Sorry madam (Destination of my enemies)

SORRY MADAM (68)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Macho ya Eddy, Sa Yoo, Shamsa na Madam Mery
wakawashuhudia Phidaya na Rahab wakiingia
kwenye moja ya gari la kifahari huku nyuma yao
akiwepo dokta Ranjiti.
“RANJITIIIIIIIIIIIIIIIIIII…………………….”
Eddy aliita kwa sauti kubwa na kumfanya dokta
Ranjiti kutazama sehemu sauti hiyo inapo tokea,
kwa haraka aliweza kuotambua sauti hiyo ni ya
Eddy, ila sura ni tofauti kabisa, ila macho yake
yalipo muona Madam Mery akiwa nyuma ya mtu
huyo akagundua kwamba kila kitu kimeharibika.
Kwa kiwewe dokta Ranjiti akajikuta akifyatua risasi
kadhaa kuelekea anapotokea Eddy na kusababisha
watu kuanza kukimbia kimbia ovyo kuyaokoa
maisha yao.
ENDELEA
Dokta Ranjiti hakuhitaji kupoteza muda au
kuangalia risasi zake zimemdhuru nani kwa haraka
akaingia ndani ya gari na kumuamuru dereva wake
waondoke kwa kasi katika eneo hilo. Risasi alizo
zifyatua dokta Ranjiti kwa muda mchache ulio pita
kwa bahati mbaya ziliwapata raia wawili ambao
walikuwa wakikatiza mbele ya Eddy. Eddy
akajairibu kulifukuzia gari hilo kwa miguu ila mbio
zake hazikuweza kusaidia chochote mbele ya
mwendo kasi wa gari hilo. Madam Mery, Sa Yoon a
Shamsa wakafika sehemu alipo simama Eddy
anaye hema kwa hasira.
“Sasa inakuwaje?”
Sa Yoo aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka
asijue ni nini afanye kwa wakati huo. Kila mmoja
wao hakujua afanye nini ubaya ni kwamba wote ni
wageni katika nchi ya Misri.
***
“Ranjiti kwa nini unatufanyia hivi lakini?”
Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika.
“Nyamaza wewe, unahisi unaweza kunikimbia
mimi, pumbavu sana wewe”
Muda wote huo, Rahab alikaa kimya asizungumze
kitu chochote akilini mwake akipanga ni kitu gani
anacho weza kukifanya kuyaokoa maisha yao.
Hakuhitaji kuonyesha uwezo wake kwa wakati huo,
alihitaji waweze kufika katika eneo ambalo dokta
Ranjiti alikusudia kuweza kufika ili aweze kufanya
atakacho weza kukifanya kwa wakati huo.
Safari yao ikachukua takribani dakika arobaini,
wakafanikiwa kufika kwenye moja ya gorofa refu
kwenda juu, ambalo kwa haraka haraka
linaonekana ni gorofa kuu kuu(limechakaa).
Wakaingia kwenye ndani, dokta Ranjiti akapolewa
na kikundi cha vijana wenye silaha mikononi
mwao, huku sura zao zikiwa zimefunikwa na
vitambaa vyeusi huku ni sehemu ya macho yao tu
ndio inayo onekana. Wakamtoa Phidaya kwenye
gari pamoja na Rahab, kila mmoja akapelekwa
upande wake jambo ambalo lilimchanganya sana
Rahab.
Rahab akaingizwa kwenye chumba kimoja chenye
kiti kimoja cha chuma pamoja na meza moja iliyo
tengenezwa kwa chuma. Akakalishwa kwa nguvu
kwenye kiti hicho, akafungwa miguu na mikono
yake kwenye kiti hicho. Lugha ya kiarabu wanayo
zungumza vijana hao wawili walio muingiza ndani
ya chumba hicho, ikazidi kumtatiza Rahab, hata
wazo la kujiokoa likapotea kichwani mwake.
Vija hao wakatoka ndani ya chumba hicho chenye
mlango wa chumba, na kuufunga kwa nje. Vijana
wawili wakabaki nje ya mlango huo kwa ajili ya
kuimarisha ulinzi.
Phidaya akaingizwa kwenye moja ya chumba,
ambacho kinakitanda kikubwa. Akarushwa
kitandani na vijana walio muingiza humo ndani
wakatoka na kumuacha dokta Ranjiti peke yake
ndani ya chumba hicho.
“Hivi wewe ni mjanja kuliko mimi, si ndio……?”
Dokta Ranjiti alizungumza huku bastola yake akiwa
ameishika mkononi, Phidaya hakujibu kitu
chochote zaidi ya kutetemeka mwili mzima na
kumwagikwa na machozi mengi.
“Umeisumbua akili yangu, umeusumbua moyo
wangu. Nashindwa kufanya vitu vya maana kwa
ajili yako wewe”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa hasira huku macho
yake yakimtazama Phidaya aliye zidi kutetemeka
na kulia kwa woga.
“Nimelimisi sana penzi lako”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akianza kuvua
nguo zake moja baada ya nyingine. Alipo bakiwa
na nguo ya ndani akapanda kitandani na kuanza
kumsogelea Phidaya taratibu huku bastola yake
akiwa nayo mkononi mwake.
***
Eddy na wezake wakajikuta wakirudi kwenye
chumba anacho lala Shamsa na Sa Yoo, kila
mmoja alijikuta akiwa mwingi wa mawazo,
hususani Eddy, alijihisi kichwa kitampasuka kwa
kuwaza. Simu ya mezani ikawatoa wote kwenye
dibwi la mawazo. Kila mmoja akaitazama simu
hiyo inavyo ita. Kwa haraka Sa Yoo akasimama na
kwenda kuipokea simu hiyo.
“Haloo”
Sauti ya kiume ilisikika upande wa pili wa simu, Sa
Yoo akajikuta akipata kigugumizi kuijibu sauti
hiyo. Eddy kwa akili ya haraka akagundua
kigugumizi cha Sa Yoo kina jambo fulani ambalo
Sa Yoo anashindwa kulijibu. Eddy akanyanyuka
kwa haraka na kumpokonya simu Sa Yoo na
kuzungumza na aliye piga simu hiyo.
“Nani?”
Eddy aliuliza kwa sauti yenye msisitizo mkubwa.
Mpiga simu wa upande wa pili akajikuta akikaa
kimya kwa muda asijubu kitu cha aina yoyote.
“Halooo”
Eddy alizungumza tena kwa msisitizo.
“Samahani nahisi nimekosea namba”
Mtu huyo mwenye sauti ya kiume alizungumza na
kukata simu. Eddy taratibu akaurudisha mkonga
wa simu kwenye sehemu husika kisha akarudi
kwenye sofa alilo kuwa amekaa.
Hadi inatimu majira ya saa tatu kasoro usiku
hapakuwa na jibu lolote walilo weza kulipata juu ya
kutekwa kwa Phidaya. Hata polisi ambao walianza
upelelezi wao hawakuweza kumpata mualifu wala
hawakujua ni wapi muhalifu huyo alipo.
“Kukiwa na chochote, mutanifahamisha, naeleka
chumbani kwangu”
Eddy alizungumza kwa sauti ya unyonge huku
taratibu akinyanyuka na kutoka katika chumba
walipo Shamsa, Madam Mery na Sa Yoo. Kila
mmoja alimtazama Eddy akitoka katika chumba
hicho.
“Mutakula nini?”
Madam Mery alizungumza huku akiwaangali
Shamsa na Sa Yoo.
“Mimi sijisikii njaa”
Shamsa alizungumza huku akinyanyuka na kueleka
katika chumba cha Eddy na kuwaacha Sa Yoo, na
madam Mery alio amua kushuka chini kabisa ya
gorofa la hoteli hiyo kwenye mgahawa mkubwa
kwa ajili ya wageni walio fika kwenye hoteli hiyo.
Shamsa akagonga kwenye chumba cha Eddy mara
kadhaa, baada ya kuona mlango haufunguliwi,
kaingia ndani na kumkuta Eddy akiwa amejilaza
kwenye sofa pasipo kuwasha taa.
“Eddy”
“Mmmmmmm”
“Usiwaze sana”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku
taratibu akikaa sofa la pembeni ya sofa alilo lala
Eddy.
“Ni lazima niwaze, sifahamu ni kitu gani kinacho
endelea kwenye hii dunia”
“Kivipi?”
“Kila kitu ninacho kikusudia kukifanya kwenye
maisha yangu naona kinakwenda kinyume na jinsi
nilivyo taraji kiende”
Eddy alizungumza kwa sauti iliyo jaa huzuni na
unyonge ndani yake huku machozi yakimlenga
lenga.
“Eddy, tambua kwamba kila jambo hutokea kwa
wakati wake. Kuna wakati wa kulia na kunawakati
wa kucheka”
“Sawa Shamsa ila mimi naona ninalia kuliko huko
kucheka. Tazama Junio mwangangu amefariki,
mbaya ameuawa na dada yangu Manka. Mama
amefariki, ameuliwa na baba yangu tena mzazi.
Mke wangu ambaye nilikuwa ninajua amefariki leo
hii namuaona yupo hai, basi nimchukue. Anatokea
mtu anamteka ni nini nitafanya hapa duniani ili
nitulie”
Maneno haya Eddy aliyazungumza huku machozi
yakimwagika, taratibu Shamsa akanyanyuka
kwenye sofa alilo kaa, akakinanyua kichwa cha
Eddy na kukaa kwenye sofa hilo kisha akakaa na
kukiweka kichwa cha Eddy kwenye mapaja yake
yaliyo jazia kiasi.
“Eddy, jinsi unavyo umia wewe ndivyo name pina
ndivyo ninavyo umia”
“Shamsa, hupaswi kuumia tena. Maisha yangu kwa
sasa ninaona hayana thamani yoyote. Nitafanya
chochote nitakacho agizwa ili kumuokoa mke
wangu”
“Bado unathamani kubwa moyoni mwangu Eddy.”
Shamsa alizungumza huku mkono wake wa kulia
akiupitisha pitisha kwenye kifua cha Eddy. Eddy
hakuliweekea maanani jambo hilo, akili yake na
mawazo yake yote yapo kwa mke wake ambaye
hadi sasa hatambui ni wapi alipo. Shamsa
akajikuta akizidi kuipeleka mikono yake yote miwili
kwenye mwili wa Eddy, hadi akaifikisha kiuno cha
Eddy na taratibu akaanza kufungua mkanda wa
suruali.
***
Dokta Ranjiti akaendelea na shuhuli ya kumuingilia
Phidaya, pasipo ridhaa yake japo ni mke wake,
aliye kuwa akiishi naye, ila kwa wakati huo Phidaya
kumbukumbu zake hazikuwepo. Muda wote dokta
Ranjiti anavyo muingilia Phidaya, aliendelea kulia
hadi dokta Ranjiti alipo maliza.
“Aghaaaaaaaa”
Dokta Ranjiti alishusha pumzi huku akitoa miguno
ya kumaliza mpambano wa ulazima alio ufanya
kwa Phidaya. Kama kawaida yake dokta Ranjiti
akajilaza pembani huku akihema kana kwamba
amekimbia umbali wa mbio nyingi.
“Utamu wako mke wangu bado haujaondoka, bado
tunda lako lina joto kali kama nilivyo liacha”
Dokta Ranjiti alizungumza maneno ambayo yalizidi
kumchoma moyo Phidaya, na kuzidi kuipandisha
hasira ya Phidaya iliyo jijenga mara baada ya
kumbukumbu zake kumrejea”
“Hivi niambie mke wangu ni wapi ulipo kuwa?”
Phidaya hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa
kimya.
“Ukikaa kimya sio swala muhimu, kwako. Ila
nimetambua kwamba kamume kako ka zamani
bado kapo hai. Kitu nitakacho kwenda kukifanya
utasikia”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akishuka kitandani
na kuanza kuvaa nguo zake. Alipo maliza kuvaa
akakaa tena kitandani kwa dharau.
“Huto toka hapa hadi nihakikishe Eddy ANAKUFA”
Phidaya alipo sikia kauli ya dokta Ranjiti, mapigo
yake ya moyo yakaanza kumuenda mbio, woga
ukazidi kumtawala maradufu na ilivyo kuwa wali.
“Tafadhali Ranjiti ninakuomba usimuue Eddy, kwa
maana hajafanya kosa lolote baya kwako”
“Nikumuacha hai atafanya kosa ambalo litakuwa
baya kwangu. Wewe ni wangu na hakuna ambaye
atakutoa wewe mikononi mwangu”
Dokta Ranjiti baada ya kuyazungumza maneno
hayo akanyanyuka kutoka kitandani na kutoka
ndani ya chumba hicho na kumuacha Phidaya
akiendelea kulia.
Dokta Ranjiti baada ya kutoka kwenye chumba
alipo Phidaya moja kwa moja akaeleka kwenye
chumba alipo shikiliwa Rahab.
“Mumempatia chakula?”
Dokta Ranjiti aliwauliza vijana wake kwa luhga ya
kiarabu, alio wakuta nje ya chumba walipo
muhifadhi Rahab.
“Ndio mkuu, ila anaonekana amekata chakula”
“Nifungulieni”
Dokta Ranjiti akafunguliwa mlango na kuingia
ndani akamkuta Rahab hajakula chochote na wala
hajafunguliwa jinsi alivyo kuwa amefungwa tangu
mwanzoni, alipo ingizwa katika chumba hicho.
Dokta Ranjiti akamtazama vizuri Rahab na kujikuta
akistuka na kumsogelea vizuri usoni mwake.
Kumbukumbu zake kwa haraka zikampelaka siku
ya msiba wa Phidaya nchini Tanzania. Aliweza
kumshudia akiletwa na msafara mkubwa na
kuheshimiwa.
“Wewe si mke wa raisi Praygod”
Dokta Ranjiti alizungumza huku macho yakimtoka
na kumuangalia vizuri Rahab, akaanza kumgeuza
geuza Rahab sura yake. Jibu alilo kuwa nalo
kichwani mwake ni sahihi kwani Rahab kweli ni
mke wa raisi Praygod. Dokta Ranjiti akakaa kimya
kwa muda kisha akatoka kwenye chumba hicho
akiwa na wasiwasi mkubwa moyoni mwake japo ni
jasiri ila kosa ambalo anahisi litayagharimu maisha
yake ni kitendo cha kuweza kumteka mke wa raisi.
Japo kuwa haelewi ni kitu gani kinacho endelea
ndani ya Tanzania.
“Nahitaji mumuachie huyu msichana”
“Kwa nini mkuu?”
“Huyu sina kazi naye. Hakikisheni kwamba
munamuachia hapa na kumtelekeza huko mtaani”
Hapakuwa na kijana aliye weza kuipinga amri hiyo
ya bosi wao dokta Rajiti, vijana hao wakaingia
ndani ya chumba walipo Rahab. Wakamvunga
macho yake kwa kitambaa cheusi kisha
wakambeba juu juu na moja kwa moja wakempeka
kwenye gari lao jeusi aina ya Toyota Land Cruser
V8. Safari ikaaza kumpeleka kwenye mtaa mmoja
ambao hauna watu wengi. Bila ya kupoteza muda
wakafungua mlango wa gari lao na kumsukumia
Rahab pembezoni mwa barabara na akaangukia
kwenye nyasi nyingi kisha wakaondoka kwa
mwendo wa kasi pasipo kumfungua kamba na
kitambaa walicho mfunga usoni mwake. Rahab
akaanza kujitahidi kujifungua kamba hizo kwa
bahati nzuri akapita kijana wa kiume aliye amua
kumsaidia Rahab na kumfungua kamba hizo
pamoja na kitambaa alicho fungwa usoni mwake.
“Asante”
Rahab alizungumza huku akijipangusa pangusa
majani yaliyoshikamana na nguo zake. Kutokana
na kijana huyo kuzungumza kiarabu na Rahab
haifahamu lugha hiyo ikamlazimu Rahab
kumshukuru kwa vitendo kijana huyo ambaye naye
pia alijibu kwa vitendo. Kwa bahati nzuri katika
eneo hilo ambalo Rahab alitelekezwa, aliweza
kulifahamu kwani ni moja ya maeneo ambayo
hupita asubuhi anapo kimbia akichukua mazoezi
ya viungo.
***
Wasiwasi ukaanza kumtawala Raisi Praygod
ambaye kila alipo itazama simu yake hapakuwa na
simu yoyote ambayo imeingia kutoka kwa mke
wake, ambaye walikubaliana baada ya kufika
hotelini na kukutana na Eddy wawasiliane. Akaanza
kuipiga namba ya simu ya mke wake Rahab, kwa
bahati mbaya ikawa haipatikani jambo lililo zidi
kukiumiza kichwa cheke. Masaa yakazidi kukatika
pasipo Rahab kurudi nyumbani. Kwa haraka
akakumbuka kwamba kuna namba ambayo mke
wake aliweza kuwasiliana na watu ambao
wanakwenda kuonana nao. Kwa haraka akaitazama
kwenye simu yake na kuipiga, kwani Rahab
alimpatia namba hiyo kipindi alipokuwa anaondoka
eneo hilo.
Namba ya simu hiyo kwa bahati nzuri inaita, baada
ya muda ikapokelewa, ila mtu aliye ipokea
hakuzungumza chochote hata pale alipo jaribu
kuzungumza neon Hallo
Sauti nzito ya kiume ilimuuliza kwa lugha ya
Kiswahili kwamba yeye ni nani. Ikamlazimu dokta
Ranjiti kuomba msamaha kwamba amekosea
namba. Raisi Praygod alizungumza hivyo baada ya
kumuona Rahab akiingia ndani, huku jasho
likimwagika. Kwa haraka akakata simu na kwenda
kumlaki mke wake.
“Phidaya ametekwa”
Rahab alizungumza huku akihema, akiwa
amemkumbatia mume wake, kipenzi.
“Ametekwa………..?”
“Ndio ametekwa na mwanaume mmoja ambaye
sina kumbukumbu naye. Ila alipo niona mimi
akanikumbuka na kujikuta akiniachia mimi huru”
Rahab alizungumza huku akihema, hii ni kutokna
na kukimbia kwa umbali mrefu.
“Huyo mtu ana asili gani?”
“Kivipi?”
“Namaanisha kwamba ni muafrika, mzungu au?”
“Ni muarabu”
Raisi Praygod alijikuta akibaki na mshangao
mkubwa kwani hakujua ni nani aliye tekeleza agizo
la Phidaya kutekwa.
“Au labda ndio huyo mume wake ambaye
alitueleza?”
“Ndio sasa nimepata picha, itabidi tuhakikishe
tunamuokoa Phidaya”
“Sasa unapakumbua sehemu alipo kuwa
amewapeleka?”
“Hapana ila nitahakikisha kwamba tunamkomboa”
***
“Shamsa stop”
Eddy alisimama na kutoka mikononi mwa Shamsa
ambaye alisha fanikiwa kuufungua mkanda wa
suruali pamoja na kifungo cha suruali.
“Kumbuka kwamba mimi ni baba yako”
“Hapana Eddy wewe si baba yangu. Mimi nimesha
kuwa na nina hisia za kupenda kama wanawake
wengine na siwezi kuendelea kuzidanganya hisia
zangu kwamba wewe ni baba yangu wakati tayari
nimesha weza kuonja mate yake.”
Shamsa alizungumza kwa kujiamini na kumfanya
Eddy abaki akiwa ameduwaa asijue amjibu nini
Shamsa.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 69 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (69)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
“Shamsa stop”
Eddy alisimama na kutoka mikononi mwa Shamsa
ambaye alisha fanikiwa kuufungua mkanda wa
suruali pamoja na kifungo cha suruali.
“Kumbuka kwamba mimi ni baba yako”
“Hapana Eddy wewe si baba yangu. Mimi nimesha
kuwa na nina hisia za kupenda kama wanawake
wengine na siwezi kuendelea kuzidanganya hisia
zangu kwamba wewe ni baba yangu wakati tayari
nimesha weza kuonja mate yako.”
Shamsa alizungumza kwa kujiamini na kumfanya
Eddy abaki akiwa ameduwaa asijue amjibu nini
Shamsa.
ENDELEA
Eddy hakuhitaji kuzungumza chochote zaidi ya
kufunga kifungo cha suruali yake kisha akamalizia
na mkanda, kisha akakaa kitandani huku
akimtazama Shamsa kwa macho makali. Ukimya
ukatawala kwa dakika kadhaa, hapakuwa na mtu
aliye weza kuzungumza kitu chochote.
Shamsa akashusha pumzi nyingi kisha akatoka
ndani ya chumba cha Eddy moja kwa moja
akaeleka kwenye baa iliyomo ndani ya hoteli hiyo.
Akaagiza mzinga wa pombe kali na kuanza
kuunywa kwa fujo japo hiyo ndio mara yake ya
kwanza kuweza kunywa kilevi, ila amefanya hivyo
ili mradi kupoteza mawazo ya kumuwazia Eddy.
‘Eddy ni lazima awe wako’
Shamsa aliisikia sauti ikimshauri kwa msisitizo
kichwani mwake.
‘Una sifa za kuwa na Eddy, hakikisha kwamba
anakuwa wakwako’
Sauti hiyo iliendelea kuzungumza jambo lililo zidi
kumpa munkari Shamsa ya kunywa kwa fujo
pombe hiyo hadi muudumu aliye muhudumi
kwenye kaunta hiyo ya kinywaji akabaki
amemkodolea macho ya mshangao kwani kwa
kipindi cha miaka minne tangu aanze kuifanya kazi
hiyo hajawahi kumshuhudia mtu akiinywa pombe
hiyo kali kwa fujo kama anavyo fanya binti huyo.
“Samahani dada”
Muhudumu huyo alizungumza huku akimtazama
Shamsa usoni, Shamsa akamtazama muhudumu
huyo kwa macho yaliyo jaa ulevi mwingi.
“Samahani ninaomba niuchukue huu mzinga, kwa
maana pombe unayo itumia ni kali sana”
“Nimekulipa au sijakulipa?”
“Natambua hilo ila kwa jinsi unavyo zidi kuinywa
hiyo pombe ni hatari kwa afya yako”
“Hembu niachi….e uu….puuzi wako”
Shamsa alizungumza huku akijaribu kuushusha
mguu wake mmoja chini, kutoka kwenye kiti kirefu
alicho kikalia, kila alivyo jaribu kuushusha mguu
wake, ndivyo jinsi alivyo jikuta akishikwa na
kizunguzungu kikali kilicho mpeleka chini na
kumuangusha chini kama mzigo. Kishindo cha
Shamsa kuanguuka kikawastusha hadi wateja
wengine.
