ATCL na Hasara ya 60 Billion: Mtazamo Wangu

Sci-Fi

Member
Jan 30, 2016
71
266
Habarini za wakati huu.

Leo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali C.A.G, ametoa Taarifa yake na kukabidhi kwa Mh. Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasan. Katika taarifa hiyo imeonesha hasara ya Tsh. 60 Billion zilizo sababishwa na shirika letu la ndege la ATCL.

Suala la ATCL kupata hasara consistently kwa miaka mitano yote ya awali na kifikia Tsh. 60 billion kwa mwaka wa 2019/20 limewashitua sana watu wengi na kuzua taharuki mitandaoni na wengine wakienda mbali na kusema kwa hasara hii ni afadhali ndege hizi ziuzwe na fedha ielekezwe kwenye miradi mingine ya kimaendeleo.

Nilipata kusoma andiko la Alex Ledsom lililohusu operations za ndege 2020, lililo chapishwa katika jarifa maarufu la Forbes lenye kichwa cha habari, "These Airlines Made a Profit in 2020 - Here's How" andiko la September 15, 2020.

Katika andiko hilo Alex Ledsom alisema, mashirika makubwa mawili ya Korean Air na Asiana ndio yaliyotengeneza faida kwa mwaka 2020 ingawa kulikua na shida kubwa hasa kushuka kwa kiasi kikubwa cha mauzo ya ticket kutokana na COVID-19. Hata hivyo, katika robo ya pili ya mwaka 2020, shirika la ndege la Korean Air lili ripoti faida ya dola za Kimarekani $125.2 million ingawa kuliku na kushuka kwa mapato ya mauzo ya ticket kwa 44%. Vile vile, Asiana waliripoti faida ya dola za kimarekani $96.9 katika robo ya pili ya mwaka 2020, wakati mapato yatokanayo na kuuzwa kwa ticket yalishuka kwa 45%.

Ledsom aliendelea kusema kwamba, faida hii isingeliweza fikiwa kwakua idadi kubwa ya wasafiri kutoka China na Asia ya Mashariki, ili shuka sana kutokana na COVID-19, lakini hata hivyo mashirika haya mawili yali manage kupata faida.

Je, yalipaje faida wakati hali ilikua ngumu hadi kwetu huku kwa mujibu wa ripoti ya C.A.G tumeoata hasara ya Billion 60 Tzs??

Mara nyingi abiria wakisafri huwa wanasafri na mizigo yao, uwepo wa COVID-19, ulisababisha watu wasisafiri, lakini vile vile mizigo ambayo watu hawa huwa wanasafiri nayo haikusafiri pia. Mashirika haya mawili, ya ndege yaliamua kutake advantage ya watu kutosafri na kuamua kuanza kufanya delivery ya mizigo ambayo abiria hawa walikua wanasafri nayo au kutuma mahali (cargo). Ni ubunifu huu wa haraka ndio uliopelekea mashirika haya kupata faida kwa robo ya pili ya mwaka 2020. Katika kipindi hicho kwakua watu walikua hawasafiri, ongezeko la kusafirisha mizigo (cargo) liliongezeka na kufikia asilimia 95%!!!

Shirika la ndege pekee lililofanya vema katika ukanda huu wa Afrika ni shirika la ndege la Ethiopia, nalo vile vile lilifanya kubadilisha jinsi lilivyo zoea kujiendesha na waka amua kubeba mizigo (cargo) kwa wingi kuliko watu ambao walikua hawasafiri.

Wengi wetu tuliweza kushuhudia Midege ya Ethiopia ilivyo kua ikibeba shehena za mizigo (cargo) ya Alibaba na kufanya delivery sehemu mbalimbali Afrika kwa kipindi chote ambacho abiria walikua hawasafiri kutokana na COVID-19 hadi hivi leo. Sasa hiyo ni sehemu tu ya adaptability ambayo Ethiopia walifanya katika kipindi kigumu cha biashara ya usafiri wa anga kutokana na COVID-19 wakati ATCL wakiwa wamelala na kusubiria wateja. Niliwahi sikia mahali, gharama za kuendesha ndege ikiwa imepaki ni kubwa zaidi kuliko ikiwa inarun.

