Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,989
- 189,583
Habari,
Hivi karibuni kampuni linalohusika na utengenezaji wa vyombo vya anga na unajimu limetoa ripoti ya mipango yao ndani ya mwaka 2022 ya kurusha rockets 52.
Elon Musk ambaye ni mkurungezi wa kampuni hilo la SpaceX alieleza kwa mwezi huu wa January watarusha Rocket 4 ambazo zote ni Falcon 9.
Huku NASA wakitoa tahadhari kwa kusema kampuni la SpaceX na wote wanaohusika wanatakiwa kuwa makini na isipelekee kuwa waanga kwa mafanikio waliyonayo hadi sasa.
SpaceX wakiwa wanaendelea kupambana kurusha rockets hizo 52 ambazo kwa wastani ni sawa watarusha rocket 1 kila wiki hadi mwaka 2022 utakapoisha.
Wakifanikiwa huu mpango watavunja rekodi yao wenyewe ya mwaka jana 2021 ambayo walifanikiwa kurusha roketi 31.
"Ni kweli kuna shauku kubwa sana ndani ya kampuni la SpaceX kurusha rockets 52 ndani ya mwaka huu, 2022" Alisema Sandra Magnus, Mnajimu na aliwahi kuwa Mkurungezi mtendaji ndani ya American Institute of Aeronautics and Astronautics kupitia kwenye mahojiano yaliyochaposhwa na website ya The Verge.
Aliendelea kwa kusema "NASA na SpaceX wanatakiwa kuchukua tafadhari zote zinazostahili na kulenge kwenye maendeleo ya Project za NASA zaidi na kwa umakini mkubwa huo ili kuleta usalama kwa pande zote mbili" Kulingana na taarifa ilivyotolewa na CNBC na The Verge.
Japo Magnus hakuweka wazi kuwa suala la kurusha rockets hizo either kutaambatana na majaribio ya Starship ambazo zililenga kuanza kusafirisha watu kwenda Space.
Hadi sasa SpaceX ndani ya mwaka huu wamekwisha rusha rocket 3, ambazo zote ni Falcon 9 katikati ya tar 9 hadi 19 ya mwezi January.
Ikumbukwe mwaka 2020 Mkurungezi wa kampuni la SpaceX, Elon Musk alisema mwaka 2021 watarusha rocket 48 ila hadi mwisho wa 2021 walifanikiwa kurusha roketi 31, ambayo bado ni record kubwa hadi sasa kwenye mambo ya unajimu na anga.
Kwa kipindi cha miaka mitano toka sasa 2022,idadi ndogo kabisa kwa kampuni la SpaceX kurusha rockets ni mwaka 2019 walirusha rockets 13 tu.
Wacha Tusubiri Na Tuone Kwa Mwaka 2022 Elon Musk Atafanikiwa Kwa Asilimia Ngapi Au Ataushangaza Ulimwengu Na Projects Zake Hizi?
Nawasilisha Mzee Mkoloni.
Cc: Kichwa Kichafu.