Sa Yoo naye macho yake aliweza kuyapeleka
sehemu ilipo tokea kishindo hicho, katika
kuangalia vizuri akamuona ni Shamsa akijikaza
kaza kunyanyuka kutoka sehemu alipo anguka.
Kwa haraka Sa Yoo akanyanyuka kutoka katika kiti
alicho kaa na kwenda alipo Shamsa.
“Shamsa vipi?”
Sa Yoo alijikuta akimshangaa Shamsa kwa jinsi
alivyo lewa, kwa msaada wa muhudumu mmoja wa
kike wakasaidiana kumnyanyua Shamsa, na kuanza
kumpeleka sehemu kulipo na lifti. Wakaingia wote
watatu na kuelekea katika gorofani kilipo chumba
cha Shamsa na Sa Yoo.
“Asante”
Sa Yoo alimshukuru muhudumu huyo mara baada
ya kumlaza Shamsa kitandani, huku akikoroma
koroma tu pasipo kujitambua. Baada ya
muhudumu huyo kutoka ndani ya chumba chao Sa
Yoo kwa unyonge akaka pembeni ya kitanda,
alicho lala Shamsa.
“EDDY NAKUPENDAAA..AA.AAAA”
Shamsa alizungumza maneno hayo huku
akikoroma, kitendo kilicho mshangaza Sa Yoo,
akajaribu kumtingisha Shamsa ila hakuitika kwa
lolote. Simu ya mezani ikaita na kumfanya Sa Yoo,
kusitisha zoezi la kumuamsha Shamsa akasimama
na kwenda kuipokea simu hiyo, japo ni majira ya
usiku ila aliamini kwamba simu hiyo inaweza kuwa
na umuhimu mkubwa kwao.
***
“Basi itabidi kuweza kujaribu kuwasiliana na huyo
binti ambaye alikuja kumuona bosi wake”
Raisi Praygod alizungumza huku akimtazama
Rahab usoni. Rahab akajipapasa mifukoni mwake
na kujikuta akiwa hana simu yake.
“Vipi?”
“Simu yangu siioni”
“Chukua hii ya kwangu, na muda fulani niliipiga ile
namba uliyo nipatia ila sikuweza kuzungumza
alipokea mwanaume tofauti na ulivyo niambia
kwamba mtu sahihi ni mwanamke”
“Hmebu naomba nijaribu kuipiga tena hiyo namba”
Rahab akaichukua simu ya mumewe na kuipiga
namba, ambayo anazungumza na Sa Yoo. Kwa
bahati nzuri namba hiyo ikaanza kuita na baada ya
muda ikapokelewa.
“Haloo”
Rahab aluzungumza huku akiwa na shauku ya
kuishikia sauti ya kike, ambayo ni sauti ya Sa Yoo.
“Haloo madam nilikuwa ninaishubiria simu yako
kwa hamu kubwa”
Sa Yoo alizungumza huku akionekana kuwa na
furaha kubwa moyoni mwake, japo hajawahi
kuonana na Rahab
“Ohhoooo asante Mungu. Sasa sib ado upo hapo
hotelini?”
“Ndio bado nipo”
“Basi asubuhi na mapema nitakuwepo hapo,
hakikisha kwamba humuelezi mtu yoyote juu ya
ujio wangu”
“Sawa, ila samahani bado sijakufahamu jina lako
kwa maana tunazungumza tu?”
“Mimi ninaitwa Rahab”
“Rahab asante kwa kukufahamu”
“Haya usiku mwema”
Rahab akakata simu na kumkabidhi mume wake.
Kwa mapenzi makubwa raisi Praygod
akamsindikiza Rahab bafuni na kumuogesha,
akamuandalia chakula cha kizuri ambacho mara
nyingi Rahab ukipenda chakula hicho.
***
Wanannchi wengi nchini Tanzania, walizidi kujikuta
wakiingia katika hali ngumu ya maisha, ukiachilia
mbali kupanda kwa uchumi na maisha kuwa
magumu, bali hata matumizi mabovu ya madaraka
yalizidi kuwaumiza. Kauli ya raisi Godwin ya
wananchi wote kupiga kura ya Ndio ya kubadilisha
mfuo wa kiserikali, kutoka katika mfumo wa raisi
hadi kwenye mfumo ufalma. Kauli hiyo ilizidi
kuzua mijadala kwenye sehemu nyingi ndani na
nje ya Tanzania. Nchi kubwa zenye ngumu duniani,
hususani na Marekani, ikaanza kutangaza vikwazo
kwa raisi wa Tanzania Mzee Godwin, kwamba
endapo mfumo wa kimadaraka utabadilika basi
wanasitisha urafiki kati ya nchi hizi mbili.
Swala hilo halikuweza kumtisha wa kumteteresha
raisi Praygod. Alicho kiamini ni kwamba anahitaji
kujitengenezea serikali yenye nguvu na
yakuogopwa ndani na nje ya bara la Afrika. Siku
iliyo pangwa kwa wananchi kuweza kupiga kura ya
kubadilisha mfumo wa kiserikali. Hapakuwa na
wananchi walio jitokeza kuweza kufanya hivyo,
hata wale ambao walikuwa wakimuunga mkono
raisi Godwin katika kipindi cha kampeni.
“Muheshimiwa kwa taarifa tulizo nazo, hakuna hata
mwananchi mmoja aliye jitokeza kupiga kura”
Mshauri wa Mzee Godwin alimuambia, mara baada
ya kupata taarifa hizo kutoka kwa mawakala walio
weza kuwatuma katika vituo vya kupigia kura nchi
nzima.
“Nini….??”
“Ndio hivyo mku”
Raisi Godwin alizungumza huku akinaynyuka
kwenye kiti chake cha ufalme ambacho tayari
kilisha endaliwa.
“Ndio hivyo muheshimiwa”
“Tuma vikosi vya polisi kuwatoa watu majumbani
mwao na hakikisheni wananchi wote wanakwenda
kupiga kura”
“Sawa mkuu, je endapo watakataa?”
“Watakao kataa wakamatwe na wawekwe rumande”
“Sawa mkuu”
Amri ikatolewa mara moja kwa makamanda wakuu
wa polisi(RPC) wa mikoa yote juu ya amri ambayo
raisi Godwin. Japo ni amri ya udikteka, ila polisi
ikawadi kuweza kufanya walicho agizwa. Polisi
wote wakaanza kupita nyumba moja baada ya
nyingine kuwachukua wananchi kinguvu na
kuwapeleka katika vituo vya kupigia kura. Kama
kawaida wapo wananchi ambao waliweza
kupingana na polisi, ila cha mtemakuni walikiona,
wengine baada ya kipigo wao wenyewe waliweza
kukubali kwenda na wengine walio kataa kabisa
waliweza kupelekwa rumande kama agizo la riaisi
Godwin lilivyo sema.
Vituo vya televishion na redio ndani na nje ya
Tanzania viliweza kurusha matangazo juu ya tukio
hilo la kusikitisha, viongozi wa nchi jirani zinazo
pakana na Tanzania walijikuta wakilaani kitendo
hicho na kushangazwa sana, kwani wengi kati yao
walihisi swala hilo lisinge fikia katika hatua ya
wananchi kuweza kulazimishwa kwa nguvu.
***
Taarifa ya ukatili unao endelea ndani ya Tanzania,
iliweza kumfikia Eddy majira ya asubu alipo weza
kufungulia televishion, huku akilini mwake akiwa
na lindi la mawazo kichwani mwake. Kwa jinsi
wananchi walivyo kuwa wakipatia kipigo na polisi,
kitu hicho kiliweza kumuumiza sana moyo wake.
Akazidi kumchukia baba yake Mzee Godwin
ambaye kwa sasa ndio anashikilia madaraka ya
nchi ya Tanzania. Eddy akajikuta akimwagikwa na
machozi, taratibu akanyanyua rimoti ya tv na
kuizima, hakuhitaji kuendelea kuiangalia taarifa
hiyo ambayo ilizidi kumachanganya.
Tangu nguo alizi zivaa jana hakuweza
kuzibadilisha kutokana na kuwa katika hali ya
msongamano wa mawazo. Akajizoa zoa kwenye
sofa alilo kalia na kunyanyuka, kwa lengo la
kwenda bafuni, kabla hajaufikia mlango wa
kuingilia bafuni, mlango ukagongwa. Taratibu
akauendelea mlango huo na kuufungua. Akamkuta
Sa Yoo akiwa amesimama, huku sura yake ikiwa
na tabasamu.
“Za asubuhi Eddy”
“Salama vipi?”
“Kuna yule mwanamke ambaye nilikuwa
ninazungumza naye kwenye simu aliye
tufahamisha kuwa yupo na madam Phidaya
amekuja”
“Kweli?”
“Ndio”
“Yupo wapi?”
“Nifwate”
Eddy hata swala la kuoga likamuondoka kichwani
mwake kwa haraka akaanza kumfwata Sa Yoo kwa
nyuma, wakaingia kwenye lifti na kushuka hadi
gorofa ya chini kabisa, wakaanza kutembea
kueleka kwenye sehemu yenye maegesho ya
magari. Wakalifikia gari ambalo amekuja nalo
Rahab, ambaye alipo muona Sa Yoo, akija na
mwanaume huyo, akafungua kioo cha gari.
“Munaweza kuingia ndani ya gari”
Kitendo cha Eddy kumuona Rahab, akahisi miguu
yake ikikosa nguvu kabisa, kwa maana
anamtambua vizuri Rahab.
“Kaka unaweza kuingia tu ndani ya gari”
Rahab alizungumza hivyo pasipo kugundua
kwamba mtu anaye zungumza naye ni Eddy hii ni
kutoka na Eddy kuibadilisha sura yake. Eddy
pasipo kuwa na ubishi akaingia ndani ya gari mara
baada ya Sa Yoo kuingia ndani ya gari hilo.
“Itakuwa ni vizuri kama tunaweza kwenda
kuzungumza mazungumzo hayo nyumbani
kwangu”
Rahab alizungumza huku akimtazama Eddy aliye
kaa siti ya nyuma. Eddy akatingisha kichwa chake,
hakuhitaji kuzungumza chochote kohofia sauti yake
kuweza kutambulika.
“Sa Yoo mwenzako anaonekana kuwa yupo serious
eheee?”
Rahab alimuuliza Sa Yoo huku akigeuza gari lake
na kuanza kutoka katika eneo hilo la hoteli.
“Anamawazo tu ya mk…..madam kutekwa”
Ilibi akili ya Shamsa kuweza kufanya kazi kwa
haraka, kwa maana anaelewa ni hali gani ambayo
anayo Eddy kwa wakati huu, na hata angesema
kwamba huyu ndio mume wa Phidaya
ingemshangaza hata Rahab kwa maana anavyo dai
anamfahamu Eddy vizuri.
Safari yao haikuchukua dakika nyingi wakawa
wamefanikiwa kuweza kufika katika nyumba anayo
ishi Shamsa na mume wake ambaye ni Raisi
Praygod. Kwa pamoja wakashuka kwenye gari na
kingia ndani. Eddy alipo muona raisi Praygod
akiwa amekaa kwenye sofa, akiitazama taarifa
inayo husiana na Tanzania.
“Honey tumerejea”
Raisi Praygod alipo waona akanyanyuka na
kuwakaribisha Sa Yoo na Eddy pasipo kuweza
kumtambua mara mojo kwa maana sura ambayo
Eddy ametengenezewa ni sura ambayo si rahisi
kwa mtu kuweza kuifahamu kwamba ni sura
bandia.
“Kama nilivyo weza kukueleza Sa Yoo. Phidaya
bado anashikiliwa na mume wake na inavyo
onekana wanaweza kuondoka ndani ya nchi hii
muda wowote na sinto fahamu ni wapi watakapo
elekea”
Eddy akataka kuzungumza kitu ila akanyamaza
kidogo, kitu kingine ambacho kinaweza kumsaidia
Eddy kuto kujilikana kirahisi ni jinsi mwili wake
ulivyo weza kujengeka kimazoezi. Watu walio weza
kumuona kipindi ni waziri wa ulinzi ni ngumu
kuweza kumgundua kwa haraka na ndivyo ilivyo
kwa Rahab na mumewe dokta Ranjiti.
“Sasa unapafahamu hiyo sehemu gani ambayo
waliweza kuwapeleka?”
“Kwa haraka haraka siwezi kupafahamu, ila
nakumbua jengo hilo kwa maana tulivyo ingia
niliweza kulitazama vizuri ila tulivyo toka sikuweza
kuliona kutokana nilifunikwa sura”
“Huyo atakuwa ni dokta Ranjiti ndio aliye mteka
madam Phidaya”
Sa Yoo alizungumza huku akiwa ameyatoa macho
yake makubwa kiasi kabla mtu yoyote
hajazungumza,
simu ya raisi Praygod ilita na kuwafanya watu wote
kukaa kimya Raisi Praygod akainyanyua simu yake
aliyo kuwa ameiweka mezani na kuitazama namba
ambayo inapiga, namba hiyo ni namba ngeni
kwenye simu yake na ni namba ya simu ya
mkononi. Taratibu dokta Ranjiti akaminya kitufe
cha kupokela na kuiweka simu yake kwenye sikio
la upande wa kulia, kuisikilizia simu hiyo.
***
Kipindi Rahab alipo kuwa anahatolewa katika jengo
la himaya ya dokta Ranjiti, kijana wake mmoja
aliweza kumchomolea simu Rahab pasipo yeye
mwenye kutambua. Walipo kamilisha zoezi la
kumtupa Rahab katika sehemu waliyo ona kwao
inafaa kumtupa wakarejea katika ngome yao.
Akaanza kuipekua semu ya Rahab kuanzia kwenye
majina yaliyo wekwa ndani ya simu hiyo hadi
picha. Aliweza kuona picha nyingi za Phidaya
akiwa amepiga na Rahab pamoja na mwanaume
mmoja ambaye hakuweza kumfahamu. Kutoka
usiku huo bosi wake aliendelea kuburudika na mke
wake aliye kuwa akimtafuta kwa muda mrefu,
kijana huyo ajulikanaye kwa jila la Adrus, aliweza
kusubiria hadi kulipo pambazuka na kwenda moja
kwa moja kwenye ofisi ndogo ya dokta Ranjiti,
iliyomo ndani ya jengo hilo. Kwa bahati nzuri
akamkuta akiwa yupo ndani ya ofisi hiyo,
wakasalimiana kwa kiarabu kisha akakaribisha na
kukaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza ya
dokta Ranjiti.
“Bosi kuna hii simu niliweza kumchomolea yule
binti tuliye muachi huru jana”
Adrus aluzingumza huku akimkabidhi dokta Ranjiti
simu hiyo, ambayo taratibu akaanza kuipekua
kama alivyo fanya Adrus, swali la kujiuliza kwamba
Rahab alikuwa ni mke wa raisi Praygod, liliweza
kupata uhakika baada ya kuona picha za raisi
Praygod akiwa amepiga na Rahab pamoja na
Phidaya. Katika kuchunguza chunguza akakuta
namba iliyo andikwa(Husband)
“Hii ni namba ya mume wake ambaye ni raisi wa
nchi ya Tanzania”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akimuonyesha
Adrus namba hiyo
“Bosi unaonaje ukamtumia mke wako kuweza
kujivunia pesa?”
“Kivipi?”
“Unaweza kumuambia kwamba ili kumpata rafiki
yao, basi watoe kiasi cha pesa ambacho utakihitaji
kisha tunawachezea pata potea”
“Hivi unahisi kwamba mpango wako unaweza
kuzaa matunda katika hilo?”
“Kama mtu ni raisi ninaamini kwamba kila kitu
kitakwenda salama na tutajipatia pesa nyingi za
kupunguza machongu ya kuweza kumtafuta mke
wako kwa kipindi chote hicho”
Dokta Ranjiti akafikiria kwa dakika kadhaa, mpango
alio shauriwa na kijana wake. Akaona kidogo ni
mpango wenye nguvu. Taratibu akaanza kuinakili
namba ya raisi Praygod kwenye simu yake, alipo
maliza, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha
akaipiga. Simu hiyo ikaanza kuita kwa muda kisha
ikapokelewa.
“Halooo, ninaamini kwamba wewe ni raisi
Praygod?”
“Ndio ni mimi”
Sauti hiyo ilisikika kutokea upande wa pili wa simu
“Unazungumza na Ranjiti, ninaamini kwamba
munamtafuta Phidaya, ambaye yupo mikononi
mwangu”
“Ndi………”
Mikwaruzano ikasikia upande wa pili wa simu na
kumfanya dokta Ranjiti kusikilizia vizuri
***
Eddy alipo isikia sauti ya Ranjiti kwenye simu ya
raisi Praygod, akasimama kwa haraka kwenye sofa
alilo kaa, kisha akaikwapua simu kutoa mkononi
mwa raisi Praygod na wafanya watu wote
wamshangae.
“RANJITI, SIKU NIKUKITIA MIKONONI MWANGU
NITAHAKIKISHA KWAMBA KICHWA CHAKO
KINAKUWA MALI YANGU”
“Wee…..weee si Eddy”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa wasiwasi mkubwa
“NDIO MIMI NI EDDY, MUME HALALI WA PHIDAYA”
Eddy alizungumza kwa sauti yanye msisitizo na
kuwafanya Rahab na raisi Praygod wote kushtuka
na kujikuta wakinyanyuka kwenye sofa na
kumshangaa, kwani kati yao hakuna aliye weza
kumgundua kwamba kijana huyo ni Eddy, ambaye
alikuwa ni waziri wa ulinzi katika serikali yao na ni
adui wa mapenzi wa raisi Praygoda, kwani aliweza
kugundua Eddy alishirikia tendo la ndoa na mke
wake kipenzi Rahab.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 70 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (70)
(Destination of my enemies)
WRITER……………………………..EDDAZARIA GERSHOM
MSULWA(Next level Author)
WEBSITE…………………………… www.storizaeddy
.blogspot.com
EMAIL…………………………………storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT…………………………….0657072588/
0768516188
ILIPOISHIA
Eddy alipo isikia sauti ya Ranjiti kwenye simu ya
raisi Praygod, akasimama kwa haraka kwenye sofa
alilo kaa, kisha akaikwapua simu kutoa mkononi
mwa raisi Praygod na wafanya watu wote
wamshangae.
“RANJITI, SIKU NIKUKITIA MIKONONI MWANGU
NITAHAKIKISHA KWAMBA KICHWA CHAKO
KINAKUWA MALI YANGU”
“Wee…..weee si Eddy”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa wasiwasi mkubwa
“NDIO MIMI NI EDDY, MUME HALALI WA PHIDAYA”
Eddy alizungumza kwa sauti yanye msisitizo na
kuwafanya Rahab na raisi Praygod wote kushtuka
na kujikuta wakinyanyuka kwenye sofa na
kumshangaa, kwani kati yao hakuna aliye weza
kumgundua kwamba kijana huyo ni Eddy, ambaye
alikuwa ni waziri wa ulinzi katika serikali yao na ni
adui wa mapenzi wa raisi Praygoda, kwani aliweza
kugundua Eddy alishirikia tendo la ndoa na mke
wake kipenzi Rahab.
ENDELEA
Simu ikakatwa na kumfanya Eddy kuishusha simu
hiyo kutoka sikioni mwake kwa hasira. Hakuhitaji
kuujali mshangao wa Rahab na raisi Praygod kwa
maana alitambua ya kwamba ni lazima watapata
mshangao huo ndio maana hakuhitaji sauti yake
iweze kusikika kwa Rahab na mumewe.
“Eddy ni wewe?”
Raisi Praygod alizungumza huku akiendela
kumshangaa Eddy aliyesimama, akionekana ni
mwingi wa hasira.
“Hilo ni jibu na si swali”
Eddy alizungumza huku akimrudishia simu raisi
Praygod. Eddy akamtazama Sa Yoo, na kumpa
ishara ya kunyanyuka ili waondoke.
“Ahaa hapana Eddy, tukae tuzungumze”
Raisi Praygod alizungumza kwa busara sana, huku
akimtazama Eddy machoni.
“Nikae wakati sifahamu mke wangu ni wapi alipo”
“Ndio maan mke wangu alimfwata huyo binti
akimini ya kwamba yupo peke yake na alihitaji
anahakikisha kwamba anamkomboa mkeo”
“Eddy, natambua haupo vizuri, hembu kaa basi
tuangalie ni nini cha kufanya kwa wakati huu, ili
kumuokoa Phidaya”
“Eddy kaa”
Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya upole. Taratibu
Eddy akakaa sehemu ambayo alikuwa amekaa kwa
mara ya kwanza.
“Ila ninawazo moja. Munaonaje tukaifwatilia simu
hiyo kupitia satelaiti”
Sa Yoo alizungumza huku akiwatazama watu wote,
Rahab akanyanyuka na kuwaomba wamsubirie.
Akaingia chumbani kwake, alipo toka akarudi akiwa
amebeba laptop aina ya Apple(macbook air), huku
mkono wake mwingine akiwa ameshika karatasi
mbili ndogo.
“Kuna namba za simu yangu ile nilizo zinunua,
hizi hapa”
Sa Yoo akanyanyuka na kusogea sehemu alipo
Rahab, akachukua karatasi hizo na kuzitazama
vizuri, akaiziona namba ambazo zimesajiliwa simu
hiyo na hata endapo itakuwa imezimwa, kwa
kupitia sateleitii ni lazima utaipata. Kwa haraka Sa
Yoo akaanza kuifanya kazi hiyo kutokana ana ujuzi
wa kazi hiyo.
Kila mtu macho yake akayaweka kwenye kioo cha
Laptop hiyo, inayo tafuta kwa kasi ni wapi ilipo
simu ya Rahab. Ndani ya sekunde arobaini na
moja, tayari ramani ikaanza kujitokeza kwenye
lapotop, alama ya kijana ikaanza kujionyesha
kwenye ramani hiyo ikiashiria kwamba ndipo
sehemu ilipo simu hiyo.
“Hii simu ipo katika mtaa El khaing, na sisi tupo
huku Al Kerdas. Ili kuweza kufika sehemu naamini
ilipo kambi hiyo ni lazima kupita katika daraja la
Qasr al-nil ili kuweza kufika. Na kwa haraka haraka
tunaweza kuchukua muda kama lisaa moja na
nusu hivi”
Sa Yoo alizungumza huku akiwaonyesha kwa
kidole jinsi ramani hiyo inavyo kwenda.
“Ila simu yangu nahisi kama niliipoteza walivyo
nitelekeza”
“Ulirudije huku?”