Katika hili la hasara ya Billion 60 zilizo ripotiwa na C.A.G ambazo ATCL wamepata katika 2019/20 nina machache ya kusema.

1. Kwanza, wazo la aliyekuwa Raisi wa JMT, Hayati Dr. John Pombe Magufuli la kufufua shirika letu la ndege lilikua jema sana ila utekelezaji wake ndio mbaya. Mashirika mengi sana ya ndege duniania yanajiendelesha kwa hasara na kutegemea ruzuku za serikali kuyaokoa..juzi juzi tumeona jinsi shirika la ndege la India lilivyo fanya vibaya sana. Lakini pia Kenya na South Africa yalivyo fanya na kupata hasara kubwa kwa miaka yote ya operations zao. Nashauri, shirika letu la ndege la ATCL lipewe muda lakini pia uandaliwe mpango na mkakati wa uendeshaji wa shirika hili. Kwakiasi kikubwa hasara hii ya ATCL haitokani tu na ukosefu wa abiria, matumizi mabaya ya fedha au sababu nyingine tusizo sijua ila pia kutokuwepo kwa mpango wa jinsi ya kuliendesha shirika tangu ndege zilipoanza kununuliwa.

2. Pili, wakati shirika la ATCL likipewa muda, Serikali isifanye biashara kwa kulitumia Shirika na serikali isiwe msemaji wa shirika. Shirika liachwe lijiendeshe lenyewe, lishindane na mashirika mengine katika soko. Wakati huo huo, Serikali itengeneze mazingira wezeshi kwa shughuli za usafiri na usafirishaji wa anga na ibaki kama mdau na si muendeshaji. Shirika la Asiana Air kwa kiasi kikubwa linamikikiwa na moja ya South Korea's largest conglomerates, inayoitwa The Hyundai Development Company. Kama shirika letu la ATCL litaachwa lijiendeshe kwa kukabidhiwa kwa makampuni yanayo weza kuliendesha, nina imani with time tunaweza fikia hatua ya kutangaza faida kama ATCL hata kama ni zero profit.

Mara nyingi watu huwa hawafanyi vizuri na kuwekeza nguvu na juhudi zao zote pale wanapokua na "options, alternatives". Na hii ni sahihi kabisa kwa shirika la ndege la ATCL na mashirka mengine yanayo tegemea ruzuku za serikali kujiendesha. Wanakua wazembe, wanakosa ubunifu na wanafanya business as usual kwakua hawaoni umuhimu wa kufanya kwa juhudi na hawawi responsible kwa hasara inayopatikana wakiamini kuna "alternatives, options" ya hasara waliyo sababisha, nayo ni rescue program ya serikali kwa jina la ruzuku.

3. Tatu, kama serikali itataka kuendelea kubaki kuwa mmiliki, msimamizi na muendeshaji wa shirika la ATCL ni muhimu Serikali ijifunze kutoka kwa mashirika mengine yanayo fanya kazi hii vizuri walianzaje, walikabiliana vipi na changamoto za ndani na wakafanikiwa kutoka nje ya nchi. Asiana Air na Korean Air si tu kwamba wanafanya vizuri katika nchi ya Korea hapana, wanafanya vema pia katika ukanda wote wa Asia, Marekani ya Kaskazini, Australia na maeneo mengine, lakini hii iliwekena baada ya kuwin soko la ndani. Tusiwaze kushindana tu na Kenya Airways, Ethiopian Airways, RwandaAir, wakati kuna mashirika ya ndege ya ndani yanatupiga chini na ushindani uwe huru.

Note: Kuna mashirika makubwa tu Duniani hadi hivi leo hayajawahi ingiza faida tokea yameanzishwa..Spotify, Uber, hata Elon Mask kaanza kufurahia investment ya ya Tesla juzi juzi tu hapa tangu 2003. So, sidhani kama ATCL ni bad investment.

Karibuni kwa Maoni na michango.
 
