South Africa nitafikaje?

Ndugu yangu shibekijijini baki bongo south unafuata nini? Huku kuna bastola nje nje hapafai kabisa
 
Kwanjia ya Bus inafaa, sema utasumbuana na askari wa mipakani, utazunguka sana, utatoa rushwa sana, ila kama una makaratasi, haina shida... Na kama una pasport bora utumie ndege tu.. Kuna watu wanakufa sana kwa njia ya bus
Watu wanafia wapi?
 
Una MTU Wa kukupokea Huko uendako?au unaenda tuu kutafuta maisha?km jibu la pili ndyo nakushauri USIENDE

Miaka 10 iliyopita tulielekea Huko vijana5,tulifika Wawili yaliyotukuta wee acha tu.
 
Fastjet laki 3 tu, hiyo lakimbili iliyobaki unaanzia maisha, naskia south Wanaruhusu raia kutoka TZ akae miezi mitatu bila visa.. So hapo ukishaingia kule utajua ufanye nini ili uwakwepe polisi au upate work permit ya professional yako..
Ivi shida yote y nin... Maisha yako uko tu?
 
kumbe hauna hata passport yet.?
 
Kwanjia ya Bus inafaa, sema utasumbuana na askari wa mipakani, utazunguka sana, utatoa rushwa sana, ila kama una makaratasi, haina shida... Na kama una pasport bora utumie ndege tu.. Kuna watu wanakufa sana kwa njia ya bus
Ivi uyu akipata matatizo unadhani ntamuurumia!!!
 
Tafuta eneo uanze kilimo cha mbogamboga hapa hapa nchini badala ya kwenda kuadhirika huko ugenini ndugu
 
Nenda tu wala usisikilize ya mtu. Ila ukae ukijua kabisa ukifika huko UTAKULA ULIKOPELEKA MBOGA
 
Fastjet laki 3 tu, hiyo lakimbili iliyobaki unaanzia maisha, naskia south Wanaruhusu raia kutoka TZ akae miezi mitatu bila visa.. So hapo ukishaingia kule utajua ufanye nini ili uwakwepe polisi au upate work permit ya professional yako..
Mkuu Tz iko kwenye jumuhiya ya SADC, hautakiwi kupata visa ila tuu wanakupa miezi mitatu free bila permit co visa
 
Unaposema uko vizuri kwa kulima hasa kwa kutumia jembe la mkono una maanisha nini? Umejuaje kama upo vizuri kwa kulima na hasa kwa kutumia jembe la mkono? Ulipata faida ya mazao au unalima heka moja kwa jembe la mkono,kwa saa moja?

Tafuta Passport,nenda kwa ndege ukajaribu maisha acha kuwasikiliza wakatisha tamaa,uamuzi unao wewe mwenyewe coz humu wapo watakao kwambia,nenda na wapo watakao kwambia usiende.
 
Ndugu yangu shibekijijini baki bongo south unafuata nini? Huku kuna bastola nje nje hapafai kabisa
Ziko nje nje hasa kwa mtu ambae ni mhalifu, ina maana hizo bastola analengwa mtu yeyote au kuna sababu za kulengwa?
 
Una MTU Wa kukupokea Huko uendako?au unaenda tuu kutafuta maisha?km jibu la pili ndyo nakushauri USIENDE

Miaka 10 iliyopita tulielekea Huko vijana5,tulifika Wawili yaliyotukuta wee acha tu.
Kwakweli nakwenda kwa ajili ya kutafuta maisha, naomba uniambie sababu kubwa ya kupoteza marafiki hao ulio kuwa nao ilikuwa ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…