Sa Yoo alimuuliza Rahab huku akiwa
amemtumbulia macho
“Nilirudi kwa kukimbia, kutokana huo mtaa walio
niacha niliweza kuufahamu kwani ni kwa mara
kadhaa ni kichukua mazoezi asubuhi huwa ninapita
hapo”
“Ulilipita hili daraja?”
Ikambidi Rahab kuitazama vizuri ramani hiyo.
“Hapana sikupita”
“Basi, inabidi kuweza kuifwatilia simu hii sehmu
ilipo”
Sa Yoo alizidi kuzungumza kwa kujiamini na kwa
msisitizo mkubwa.
“Sa Yoo unaweza kuitafuta namba ya huyo Ranjiti
sehemu ilipo tokea”
“Yaa ngoja mara moja”
Sa Yoo akaaiombanamba hiyo na kuonyeshwa na
raisi Praygod, ndani ya dakika moja akafanikiwa
kujua ni wapi namba hiyo inapotokea.
“Sehemu ni ile ile kama nilivyo sema”
Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo huku
akiwaonyesha sehemu alama ya simu hiyo inapo
onekana.
“Inabidi twende muda huu huu”
Raisi Praygod alishauri, hapakuwa na mtu aliye
weza kupinga swala hilo, wakatoka wote huku Sa
Yoo akiwa ameibeba laptop. Wakaingia kwenye
gari, na Rahab akawa dereva wa safari hiyo.
***
Dokta Ranjiti akakata simu huku mwili mzima
ukiwa unamtetemeka, akahisi kitu alicho kisikia
labda inaweza kuwa ni ndoto. Adrus akabaki
akimtumbuli macho bosi wake huyo asijue ni kitu
gani ambacho amezungumza na mtu aliye mpigia
simu.
“Bosi”
Adrus aliita, ila dokta Ranjiti hakuzungumza
chochote zaidi ya kubaki akimtazama, Adrus aliye
jawa na shauku ya kuhitaji kujua ni kitu gani
ambacho kimetoka.
“Bosi kuna kitu gani kilicho endelea?”
“Amepokea EDDY”
“Eddy ndio nani?”
Dokta Ranjiti hakujibu kitu chochote zaidi ya
kunyanyuka kwenye kiti alicho kalia, akatoka ofisini
kwake pasipo kulijibu swali la Adrus, moja kwa
moja akaelekea chumbani alipo muacha Phiday,
akamkuta akitoka bafuni kuoga.
“Vaa vaaa nguo tunaondoka”
Dokta Ranjiti alizungumza huku jasho likimwagika,
mwili mzima. Phidaya akagundua kwamba kuna
tatizo ambalo limetokea kwa Ranjiti.
“Tnakwenda wapi?”
“Kwani hapa ni kwako. Vaa tuondoke sasa hivi”
Ikambidi dokta Ranjiti aanze kutafuta nguo za
Phidaya alizokuwa amezitupa chini, kipindi
akimlazimisha kufanya tendo la ndoa.
“Vaa vaaa…mama”
Ranjiti akaendelea kumsisitiza Phidaya, ambaye
akaanza kuvaa huku kichwani mwake akijiuliza ni
nini kinacho endelea. Alipo maliza kuvaa nguo
zake, dokta Ranjiti akamshika mkono na wote
wawili wakatoka kwenye chumba hicho na moja
kwa moja dokta Ranjiti akaelekea sehemu kulipo
na gari lake.
“Adrus ingia ndani ya gari munisindikize bandarini”
“Sawa mkuu”
Adrus akaingia ndani ya gari, akawasha gari hilo
aina ya BMW X5. Wakati wote huo Phidaya, alikaa
kimya, ila moyoni mwake akawa anaomba Mungu
amsaidie lolote liweze kutokea, ila si kuendelea
kukaa mikononi mwa Ranjiti. Wakaondoka eneo la
ngome yao kwa mwendo wa kasi hadi walinzi
wengine wakabaki wakishangaa.
***
Madam Mery baada ya kuamka moja kwa moja
akaelekea chumbani kwa Eddy kutazama kama
yupo, ila hakumkuta. Hakuwa na wasiwasi wowote
zaidi ya kuamua kueleka katika chumba wanapo
lala Shamsa na Sa Yo, akaugonga mlango mara
tatu, hakusikia kitu chochote, alicho kifanya ni
kuusukuma mlango huo na kuukuta upo wazi,
akaingia ndani na kumkuta Shamsa akiwa amelala
kitandani. Akamsogelea huku akimuita jina lake, ila
Shamsa hakuitika. Akafika kitandani na kuanza
kumtingisha, ila Shamsa hakuitika, kitu kilicho anza
kumpa wasiwasi madam Mery. Akajaribu kumpima
mapigo yake ya moyo na kukuta yakiwa hayafanyi
kazi.
“Mungu wangu”
Madam Mery alistuka, kiasi cha kuanza kutokwa na
kijasho chembamba usoni mwake.
“SHAMSA, SHAMSA, SHAMSA”
Madam Mery akajaribu kumtingisha tena, ila
Shamsa hakujibu chochote, Madam Mery kwa
haraka akanyanyuka kitandani hapo, kwa haraka
akafungua mlango wa bafuni na kuchungulia kama
Sa Yoo atakuwepo, ila hakukuta
mtu.
“Sa Yoo, Sa Yoo”
Madam Mery kwa kuchanganyikiwa, alijikuta akiita
huku akimtafuta Sa Yoo hadi ndani ya kabati la
kuhifadhia nguo. Hakumkuta mtu, wazo la kuomba
msaada katika uongozi wa hoteli hiyo ukamjia
kichwani, akataka kukimbia na kutoka nje, ili
kwenda kuwaita, ila akahisi kwamba atachelewa
zaidi, akaisogelea simu iliyopo mezani na kuminya
namba za wahudumu.
“Nahitaji msaada”
Madam Mery alizungumza kwa sauti iliyo jaa
wasiwasi mwingi, muhudumu akauliza ni chumba
namba, ngapi. Akamtajia namba ya chumba.
Hazikupita dakika tatu wahudumu wawili wa kike
walio valia sare zilizo wakaa vizuri mwilini mwao,
wakaingia ndani ya chumba hicho.
“Mwanangu hapa anatatizo”
Madam Mery alizungumza huku akiwaonyesha
wahudumu hao sehemu alipo Shamsa. Wahudumu
hao, wakamsogela Shamsa, wakajaribu
kumtingisha, kila mmoja wasiwasi ukamuingia
kwani Shamsa hakujibu chochote. Muhudumu
mmoja akajaribu kumpima kama ana pumua, ila
jibu alilo lipata ni sawa na jibu alilo lipata Madam
Mery.
“Piga simu kitengo cha dharura”
Muhudumu huyo alimuambia muhudumu
mwenzake, kwa haraka akatoa simu zao maalumu
wanazo zitumia wakiwa kazini, akapiga simu
kwenye kitengo cha dharura kilichopo hapo
hotelini. Muhudumu akaelezea tatizo lililomo ndani
ya chumbu hicho.
“Tunakuja”
Sauti nzito ya kiume ilizungumza, na simu
ikakatwa.
“Amefanya nini huyu?”
Muhudumu mmoja alimuuliza Madam Mery,
ambaye macho yote yalisha anza kutwaliwa na
wekundu na machozi kwa mbali yalisha anza
kumwagika.
“Mimi sifahamu nimekuja kuwatembela asubuhi,
wezake hawapo nay eye nimemkuta hapo kalala,
nimemuita ila hakujibu chochote.”
“Mwenzake ameenda wapi?”
Kabla madam Mery hajajibu chochote, mlango
ukafunguliwa, wakaingia wanaume watatu huku
wote wakiwa wamevalia makoti meupe, mmoja wao
akiwa amevalia kipimo cha kupimia mapigo ya
moyo shingoni mwake. Kwa haraka haraka Madam
Mery akatambu kwamba hao watakuwa ni
madaktari.
“Mgonjwa yupo wapi?”
Dokta aliye valia kipimo hicho alizungumza,
muhudumu mmoja akamuonyesha kwa kidole.
Pasipo kupoteza muda daktari huyo akaanza
kumpima Shamsa kifuani mwake. Madam Mery
alipo yatupia macho yake usoni mwa dokta huyo
akagundua kwamba kuna tatizo, kwa maana sura
ya daktari, ilanza kubadiliika kila alipo jaribu
kukihamisha hamisha kipimo chake kifuani mwa
Shamsa.
***
“Ngoja ngoja mara moja”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakiwa yametoka
akiitazama laptop. Alama inayo onyesha simu ya
dokta Ranjiti lianza kutembea. Kitu kilicho ashiria
kwamba dokta huyo anaondoka katika sehemu
alipo kuwepo.
“Kuna nini?”
Rahab aliuliza huku akipunguza mwendo kasi wa
gari.
“Anaondoka katika eneo alilo kuwepo”
Sa Yoo aliye kaa siti ya nyuma na Eddy
alimuonyesha Eddy kwa kidole.
“Hembu nione”
Rahab alizungumza na kumfanya Sa Yoo kumpa
laptop, hiyo. Rahab akasimamisha gari pembani na
kuanza kuangalia ramani hiyo. Akashuhudia jinsi
alama hiyo inavyo tembea kwa kasi kueleka
upande mwingine ambao si ule ambao wanao
tokea.
“Honye hembu naomba umpishe Sa Yoo akae hapa
mbele”
Raisi Praygod hakubisha, Sa Yoo akapita katikati
ya siti baada ya raisi Praygod kushuka, kisha
akaka mbele na kuichukua laptop hiyo.
“Naamini unatambua kazi ambayo imekuweka hapa
mbele”
“Ndio, twende”
Rahab akawasha gari na kuanza kuondoka kwa
mwendo wa kasi kiasi, kila muda ulivyo zidi
kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kuongeza mwendo
kasi wa gari. Sa Yoo kazi yake ikawa ni kumpa
maelekezo ya kuweza kukunja katika njia za
vichochoro zinavyo onekanana kwenye ramani hiyo
ili kuweza kuiwahi gari hiyo.
“Tunaikaribia, ipo kama kilomita moja mbele”
“Usijali”
Kwa muda wote huo, Eddy hakuzungumza kitu cha
aina yoyote, akilini mwake akawa anafikiria ni
adhabu gani ambayo anaweza kumpatia dokta
Ranjiti pale tu atakapo mtia mikononi mwake.
Picha ya jinsi Phidaya akiingiliwa kimwili na dokta
Ranjiti ikaanza kumjia kichwani mwake, jambo lililo
mfanya hasira yake izidi kumpanda. Raisi Praygod,
mara kwa mara akawa anamtazama Eddy kwa
jicho la kuiba, akaweza kugundua hasira aliyo
kuwa nayo Eddy, kwa maana kwa mara kadhaa,
aliweza kuona jinsi kifua chake, kinavyo panda na
kushuka kwa kuhema kwa nguvu. Breki za gafla
alizo zifunga Rahab, zikamstua Eddy na kumtoa
kwenye dibwi la mawazo mabaya aliyo kuwa nayo.
“Fala kweli huyu”
Rahab alizungumza huku akiminya honi, akimpigia
dereva wa gari ndogo aliye simama gafla
barabarani kwa lengo la kugeuza, pasipo
kuonyesha ishara yoyote.
“Pita huko pembeni”
Raisi Praygod alimshauri, Rahab akafanya hivyo,
uzuri ni kwamba Rahab, katika swala zima la
uendeshaji wa gari yupo makini sana na ni
mtaalamu wa kufanya hivyo. Alipo hakikisha gari
limekaa sawa barabarani, akaendelea kuongez
amwendo kasi wa gari hilo.
“Inavyo onyesha hapa, wanaelekea baharini”
Sa Yoo alizungumza huku akiitazama Ramani hiyo.
“Si tunakaribia kuwafikia?”
“Ndio, tunawawahi”
Rahab kusikia hivyo, ikawa ndio kama
ametekenywa, akazidi kuendesha gari hilo kwa
kasi, hadi mlio wa hatari ukaanza kupiga taratibu.
Kila mtu ndani ya gari akawa kimya, hakuna aliye
hitaji kumshauri Rahab kupunguza mwendo, kwani
wote lengo lao ni kumuwahi dokta Ranjiti
asikimbie, wakiamini atakuwa yupo na Phidaya.
***
Adrus alizidi kuongeza mwendo kasi wa gari,
pasipo kujua kwamba wanafwatiliwa. Alicho weza
kukiamini hapo ni kufwata amri ya bosi wake,
ambaye alimuamuru kuendesha kwa kasi ili
kuweza kuwahi boti inayo ondoka saa sita kamili
machana. Simu ya dokta Ranjiti ikatoa mlio
mmoja, ulio mfanya kuitoa simu yake mfukoni.
“Ahaaa”
Dokta Ranjiti alitoa mguno wa kukasirika, kwani
simu yake imeonyesha alama ya kuishiwa kwa
chaji.
“Simu linazima chaji, alafu sijawampigia nahodha
wa boti anisubiri”
“Mpigie kabla haijazima”
Adrus alishauri na kumfanya dokta Ranjiti kupiga
simu kwa nahodha wa boti anayo iwahi. Simu ya
nahodha huyo ikaanza kuita, baada ya sekunde
kadhaa ikapokelewa.
“Haloo”
“Vipi muheshimiwa Ranjiti”
“Safi nipo karibu na bandari hapo nahitaji kusafiri
kwenye boti yako”
“Ohooo muheshimiwa leo sijaingia kazini nipo
likizo, labda nikupatie namba ya nahodha
mwengine”
“Sawa fanya hivyo”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akikata simu.
Simu yake ikarudia kupiga mlio wa kuishiwa na
chaji. Baada ya dakika moja meseji ikaingia,
kitendo cha dokta Ranjiti kuufungua ujumbe huo
wa meseji, simu ikazima chaji na kumfanya macho
yamtoke na kukasirika.
***
“Shiitiiiii SIGNAL IMEPOTEA”
Sa Yoo alizungumza huku macho yakimtoka,
alama aliyo kuwa akiifwatilia ilipotea kwenye
ramani inayo waongoza.
“Unasemaje?
“Rahab aliuliza huku naye macho yakimtoka, Sa
Yoo akamgeuzia laptop ili kudhibitisha kwamba ni
kweli alama hiyo imepotea.
“Sasa tutafanyaje?”
Rahab aliuliza kwa sauti inayo onyesha kukataa
tamaa, jambo lililo mfanya Eddy kuzidi
kuchanganyikiwa.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 71 YA SIMUHILI HII.
 
Story Za Eddy
SORRY MADAM 71
WRITTER……………………………………….EDDAZARIA
G.MSULWA
www.storyzaeddy.blog.com
UNAWEZA KUJITOLEA KATIKA KUIKUZA KAZI
YANGU HII YA UANDISHI IKIWEMO, KUSAIDIA
UCHAPISHAJI WA KITABU CHANGU CHA MY
MOMMY’S FRIEND SIMI NO 0657072588(Tigo
pesa) AU 0768516188(m-pesa)
ILIPOISHIA
“Nafanya hii, kwa ajili yakulipiza kisasi cha mume
wangu”
“Ngoja kwanza, nipo tayari kufa, ila ninakuomba
usimuue mke wangu”
Nilizungumza kwa ujasiri, nikiwa nipo tayari kwa
kufa, Madam Mery akalinyanyua panga lake juu,
akalishusha kwa kasi kwenye mkono wangu wa
kulia
ENDELEA
Nikatoa ukulele mkali, ulio mfanya madam Mery
kusitisha zoezi lake kuukata mkono wangu, panga
lake likiwa limesimama sentimita chache kutoka
ulipo mkono wangu
“Madam, ninakuomba unisamee”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea
kunimwagika usoni mwangu, madam Mery
akanitazama kwa macho ya hasira yaliyo jaa ukatili
mkubwa, akawatazama Victoria na John ambao
macho yao yote yalikuwa kwetu
“Natambua kwamba mimi nimkosaji sana kwako,
ninastahili kufa mbele yako, ila si mbele ya macho
ya mke wangu.Mtazame jinsi alivyo katika hali
yake.Mule ndani amebeba kiumbe kama ulicho
kuwa umekibeba wewe, miezi tisa, na Derick
akakiangamiza mbele yetu.Yule ni mwanamke
mwenzako ambaye anauchungu kama wewe”
Nilizungumza huku machozi yakiendelea
kunimwagilka usoni mwangu, madam Mery kwa
mbali machozi yakaanza kumlenga lenga, macho
yake yamebadilika rangi na kuwa mekundu kiasi
huku sura yake ikiwa imejaa mikunjo kwenye paji
lake la uso akinitazama kwa uchungu sana
“Mery mimi pia ni binadamu, kumbuka ni mambo
mangapi tuliyafanya tukiwa pamoja, vuta
kumbukumbu ni vitu vingapi tulishiriki tukiwa
pamoja, Eheeee, leo hii unataka kuimwaga damu
yangu, leo hii unataka kunisulubu kikatili, le……..”
“Eddy STOP TALKING”(Eddy nyamaza kuzungumza)
Madam Merry alizungumza kwa sauti ya juu, yenye
uchungu ndani yake.Akalitupa chini panga lake
alilokuwa amelishika.Machozi mengi yakaanza
kumbubujika usoni mwake, John na Vivtoria
wakabaki wakimtazama madam Mery, ambaye
taratibu alianza kupiga hatua za kuelekea kwenye
gari lake alilo kuja nalo
“Madam Vipi?”
John alizungumza huku akimwafwata madam Mery
kwa nyuma
“John ninakuomba uniache”
Madam Mery aluzungumza huku akiunyanyua
mkono wake mmoja akimzuia John asimfwae
anapo elekea
“Ila madam haya sio makubaliano yetu”
“John sipo sawa nimekuambia usinifwate”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya ukali, huku
machozi yakiendelea kumchuruzika usoni mwake.
“Sasa Madam tumfanye nini Eddy?”
Madam Mery akageuka kwa hasira, hadi John
akastuka kidogo, akanitazama jinsi machozi
yanavyo nimwagika, akayafumba macho yake kwa
sekunde kadhaa, akionekana akifikiria kitu cha
kufanya juu yangu.
“Kesho nimkute akiwa hai”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya upole,
kisha akaelekea lilipo gari lake, akafunguliwa
mlango na mlinzi wake, akaingia ndani ya gari na
wakaondoka zao.John akalisindikiza magari ya
Madam Merry yanayotoka kwenye geti kubwa la
Godauni, lilipo fungwa taratibu John akanigeukia,
akanitazama kwa macho ya dharau huku Victoria
akiwa amejichokea, kwani ninaamini mipango yao
waliyo kuwa wameipanga dhidi yangu
imeharibika.John akamfwata Victoria sehemu alipo
simama, wakanong’onezana kwa muda kisha
wakamtama Phidaya ambaye muda wote, amejilaza
chini huku machozi yakimwagika kwa uchungu
“Mchukueni huyo Malaya mumrudishe mulipo
mtoa”
John aliwaamrisha watu wake, wakamnyanyua
Phidaya na kumbeba juu juu, japo anajitahidi
kujitoa mikononi mwa watu walio mbeba, huku
aikiliita jina langu kwa sauyti ya juu, ila
hakuifanikiwa kujitoa mikononi mwao
John akapiga hatua hadi katika sehemu nilipo
fungwa, akanitazama kwa muda, huku macho yake
yakiwa yamejaa dharau kubwa, akanitemea mate ya
usoni, akiyasindikiza kwa kofi zito lililo tua kwenye
shavu langu la kushoto
“Mmmmmm Eddy, unajisikiaje?”
John alizungumza huku akivifikisha viganja vyake,
na kuvipuliza taratibu taratibu.Akanishika sikio
langu la upande wakulia, akaanza kulivuta kwa
nguvu zake zote, nikaendelea kuugulia maumivu
ndani kwa ndani, sikutoa sauti yoyote kwenye
kinjwa changu
“Waooo, unajifanya komandoo usikii maumivu
eheeee?”
John alizungumza, huku akiliachia sikio
langu.Akaanza kunitandika vibao mfululizo kwenye
mashavu yangu, hasira ikazidi kumiliki nafisi
yangu.
“John, tumpeleke kisimani, hapo unajisumbua
bure”
Victori alitoa wazo ambalo John alilikubali,
wafanyakazi wao wakanishusha kwenye meza,
majamaa wawili wakanibeba kwenye mabega yao.
kama wawindaji walio beba swala waliye muua
kwenye mawindo yao.Tukaingia kwenye moja ya
ukumbi mkubwa wenye mwanga hafifu, unao pita
kwa kutumia madirisha machache yaliyopo juu
yake.Wakanibwaga chini, na kunifanya nitoe
mguno wa maumivu kutokana na kujiumiza
sehemu ya paja langu, nililo pigwa risasi
Taa kubwa zenye rangi nyeupe zikawaka na
kulifanya eneo zima la ikumbu kuponekana vizuri,
kuna mashimo makubwa mawili, kwa haraka
nikatabua ndio hivyo visima wanavyo vizungumzia,
mabaunsa walio kuwa wamenibeba, wakaufunga
mwili wangu kwa kamba ngumu aina ya manila.
“Eddy utakufa kifo kibaya sana”
John alizungumza huku akiwa ameniinamia
“Usiombe nikatoka, kwenye mikono yeno, utajuta”
Nilizungumza kwa kujiamini sana, John akaanza
kucheka kwa dharau, huku akinipiga piga
mashavuni mwangu
“Eddy huwezi kutoka mikononi mwangu, nakujua
wewe vizuri sana.Huwezi fanya chochote dhidi
yangu.Muda wako umekwisha kaka”
“Angalia wakwako ndio utakuwa umekwisha”
John akaanza kunipiga mateke mfululizo kwenye
mbavu zangu, nikaendelea kutoa sauti ya maumivu
ila John hakunionea huruma zaidi ya kuendelea
kunipiga kwa nguvu zake zote
“Mchukueni na mukamdumbukize kwenye kisima”
John aliwaamrisha watu wake, wakanibeba, kabla
hawajaondoka na mimi, Victoria akawazuia.Akapi
ga hatua hadi sehemu tulipo simama
“Eddy nakupenda kaka yangu, kwaheri”
Victoria alizungumza huku akinibusu shavuni
mwangu, akawarusuhu watu kuonipeleka kwenye
kisima kilichopo kwenye huu ukumbi, kwa jinsi
walivyo nifunga kamba mwili wangu sikuweza
kufanya kitu cha aina yoyote zaidia ya mwili wangu
kunyooka moja kwa moja, mithili ya mtu aliye fariki
dunia.Wakanifunga kwenye kamba nene, tartibu
wakaanza kunishusha kwenda chini, taratibu.Giza
jingi lililo tawala ndani ya shimo hili, likazidi
kuniogopesha na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa
.Nikastuykia nikigusa chini, kwenye shimo hili
lenye futi zaida kumi na mbili.
