'South Africa Airways' Hatarini, linajiendesha kwa hasara tangu mwaka 201i

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1570614508093.png

Wale Magwiji wa Kuponda mwenendo wa Shirika letu la Ndege la Air Tanzania kaeni mkijua kufanya biashara hii siyo lelema na tunatakiwa kulipongeza sana Air Tanzania na Rais wetu Jemadari Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI kwa uamuzi wake wa kulifufua na hadi sasa linafanya vizuri.

Shrika la Ndege la Afrika Kusini (South Africa AIRWAYS) lina hali mbaya na kupelekea hata kushindwa kutoa taarifa yake ya fedha ya Mwaka kutokana na hali mbaya ya kifedha inayolikumba.

kufuatia hali hiyo, Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines) linafikiria kuingilia kati ili kuokoa jahazi.

Facts zinajibiwa kwa Facts,sio kweli SAA linakaribia kufa au kuwa na hali mbaya kiasi hicho,hizi SOEs zote za SA zilinyonywa na kuvurugwa sana kipindi cha President Zuma kuanzia Eskom,SAA,DENEL,etc etc,na juzi kati hapa SAA wamepata bail out pamoja na SABC,ni vema mkuu unapoelezea kitu read and read ili uwe na story for both sides,na kwa utendaji wa sitting President CR hakuna uwezekano wa SAA kuzama chini,na elewa kuwa uendeshaji wa mashirika ya ndege ni gharama kubwa na yanahitaji ufanisi wa hali ya juu,sasa sisi ni vema tukajipanga vema na kujifunza wa wenzetu(kuna uwezekano wa SAA,MANGO,SA EXPRESS KUUNGANISHWA PAMOJA),pia mkuu usielezee hoja kisiasa yes president wetu anafanya kazi nzuri ila sio all credit ziende kwake.
 
Maneno mengi halafu unazunguka pale pale, kwani issue ni nini kilisababisha wafikie hapo au issue ni wana hali mbaya?
Tatizo lenu mnapokosa hoja mnatapatapa sana.
 
ATCL iko na hali mbaya sana
Uzuri ni kuwa hatuambiwi ukweli
 
ATCL iko na hali mbaya sana
Uzuri ni kuwa hatuambiwi ukweli

Ukweli upi unaotaka? JPM alipoingia hawakuwa na ndege, leo wanazo 7 na wamenunua nyingine zipo njiani. Hao SAA ambao ndio chanzo cha kuua Air Tanzania, NBC na Tanesco walipobinafsishwa na Che-nkapa. Kama wangekuwa werevu tungeona maendeleo japo kwenye kimoja walichochukua. SA wale walowezi hawawezi kuipenda Tanzania hata siku moja maana sisi ndio tulinyang'anya keki yao mdomoni. Che-nkapa hesabu zake zilikuwa sifuri.

BTW karibu kwenye safari ya kwanza ya ATC kwenda London mwakani. Kama ukiwahi nitagharimia tiketi.
 
Maneno mengi halafu unazunguka pale pale, kwani issue ni nini kilisababisha wafikie hapo au issue ni wana hali mbaya?
Tatizo lenu mnapokosa hoja mnatapatapa sana.
mnukuu Rais wetu wa awamu ya nne,hoja inapingwa na hoja iliyobora zaidi sio kupigwa rungu,nijibu kwa hoja kama nilivyokujibu wewe kwa hoja,SAA HAIPO kwenye hali mbaya kama wewe unavyotaka mimi niamini,nimesoma sana kuhusu issue hii ili nipate upande wa pili wa story,sio wako tu.operations zote za shirika zinaenda vema na tatizo lililotokea ambalo kwa kiasi kikubwa kimechangiwa na rushwa linashughulikiwa na amini usiamini hakuna serikali ya SA ITAKAYORUHUSU hili shirika life including SABC,ESKOM,DENEL,TRANSNET.ni vema tukampongeza rais wetu kwa juhudi ILA SIO yeye tu asiyefanya makosa,yes ndege tunahitaji BUT timing ipo right?je kwa hali yetu ya kiuchumi kwa sasa tunahitaji tuwe na ndege zaidi au barabara bora zaidi?,always sisi middle class tuelewe tu sehemu ya watanzania ,tusijione tupo bora zaidi kwa sababu ALLAH ametupa kidogo cha ziada ukilinganisha na wenzetu.
 
Back
Top Bottom