TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Wale Magwiji wa Kuponda mwenendo wa Shirika letu la Ndege la Air Tanzania kaeni mkijua kufanya biashara hii siyo lelema na tunatakiwa kulipongeza sana Air Tanzania na Rais wetu Jemadari Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI kwa uamuzi wake wa kulifufua na hadi sasa linafanya vizuri.
Shrika la Ndege la Afrika Kusini (South Africa AIRWAYS) lina hali mbaya na kupelekea hata kushindwa kutoa taarifa yake ya fedha ya Mwaka kutokana na hali mbaya ya kifedha inayolikumba.
kufuatia hali hiyo, Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines) linafikiria kuingilia kati ili kuokoa jahazi.