Gafla nikaanza kuhisi vitu vidogo vidogo
vikinitambalia mwilini mwangu, nikastukia mwili
wangu ukianza kupata maumivu maklali yaliyo
tokana kung’atwa na wadudu wadogo ambao
sikujua ni waduudu wa aina gani, jambo lililo
nifanya nitoe ukelele mkali sana
ITAENDELEA
 
SORRY MADAM (81)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
ILIPOISHIA
Mlango wa kuingilia sebleni mwa Agnes
ukagongwa na kumfanya anyanyuke na kwenda
kuufungua. Sauti za makelele ya kike zikasikika na
kumfanya Eddy kustuka. Wakaingia wasichana
wengi huku mmoja akiwa ameshika keki kubwa
huku wakiimba wimbo wa’ Happy birthday to you’.
Wasichana hao wanao onekana kwamba ni
miongoni mwa wafanyakazi wezake huku watatu
wengine aliwaona jana usiku wakiwa na marafiki
zake Agnes hawakumtisha sana Eddy. Ila msichana
wa mwisho kuingia hapo ndani ndio alimstua Eddy
na kumfanya asimama huku akiwa amemkodolea
macho. Hakuwa mwengine bali ni MANKA,
msichana ambaye ni dada yake wa damu moja, ila
ni adui yake namba moja.
ENDELEA
Eddy akashusha pumzi taratibu huku akiwatazama
wasichana hao walio ingia na kuanza kumkumbatia
Agnes na kumpiga mabusu ya shavu. Hakutaka
kabisa kumtazama Manka ambaye alimtazama kwa
muda na kuachia tabasamu pana. Wasichana
baadhi wakawa wamemkazia macho Eddy, kila
mmoja aliwaza lake kichwani mwake.
“Kaleteni maji tumuogeshe”
Msichana mmoja alizungumza na kumfamfanya
msichana mmoja kati ya wasichana aliye waona
jana usiku kuondoka hapo sebleni na kuelekea
jikoni, akarejea akiwa ameshika kindoo kidogo
kilicho jaa maji. Pasipo kujali wakamwagia Agnes
maji yote huku wakishangilia.
“Jamani ni suprize gani hii?”
Agnes alizungumza huku akitabasamu.
“Wewe ulitaka tukuambie ili utukimbie”
“Fetty kweli mumeniweza leo”
Eddy hakuzungumza chochote zaidi ya
kuyakwepesha macho yake na Manka ambaye
mara kadhaa alimtazama Eddy huku akiiachia
tabasamu. Wakaiweka keki mezani na kuizunguka,
mmoja wao akawasha kiberiti na kuiwasha
mishumaa midogo iliyopo juu ya keki hiyo.
“Haya mtoto njoo uzime mishumaa”
Agnes akainama karibu na meza, akaipuliza
mishumaa hiyo, iliyo zimika kwapamoja, watu wote
wakashangilia.
“Weee Paulina umeacha Shampen kwenye gari”
“Ohooo ngoja nikailete”
Paulina akatoka na baada ya muda akarudi na
mizinga mitatu ya shampen, akamkabidhi Anna,
Halima na Fetty, wote kwa pamoja wakazifungua
chupa hizo na kuwafanya wasichana wengine
kushangilia.
“Jamani kabla hatujaendelea mbele ninahitaji
kuwatambulisha”
Agnes alizungumza maneno yaliyo wafanya watu
wote kukaa kimya na kumsikiliza. Manka moyo
wake akaihisi unataka kutoka kwa kumdunda,
baada ya kuyasikia maneno hayo ya Agnes. Agnes
taratibu akapiga hatua hadi alipo simama Eddy,
akaupitisha mkono wake wa kulia kiunoni mwa
Eddy huku mkono wa kulia akiuweka kifuani mwa
Eddy.
“Jamani huyu ni mchumba wangu, anaitwa
Erickson Forrd”
“Erick hawa ni marafiki zangu, yule pale anaitwa
Fetty, yule pale anaitwa Halima, yule pale anaitwa
Anna na huyu hapa anaitwa Manka. Hawa wengine
ni wafanyakazi katika wizara yangu”
Agnes alizungumza kwa sauti ya kujidai, kitu
kilicho zidi kumuumiza Manka moyo wake.
“Nashukuru kuwafahamu”
“Hata sisi shemeji”
Mmoja wa wasichana alizungumza na kumfanya
Eddy kutabasamu. Halima akeelekea kwenye friji
akarudi akiwa emebeba mizinga mikubwa ya
wicky.
“Jamani ni self service sasa nyinyi shangaeni
shangeni”
Halima alizungumza huku akijimiminia wcky
kwenye glasi.
“Honey utatumia hii?”
“Hapana, naomba unielekeze toilet”
Eddy alimnong’oneza Agnes sikioni mwake. Agnes
akamshika Eddy mkono na kuwaeleza wezake
kwamba wanarudi muda si mrefu. Wakaondoka
sebleni huku Agnes akiwa amemshika mkono
Eddy. Manka akawasindikiza kwa macho nusu
machozi kumtoka ila akajikaza ili asijulikane.
“Vipi Manka mbona macho yamekuwa mekundu
gafla?”
Halima alimuuliza Manka, baada ya kumtazama
jinsi anavyo watazama Agnes na Erickson.
“Ahaa hapana kichwa kidogo kinanisumbua”
“Nikuletee dawa”
“Hapana, mimi ngoja niondoke nikapumzike
nyumbani”
“Ila shuhuli haijaisha”
“Tutaonana baadaye hotelini kwenye tafrija tuliyo
panga”
“Sawa, ila kuwa makini barabarani”
“Usijali”
Manka akachukua kipochi chake kidogo kwenye
sofa, akawaaga watu wengine na kuondoka,
moyoni akiwa amejawa na uchungu mwingi kiasi
kwamba akahisi kufa kufa. Akaingia kwenye gari
lake, na kuondoka kwa kasi hadi mlinzi akabaki
amemkodolea macho.
Agnes na Eddy wakaingia wote choo kilichopo
ndani ya chumba cha Agnes. Eddy akashusha
pumzi nyingi akijitahidi kuishusha hasira yake ya
kumuona Manka mbele ya macho yake.
“Honey mbona unashusha pumzi hivyo?”
“Ahaaa ujue sikutegemea kuona watu wengi wakija
kwako”
“Yaani wee acha tuu mimi wameniboa, japo kuwa
leo ni siku yangu ya kuzaliwa, ila wasinge nifanyia
suprize kama hii”
“Mmmm mimi huko nje sitoki tena”
“Jamani honey, unaogopa wasichana eheee?”
“Sio nawaogopa kwa maana sipendi kukaa karibu
na watu wengi”
“Basi nisubirie humu ndani nikawazuge zuge kisha
nitarudi baada ya muda mfupi sawa baby”
“Poa”
Agnes akambusu Eddy mdomoni na kutoka
chooni. Eddy akasubiria kwa muda hadi alipo sikia
mlango wa chumbani ulipo fungwa, akatoka chooni
na kusimama nje ya mlango wa choo hicho na
kuanza kuangali jinsi chumba cha Agnes kilivyo
pangika vizuri. Kwa asilimia kubwa chumba cha
Agnes kimejaa midoli mingi sana huku kitanda
chake kikiwa ni cha duara.
“Wanao kula pesa ya serikali hawa”
Eddy alizungumza huku akijirusha kwenye kitanda
hicho kinacho onekana ni kitanda cha gharama
sana.
‘Kama Manka hajanijua basi kazi yangu inakwenda
kuwa rahisi sana’
Mlango ukafunguliwa, Agnes akarudi huku akiwa na
furaha. Agnes akajirusha kitandani na kulala
pembeni ya Eddy.
“Mbona umewahi kurudi hivyo”
”Ahaa watu wameondoka wamekwenda kujiandaa
badae kuna pati wameamua kunifanyia Serena
Hotel”
“Waoooo hongera”
“Asante ila honey si tutakwenda wote?”
“Sawa, ila si kutakuwa na watu wengi?”
“Hapana ni watu wachache walio alikwa”
“Mmmmm basi sawa tutakwenda”
“Kweli baby?”
“Ndio”
Kwa furaha Agnes akampandia Eddy juu na
kumkalia kiunoni, kwa mara ya kwanza wakaanza
kunyonyana midomo, kila Eddy alipo pitisha
mikono yake Agnes alitoa miguno ya raha, iliyo
fufua uhai wa tango la Eddy.
“Erickson nakupenda sana”
Agnes alizungumza huku, akizidi kulegea. Kwa jinsi
Eddy alivyo yaminyaminya maziwa yake ndivyo
jinsi Agnes alivyo zidi kuchanganyikiwa na
kupagawa. Agens akavua nguo zote na kubaki
kama alivyo zaliwa. Akamvua Eddy nguo zake zote,
kitu kilicho mfanya Agnes kushangaa ni tango la
Eddy lilivyo simama huku likinesa nesa.
“Ahaaaaaa….”
“Mbona unashangaa?”
“Mmmmm”
Agnes aliguna huku akilishushia tango la Eddy
mdomo taratibu hadi kwenye lipsi zake , akautoa
ulimi wake taratibu na kuanza kuuchezesha
chezesha kila upande wa tango hilo na kumfanya
Eddy kutoa miguno. Agens akalidumbukiza nusu
ya tango mdomoni mwake na kuanza kulinyonya
taratibu.
Kwa midadi Eddy akamchomoa Agnes kwenye
tango lake na kuminamisha kitandani, kazi ya
kulila tunda la Agnes ikaanza.
“Eri…….. Uuu…..unaniu……aaa”
Agnes alizungumza huku aking’ata shuka lake,
kwa maana kwa kasi anayo kwenda nayo Eddy,
hakuwahi kukutana nayo kwenye maisha yake hata
kipindi alipo kuwa anajiuza hakuwai kukutana na
mwanaume kama Eddy anaye mjua kwa jIna la
Erickson Forrd. Kwa utamu anao upata Agnes
akajikuta akimwagikwa na machozi mengi, huku
akiendela kujitahidi kuling’ata shuka lake. Kwa
dakika ishirini pasipo kupumzika, Eddy akafika
kileleni na kumuachia Agnes, aliye lala kifudifudi
huku akihema taratibu kana kwamba anataka
kupoteza fahamu. Baada ya muda Agnes
akajigeuza taratibu na kulala chali huku
akimtazama Eddy kwa macho ya kusinzia.
“Eheeee Erickson ungeniua aisee”
“Kwa nini?”
“Mmmm sijapata ona, yaani umenipelekesha hadi
nimekojoa zaidi ya mara sita”
“Pole”
“Pole ya nini wakati umenifanya kitu ambacho
hakuna mwaume aliye wahi kunifanya”
“Usijali nitakufanya hivi kila siku”
“Mmmmm utanifanya nimuue yoyote atakaye
kutamani”
‘Amuue yoyote, na Phidaya je?’
Eddy aliwaza akilini mwake huku akimtazama
Agnes huku akiwa ametabasamu.
“Mimi nina wivu sana, sitaki hata mwanamke
mmoja akushike hata mkono”
“Sasa huo utakuwa ni wivu wa kijinga kwa maana
mimi nimtu mzima ambaye najitambua”
Eddy alizungumza kwa sauti ya msisitizo iliyo
mfanya Agnes kukaa kimya kwa maana ndio
kwanza penzi lake linaanza na isitoshe
hajamchunguza Erickson na wala
hawakuzungumza chochote juu ya hayo
mahusiano waliyo yaanzisha zaidi ya yeye kuwa na
kiherehere cha kumtambulisha kwa marafiki zake.
“Ok tuachane na hayo honey, hivi nyumbani kwako
wewe ni wapi?”
“Ahaa mimi naishi Mbezi”
“Mbezi ipi?”
“Mbezi ya kimara”
“Ahaaaa, usione ninakuuliza maswali mengi ila si
unajua ni vyema kuweza kujua mpenzi wako
anafanya nini, anaishi wapi hata kukitokea tatizo
iwe ni rahisi kuweza kujua mtu unaanzia wapi”
“Ni kweli”
Agnes akataka kumuuliza Erickson ni kazi gani
anayo ifanya ila akasita ili kutoa kuiharibu furaha
ya mpenzi wake huyo kwa maana kwa haraka
haraka Agnes aligundua kwamba Erickson ni mtu
mwenye hasira za karibu sana.
“Nakuomba nioge, kisha nikimbie nyumbani haraka
kwenda kubadili nguo kisha nitarudi hapa kwako
twende wote pamoja kwenye sherehe yako”
“Sawa mpenzi twende tukaoge”
Wakanyanyuka kwa pamoja na kuelekea bafuni,
huku Agnes akiwa amejawa na furaha kubwa.
***
Shamsa kwa siku nzima furaha yake akaihisi
inakwenda kupotea, kwani tangu mke asubuhi
hajamuona Eddy hadi inafika jioni. Akaelekea
chumbani kwa Eddy na kugonga, ila hakujibiwa,
akajaribu kusukuma mlango akakuta umefungwa.
Akaondoka na kuelekea sehemu ya baharini
kwenye vibanda vingi vya kupumzikia. Akamkuta
Phidaya akiwa amekaa peke yake huku akioneka
kuwa mwingi wa mawazo.
“Mama”
Shamsa aliita huku akikaa kwenye kiti cha
pembeni, Phidaya akamgeukia huku macho yake
yakiwa yamelengwa lengwa na machozi.
“Mama mbona unalia”
Phidaya akajifuta machozi yake kwa haraka haraka.
“Ahaa hapana hakuna kitu”
“Mama ninakujua vizuri, kwa nini unalia. Niambie
tafadhali kama kuna tatizo ninaweza kukusaidia
hata kwa mawazo”
Shamsa alizungumza huku akiwa na wasiwasi
moyoni mwake akihisi labda ishu aliyo ifanya jana
na Eddy imegundulika. Phidaya hakuzungumza
kitu chochote zaidi ya kukaa kimya huku
akishindwa kuyazuia machozi yake kumshuka
usoni.
“Mama niambie basi”
“Ni Eddy”
“Eddy, amefanyaje?”
Shamsa alizungumza huku wasiwasi ukianza
kumuenda mbio ukitwaliwa na wasiwasi mwingi
sana.
“Eddy ananisaliti kwelii…….”
Shamsa akatamani ardhi ipasuke, na aingie kwa
maana akilini mwake, akagundua ukweli wa
mambo umesha julikana na kitu anacho kwenda
kukizungumza Phidaya ni kumdhibitishia kwamba
anafahamu kila kitu. Japo kuna upepo mwanana
wa bahari ila jasho lilianza kumwagika Shamsa.
“Hivi kweli Junio angekuwa hai, Eddy angenisaliti
kweli?”
Phidaya alizidi kuzungumza maneno yaliyo
muweka Shamsa njia panda na kushindwa hata
kuuliza, Eddy amemsaliti vipi.
“Mama nakuomba unyamaze tu”
Kabla Phidaya hajazungumza, wakamuona Eddy
akija kwa mwendo wa kasi katika eneo hilo.
Shamsa kwa haraka akafuta machozi yake na
kujikausha kama si yeye aliye kuwa analia, hata
Shamsa mwenyewe akakaa kimya.
“Honey naomba funguo”
Eddy alizungumza pasipo kumsalimia mtu yoyote,
Shamsa aliweza kuligundua hilo kwamba ni
kwasababu ya yeye kuwapo katika eneo hilo ndio
maana Eddy anazungumza kwa ukali. Kwa
unyonge Phidaya akatoa funguo kwenye mfuko wa
suruali yake na kumkabidhi Eddy.
“Leo naweza nisirudi kabisa”
“Kwa nini?”
Shamsa aliuliza kwa wasiwasi huku akimtolea
macho Eddy, ila jicho alilo kutana nalo kwenye
sura ya Eddy likamfanya Shamsa kukaa kimya
kabisa na kuto kutamani kuuliza tena swali lolote.
Eddy akaondoka na kumuacha Phidaya kwenye
majonzi makubwa. Eddy moja kwa moja akaelekea
chumbani, akatafuta nguo alizo hisi zitamfaa,
akavaa. Alipo hakikisha amependeza kutokana na
nguo hizo. Akachukua bastola yake yenye
magazine iliyo jaa risasi za kutosha.
‘Am sorry Phidaya mke wangu. Nipo kazini
inanibidi kuwa hivi’
Eddy alizungumza kimoyo moyo huku akisimama
mbeke ya kioo, akajitazama vizuri na kujiweka
vizuri nguo yake. Akachukua kiasi cha kutosha cha
dola kutoka kwenye suruali yake aliyo kuwa
ameivaa. Akafungua mlango na kutoka, akaanza
kutembea kwenye kordo ndefu ya hoteli hiyo.
“Eddy Eddy”
Sauti ya Madam Mery ikamfanya Eddy kusimama
na kugeuka nyuma. Madam Mery akamfwata huku
akiwa ameshika tablet yake mkononi mwake.
“Vipi?”
“Naelewa ni ishu gani ambayo inaendelea, ila nina
taarifa ambayo ninahitaji kukupatia”
Madam Mery alizungumza huku akiminya minya
kioo cha tablet yake. Akaanza kumuonyesha Eddy
ni kitu gani alicho panga kumuambia.
“Shambulizi limepangwa kufanyika katika ukumbi
wa Dar Live, kesho kwenye show ya msanii kutoka
Marekani”
“What…..?”
“Ndio hii ni taarifa waliyo iweka kwenye mtandano
na nimesha mueleza kila mmoja juu ya hii taarifa,
wewe ndio wa mwisho kukueleza. Na mheshimiwa
raisi alisha nieleza swala zima unalo lifanya”
“Basi sawa asubuhi nitakuwa hapa, hakikisha kila
jambo linakwenda kimya kimya na asijue mtu
mwengine zaidi ya sisi saba”
“Sawa”
Eddy akaondoka, kabla hajafika maeneo ya
maegesho ya magari akakutana na Shamsa akiwa
amefura kwa hasira, akamzuia Eddy.
“Pisha nipite”
“Sitaki, hivi unaakili kweli wewe?”
“Unapo zungumza na mimi utambue unazungumza
na nani sawa”
“Hata kama, ila si kufanya kazi ya kijinga kama hii.
Hivi unadhani kwamba sisi hatuumii mioyo yetu
eheeee”
Eddy akatazama kila pande hakuona mtu karibu
yao anaye watazama, kisha akamgeukia Shamsa
na kumtazama na macho makali yaliyo jaa hasira
hadi Shamsa akatetemeka.
“Ungekuwa na moyo usinge jiingiza kwenye njia
yangu. Heshima ibaki kuwa pale pale, kakae na
Phidaya umfariji”
Eddy akampiga kikumbo Shamsa na kuondoka,
akaingia kwenye gari lake na kuondoka na
kumuacha Shamsa akishangaa sana.
***
Eddy akafika nyumbani kwa Agnes na kumkuta
akiwa amesha maliza kujiandaa.
“Tunatumia gari lako au la kwangu?”
Agnes alimuuliza Eddy mara baada ya kushuka
kwenye gari.
“Mmm naona tutumie langu”
“Ok ngoja nirudishe funguo ndani”
Agnes akaondoka huku akiwa ataingishika makalio
yake, hadi Eddy akajikuta akiguna na kuachia
tabasamu pana usoni mwake.
“Kweli wanawake hawa wameumbwa”
Agnes baada ya muda akarudi huku akitembea kwa
mwendo wa haraka. Agnes aliweza kupendeza kwa
gauni refu jeupe lenye mpasuo mkubwa hadi
kwenye paja.
“Umependeza honey”
“Kweli?”
“Ndio, hata wewe pia umependeza mume wangu
mtarajiwa”
“Asante”
Wakaingia kwenye gari na kuondoka,
hawakuchukua muda sana wakafanikiwa kufika
Serena Hoteli. Agnes akampigia simu Halima na
kumuuliza ni ukumbi gani walipo. Halima akawapa
maelekezo yote. Wakashuka kwenye gari na
kuelekea ndani. Kutokana Agnes yupo na mpenzi
wake, hakukaguliwa na polisi pasipo kugundua
kwamba Eddy ameingia na silaha. Ndani ya
ukumbi huo ulio pambwa vizuri kuna idadi chache
ya wageni waalikwa huku wengi wao wakiwa ni
viongozi ngazi ya juu serikalini.
“Honey kakae meza ile, mimi nimeandaliwa kukaa
hapa mbele”
“Sawa hakuna shida”
Eddy akaka kwenye meza yenye viti vinne tu iliyo
pambwa vizuri ambayo ipo tofauti sana na meza
nyingine. Watu wakaendelea kuingia taratibu huku
wakipatiwa vinywaji kila pale walipo kaa kwenye
meza zao huku mshereheshaji akimuamuru Dj
kupiga nyimbo nzuri za kuvutia.
“Jamani hii ni kama suprize kwa waziri wetu
Agnes, kwa mana hakutarajia ujio kama huu wa
watu katika siku kama hiiya leo”
Mshereheshaji alizungumza, akawaomba watu wote
kusimama. Wakatii hadi Eddy mwenyewe.
Mshereheshaji akawaalika wageni rasmi. Ambao
walianza kuingia ndani ya ukumbi huo wenye
mlango nyuma. Eddy na wageni wengine waalikwa
wakageuka kuangalia ni wageni gani hao rasmi.
Macho yakamtoka Eddy baada ya kuwaona raisi
Godwin akingiia ukumbini hapo huku mbele yake
akimuona John akisukumwa kwenye kiti cha
matairi, na wote wakapitiliza moja kwa moja hadi
kwenye meza ambayo Eddy ameketi, na taratibu
raisi Godwin akampa mkono Eddy kama salam,
aliye utazama pasipo kuupokea.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 82 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (82)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
ILIPOISHIA
“Jamani hii ni kama suprize kwa waziri wetu
Agnes, kwa mana hakutarajia ujio kama huu wa
watu katika siku kama hiiya leo”
Mshereheshaji alizungumza, akawaomba watu wote
kusimama. Wakatii hadi Eddy mwenyewe.
Mshereheshaji akawaalika wageni rasmi. Ambao
walianza kuingia ndani ya ukumbi huo wenye
mlango nyuma. Eddy na wageni wengine waalikwa
wakageuka kuangalia ni wageni gani hao rasmi.
