

  Kama CDM haita kuwa makini inaweza kujikuta inakufa kifo cha mende dk90; maana kilichoiuwa CCM ni hicho hicho, walipojuwa kuwa ukiwa na ticket na CCM tayari wewe ni Mbunge kwa 70% dhidi ya mgombewa Upinzani walikuwa wanajitokeza kwa wingi sana huko CCM lakini matoke yake hawa kuwa na ufanisi bunge hadi wananchni wamewachoka, sasa wanajuwa ukiwa mgombe wa CCM kushinda ni -30% dhidi ya wa CDM wanakimbilia CDM. Nilisifia sana CC katika uchaguzi wa Vijana, sijui hapa itakuwa na hasa si huu uchaguzi tatizo ni uhai wa chama na uimara wa chama mbeleni. Tayari wameshaleta majeruhi Arusha, Singida na Mbeya, wote hao ni opportunists subiri 2015 uone kazi yake maana hapo CCM nao wataleta wao kwa ajili kufanikisha wizi wa kura kilaini.
   
 20. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  sasa kama hizi taarifa zinawahusu wana Igunga wa CDM kwanini umeileta Jamvini?

  ushauri.

  wape masunduku ya maoni jimboni.
   
Loading...