Tatizo kubwa ni kwamba shirika limekuwa likiendeshwa na watu wasio sahihi ambao hawana mpango mkakati wa kibiashara. Hayati aliwajaza washikaji zake ambao mwisho wa siku wamemuangusha.
 
Habarini za wakati huu.

Leo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali C.A.G, ametoa Taarifa yake na kukabidhi kwa Mh. Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasan. Katika taarifa hiyo imeonesha hasara ya Tsh. 60 Billion zilizo sababishwa na shirika letu la ndege la ATCL.
Tueleze, ATCL wataweza vipi kushindana na mashirika kama Ethiopian Airways, Kenya Airways, au hata Rwandan Air, na hizi ni hapa hapa karibu, sababu kila ATCL anakotaka kwenda hawa walikuwepo na wapo bado, na hata isitoshe wanashirikiana na mashirika makubwa kama Kenya na KLM,

Bado sijataja Qatar na Emirate, kama kuna wasafiri wengi wanakwenda hizi nchi kutoka Tanzania, ATCL ina uwezo kweli kushindana na haya mashirika yanayopewa ruzuku ya mafuta na nchi zao ambao ni wazalishaji wa mafuta, na vipi tutaweza kupeleka abiria Dubai au Qatar kutumia ATCL, haitokaa itokee hivyo, Qatar na Emirate zimewafukuza kina British Airways, SAS, Lufthansa kuja Tanzania sababu wameshindwa ushindani wa biashara haya mashirika.

Biashara ya ndege kwa Taifa ni ngumu sana hata mashirika makubwa duniani yanasota sana ukilinganisha na Qatar na Emirate, haitowezekana, tulikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu sana
 
Kosa jingine la Hayati , ni kudorora Kwa uhusiano wake na mataifa mengine, alijifungia Tu ndani ili kutukaba koo na kutujaza ujinga ....akiwa na watu wake ambao hawapo smart kwenye hzi mambo , na pia
akiwa hashauriki .....
 
..it is a bad business, period.

..haipaswi kufanywa na serikali ya nchi yenye watu wengi na changamoto nyingi kama Tz.

..hiyo biashara inawafaa WAARABU wenye hela za mafuta za kuchezea.

..hata Rwanda waliotushauri tununue ndege wameamua kuuza shirika lao kwa QATAR.
 
Magufuli aliwekeza zaidi ya trilioni 2 kununua ndege za ATCL ili tupate faida za kiuchumi. Tunaelezwa life span ya zile ndege ni wastani wa miaka 25. Mpaka sasa tayari ni miaka mitano tumeshatumia (20% ya life span ya ndege zetu), na hatujavuna faida zaidi ya kuambulia hasara ya mabilioni ya pesa.

Sasa, maswali muhimu ni haya.
-Serikali ilikaa chini na kutafakari hayo kabla ya kufanya huo uwekezaji?

-Huu mwenendo wa kupata hasara tu, tuliutegemea kutokea au umeibuka tu tofauti na mategemeo yetu?

-Kulikuwa na umuhimu wowote kuwekeza pesa zote hizo kwenye biashara kichaa ya ndege?

-Kwanini ATCL wamekuwa wakisema wanavuna faida na kuipa serikali gawio wakati wako kwenye hasara?

-ATCL walikuwa wamejipanga kuanza kupata faida lini, kwa namna ipi hasa?
 
Serikali iache kuhangaika na mambo ambayo haitakaa ije kufanikiwa. Hizo ndege zote ziuzwe pesa zipelekwe kwenye maji na kuajiri wafanyakazi wa hospitali. Kabla ya hayo madrimulaina ya atcl watu walikuwa wanasafiri vizuri bila shida kwa ndege tena kwa nauli za bei ya chini kuliko zilizopo sasa, sijui nani aliwaloga kwenda kuchukua hayo makitu ya kuteketeza pesa za walipa kodi.
 