Macho yakamtoka Eddy baada ya kuwaona raisi
Godwin akingiia ukumbini hapo huku mbele yake
akimuona John akisukumwa kwenye kiti cha
matairi, na wote wakapitiliza moja kwa moja hadi
kwenye meza ambayo Eddy ameketi, na taratibu
raisi Godwin akampa mkono Eddy kama salam,
aliye utazama pasipo kuupokea.
ENDELEA
Taratibu Eddy akaupokea mkono wa raisi Godwin,
huku akiachia tabasafu usoni mwake ambalo fika
alifanani na kitu anacho kifikiria akilini kmwake.
Eddy akamsalimia John kwa ishara, naye akaachia
tabasamu. Msherehekaji akwaruhusu watu kuweza
kukaa kwenye viti vyao na kuendelea na ratiba
iliyopo mbele yao. Kwa mara kadhaa Eddy aliweza
kumtazama raisi Godwin na John ambao
wanaonekana hadi sasa hivi hadi sasa
hawajamgundua Eddy.
“Kijana unaitwa nani?”
Raisi Praygod alizungumza huku akimtazama Eddy
usoni.
“Naitwa Erickson. Erickson Forrd”
“Ahaa ninaamini unanifahamu?”
“Ndio ninakufahamu, wewe ndio raisi wetu. Mimi ni
mmoja kati ya watu nilio kuwa mstari wa mbele
kukupigia kampeni chuoni”
Eddya alizungumza kwa sauti ambayo sio rahisi
kwa mtu kuweza kuigundua kwa haraka haraka.
Uso wa raisi Praygod ukatawaliwa na tabasamu
baada ya kusikia maneno ya Eddy.
“Kweli kijana?”
“Kweli muheshimiwa, nilihakikisha kwamba
wanavyuo wanakuchagua na kuhitaji mabadiliko ya
kisiasa. Hatuwezi vijana tangu tunazaliwa tuwe
tunatawaliwa na chama kimoja”
“Unachukua fakati gani?”
“Nachukua utawala bora”
“Ahaaa, sawa sawa. Hivi unauonaje uongozi
wangu?”
“Kusema kweli machoni mwa watu wengi
wanaweza kusema uongozi wako unamapungufu.
Ila kwa sisi waelewa tunaelewa uongozi wako ni
mzuri kwa maana serikali yetu inapunguza
matumizi ambayo si ya msingi. Kwa mfano hili
swala la kutaka kuibadili nchi na kuwa nchi ya
kifalme, ninakuunga mkono wa asilimia mia”
Eddy alizungumza kwa kuajiamini na kumfanya
raisi Godwin kuzidi kufurahi pasipo kugundua
kwamba Erickson Forrd ndio Eddy Godwin
mwanaye wa pekee wa kiume ambaye ni adui yake
namba moja.
“Unajua muheshimiwa, ukiweka nchi kuwa na
uongozi wa kifalme, tutapiga hatua kubwa ya
kiuchumi. Tazama Uingereza hadi leo
wanamilikiwa na Malikia. Tazama uchumi wao
ulipo kwa sasa. Wapo mbali sana muheshimiwa, na
mimi ninazidi kukuunga mkono hata chuoni
nitahakikisha kwamba uongozi unabadilika”
Muda wote Eddy akizungumza John alimtazama
kwa umakini mdomoni mwake, akataka
kuzungumza kitu ila akanyamaza.
“Unaonekana upo vizuri kijana”
“Kidogo tu muheshimiwa”
“Na unasoma chuo gani?”
“Ninasoma Mlimani”
“Ahaaa kumbe ni hapa hapa Dar es Salaam”
“Ndio muheshimiwa”
“Basi nitafanya mawasiliano na wewe ili
tuyazungumze mengi”
Raisi Godwin kwa ishara akamuita mlinzi wake na
kumnong’oneza kitu. Mlinzi wake akatoa kadi ya
mawasiliano na kumkabidhi raisi kisha raisi
Godwin akampatia Eddy.
“Tutawasiliana kijana hii ni namba ya simu yangu
ya mkononi”
“Asante sana muheshimiwa”
“Hivi umesema unaitwa nani?”
“Erickson Forrd muheshimiwa”
“Jamani naona mtoto wetu leo anahitaji
kuzungumza kitu, ngoja nimpatie maiki”
Mshereheshaji alizungumza na kuwafanya Eddy na
raisi Godwin kuangalia alipo Agnes, aliye kabidhiwa
maiki namshereshaji. Agnes akasimama kwenye
kiti huku macho yake akimtazama Eddy aliye kaa
meza moja na raisi Godwin.
“Napenda kuwashukuru jamani kwa kuweza
kunifanyia sherehe hii, ambayo siku ya leo kwangu
ni muhimu sana kwangu. Nikisema niwataje mmoja
mmoja basi nahisi nitataja ukumbi mzima. Ila
kusema kweli shukrani yangu inatoka ndani ya
moyo wangu.”
Agnes alizungumza na kuwafanya watu wote ndani
ya ukumbi kuwa kimya na kuendelea kumsikiliza
kwa kile ambacho anakizungumza.
“Katika maisha yangu, naamini rafiki zangu wa
karibu hawajawahi kusikia wala kuniona nikiwa
nina mchumba. Ila leo ninahitaji kuwaeleza hili.
Nina mchumba wangu na yupo hapa, nitakapo
mtaja basi nitaomba aje hapa mbele watu wote
mumuone”
Eddy kidogo mapigo ya moyo yakamuenda kasi
kidogo ila akajikaza na kujidai kama sio yeye
ambaye atakwenda kutajwa.
“Laazizi wangu, Asali wangu, mume wangu
mtarajiwa Erickson Ford popote ulipo ninakUomba
unyanyuke”
Watu wote wakaanza kutazama tazama, raisi
Godwin na John wakabaki wakimkodolea macho
Eddy waliye kaa naye kwenye meza moja.
“Kumbe ni wewe bwana mdogo?”
Raisi Praygod alizungumza huku akitabasamu na
kumtazama Eddy aliye achia tabasamu pana. Eddy
akatingisha kichwa na kusimama taratibu, akaanza
kupiga hatua za taratibu hadi alipo kaa Agnes,
aliye mkumbatia kwa muda kisha akamuachia.
John sura yake dhairi ikaonyesha kujawa na hasira
kwa kitendo hicho hadi raisi Godwin akakigundua.
“Vipi mbona umekasirika ?”
“Ahahaa hapana muheshimiwa”
John alizungumza kwa kuzuga, ila kusema kweli
moyoni mwake kwa haraka ametokea kumchukia
Erickson Forrd, hii yote ni kutokana na hisia za
mapenzi alizo kuwa nazo juu ya Agnes, ila ukaaji
kimya wake ndio ulio mponza.
‘Erickson Forrd lazima nikuue’
John aliwaza huku akimtazama Eddy jinsi anavyo
lishwa kipande cha kike na Agnes. Si John peke
yake bali hata Manka aliyte kaa viti vya nyuma
kidogo hasira kali, ikazidi kuutesa moyo wake, kwa
mara kadhaa akawa anafikiria ni jinsi gani anavyo
weza kumuangamiza Agnes ili kubaki na Erickson
Forrd peke yake.
‘Lazima nimuue, Erickson ni wangu. TENA WANGU
PEKA YANGU’
Manka alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga, kiasi kwamba akatamani anyanyuke na
kwenda kuwatengenisha Erickson na Agnes wanao
pigana mabusu kiholela holea. Sherehe ikazidi
kuendelea hadi ikafikia tamati. Raisi Godwin
akawafwata Eddy na Agnes walipo simama kwa ajili
ya kuwaaga.
“Agnes hongera, umechagua kijana mzuri sana”
“Asante sana muheshimiwa nakushuru sana kwa
kuweza kuhudhuria”
“Usijali, unajua nilikwenda Marekani kwa ajili ya
mapumziko, ila Manka alipo nieleza juu ya sherehe
yako ikanilazimu jana turudi”
“Asante sana muheshimiwa, umenipa nafasi
ambayo ni ya pekee sana”
“Usijali wewe ni kati ya watu ninao waheshimu na
kuwajali sana, ingeuwa si vyema kama leo nisinge
weza kuhusika katika hafla hii, naamini usinge
jisikia vizuri”
“Hapana muheshimiwa, mimi ni muelewa kwa
maana sikutegemea kabisa ujio wako”
“Usijali, Erickson Forrd ngoja mimi niwaache
mukapumzike. Ila kesho wasiliana na mimi na
kama ikiwezekana njooni wote ikulu tuzidi
kuyajenga”
Raisi Praygod alizungumza huku akimpa mkono
Eddy, ambaye kwa haraka akaupokea huku akiwa
na furaha kubwa ambayo furaha yote ni feki, kwani
kisasi na chuki dhidi ya mzee Godwin imejaa
moyoni mwake.
“Asante sana muheshimiwa nina amini bibie
atanileta”
“Haya ngoja tuondoke nawatakia usiku mwena”
“Nawe pia muheshimiwa raisi”
Eddy akamtazama kwa macho makali jinsi raisi
Praygod wanavyo ongozana na John anaye
sukumwa kwenye kiti cha matairi na mlinzi wake.
“Honey mbona umewakazia macho”
“Ahaa hapana honey katika maisha yangu sijawahi
kuonana na raisi uso kwa uso”
“Kweli mpenzi wangu”
“Kweli siwezi kukutani, leo ndio mara yangu ya
kwanza”
Eddy aliongopea ila anacho kijua moyoni mwake ni
kulipiza kisasi dhidi ya Mzee Godwin pamoja na
John ambaye amepunyuka punyuka katika kisasi
cha kwanza alicho kuwa anahitaji kuweza
kumfanyia. Agnes na Eddy wakaondoka na
kuelekea katika hoteli walio lipiwa kama zawadi ya
kwenda kustarehe kwa siku mbili mfululizo.
***
John njia nzima akiwa kwenye gari pamoja na
mlinzi wake aliwaza ni jinsi gani ya kumuuErickson
Forrd, kwa maama ameingia katika kumi na nane
zake.
“Ninakazi ambayo ninahitaji kukupatia”
John alimuambia mlinzi wake, kwa sauti iliyo jaa
mikwaruzo mingi dhairi akionekana kusumbukiwa
na jambo fulani moyoni mwake ambalo hakulihitaji
kuliweka wazi kwa mtu yoyote kwani, katika
maisha yake hakuwahi kujikuta akiingia kwenye
hisia hali za mapenzi kama alizo hizo.
“Kazi gani bosi?”
“Ulimuona yule kijana anaye itwa Erickson Forrd?”
“Ndio bosi nilimuona”
“Nahitaji umfwatile hatua kwa hatua, kila detail zake
ninaomba uniletee”
“Sawa muheshimiwa”
“Na akionekana humuelewi, hakikisha unampoteza”
“Sawa mkuu”
***
SiPhidaya wala Shamsa aliye weza kupata lepe la
usingizi, kila mmoja akili yake ameielekezea kwa
Eddy. Kila mmoja aliamuwazia jinsi Eddy anavyo
banjuka na mwanamke ambaye anaye kwa usiku
huo. Shamsa maumivu aliyo yapata yaliweza
kujidhihirisaha hadi usoni mwake na kumfanya Sa
Yoo kuweza kumuuliza ni kitu gani kinacho
endelea.
“Ahaaa wee acha tu”
“Si wezi kuacha tu, ikiwa ninakuona unajambo
ambalo linakusumbua. Ni vyema tuzungumze kwa
pamoja kama ni mawazo niweze kukusaidia”
“Sa Yoo si kila jambo ni la kukushirikisha wewe,
mengine ni mambo binafsi”
Shamsa alizungumza huku kwa mbali machozi
yakimlenga lenga. Sa Yoo akaka kitako kitandani,
akamuangalia vizuri, taratibu Sa Yoo akashuka
kitandani na kwenda hadi sehemu ilipo swichi,
akawasha taa na kurudi kurudi kitandani.
“Shamsa nakuomba uzungumze, ni nini kinacho
kusumbua eeheee”
Sa Yoo alizungumza huku taratibu akimnyanyua
Shamsa kutoka kitandani. Kichwa cha Shamsa
akakiweka kwenye bega lake..
“Niambie sasa, ni nini kinacho kusumbua rafiki
yangu?”
“Ni Eddy”
“Eddy kafanya nini?”
Shamsa akashusha pumzi kidogo huku akijifuta
machozi usoni mwake.
“Eddy ana mwanamke mwengine”
“Sasa Shamsa huyo mwanamke ambaye anaye si
anatusaidia katika kuikamilisha kazi yetu”
“Ndio Sa Yoo, ila roho yangu inaniuma”
“Inakuuma kwa nini sasa?”
“Bado ninampenda Eddy, huyu ndio Black Shadow
wangu. Upendo wangu kuondoka kwake ni ngumu
kama unavyo fikiria”
Sa Yoo akajikuta akishusha pumzi kidogo huku
akimtazama Shamsa anaye endelea kutiririkwa na
machozi.
“Lakini Shamsa, si umesha ufahamu ukweli
kwamba Eddy ni baba yako, inakuwaje sasa bado
una hisia za mapenzi juu yake?”
“Hata kama ukweli ni kwamba tayari amesha
nivunja bikra yangu?”
“NI NANI AMEKUVUNJA BIKRA YAKO?”
Sauti ya Phidaya ikawastua wote na kujikuta
macho yao wakiyaekekezea mlangoni, na kumuona
Phidaya akiwa amesimama huku akiwa amevalia
nguo zake za kulalia.
***
Asubuhi na mapema Eddy akawa wa kwanza
kuamka kitandani, moja kwa moja akaelekea
bafuni, akaoga kisha akarudi chumbani akavaa
nguo zake alipo hakikisha amemaliza, akamtazama
Agnes kwa muda akamtingisha huku anamuita.
“Honey honey”
“Mmmmmmm”
Agnes aliitika kivivu huku akijigeuza kitandani na
kumtazama Eddy usoni.
“Nahitaji kwenda nyumbani kwangu mara moja”
“Kwa nini jamani, wakati tunakaa hapa siku mbili”
“Nalitambua hilo mpenzi, nakwenda kuchukua
nguo. Unahisi ikulu tutakwendaje”
“Mmmm kama ni hivyo tutakwenda kununua
madukani”
“Mmmm honey kuna vitu nahitaji kuvikamilisha
asubihi ya leo kisha nitatarudi kabla ya saa nne
asubuhi”
“Sawa naomba unibusu”
Eddy taratibu akamuinamia Agnes na kumbusu
mdomoni.
“Usichelewe mume wangu”
“Sawa”
Eddy akatoka chumbani, akaingia kwenye moja ya
lifti iliyopo hapo gorofani. Akashuka hadi chini
moja kwa moja akaelekea kwenye gari lake. Kitu
cha kwanza kukifanya akaiwasha simu yake, kwa
haraka akaitafuta ni sehemu gani ilipo namba ya
raisi Praygod, akampigia.
“Habari za asubihi muheshimiwa?”
“Salama, vipi mpango waku upo vipi?”
“Nimefanikiwa kuonana na raisi Godwin, cha
kumshukuru Mungu hajanistukia. Na kikibwa zaidi
amenipatia namba yake ya simu”
“Kweli?”
“Ndio muheshimiwa na hapa amehitaji leo niweze
kwenda ikulu kuonana naye”
“Safi sana ni mwanzo mzuri ninaimani kazi
inakwenda kuwa rahisi kwa upande wetu”
“Ni kweli hapa nahitaji kurudi huko nibadilishe
nguo, kisha nionana na huyu mwanamke, ila mke
wangu nikionana naye nahisi uchungu mwingi
moyoni mwangu”
“Basi usirudi nyumbani cha kufanya tuonane
Mlimani City tuzungumze”
“Kwa nini nisirudi?”
“Kwa maana ukimuona Phidaya unaweza
kushindwa kuifanya kazi yako, na kumbuka kuna
shambulizi leo limepangwa kufanywa kwenye
onyesho la huyo msanii”
“Kweli muheshimiwa nitajitahidi kuhakikisha
halifanikiwi”
“Sawa tuonane Mlimani City”
Eddy akakata simu, akawasha gari lake na
kuondoka eneo hilo la hotelini. Mlinzi akafungua
geti na Eddy kuondoka, safari ya Mlimani City
ikianza. Akiwa njiani akahisi kuna gari nyeusi
inamfwatilia, tangu alipo toka pale hotelini, ila
hakuitilia mashaka sana kwa maana anajiamini
kutokana na sura ya bandia aliyo kuwa nayo. Hadi
anafika Mlimani City, gari hiyo bado ilizidi
kumfwata, akaegesha gari lake kwenye maeneo ya
maegesho, gari hilo nalo lilifika kwenye maegesho
likasimamishwa.
Eddy akashuka kwa kujiamini moja kwa moja
akeleeka kwenye mgahawa wa Samaki Samaki,
akatafuta sehemu na kukaa. Mwanaume mwenye
asili ya kizungu akashuka kwenye gari hilo jeusi,
naye akaenda kuketi kwenye moja ya mgahawa
uliopo karibu na mgahawa wa Samaki Samaki.
Haukupita muda mrefu Raisi Praygod akiwa
amevalia kofia kubwa ambayo si rahisi kwa mtu
kuweza kumtambua akafika eneo hilo akiwa
ameongozana na Rahab aliye valia dera na
kujitanda mtandio. Moja kwa moja wakafika katika
meza aliyo kaa Eddy.
“Karibuni”
Eddy alizungumza huku akiwapa mikono. Wakakaa
kwenye viti na kuagiza kinywaji walicho kihitaji
kwa wakati huo.
“Jamani inakwenda kuwa rahisi sana”
Eddy alizungumza huku akitabasamu.
“Wewe ndio utakayo ifanya iwe rahisi na wewe ndio
utakayo ifanya iwe ngumu”
“Kwa nini unasema hivyo Rahab”
“Kwa sasabu uhalisia wako endapo utajulikana basi
tambua kila jambo kwetu litaharibika”
“Ni kweli ndio maana najitahidi uhalisia wangu
usiweze kujulika”
Muda wote wakiwa wanazungumza raisi Praygod
macho yake, akawa anayaangaza angaza, hadi
kwenye mgahawa wa pili, akamshuhudia
mwanaume mwenye asili ya kizungu akinyanyuka
kwenye kiti alicho kikalia na kuelekea kwenye
maesho ya magari.
“Nakuja”
Raisi Praygod alizungumza huku akinyanyuka,
akaelekea kwenye kiti alicho kuwa amekalia
mwanaume huyo wa kizungu na kuisahau simu
yake inayo onekana ni ya gharama sana. Raisi
Praygod akaitazama kwa sekunde simu hiyo, kisha
akaichukua, kitendo cha kupiga hatua mbili mbele,
simu hiyo ikatoa kijimlio, huku kwenye kioo chake
sekunde zilizo baki tatu zikaanza kurudi nyuma na
kumfanya raisi Praygod kushangaa. Hadi inafika
sekunde sifuri, mlipuko mkubwa ukatokea eneo
hilo na kusambaratisha kila aliye kuwepo katika
eneo hilo.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 83 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (83)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
ILIPOISHIA
“Nakuja”
Raisi Praygod alizungumza huku akinyanyuka,
akaelekea kwenye kiti alicho kuwa amekalia
mwanaume huyo wa kizungu na kuisahau simu
yake inayo onekana ni ya gharama sana. Raisi
Praygod akaitazama kwa sekunde simu hiyo, kisha
akaichukua, kitendo cha kupiga hatua mbili mbele,
simu hiyo ikatoa kijimlio, huku kwenye kioo chake
sekunde zilizo baki tatu zikaanza kurudi nyuma na
kumfanya raisi Praygod kushangaa. Hadi inafika
sekunde sifuri, mlipuko mkubwa ukatokea eneo
hilo na kusambaratisha kila aliye kuwepo katika
eneo hilo.
ENDELEA
Ukimya wa takribani dakika tano ukatawala eneo
zima la Mlimani City. Eddy kwa mbali akaanza
kufumbua macho yake, kuangalia kitu kilicho toke.
Moshi mwingi mweusi, uliendelea kutawala katika
anga zima la mlimani city. Vilio na kelele za
ving’ora vya zima moto vikaendelea kusikika
masikioni mwa Eddy, anaye jizoa zoa kunyanyuka
kutoka chini alipo angukia, ambapo ni umbali
mkubwa sana kutoka sehemu alipo kuwa amekaa.
Kizunguzungu, kikali kikaanza kumuandama Eddy
kila alipo jaribu kusimama, alijikuta akiyumba.
Eneo zima lililokuwa na mgahawa uliopo
pembezoni mwa mgahawa wa samaki kujijaa damu
nyingi za watu walio kuwa katika sehemu hiyo.
Taratibu Eddy akajikaza hivyo hivyo na kusimama
wima.
“Raisi”
Ndio kitu cha kwanza Eddy kuweza kukifikira,
akaanza kutembea huku akiyumba yumba kwa
kizungu zungu, ila akazidi kujikaza.
“Mr hutakiwi kuingia sehemu hii sio salama”
Askari mmoja alijaribu kumzui Eddy katika kuingia
katika eneo lilipo tokea mlipuko, ila Eddy
akamsukumia mbali askari huyo na kuzidi
kutembea kwa kuyumba yumba. Macho yake
yaliweza kushuhudia jinsi vipande pande vya
nyama za wanadamu vilivyosambakaa chini, huku
damu ikiwa ni nyingi sana. Eddy akaweza kuona
kiatu cha raisi Praygod alicho kuwa amekivaa
kipindi amekuja eneo hilo kikiwa kimebakia na
kipande cha mguu wa raisi.
“Ohooo Mungu wangu”
Eddy alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga, hakuamini kitu kilicho tokea. Waandishi wa
habari nao hawakucheza mbali, mara moja
wakaweza kufika katika eneo la Mlimani City na
kuyarusha matangazo hayo moja kwa moja kwenye
vituo vyao ya televishion na radio. Eddy akahisi
nguvu zikimuishia, baada ya kuuona kiwili wili cha
kati cha raisi Praygod kikiwa hakina mikono, huku
kichwa chake kikiwa kimechanguliwa vibaya sana.
“Khgaaaaaaaaaa”
Eddy alipiga ukunga mkubwa huku akikaa chini
machozi yakimwagika kama mtoto mdogo.
Wanajeshi na askari walio weza kufika eneo hilo,
wakajitahidi kumtoa Eddy katika eneo hilo huku
wakiwasaidia watu wengi walio jeruhiwa vibaya
mno.
