Bantugbro
JF-Expert Member
- Feb 22, 2009
- 4,476
- 4,250
Nimeipenda gea ya kuhamia kwenye Kiswahili. Pengine mtapunguza hoja za kupimana viingereza hapa, ili muweze kujadili maendeleo.
Bukyanagandi said:Baadhi yao nimesoma nao majigambo tu hawana lolote, labda niwachekeshe kidogo: Kuna siku tuliwahi kukaribishwa mahali, wenyeji wetu walihanza kutudadisi kwa kusema nasikia Wafrica mnaweza kuzungumza lugha zaidi ya moja yaani: lugha ya kienyeji, lugha ya Taifa nk - nakahulizwa mimi, eh lugha yenu ya Taifa ni hipi nikajibu "KISWAHILI" mwenyeji wetu alionekana kufurahishwa na jibu langu, ikafika zamu ya Mzambia yeye alisema kusema kweli sisi huwa tunazungumza zaidi Kinyanja tukiwa Lusaka na Kibemba nje ya mji mkuu na kwa bahati nzuri wote tunazijua lugha hizo, isipokuwa mashuleni na makazini tunatumia kingereza kama official language. Sasa ikaja zamu ya Mkenya yeye akamweleza mwenyeji wetu kwa mbwembwe kwamba national language yao ni kingereza! Mwenyeji wetu alicheka sana akamwambia taifa lenu halina lugha walao ya kienyeji mkakifanya a national language, jamaa niliona alishtuka kidogo na kusema "oh sorry, pia na sisi tunazungumza kiswahili". Ninacho taka kueleza humu ni kwamba wakati mwingine hawa wenzetu wanakuwa na majivuno yasiyo na tija - nadhani yeye alifikili akisema national language yao ni kingereza basi mwenyeji wetu atawaona wame endelea sana na si kinyume chake.
Well said wakuu, tatizo ni kuwa wengi wa hawa vijana wetu toka nchi jirani hakuna lugha wanayoielewa vizuri, iwe kiswahili ama kiingereza) ndo maana kama mnafuatilia vizuri mijadala mingi humu jamnvini (Int. forum) mtaona kila baada ya sentensi moja lazima wabandike mitusi ya nguoni ili kujihami/kuzima mjadala...Kwa sababu hawawezi kujenga wala kujibu hoja vizuri, hii ni dalili ya tatizo linalotokana na kutojua matumizi sahihi ya lugha.