Tillion moja utawekeza maji kiasi gani,,na jem mkradi itarudisha sh ngapi kw serikali
 
Mh
 
Wajibu mkuu wa serikali sio hata kuwekeza bali ni kutoa huduma muhimu za kijamii ambazo sekta binafsi ingezitoa kwa gharama kubwa sana. Serikali kazi yake kubwa inapaswa kuweka mazingira rafiki kwa biashara na kisha ipate kodi ya kutosha kutoka sekta binafsi.
Tillion moja utawekeza maji kiasi gani,,na jem mkradi itarudisha sh ngapi kw serikali
 
Tufupishe story; Haukua uamuzi sahihi kupeleka fedha za walipakodi kwenye mradi huo wa ndege. Angalau zingepelekwa kwenye treni ya umeme au huduma nyinginezo za kijamii.
 
Tillion moja utawekeza maji kiasi gani,,na jem mkradi itarudisha sh ngapi kw serikali
Kwani hizo ndege zimerudisha kiasi gani!??? Ni bora hayo maji yatawasaidia wananchi wengi na hayatatutia hasara kama hizo ndege wanazotumia wachache.
 
Magufuli aliwekeza zaidi ya trilioni 2 kununua ndege za ATCL ili tupate faida za kiuchumi. Tunaelezwa life span ya zile ndege ni wastani wa miaka 25. Mpaka sasa tayari ni miaka mitano tumeshatumia (20% ya life span ya ndege zetu), na hatujavuna faida zaidi ya kuambulia hasara ya mabilioni ya pesa.

Sasa, maswali muhimu ni haya.
-Serikali ilikaa chini na kutafakari hayo kabla ya kufanya huo uwekezaji?

-Huu mwenendo wa kupata hasara tu, tuliutegemea kutokea au umeibuka tu tofauti na mategemeo yetu?

-Kulikuwa na umuhimu wowote kuwekeza pesa zote hizo kwenye biashara kichaa ya ndege?

-Kwanini ATCL wamekuwa wakisema wanavuna faida na kuipa serikali gawio wakati wako kwenye hasara?

-ATCL walikuwa wamejipanga kuanza kupata faida lini, kwa namna ipi hasa?
Kama lifespan ni 25 yrs, and the National Airline is just 5yrs of age from the scratch, what is your worry?
 
Wajibu mkuu wa serikali sio hata kuwekeza bali ni kutoa huduma muhimu za kijamii ambazo sekta binafsi ingezitoa kwa gharama kubwa sana. Serikali kazi yake kubwa inapaswa kuweka mazingira rafiki kwa biashara na kisha ipate kodi ya kutosha kutoka sekta binafsi.
Inategemea na aina uchumi.
 
Tueleze, ATCL wataweza vipi kushindana na mashirika kama Ethiopian Airways, Kenya Airways, au hata Rwandan Air, na hizi ni hapa hapa karibu, sababu kila ATCL anakotaka kwenda hawa walikuwepo na wapo bado, na hata isitoshe wanashirikiana na mashirika makubwa kama Kenya na KLM,

Bado sijataja Qatar na Emirate, kama kuna wasafiri wengi wanakwenda hizi nchi kutoka Tanzania, ATCL ina uwezo kweli kushindana na haya mashirika yanayopewa ruzuku ya mafuta na nchi zao ambao ni wazalishaji wa mafuta, na vipi tutaweza kupeleka abiria Dubai au Qatar kutumia ATCL, haitokaa itokee hivyo, Qatar na Emirate zimewafukuza kina British Airways, SAS, Lufthansa kuja Tanzania sababu wameshindwa ushindani wa biashara haya mashirika.

Biashara ya ndege kwa Taifa ni ngumu sana hata mashirika makubwa duniani yanasota sana ukilinganisha na Qatar na Emirate, haitowezekana, tulikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu sana
Ushidani ni rahisi ukijua competitive advantage ya mwenzio na ukaamua kufanya kama yeye au zaidi yake. Ila nime elezea kwa suala la ATCL kupewa muda. Its just 5 years sasa, kuna Giants company za usafiri wa anga hazikuanza jana, ila baada ya muda zilianza ku make profit.
 
Back
Top Bottom