***
“Ahaa….ahaa hakuna mama ni stori tu”
Sa Yoo akawa mtu wa kwanza kuweza kujibu swali
la Phidaya alilo ulia akiwa anaingia ndani ya
chumba chao pasipo kubisha hodi.
“Mmmm ya kweli hayo?”
Phidaya alizungumza huku akikaa kitandani,
macho yake akimtazama Shamsa anaye endelea
kuyapangusa macho yake akionekana kuwa kuja
jambo ambalo linamsumbua.
“Ndio madam”
“Shamsa kuna kitu gani ambacho kina kusumbua?”
“Hakuna mama”
“Shamsa ninakutambua wewe na ninakuelewa,
kuna jambo ambalo linakusumbua nieleze mimi ni
mama yako. Hata kama kuna mwanaume
amekuumiza nieleze niweze kukupa ushauri”
“Hapana mama ni stori ya nyuma ndio
niliikumbuka ikaniumiza moyo wangu”
“Inahusiana na mapenzi?”
“Ndio”
Phidaya akatabasamu huku akimtazama Shamsa
usoni mwake, taratibu akaupeleka mkono wake wa
kuli hadi kwenuye uso wa Shamsa, akamfuta
machozi ambayo yanatiririka tena kwenye uso
wake.
“Wanaume ni watu ambao mioyo ya wanawake
wanaichukulia ni kama eneo la majaribio katika
maisha yao. Wapo tayari kumtumia mwanamke na
kumuumiza ili mradi tu waweze kufanikiwa katika
mpango ambao anahitaji kuufanya hadi ufanikiwe”
Phidaya alizungumza kwa sauti iliyo jaa usikivu
mkubwa na kuwafanya Shamsa na Sa Yoo
kumsikiliza kwa umakini huku wakimtazama usoni.
“Pia wanaume ni watu ambao, pasipo sisi kuweza
kuwaelekeza na kuwaeleza juu ya hisia zetu
usidhani wanaweza kuziheshimu. Mwanaume ni
sawa na mtoto, hata kama anafanya kosa
unatakiwa kuweza kumuelewa na kumshauri juu ya
hilo na akabadilika”
“Eddy ni mume wangu, tena ni mwanaume wa
ndoto zangu. Eddy katika maisha yake yote
hakuweza kuishi kwa furaha na amani zaidi ya
kunihangaikia mimi na marehemu mwanangu
Junio”
Phidaya alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga na kumfanya Shamsa kuzidi kumwagikwa na
machozi.
“Eddy ninampenda kuliko hata maisha yangu, nipo
tayari kufa kwa ajili yake. Hata swala hili ambalo
analifanya analifanya kwa uchungu na maumivu
makali moyoni mwake, naelewa sababu ya yeye ni
kwanini akija hapa haitaji kuzungumza na mimi
muda mrefu”
“Ila mama si kwamba anakuwa na mama
mwengine na atakuacha wewe”
Swali la Shamsa likamfanya Phidaya kutabasamu
kwa muda huku akimtazama Shamsa usoni.
“Eddy ananipenda, ila kazi hii ikimalizika ninaamini
tutaishi kwa amani na upendo”
“Jamani tubadilisheni mada”
Sa Yoo alizungumza baada ya kuona Shamsa na
Phidaya wametawaliwa na huzuni kubwa kati yao.
Sa Yoo akasimama, akavaa jinzi yake haraka
haraka pamoja na tisheti yake.
“Unakwenda wapi?”
“Nakwenda kaunta kuchukua vinywaji. Madam
unakunywa nini?”
“Niletee red’s”
“Shamsa na wewe?”
“Na mimi niletee hicho hicho kinywaji alicho kihitaji
mama”
“Ok dakika sifuri nitakuwa nimesha rudi”
Sa Yoo akavaa vindala vya kuogea na kutoka
chumbani hapo, akatembea kwa haraka hadi
kwenye kaunta ya vinywaji, akaagizia vinywaji
anavyo hitaji, Akachukua katoni mbili za bia hizo
za kopo na kurudi nazo chumbani.
“Yaani hapa tungepata na nyama choma,
zingeenda kama nini”
Phidaya alizungumza huku akitabasamu, baada ya
vinywaji hivyo kuwekwa mezani.
“Ohooo ungeniambia madam, basi ngoja niende
kutoa oda jikoni”
“Ahaaa ngoja niwapigie simu”
Shamsa alizungumza huku akishuka kitandani,
akachukua mkonga wa simu ya mezani, akaminya
namba zinazo onyesha zainahusiana na watu
wajikoni katika hoteli hiyo.
“Ninahitaji nyama choma ya ng’ombe kilo tatu”
Shamsa alizungumza na muhudumu, aliye hitaji
kuelezwa oda hiyo inatokea chumba namba ngapi,
Shamsa akamueleza namba ya chumba.
“Ohooo ngoja ngoja. Weka kachumari nyingi
pamoja pilipili”
“Weee Shamsa, muambie pilipili aweke pembeni”
Sa Yoo aliingilia mazungumzo hayo ya Shamsa na
muhudumu wa jikoni.
“Pilipili weka pembeni, na usiniwekee mifupa fupa,
weka steki ya kutosha “
“Sawa ndugu mteja”
Shamsa akaurudisha mkonga wa simu hiyo alipo
utoa, akawageukia Phidaya na Sa Yoo na kuwakuta
tayari kila mmoja amesha fungua bia yake na
kuendelea kunywa taratibu.
“Jamani mumesha anza kunywa”
“Ndio njoo uchukue ya kwako”
Shamsa akachukua kopo moja la bia, akafungua na
kuanza kunywa taratibu, yote wanayafanya kwa
kupoteza mawazo ya mambo yanayo endelea.
Baada ya robo saa mlango ukangongwa, Sa Yoo
akanyanyuka na kuufungua mlango, akakuta
muhudumu wa hoteli akiwa amewaletea nyama
walizo ziagiza. Akamruhusu kuingia ndani, alipo
weka chakula hicho meza, akampatia pesa ya
chakula hicho na muhudumu akatoka.
Wakaendelea kunywa huku wakipiga stori ambazo
hazina mbele wala nyuma, kila aliye jisikia
kuzungumza aliweza kuzungumza. Wa kwanza
kupitiwa na usingizi akiwa amejawa na kilevi ni
Phidaya mbaye pombe hajaizoa sana. Shamsa na
Phidaya wakaendelea kupiga stori za hapa na pale
na wao wakajikuta wakipitiwa na usingizi na kulalal
fofo.
Kwa jinsi mlango unavyo gongwa kwa nguvu,
ukamfanya Sa Yoo kunyanyuka akiwa na malepe
ya usingizi. Kitu cha kwanza kukitazama ni dirisha,
mwanga mkali wa jua unao ingia katika chumba
chao ukamtamjulisha tayari kumesha pambazuka.
Kabla ya kunyanyuka kwenye kochi alilo kuwa
amekalia, akashangaa mlango ukafunguliwa, na
madam Mery akaingia akinekana kuhema na
wasiwasi mwingi ukiwa umemtawala.
“Madam Mery kuna nini mbona hivyo?”
“Washa washa Tv uoneeee”
Madam Mery alizungumza huku mikono na macho
yake yote akiyaelekezea kwenye Tv iliyopo ndani
ya chumba hicho. Sauti ya madam Mery
ikawaamsha Shamsa na Phidaya ambao hadi
madam Mery anaingia ndani humo bado walikuwa
wamelala. Sa Yoo akachukua rimoti ya Tv,
akaiwasha na kusimama huku akitazama Tv hiyo.
“Weka chaneli ten”
“Ni namba ngapi?”
Madam Mery alipo ona Sa Yoo ana maswali mengi
kwa haraka akaichukua rimoti ya king’amuzi na
kuweka chaneli ten na wote wakabaki wakitazama
taarifa hiyo ya dharura(Breaking News), inayo
rushwa muda huu. Gafla Phidaya akasimama wima,
wenge lote la pombe likakata kichwani mwake,
macho yakamtoka na kupiga hatua mbili mbele
kuangalia vizuri mtu anaye muona ndio yeye au ni
pombe alizo amka nazo.
“Huyu si Eddy?”
Phidaya aliuliza huku akimtazama Shamsa aliye
itikia kwa kutingisha kichwa na kuwafanya waanze
kuchachawa kwa wenge.
“Ni nini kimetokea Mery?”
“Bomu, bomu limelipuka”
“Wapi?”
“Mlimani City”
“Ohooo jamani mume wangu”
“Jamani twendeni twendeni”
Wote wakatka pasipo kujali kama Phidaya amevaa
nguo za kulalia zinazo muonyesha nguo zake za
ndani alizo vaa. Wote wanne wakakimbilia hadi
kwenye maegesho ya madereva taski, wakavamia
kwenye moja ya taski na kuingia pasipo hata
kukaribishwa na dereva taski.
“Niwapeleke wapI?”
Dereva taksi alizungumza mara baada ya kuwaona
abiria wake wakiwa ameingia hata ya kutoa
salamu, kwa haraka haraka akagundua kwamba
wateja wake wana matatizo.
“Tupeleke mlimani City?”
“Jamani Mlimani City mimi siendi kuna mabomu
huko”
Dereva taksi alizungumza huku akizima gari lake
mara baada ya kusikia habari ya kwenda Mlimani
City.
“Wee kaka fala kweli mbona kuna waandhisi wa
hahbari hembu tupeleke bwana usituletee mambo
ya kifala”
Shamsa alizungumza kwa kufoka, ndio kwanza
dereva taski akashuka kwenye gari na kufunga
mlango wa ke alio tokea. Kwa haraka Shamsa
akashuka kwenye gari akiwa amejawa na hasira,
akazunguka upande wapili wa gari na kumshika tai
dereva taski aliye baki ameshikwa na mshangao
mkubwa.
“Inakuwaje dada yangu, huvi unataka na mimi
niende kufa huko ehee”
Derevs taksi alizungumza huku akimtoa Shamsa
mikono yake kwenye kifaa chake.
“Shamsa, Shamsa achana naye bwana twende kwa
mwengne”
Sa Yoo alizungumza huku akiongoza kwa
madereva taksi wengine waliopo upande wa pili wa
barabara. Sa Yoo akamueleza mmoja wao juu ya
safari ya kwenda Mlimani City, ila kila mmoja
akaonekana kusita sita.
“Dada kama unalaki na nusu twende”
“Sawa twende”
Dereva taksi huyo alikubali na kumfanya Sa Yoo
kuwaita wezake walio vuka varabara na kwenda
kuingia kwenye taski hiyo, na kuondoka kwa
mwendo wa kasi katika eneo hilo.
***
Mlio wa simu inayo ita, ukamuamsha Agnes kitani,
taratibu akapapasa pembeni ya mto wake,
akaichukua simu hiyo huku akiwa na tabasamu
akitambu anaweza kuwa ni Erickson mpenzi wake
aliye toka na kumuacha akiwa amelala kitandani.
Akakuta ni namba ya Halima, akashusha pumzi
kidogo huku akiitazama namba hiyo, akaipokea na
kuiweka sikioni mwake.
“Hallooo”
“Shosti upo na Erickson wako hapo ulipo?”
“Mmmmm Halima umesha anza, asubuhi asubuhi
yote hii unamuulizia mume wangu”
“Hapana sina nia hiyo ya kumuulizia yeye, nijibu
yupo au hayupo, ili nijue kama nimemfananisha au
laa”
Agnes kusikia hivyo kwa haraka akaka kitako
kitandani ili kujua Halima anamaanisha nini kwa
maana wivu wa mapenzi tayari umesha utawala
moyo wake na akili yake ikaanza kuwaza labada
Erickson yupo na mwanamke mwengine.
“Hayupo ameondoka hapa asubuhi na mapema”
“Si upo karibu nba Tv?”
“Ndio”
“Hembu iwashe na weka ITV”
“Kuna nini kwani?”
“Wewe washa utajionea wewe mwenyewe, nisije
nikakupa presha bure”
Kwa haraka Agnes akashuka kitandani, akachukua
rimoti ya Tv, akawasha haraka haraka kwa bahati
nzuri, king’amuzi jana usiku walisahau kikizima na
chanel walio kuwa wakiitazama ni hiyo hiyo ITV.
Macho yakamtoka Agnes, baada ya kuona habari
hiyo ya kuogopesha juu ya mlipuko wa bomu ulio
tokea Mlimani City. Katika kutazama tazama
akamuona Erickson akiwa ananyanyuliwa na askari,
huku akilia kwa uchungua, akijitahidi kutoa
kuondoka katika eneo lililo jaa damu.
Agnes bila ya kujiuliza mara mbili, akavaa nguo
zake haraka haraka, akatoka ndani ya chumba
chake huku simu yake ikiwa sikioni akimpigia
Erickson. Simu ya Erickson, iliita pasipo
kupokelewa. Mapigo ya moyo yakazidi kumenda
kasi Agnes, kwa mbali machozi yakimlenga lenga
machoni mwake. Kitu kilicho mtoa wasiwasi ni
jinsi alivyo muna Erickson wake kwenye Tv, na
hicho ndicho kinacho mfanya atembee kwa kasi
kuelekea nje ya hoteli hiyo. Akatoka kwenye lifti
huku akiendelea kupiga simu ya Erickson ila
haikupokelewa, kitendo kilicho zidi kumpa
wasiwasi.
“Nipeleke Mlimani City”
Agnes alimuambia dereva bodaboda, ambaye
alibaki kumshangaa kwa maana anamtambua vizuri
kwamba huyu ni waziri.
“Unanitolea nini mimacho nipeleke Mlimani City”
Agnes alizungumza kwa sauti ya kufoka na
kumfanya dereva huyo wa bodaboda kusha pikipiki
yake haraka, Agnes akapanda, hakujali mpasuo wa
gauni lake, limeacha paja lake wazi. Yeye alicho
kijali ni kuweza kufika mlimani City kwa muda huo.
“Ongeza kasi wewe, unaogopa hapo kupita eheeee”
Agnes alifoka, baada ya bodaboda kusimama
kusimama kwenye mataa ya Mwenge.
“Muheshimiwa magari hayajaruhusiwa ya upande
wetu”
“Wewe ingia bwana acha woga wa kike kike. Mimi
mtoto wa kike si muoga wewe dume zima ndio
unaogopa”
Dereva bodaboda wa watu hakuwa na jinsi zaidi ya
kuingia barabarani japo anatambua anahatarisha
maisha yake na maisha ya mteja wake. Ila
kutokana yupo na kiongozi akaamini usalama wake
utakuwa upo pale atakapo kamatwa na polisi wa
usalama barabarani. Dereva bodaboda akajitahida
na kuendelea kuendesha kwa kasi huku akiyapita
magari kwa kupenya penya.
Wakafanikiwa kufika mlamani City, Agnes akaruska
kwenye pikipiki hata kabla haijasimama na
kuwafanya watu wote walio ona tukio hilo
kushangaa, hadi dereva bodaboda anasimamisha
pikipiki yake na kuangalia nyuma, hakumuona
Agnes. Akaangaza macho yake huku na kule
akamuona Agnes akiwa amesimama kwenye geti
alilio jaa askari ambao waliwazuia watu kuingia
eneo la Mlimani City zaidi ya wakaruhuhu walio
salimika kutoka.
“Mimi waziri”
Agnes alimfokea askari mmoja aliye jaribu
kumzuia.
“Hata kama huruhusiwa kuingia humu ndani si
eneo la salama”
Agnes akamshushia kibao kizito askari huyo, aliye
shangaa. Askari huyo akajaribu kurudisha kibao
hicho, ila akashtukia akichotwa mtama mkali na
Agnes ulio muangusha chini wezake wakabaki
wamemtumbulia macho. Dereva bodaboda baada
ya kuliona tukio hilo hata hamu ya kwenda kudai
pesa yake ikamuisha kabisa. Agnes akapita pasipo
askari yoyote kuweza kumzuia. Macho yake akawa
anayaangaza huku na kule ndipo alipo weza
kumona Erickson akiwa amezungukwa na askari
wapata sita wakiwa na mitutu ya bundiki,
wakimzuia kunyanyuka katika eneo hilo.
Kwa haraka Agnes akafika katika eneo hilo, akapita
katikati ya askari na kumkumbatia Eddy kwa
mapenzi mazito huku machozi yakimwagika usoni
mwake. Phidaya akwa wa kwanza kushuka kwenye
taski hiyo iliyo chelewa chelewa kutokana na foleni
za hapa na pale. Shamsa na Madam Mery
wakafwatia kwa nyuma na kumuacha Sa Yoo
akimlipa dereva taski aliye walete. Askari
wakawazuia kuingia ndani kama wanavyo fanya
kwa watu wengine.
“Twendeni huku”
Shamsa alizungumza huku akiongoza jahazi,
wakeelekea hadi kwenye moja ya ukuta.
Wakatazama pande zote na kuona hakuna askari
wanaye mfwatilia. Kwa haraka wakapanda kwenye
ukuta huo ulipo karibu na maegesho ya magari.
Wote wakafanikiwa kuingia hadi Sa Yoo. Ikabidi
kusimama kwa pamoja kuangalia ni wapi
wanaweza kumuona Eddy.
“Eddy…yu…..”
Sa Yoo hakumalizia sentensi yake kwa maana
aliweza kumona Eddy akiwa amekumbatiwa na
mwanamke wengine, tena mwanamke huyo
akionekana kumpiga mabusu mfululizo kila
sehemu ya uso wake. Madam Mery akafanikiwa
kuona tukio hilo.
“Yupo wapi?”
Phidaya aliuliza, huku akitazama sehemu aliyo
kuwa ameangalia Sa Yoo, Phidaya na Shamsa
wote wakastuka kwa kumuona Eddy akiwa
anadendeka na mwanamke mwengine, wote wawili
kwa pamoja wakaanza kutembea kwa mwendo wa
haraka kuelekea katika eno alilo simama Eddy na
Agnes, wanao dendeka pasipo kujali wingi wa watu
walio kuwa katika eneo hilo.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 84 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (84)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
ILIPOISHIA
“Eddy…yu…..”
Sa Yoo hakumalizia sentensi yake kwa maana
aliweza kumona Eddy akiwa amekumbatiwa na
mwanamke wengine, tena mwanamke huyo
akionekana kumpiga mabusu mfululizo kila
sehemu ya uso wake. Madam Mery akafanikiwa
kuona tukio hilo.
“Yupo wapi?”
Phidaya aliuliza, huku akitazama sehemu aliyo
kuwa ameangalia Sa Yoo, Phidaya na Shamsa
wote wakastuka kwa kumuona Eddy akiwa
anadendeka na mwanamke mwengine, wote wawili
kwa pamoja wakaanza kutembea kwa mwendo wa
haraka kuelekea katika eno alilo simama Eddy na
Agnes, wanao dendeka pasipo kujali wingi wa watu
walio kuwa katika eneo hilo.
ENDELEA
Sa Yoo na Madam Mery wote kwa pamoja
wakawawahi Phidaya na Shamsa ambao kwa
pamoja wanaonekana kujawa na hasira ya
kumuona Eddy akiwa anafanya uchafu huo mbele
yao.
“Munatuzuia nini?”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku akijaribu
kutaka kumpita Sa Yoo aliye simama mbele yake.
“Munataka mufanye nini sasa?”
Sa Yoo aliwauliza kwa sauti ya juu hadi baadhi ya
askari wakawatazama. Wanajeshi wanne walio valia
vitambaa vilivyo andikwa MP, wakawafwata
Shamsa na wezake walipo simama.
“Hamruhusiwi kuingia katika eneo hili”
Mwanjeshi mmoja alizungumza huku akiwa
amewakazia macho Shamsa na Phidaya ambao
wanaonekana kwamba ni vigego wanao taka
kwennda katika eneo ambalo limesha zungushiwa
utepe wa alama ya njao wenye maandishi meusi
yaliyo andikwa ‘DANGER’
“Sisi tunataka kumuona Ed…..”
Shamsa alijikuta akiropoka ila kwa haraka Sa Yoo
akawahi kumzimba mdomo.
“Waheshimiwa tumewaelewa, kidogo wezetu
wamechanganyikiwa na hili tukio”
Madam Mery alizungumza huku akimshika mkono
Phidaya, wakaondoka eneo hilo huku wakisindikiwa
na wanajeshi hao wenye mitutu ya bunduki. Mara
kwa mara Shamsa aligeuka nyuma na kumuangalia
Eddy anaye onekana kusahau kabisa kama ana
mke wake.
“Ndio mumefanya nini sasa?”
Shamsa alizungumza kwa kufoka huku akimtazama
Sa Yoo kwa macho ya hasira, Sa Yoo hakulijali
hilo zaidi ya kutafuta sehemu na kukaa, kwani
wote hawakujua ni nini kilicho tokea hadi
wakamuona Eddy akiangua kilio akiwa katika eneo
hilo.
“Tunatakiwa kujua ni kitu gani kinacho endelea, na
si muda wa kakaa na kugombana”
“Madam Mery nakuheshimu sana, ila wewe
umekuwa chanzo cha Eddy kuwa na yule
mwanamke na bado munaendelea kumtetea tetea,
inabidi yule mwanamke tumshike tumbamize hadi
akome”
Shamsa alizidi kuzingumza kwa hasira, madam
Mery hakumjibu kitu cha aina yoyote kwa maana
anatambua hiyo ni hasira na baada ya muda fulani
itakwenda kupotea. Phidaya alikaa kimya huku
akiendelea kuumia kimoyo moyo. Picha ya
mwanamke ambaye yupo na Eddy, mara kadhaa
ikawa inamrudia kichwani mwake. Hakuweza
kuyazuia machozi yake kwa maana maumivu aliyo
nayo ni makali sana japo anatambua mume wake
yupo hapo kwa kazi fulani.
‘Inakuwaje wapigane mabusu hadharani?’
Hilo ni swali alilo liwaza Phidaya mara kadhaa
kichwani mwake, akijaribu kutazama ndani kama
anaweza kumuona Eddy na huyo mwake, ila
hakuweza kuwaona kutokana na wingi wa watu
wanao zidi kumiminika kutoka maeneo mbalimbali
kujua kushuhudia tukio hilo la kutisha.
