Spana Malaya!

Aluta

Member
Aug 16, 2008
69
3
Namfundisha mwanangu kiswahili sasa kaniuliza hii spana inayofungua bolts nyingi tofauti inaitwaje? Jibu najua ni Spanna Malaya..lakini hili jina halijakaa sawa kwa mtoto mdogo, maana anaweza uliza Malaya maana yake nini?maana sidhani kama ni vizuri kumfundisha mtoto mdogo maana ya Malaya. Je; kuna jina mbadala la hilo?naona kama jina hili limekaa kama isivyo.
 
Kwani ni nini maana ya MALAYA isije ukawa na maana yako kichwani tofauti na maana halisi ya neno.
 
Sio ni spana ya kurekebishika? Halafu kama spana malaya ni lugha ya kwawaida basi utamweleza ya kwamba "malaya" ni kitu kinachorekebishika kupokea vitu vyenye ukubwa tofautitofauti.

Akikua na kuona upande mwingine ataelewa falsafa ndani yake, au la?
 
Katika maeneo nilikokulia tulikuwa tunaiita 'matundu mengi' kama muktadha hauruhusu kusema 'spana malaya'.
 
Sio ni spana ya kurekebishika? Halafu kama spana malaya ni lugha ya kwawaida basi utamweleza ya kwamba "malaya" ni kitu kinachorekebishika kupokea vitu vyenye ukubwa tofautitofauti.

Akikua na kuona upande mwingine ataelewa falsafa ndani yake, au la?

Nakubaliana na wewe Mkubwa
 
Back
Top Bottom