***
“Erickson haupo sawa mume wangu madaktari
wamekuja kukuchukua wakuwahishe hospitalini”
“Nipo sawa Agnes”
“No haupo sawa, madaktari mchukueni”
Agnes aliwaambia madaktari ambao wamefika
sehemu hiyo kwa ajili ya kuwachukua majeruhi
kama Eddy. Eddy akatazama pende zote haswa
sehemu ulipo mwili wa raisi Praygod, ili
utambulisho wake usijulikane, taratibu akaondoka
na kuongozana na madaktari huku Agnes akifwata
kwa nyuma. Eddy akalala kwenye kitanda kidogo
cha wagonjwa, kikanyanyuliwa na kuingizwa
kwenye gari ya wagonjwa. Madaktari hao wawili
wakaingia kwenye gari hilo huku wakifwatiwa na
Agnes aliye kaa karibu sana na Eddy.
Wakafika katika hospitali ya Muhimbili. Eddy
akashushwa kwenye kitanda na moja kwa moja
akapelekwa kwenye chumba cha kupatiwa huduma
ya kwanza.
“Dokta mimi nipo salama, naomba niondoke
zangu”
Eddy alizungumza huku akikaa kwenye kitanda
hicho, daktari akabaki amemtumbulia macho. Eddy
akasimama wima, akapiga hatua hadi mlangoni,
akafungua na kuondoka zake na kumuacha daktari
akiwa bado ameduwaa.
“Honey vipi mbona umetoka?”
“Nipo salama”
“Kweli mpenzi wangu?”
“Ndio, nahitaji kuelekea nyumbani muda huu”
“Ok basi twende pamoja nikapafahamu kwako”
“Hapana tutakwenda siku nyingine kwa leo
ninakumba niende peke yangu na sinto hitaji
unifwate”
Eddy alizungumza kwa sauti yenye msisitizo hadi
Agnes mwenyewe akajikuta akimuogopa. Eddy
ahakutaka kupoteza muda. Moja kwa moja akatoka
eneo la hospitali huku Agnes akimfwata kwa
nyuma. Eddy bila yakujali, akamuita bodaboda
mmoja wa pikipiki, akapanda na kuondoka.
“Nipeleke bahari beack hoteli”
“Sawa”
Dereva bodaboda akaondoa pikipiki na kumuacha
Agnes akiwa anashangaa shangaa asijua ni nini
cha kufanya.
***
Katika maiti zilizo pangwa sehemu moja zilizo
jeruhiwa kwa bomu hilo, huku baadhi ya maiti hizi
zikiwa zimepoteza viungo huku nyingine zikiwa
zimejeruhiwa kwa majeraha madogo madogo,
mwili wa Rahab ukawa ni mmoja wapo. Madaktari
ambao mara kwa mara walizipitia maiti hizo ili
kuzifanyia vipimo kwamba ni kweli wamefariki au
laa, wakajikuta wakishangazwa kumuona dada
mmoja aliye valia baibui jeusi akinyanyuka taratibu
huku macho yake akiwa ameyafumba.
Askari polisi baadhi waliokuwa katika eneo hilo
waliweza kulishuhudia hilo jambo ambalo
liliwaogopesha sana madaktari kwani ni zaidi ya
mara sita waliweza kufanya vipimo kwa kila maiti
na kudhibitisha kwamba wameiaga dunia na kitu
kilicho kuwa kinasubiriwa ni gari ambalo litakua
katika eneo hilo na kubebe maiti zote hizo.
Rahab akayafumbua macho yake na kutazama
eneo zima jinsi lilivyo haribiwa vibaya.
Hakumsemesha mtu zaidi ya kuangalia maiti zilizo
mzunguka. Akamuona mume wake raisi Praygod
akiwa amelazwa pembeni sana huku mwili wake
wote ukiwa umechanguka vibaya sana, hata sura
yake si rahisi kuigundua kwa haraka. Kitu cha
kuweza kukifahamu kwa haraka ni nguo alizo kuwa
amezivaa. Taratibu Rahab akapiga hatua hadi
kwenye mwili wa raisi Praygod huku machozi
yakimwagika, hakujali kwamba umechanguka
changuka vipi, akaukumbatia huku akiachia kilia
kikubwa.
Waandishi wa habari baadhi hawakusita kulirusha
tukio hilo, moja kwa moja kwenye televishion zao.
Madaktari baadhi wakapata ujasiri na kwenda
kumtoa Rahab katika mwili huo na kumuweka
pembei wakisaidiana na askri polisi, walio anza
kumfariji Rahab kunyamaza.
‘Hii sura kama sio ngeni kwangu’
Mkuu mmoja wa polisi alijiuliza swali kimoyo moyo
huku akimtazama Rahab usoni. Mtu anaye muona
hapo ndiye mwenyewe mke wa rasisi Praygod aliye
achia madaraka baada ya kuangushwa kwenye
uchaguzi.
“Koplo Ludovic mchukueni huyo mwanamke
mumpeleke sehemu sala, kisha nitakuja huko
mutakapo mpeleka”
“Sawa mkuu”
Wakamchukua Rahab aliye legea tikitiki kwa
kuishiwa na nguvu za mwili kwa maana alicho
kiona hakukitarajia kabisa kwenye maisha yake.
Wakampeleka Rahab kwenye moja ya hoteli, huku
daktrari maalumu akiwa akiwa ameandaliwa katika
kumtunza. Koplo Ludovick pamoja na Koplo
Mwanamkasi, waliweza kumgundua Rahab na kila
mmoja akwa na swali ya kitu alicho weza kukiona.
“Huyu ni mke wa raisi mstaafu”
“Ndio koplo Mwanamkasi, nashangaa kuweza
kumuona anaililia ile maiti pale”
“Mmmm kuna kitu kitakuwa kinaendelea hapa”
“Ngoja R.P.C aje naamini atakuwa na jibu sahihi
katika hili”
Kopla Ludovick akampigia simu R.P.C John
Massawe, wakamtaarifu sehemu walipo na huduma
waliyo anza kumpatia mgonjwa wao.
“Nitakuja hapo baada ya nunu saa”
“Sawa mkuu”
***
Eddy akafika hotelini aiwa amechoka huku mawazo
mengi yakiwa yamemtawala kichwnai mwake. Moja
kwa moja akaelekea hadi chumbani kwake. Cha
kushangaza hakumkuta Phidaya. Kwa haraka
akaelekea chumbani kwa Shamsa pia hakumkuta,
akaenda chumbani kwa madam Mery naye pia
hakumkuta.
“Watakuwa wamekwenda wapi hawa?”
Eddy alizungumza huku akirudi chumbani kwake,
akajitupa kitandani, huku nguo zake zikiwa
zimechafuka sana. Gafla mlango ukafunguliwa na
kumfanya Eddy kunyanyuka haraka kitandani.
Macho yake yakakutana na macho ya Phidya yaliyo
vimba kwa kulia muda mrefu. Wakabaki wakiwa
wametazamana kwa dakika kama mbili kisha kwa
haraka Phidaya akamfwa Eddy akasimama mbele
yake, akampiga kofi zito Eddy lililo tua shavuni
mwake, kisha akamkumbatia huku akilia.
“Kwanini, kwanini, kwanini”
Phidaya alizungumza huku akilia, akizidi
kumkumbatia Eddy, mkono wake wa kulio
ukimpiga piga Eddy mgongoni. Eddy hakujibu kitu
chochote zaidi ya kuzidi kumkumbatia Phidaya
wake. Phidaya akaendelea kulia huku akiwa
ameegemeza kichwa kifuani mwa Eddy.
“Shiiiiiiiiii, usilie mke wangu nipo hapa”
Eddy alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa
mapenzi mazito, hadi Phidaya mwenyewe akatulia,
hata kasi ya kulia ikapungua. Taratibu wakaachiana
na wote wakaka kitandani. Phidaya akamtazama
Eddy kuanzi juu hadi chini akionekana
kumshangaa sana.
“Imekuwaje mume wangu?”
Swali la Phidaya, likamfanya Eddy kukaa kimya
kwa sekunde kadhaa, akashusha pumzi nyingi na
kumtazama Phidaya usoni anaye onekana kuwa na
shahuku kubwa ya kutaka kufahamu ni kitu gani
kimempata mume wake.
“Raisi Praygod, ame……”
“Amefanyaje?”
“Amefariki”
Mungu wangu!!”
Phidaya kwa mshangao akajikuta akisimama wima
huku macho akimtolea Eddy. Phidaya mwili mzima
akahisi ukishikwa na ganzi, taarifa aliyo isikia
hakutarajia kwani raisi Praygod ni jana tu alikuwa
akizungumza naye na akimshawishi juu ya swala
kumpa ruhusa Eddy katika kazi yake ya kuhitaji
kulipiza kisasi.
“Eddy sijakusikia vizuri, hee……hee hembu rudia
tena”
“Raisi Praygod amefariki kwa kulipuka kwa bomu,
hata Rahab mwenyewe sina uhakika kama yupo hai
au laa”
Phidya taratibu akajikuta akikaa chini kabisa, huku
machozi yakimwagika usoni, taarifa aliyo ipata
aimenyong’onyeza kwa kiwango kikubwa sana.
“Sasa Eddy tutafanyaje jamani, ahaaaaaa”
Phidaya alizungumza huku akiendelea kulia. Sa
Yoo akatoka chumbani kwake na kwenda kumuona
Phidaya, akafika mlangoni na kujikuta akisimama
baada ya kusikia Phidaya akilia. Wasiwasi
ukampata akataka kuondoka hapo mlangoni, ila
akasita na kusimama ili kusikiliza vizuri.
“Hata mimi nimechanganyikiwa, akili yangu hapa
haifanyi kazi kabisa”
“Aahahaaa Praygod kwanini umekufa lakini. Wewe
ndio tulikuwa tunakutegemea”
Sauti ya Phidaya, Sa Yoo aliweza kuisikia vizuri,
taratibu Sa Yoo akajikuta akiufungua mlango na
kuingia ndani akiwa kama haamini kitu alicho weza
kukisikia masikioni mwake.
“Umesema raisi amekufa?”
Sa Yoo alimuuliza Eddy swali, na kumfanya Eddy
kutingisha kichwa akimdhibitishia Shamsa kwamba
ni kweli alicho kisikia ndicho kilichopo mbele yao
***
Macho ya John muda wote hakuyabandua kwenye
televishion chanel baadhi kuweza kusubiria juu ya
mpango wake wa kumuangamiza Erickson,
mwanaume aliye weza kuteka penzi la msichana
ambaye ni muda mwingi amekuwa anamfikiria japo
kuwa hakuweza kumueleza ukweli juu ya hisia
zake. ‘Breking News’ iliyo weza kuonyeshwa
kwenye kituo cha televishion cha ITV, ilimfanya
kuweza kukaa kwa umakini akisikilizia ni kitu gani
kijana wake alicho kifanya.
Kitu kilicho mshangaza ni kumuona Erickson akiwa
analia huku akiwa karibu na mwili wa mtu aliye
lipuliwa na bomu hilo la kisasa lenye muonekano
kama simu ya mkononi ila sivyo na si rahisi kwa
mtu kuweza kuligundua kwa haraka.
“Fu*k”
John alituka kwani hakutegemea kumuona
Erickson tena kwenye maisha yake.
“Lazima ufe Erickson siwezi kushare demu na
wewe”
John aliendelea kuzungumza peke yake, ndani ya
chumba cha hoteli alipo panga kwa muda
machache. Akaendelea kutazama taarifa hiyo, ila
baada ya muda fulani, akaweza kulishuhudia tukio
la Agnes akikumbatiana na Erickson huku
wakipena mabusu motomoto mbele ya waandishi
wa habari. Laiti kama angekuwa na miguu na
mikono ninaamini angenyanyuka na kwenda
kulizuia tukio analo lifanya Erickson an Agnes. Ila
kutokana na kutoa kuwa na viungo hivyo John
alijikuta kimwaga matusi mfululizo juu ya tukio
hilo. Mlango wa chumbani kwake ukafunguliwa,
akaingia kijna wake aliye kuwa amemuagiza.
“Ndio umefanya nini sasa?”
John alizungumza kwa hasira huku akiwa
amemtolea macho kijana wake huyo.
“Nimefanya kama vile ulivyo niagiza”
“Unaona jamaa bado yupo hai, hajafa”
Mlinzi wa John akaigeukia luninga iliyopo kwenye
chumba hicho, akamshuhudia Eddy akiwa
amekumbatiana na Agnes.
“Bosi nipe siku kadhaa nitakuwa nimekamilisha hii
kazi”
“Fanya uniletee kichwa cha Erickson hapa”
“Sawa mkuu”
***
Swala la mlipuko katika jengo la kibiashara la
Mlimani City, likamstua hata raisi Godwin ambaye
hakutegemea kama mpango wao walio upanga
katika chama chao cha D.F.E umeweza kuwahi
kwa kiasi hicho. Kwa haraka akachukua simu yake
ya mkononi na kumpigia John na kumuagiza afike
ikulu mara moja.
K itu kingine kilicho zidi kumuumiza akili ni jinsi
alivyo weza kumuona Erickson kwenye televishion
akiwa analia, ikionekana ni mmoja wa waadhiriwa
wa mlipuko huo wa bomu.
‘’Baba baba kuna mlipuko um…….”
Manka hakuweza kuimalizia sentensi yake mara
baada ya kuingia ndani ya ofisi ya baba yake na
kumkuta akitazama taarifa hiyo ya habari.
“Baba kuna mtu anataka kumuua Erickson wangu”
Manka alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga na kumfanya raisi Godwin kumgeukia na
kumtazama kwa macho ya mashangao.
“Erickson wako. Unamaanisha nini?”
Manka hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya
huku akiendelea kumwagikwa na machozi. Kwa
mara ya kwanza raisi Godiwn ndio ameweza
kuziona hisia za mapenzi za mwanae mpendwa
Manka akimlilia mwanaume.
“Ina maana unampenda ERICKSON FORRD?”
“Ndio baba”
Manka alijibu na kuzidi kumpandisha hasira raisi
Godwin, kwa mtu aliye taka kusababisha kifo cha
kijana aliye pendwa na mwanae.
“Mshezi aliye fanya hivyo nakuahidi nitamuua aliye
tegesha bomu hilo sawa mwanangu”
“Sawa baba”
Manka alizungumza huku akimkumbatia Mzee
Godwin, pasipo wao kuweza kujua kwamba huyo
wanaye muita Erickson Forrd ndio Eddy Godwin.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 85 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (85)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
INGHIA GOOFLE PLAYSTORE NA DOWNLOAD
APPLICATION(APP) YA STREAM NATION UWEZA
KUSOMA STORI ZA WAANSHI MAHIRI EDDAZARIA
G.MSULWA NA GIFT KIPAPA KWA VIFURUSHI VYA
MWEZI KWA SH 5000 NA KIFURUSHI CHA WIKI
MBILI KWA SH 3000.
ILIPOISHIA
“Baba kuna mtu anataka kumuua Erickson wangu”
Manka alizungumza huku machozi yakimlenga
lenga na kumfanya raisi Godwin kumgeukia na
kumtazama kwa macho ya mashangao.
“Erickson wako. Unamaanisha nini?”
Manka hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya
huku akiendelea kumwagikwa na machozi. Kwa
mara ya kwanza raisi Godiwn ndio ameweza
kuziona hisia za mapenzi za mwanae mpendwa
Manka akimlilia mwanaume.
“Ina maana unampenda ERICKSON FORRD?”
“Ndio baba”
Manka alijibu na kuzidi kumpandisha hasira raisi
Godwin, kwa mtu aliye taka kusababisha kifo cha
kijana aliye pendwa na mwanae.
“Mshezi aliye fanya hivyo nakuahidi nitamuua aliye
tegesha bomu hilo sawa mwanangu”
“Sawa baba”
Manka alizungumza huku akimkumbatia Mzee
Godwin, pasipo wao kuweza kujua kwamba huyo
wanaye muita Erickson Forrd ndio Eddy Godwin.
ENDELEA
Haukupita muda mwingi John pamoja na mlinzi
wake tayari wakawa wamesha fika ikulu, moja kwa
moja John akapelekwa katika ofisi ya raisi Godwin,
akamkuta akiwa yupo na Manka, sura zao wote
zinaonyesha wana jambo ambalo limewaudhi sana.
“Naamini umeliona tu hilo tukio lililo tokea leo”
“Tukio gani muheshimiwa”
“Tazama kule kwenye tv, hili tukio limetokea
makusudi kwa mtu, aliye fanya hili alilenge
kumuangamiza Erickson Forrd, Je unavyo hisi
wewe ni nani aliye fanya hili tukio?”
Swali la raisi Godwin likamstua sana John, taratibu
akashusha pumzi yake na kuwatazama wote,
Manka na baba yake kisha akameza fumba la mate
na kuzungumza.
“Muheshimiwa, inabidi nitume vijana waweze
kuchunguza hili tukio kwa maana lipo nje ya
mpango wetu tulio panga kulipua kwenye ukumbi
wa Dar Live”
“Hayo mamabo ya Dar Live, leo yasimamisheni.
Kwa hiki kilicho fanyika leo Mlimani City nitahitaji
jibu ndani ya masaa ishirini na nne sawa”
Raisi Godwin alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo
mfanya hadi John kuogopa na kuhisi
amegundulika, ila hakuwa na uhakika kama ni
kweli raisi Godwin ametambua ni yeye au laa.
“Sawa mkuu nitakuletea jibu”
“Ondoka nenda kalishuhulikie sasa hivi”
“Sawa mkuu”
Mlinzi wa John akaingia na kumchukua bosi wake,
wakaondoka. Njia nzima ndani ya gari John
hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya
kufikiria ni kitu gani ambacho anaweza kukiunda
kikaendana na ukweli wa tukio lililo tokea.
***
Taratibu Sa Yoo akanyanyuka na kutoka katika
chumba cha Eddy, uso wake ulio jaa huzuni nyingi
pamoja na machozi uliweza kumstua madam Mery
aliye kuwa akitoka chumbani kwa Shamsa.
“Sa Yoo vipi, mbona hivyo?”
Shamsa hakujibu chochote zaidi ya kutembea
kama kama hajamuona madam Mery anaye
msemesha. Wote wakainngia chumbani na
kumkuta Shamsa akiwa amejifunga taulo akitaka
kwenda kuoga.
“Vipi tena, Sa Yoo mbona hivyo”
Shamsa alizungumza huku akiwa amekodolea
macho Sa Yoo, aliye kaa taratibu kwenye sofa,
huku akiendelea kumwagikwa na machozi.
“Sa Yoo eleza kama kuna tatizo na sisi tufahamu
basi ukikaa kimya hivyo unatuweka wezako katika
hali tata”
“Raisi Praygod na madam Rahab wamefariki dunia”
“What……….?”
“Ahahaaa acha utani Sa Yoo bwana watakufaje
kufanye wakati jana tulikuwa nao”
Shamsa alizungumza huku akitabasamu, akiamini
kabisa kwamba kitu kilicho zungumzwa ni uongo.
Kwa jinsi Madam Mery alivyo tulia kwa mbali
machozi yakimlenga lenga, ndio kitu kilicho anza
kumstua Shamsa.
“Unataka kusema wamekufa. Nani kakuambia hiyo
taarifa?”
“Eddy amedhibitisha hilo”
“Eddy. Eddy yupo wapi?”
“Chumbani kwake”
Shamsa akatoka hivyo hivyo na taulo lake alilo
jifunga hadi chumbani kwa Eddy na kumkuta
wakiwa wamekaa kitandani pamoja na Phidaya
huku wamekumbatiana.
“Eddy eti ni kweli raisi Praygod na madam Rahab
wamefariki dunia?”
Sauti ya Shamsa inawafanya Eddy na Phidaya
kuachiana. Wanamtazama Shamsa aliye simama
mbele yao akionekana kuwa na mashaka.
“Ndio amefariki, kwenye mlipuko wa bomu”
Shamsa taratibu anajikuta akipoteza furaha yake
huku akimtazama Eddy usoni anaye onekana
kujawa na huzuni. Hakuna aliye weza kuzungumza
kitu cha ina yoyote zaidi ya ukimya kutawala kwa
maana katika mpango wao, umeingia dosari kubwa
inayo onyesha dalili ya kushindwa katika
kuukamilisha mpango wao wa mapinduzi.
***
Taratibu Rahab akanyanyuka kitandani na kukaa
kitako. Macho yake yakamtazama daktari aliyopo
pembeni yake akimchunguza afya yake.
“Unaendeleaje?”
“Nahitaji kuondoka”
“Sahanani muheshimiwa hauwezi kuondoka pasipo
amri ya R.P.C John Masawe”
“Nimekuambia ninahitaji kuondoka na sihitaji
kusubiria amri ya mtu yoyote”
Kabla daktari hajajibu koplo Mwanamkasi akaingia
ndani humo huku akiwa ameongozana na koplo
Ludovick.
“Hawa ndio walio wekwa ili kunilinda?”
Rahab alizungumza huku macho yake yakiwa
mekundu, dhairi anaonyesha ana hasira kali sana.
Rahab akanyanyuka kitandani na kuchomo sindano
ya dripu iliyo chomwa kwenye mkono wake wa
kulia. Kopla Mwanamkasi akajaribu kumzuia Rahab
asitoke hapo, ila gafla akastukia akipigwa mtama
ulio muangusha chini na kumlaza sakafuni hadi
daktari pamoja na koplo Ludovick wakabaki
wameduwaa.
“Sihitaji mtu anifwatlie, nitamuua. Na wewe pisha
njia”
Taratibu koplo Ludovick akampisha Rahab, aliye
toka chumbani hapo na kuubamiza mlango huo
kwa kasi. Akiwa katika lifti ya kushukia kwenye
gorofa hilo la hoteli, akavua baibui alilo kuwa
amelivaa lililo jaa vumbi pamoja na damu damu.
Akabakia na suruali pamoja na shati alilo kuwa
amevalia kwa ndani. Lifti ilivyo funguka
hakutazama na watu usoni walio kuwa wakiisubiria
lifti hiyo kushuka, ili wapende kwenda juu. Akatoka
kwenye hoteli hiyo na kupishana na gari la R.P.C
likiingia katika eneo hilo.
“Nipeleke bahari beach”
Rahaba alimuambia dereva mmoja wa bodaboda,
wakaondoka eneo la hoteli. Safari yao ikachukua
nusu saa, wakawa wamesha fika hotelini. Akatoa
noti mbili za shilingi elfu kumi na kumkabidhi
dereva huyo ambaye hawakukubaliana hata bei.
Moja kwa moja akaelekea chumbani kwake,
akaingia bafuni na kuoga kisha akavaa nguo
nyingine za kikikazi na kutoka chumbani kwake.
Macho ya Rahab yakakutana na macho ya Shamsa
anaye toka kwenye chumba cha Eddy. Shamsa
pasipo kutegemea akajikuta akipiga kelele za
kuogopa na kuanguka chini. Kwa haraka Eddy na
Phidaya wakatoka chumbani kwao na kumkuta
Rahab akiwa anajaribu kumnyanyua Shamsa aliye
anguka chini. Kila mmoja akabaki akiwa
ameduwaa. Madam Mery pamoja na Sa Yoo nao
wakatoa katika chumba chao baada ya kuzisikia
kelele za Shamsa.
“Rahab!”
Madam Mery akashangaa huku akianza kupiga
hatua za kumfwata Rahab sehemu alipo
chuchumaa, akimsaidia Shamsa kunyanyua.
“Imkuwaje?”
“Hata mimi sifahamu. Mnyanyue kwa huko”
Madam Mery na Rahab wakasaidiana katika
kumyanyua Shamsa, wakampeleka katika chumba
cha Shamsa huku Eddy, Phidaya na Sa Yoo
wakifwata kwa nyuma. Wakamwagia maji ya baridi
Shamsa kichwani, akazinduka kutoka katika hali ya
kupoteza fahamu.
“Tulia ni salama”
Eddy alizungumza huku akimshika Shamsa mkono
aliye kurupuka tena baada ya kumuona Rahab.
Shamsa akatulia taratibu huku akiwatazama watu
wote waliomo ndani ya chumba hicho.
“Shamsa, najua utakuwa unahisi kwamba nimekufa,
ila kusema kweli sijakufa nipo hai”
“Mbona Eddy alisema umekufa?”
“Hapana hata mimi mwenyewe nilijua kwamba
Eddy amekufa, ila kusema kweli aliye kufa ni
Praygod.”
Wau wote wakaka kimya ndani ya chumba
wakimtazama Rahab usoni anaye zungumza kwa
huzuni kubwa sana.
***
Mpango wa mazishi ukaanza kufanyika, Eddy
pamoja na Madam Mery wakaufwatilia mwili wa
raisi Praygod na kufanikiwa kuupata katika
hospitali ya muhimbili. Japo ni mwili ulio haribika
sana ila hapakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya
kuhakikisha wanaupeleka katika nyumba yake ya
milele. Mwili wa raisi Praygod ukaandaliwa vizuri,
kisha ukapakizwa kwenye magari ya kukodisha
yanayo beba masanduku ya maiti. Moja kwa moja
wakaeleka bagamoyo kwenye nyumba ya raisi
Praygod, aliyo ijenga kipindi yupo katika uongozi
wa nchi.
Mazishi hayo yaliyo udhuriwa na watu wachache
sana, waliopo kwenye mpango wa kuupindua
uongozi wa raisi Godwin, yakafanyika huku Eddy
akishika nafasi ya kuwa kama mchungaji wa
kumfanyia maiti ibada takatifu.
“Kifo cha muheshimiwa raisi ni changamoto
kwenye maisha yetu. Tuamini kwamba kufa kupo.
Tupo kwenye mapambano, mapambano ya
kuyaokoa maisha ya wamiliomi ya Watanzania.
Tusilie hadi kumkufuru Mungu kwa maana hatujui
kesho zamu itakuwa ni ya nani”
Eddy alizungumza kwa uchungu mkubwa huku
biblia yake ikiwa mkononi mwake. Macho yake
aliwatazama Shamsa, Rahab, Madam Mery, Sa Yoo
pamoja na Phidaya. Wote wapo katika hali ya
majonzi mengi sana.
“Alikuwa ni kiongozi mmoja mahiri, hodari aliye
weza kuipigani na kuitete Tannzani kwa hali na
mali. Hadi juzi tukio la kufariki kwake, alikutana na
mimi pale Mlimani City, ili kunipa moyo katika
kuendeleza mapambano juu ya sisi kuweza
kufanya”
“Kwangu ninamchukulia kama mjomba. Nisiongee
sana, kwa maana nina imani tukianza kufwatilia juu
ya nani aliye weza kutega bomu, nina imani
tutaweza kumpata na kujua adui zetu ni nani na
nani”
“Katika jina la baba la na la mwana na la roho
mtakatifu, Amen”
“Amen”
Wote wakaitika kwa paoja. Eddy akachukua chepe
na kuanza kufukia kaburi la raisi Praygod. Shamsa,
akaona .naye akachukua chepe jengine na
kuendelea kufukia kaburi la Raisi Praygod. Wote
walio salia, wakaelekea stoo, kila mmoja akarudi na
chepe lake na kuendelea kusaidiana katika kuufukia
jeneza. Haikuwachukua muda mwingi wakawa
tayari wamesha maliza kuufukia mwili wa
marehemu. Siku hiyo hiyo wakalitengenezea
kaburi hilo kwa simenti, hadi inafika saa tatu usiku
kazi ikawa imesha malizika ya kulijengea kaburi.
“Nawashukuru kwa kujitoa kwenu katika
kuhakikisha kwamba munaulaza mwili wa mume
wangu katika sehemu husika. Nyinyi kwangu ni
familia kwa sasa, sina ndugu zaidi ya nyinyi na
wala sina mtu ninaye weza kusama kwamba
nitamkimbilia pale nitakapo kuwa na tatizo.
Nawapenda sana na nitaomba kuanzia leo tuwe
kitu kimoja”
Rahab alizungumza na wezake wakiwa katika meza
ya chakula.
“Hilo lisikupe wasiwasi kwa upande wangu,
nitahaikisha kwamba tunasaidiana wote katika
kufanya mapinduzi kaika nchi hii”
Sa Yoo alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti
alicho kuwa amekaa. Akanyoosha mkono wake wa
kulia kwenye meza, Shamsa naye akanyanyuka na
kuuweka mkono wake juu ya mkono wa Sa Yoo.
Watu wote walio bakia wakanyanyuka na kuiweka
mikono yao sehemu ilipo mikono ya Sa Yoo na
Shamsa.
“Kwa pamoja tunaweza, kwa pamoja mabadiliko ni
lazima kuweza kuyafanya”
“Kuanzia leo hii ni timu, ambayo nakwenda kuipa
jina la SHADOW TEAM”
Eddy alizungumza huku akiwatazama wote
machoni.
“Shadow, kwa nini umeiita Shadow team?”
Madam Mery aliuliza huku akitabasamu.
“Timu yetu itafanya kazi kama kivuli. Akili,
Umakini, na Maarifa ndio vitu vya pekee vitakavyo
weza kutupatia ushindi katika mpango wetu”
“Eddy mimi sijui kutumia bastola naomba
unifundishe”
“Usijali Sa Yoo, kuanzia kesho mazoezi yatakuwa
ni kwa wote”
“Hakuna haja ya kuondoka haoa nyumbani
kwangu. Kama ni silaha na kiwanja cha mazoezi
kipo kama munavyo weza kuona wenyewe”
Rahaba alizungumza na kuzidi kuwapa watu moyo
juu ya kazi wanayo kwenda kuifanya.
Wakakubaliana Eddy atarudi katika hoteli waliyo
kuwepo atakusanya mizogo yao yote ksha atarudi
nayo Bagamoyo walipo wezake.
Alfajiri na mapema Eddy akaondoka Bagamoyo na
moja kwa moja akaelekea hadi ilipo nyumba yake,
kwa haraka akaelekea katika chumba chake cha
siri, akachukua silaha za kutosha pamoja na pesa
za kutosha, akazipakiza katika gari alilo pewa na
Rahab kwa ajili ya atumizi. Akaelekea katika
maduka ya Laptop, akanunua Laptop sita aina za
Apple Mackbook zenye uwezo mkubwa katika
matumizi yake, kisha akanunua simu sita zenye
uwezo ambao anaamini zitarahisisha kazi yao.
Alipo hakikisha kwamba kila kitu kipo sawa alicho
kihitai, akaelekea hotelini na kuchukua kila kilicho
chao, japo pesa waliyo kuwa wamelipia hapo
hotelini haikuwa imekwisha.
***
Katika maisha yake yote, Agnes ndio ameanza
kuyapata maumivu ya mapenzi. Tanngu siku ya
mwisho anaachana na Erickson wake katika
hospitali ya Muhimbili, hadi leo hajaonana naye
wala namba ya simu anayo ipiga haipatikani. Kitu
kilicho zidi kumchanganya akaanza kuingiwa na
hisia mbaya za wivu na kuhisi kwamba huenda
Erickson anaweza kuwa na mwanamke mwengine.
“No niamuamuamini Erickson wangu hawezi
kunifanyia kitu kama hichi”
Agnes alizungumza mwenyewe kama mwenda
wazimu ndani ya ofisi yake. Akiwa katika mawazo
hayo huku simu yake ikiwa mkononi akijaribu
kupiga simu mara kadhaa namba ya Erickson
ambayo hadi wakati huu haipatikani hewani,
mlango wake ukagongwa.
“Ingia”
Akaingia secretary wake, aliye valia suti nzuri iliyo
ukaa mwili wake vizuri.
“Eheee, kuna nini?”
“Kuna wageni wamekuja wanahitaji kukuona wewe”
“Ila Happynes si nilisha kuambia kwamba sihitaji
mgeni yoyote leo ofisini kwangu sipo vizuri”
“Ndio nilijaribu kuwaambia hivyo, ila wakaniambia
kwamba wametoka ikulu”
Agnes baada ya kusikia ikulu ikambidi kuwa
mpole, akaiweka simu yake pembeni na
kumuambia awaruhusu watu hao kuweza kuingia
ofisini kwake. Secretary wake akatoka, na
kuwaambia wageni hao waweze kuingia ofisini
kwake.
Agnes hakuamini kumuona John akiwa
ameongozana na mlinzi wake anaye msukuma
kwenye kiti chake cha matairi sehemu yoyote
ahayo hitaji kwenda.
“Karibuni”
Agnes alizungumza huku akiachia tabasamu la
kawaida akionyesha kuto kuufurahia ugeni huo
uliopo mbele yake. John akamuomba mlinzi wake
kuweza kutoka nje ya ofisi kwa maana
mazungumzo anayo kwenda kuyazunumza hapo ni
muhimu sana.
“Nikusaidie nini?”
“Naamini huna la kunisaidia ila mimi ndio
ninapaswa kuweza kukusaidia”
John alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama
Agnes usoni anaye onekana kustushwa kidogo na
kauli hiyo.
“Usistuke sana kwa maana mimi ni mtu mwema
sana kwako, na siku zote sihitaji kukuona una
wasiwasi mwingi katika moyo wako wala maisha
yako”
“Samahani John, sijajua una maanisha nini?”
“Ninacho kimaanisha ni kuhusiana na Erickson si
ndio?”
Agnes baada ya kusikia jina la Erickson akajikuta
akikaa vizuri kwenye kiti huku akimtazama John
usoni kwa umakini sana.
“Labda nikuulize swali, tangu siku ulipo achana na
Erickson uliweza kuwasiliana naye?”
“Hapana, nampigia hapatikani”
“Na unatambua ni nani aliye sababisha mlipuko wa
juzi?”
“Ngoja kwanza mbona unauliza swali ambalo
unatambua mimi simjui huyo muhusika”
“Ok nitakueleza. Mtu aliye weza kufanya
shambulizi la ugaidi ni Eddy”
“Eddy, Eddy yupi?”
“Nyanyuka utoe simu kwenye mfuko wangu wa
shati”
Agnes kwa haraka akanyanyuka kwenye kiti chake
moja kwa moja akamfwata John sehemu alipo kaa,
akaitoa simu ya John.
“Ingia sehemu ya picha, humo ndani ipo picha
moja na huyo utakaye muona ndio mtu ambaye
kwa sasa pia ndio anaye mshikilia mpenzi wako
Erickson”
Kwa haraka Agnes akiwa kama amchanganyikiwa,
akaingia upande wa picha, akaufungua kwa haraka.
Sura ya picha aliyo kutana nayo si ngeni kabisa
katika kumbukumbu zake, kwa maana ni miongoni
mwa mtu waliye pewa kazi ya kumtafuta.
Agnes mwili mzima akaijikuta ukimtetemeka kwa
hasira kali huku akiendela kuitazama picha ya
Eddy.
“Huyo ni mtu aliye weza kutambua mpango wenu
wa nyinyi kumtafuta. Na kitu alichokuwa anapanga
kukifanya ni kuhakikisha anaanza kuwatanguliza
nyinyi kuzimu, kisha anawafwatia wale walio wapa
kazi ya kumfwalia. Ameona akimuua Erickson basi
wewe utateteraka na itakuwa ni rahisi kwa wewe
kuweza kufa”
Uongo wa John ukazidi kumuingia Agnes akilini
kisawasawa, kila jinsi alivyo zidi kuitazama picha
ya Eddy ndivyo jinsi hasira ilivyo zidi kumpanda
hadi akajikuta akitamani kuivunja simu hiyo aliyo
ishika.
“Kumbuka mtu anye fata katika kuuawa ni wewe
Agnes, Eddy amemteka Erickson kuwa makini”
Kwa hasira Agnes akaitupa chini simu ya John,
huku akihema kwa hasira kama Simba jike aliye
uliwa watoto wake alio wazaa muda mchache ulio
pita.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 86 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (86)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
INGHIA GOOFLE PLAYSTORE NA DOWNLOAD
APPLICATION(APP) YA STREAM NATION UWEZA
KUSOMA STORI ZA WAANSHI MAHIRI EDDAZARIA
G.MSULWA NA GIFT KIPAPA KWA VIFURUSHI VYA
MWEZI KWA SH 5000 NA KIFURUSHI CHA WIKI
MBILI KWA SH 3000.
ILIPOISHIA
Agnes mwili mzima akaijikuta ukimtetemeka kwa
hasira kali huku akiendela kuitazama picha ya
Eddy.
“Huyo ni mtu aliye weza kutambua mpango wenu
wa nyinyi kumtafuta. Na kitu alichokuwa anapanga
kukifanya ni kuhakikisha anaanza kuwatanguliza
nyinyi kuzimu, kisha anawafwatia wale walio wapa
kazi ya kumfwalia. Ameona akimuua Erickson basi
wewe utateteraka na itakuwa ni rahisi kwa wewe
kuweza kufa”
Uongo wa John ukazidi kumuingia Agnes akilini
kisawasawa, kila jinsi alivyo zidi kuitazama picha
ya Eddy ndivyo jinsi hasira ilivyo zidi kumpanda
hadi akajikuta akitamani kuivunja simu hiyo aliyo
ishika.
“Kumbuka mtu anye fata katika kuuawa ni wewe
Agnes, Eddy amemteka Erickson kuwa makini”
Kwa hasira Agnes akaitupa chini simu ya John,
huku akihema kwa hasira kama Simba jike aliye
uliwa watoto wake alio wazaa muda mchache ulio
pita.
ENDELEA
John akabaki akishangaa jinsi simu yake ilivyo
gawanyika vipande vipande chini. Hakuzungumza
chochote zaidi ya kumeza mate tu. Agnes kwa
haraka akrudi kwenye kiti chake na kukaa.
“Nitampata vipi huyo Eddy?”
Agnes alizungumza huku sura yake ikiwa
imejikunja ndita zilizo upoteza uzuri wak wote
ambao, John muda mchache alivyo ingia ofisini
hapo alikuwa akiufurahia sana.
“Ungana na mimi, na utaweza kumpata Eddy”
Kabla Agnes hajazungumza kitu cha aina yoyote,
simu ya Agnes ikaita na kumfanya kuitazama kwa
haraka, kitu kilicho mshangaza ni kuona jina la
Erickson likijitokeza kwenye simu yake, kabla
hajaipokea akamtazama John kwa macho makali
kisha akaipokea.
***
Eddy taratibu akajikuta akipunguza mwendo kasi
wa gari lake, baada kwa mbali kidogo kuona
msusuru wa magari ukiwa umesimama. Hakujua ni
kitu gani kilicho polekea gari hizo kusimama.
Taratibu akalisimamisha garni lake nyuma ya gari
lililpo mbele yake.
“Kuna nini?”
Eddy alizungumza mwenyewe huku akiitooa simu
yake mfukoni. Akakuta ikiwa imezima kutokana na
kuisha kwa chaji, na siku mbili hizi hakuitumia
kabisa kutokana na matatizo yaliyo weza kujitokea.
Akachukua waya wa chaji na kuuchomeka katika
sehemu ya USB, iliyo kwenye gari lake, taratibu
chaji ikaanza kuingia. Pasipo kujua ni kitu gani
kipo mbele yake, akazidi kusogeza gari lake
taratibu kuifwata foleni hiyo. Hadi zimebaki gari
mbili mbele yake ndipo Eddy anagundua foleni
hiyo imesababishwa na ukaguzi mkali wa jeshi la
polisi wakisaidiana na jeshi la kujenga taifa
wakikagua magari yote yanayo ingia na kutoka
katika mkoa wa Dar es Salaam.
“Shitii”
Eddy akajikuta akitoa macho na kuanza cha
kufikiria ni nini cha kufanya kwa maana askari hao
wanakagua gari zima hadi kwenye buti. Bahati
mbaya ni kwamba kwenye buti ya gari lake
amebeba silaha anazo zimiliki kinyume na sheria.
Kitu kingine kinacho zidi kumpagawisha nyuma
yake kuna magari mengi ambayo nayo yapo
kwenye msururu huo wa kukaguliwa.
“Agnes Agnes”
Eddy alizungumza huku kwa haraka akijitahidi
kuiwasha simu yake, kwa bahati nzuri akaiwasha
japo ina asilimia tano za chaji, ila akajitahidi hivyo
hivyo kumpigia Agnes akiamini anaweza kuapata
msaada kwake. Tayari gari la mbele yake lilisha
anza kukaguliwa, huku askari wengine wawili walio
shikilia mbwa wawili wakubwa, wakilisogelea gari
lake huku bunduki zao zikiwa begani. Kitendo cha
Agnes kupokea simu, simu ya Eddy ikazima chaji
tena.
“Fu*k”
Eddy akajikuta akiachia tusi zito huku akiitazama
simu hiyo, kwa haraka akakumbuka anasimu
ambazo ni mpya ameziweka siti ya nyuma,
akageuka kwa haraka na kuichukua moja, akatoa
chip kwenye simu yake na kuiweka kwenye simu
moya. Kwa haraka akaiwasha, simu ikiendelea
kuwaka tayari askari wa mbele alisha anza kumpa
isha ya kulisogeza gari lake kwenye sehemu
yanapo kaguliwa. Ikambidi taratibu kulizogeza gari
lake, mbaya zaidi mbele kuna geti la chuma
pamoja na miba mirefu iliyo kaa mfumo wa chuma
iliyo tandazwa barabarani endapo utajaribu
kukimbia na kuikanyaga miba hiyo basi tairi za
gari lako zote zitapata pancha. Kitu kingine
ambacho ni ngumu kuweza kuwakimbia askari hao,
ni magari makubwa ya jeshi yaliyo katika pande
zote mbili za barabara yakiwa yamefungwa mitutu
mikubwa ya bunduki, zenye uwezo wa kulichakaza
gari lako vibaya ndani ya dakika moja pale tu
utakiuka sheria na kuwakimbia. Mbwa hao
wakubwa, walio fundishwa mbinu za kunusa kitu
chochote ambacho si cha usalama, wakanza
kulizunguka gari la Eddy hususani sehemu ya buti,
ambapo ndipo zilipo bunduki, mabomu pamoja na
vibunda vya pesa za kigeni. Askari mmoja
akagonga kioo cha upande wa Eddy alipo kaa kwa
ishara akimuomba kushuka haraka.
Eddy akamtazama askari huyo, aliye anza kuishika
bunduki yake vizuri huku akiwa amemkazia macho,
taratibu akashuka kwenye gari huku akiwa
ameshika simu yake mkononi.
“Muheshimiwa fungua buti, tunahitaji kukagua”
Askari mmoja alizungumza huku akimtazama Eddy
kwa umakini.
“Munataka kukagua nini?”
“Hilo wewe halikuuhusu fungua buti tukague
usitupotezee muda bwana”
“Siwezi kukagua gari kwa maana mzigo ulio
kuwemo humo ni wa muheshimiwa waziri Agnes”
“Bwana wewe, sisi hatujali kama ni mzigo wa
waziri au laa. Tutancho hitaji fungua buti tuangalie
ni kitu gani ulicho bebe. Utakuta nyinyi ndio
munao lipua lipua raia wema”
Askari huyo mwenye nyota mbili begani mwake,
akazidi kumuamrisha Eddy kwa sauti kali yenye
msisitizo na kuwafanya askari pamoja na
wanajeshi walio kuwa eneo hilo kuwa makini kila
mmoja na silaha yake.
“Muheshimiwa mimi siwezi kufungua, kwa maana
sio makubaliana niliyo agizwa”
Eddy alizungumza huku akifunga mlango wa gari
lake na funguo, kitendo kilicho zidi kumkasirisha
askari huyo aliye jikuta akitandika ngumi ya tumbo
Eddy na kuwaamrisha askari wake, kumpigisha
magoti Eddy huku waking’ang’aniana kumpokonya
funguo ya gari.
***
Agnes akaitolea macho simu yake baada ya kuona
imekata, kwa haraka akaipiga namba ya Erickson
na kuambiwa kwaba haipatikani kwa wakati huu,
jambo lililo mfanya kunyanyuka tane kwenye kiti
chake na kuipiga tena namba ya Erickson na
majibu akayakuta ni yale yale, kwamba haipatikani.
“Mbona hapatikani”
Agnes alizungumza mwenyewe huku akiitazama
simu yake kwa umakini. John kwa kiherehere
akajikuta akiuliza ni nani huyo, Agnes akamtazama
kwa jicho kali kisha akaachia msunyo mkali, huku
akimpandisha na kumshusha John.
“Unataka kujua ni nani ikiwa wewe kama nani?”
“Ahaaa labda naweza kukusaidia”
“Kwanza nakuomba utoke ofisini kwangu, nahitaji
kuwa peke yangu”
“Ila hatijazungumza mazungumzo”
“John kama ni mazungumzo ya mtu aliye mteka
Erickson wangu naomba yaishie hapa kwa leo
sawa, kichwa change hakipo sawa”
Agnes alizungumza huku akiupiga hatua hadi
mlangoni, akaufungua na kuuacha wazi, kwa ishara
akamuomba John kutoka ofisini hapo.
“Ahaaa kumbe mwenyewe huwezi kutoka, Weee
njoo umchukue mtu wako”
Agnes alizungumza kwa dharau na kumfanya John
kujisikia vibaya moyoni mwake, ila ndio hivyo
hawezi kufanya kitu chochote ukiachilia kutokuwa
na viungo ila mtu anaye zungumza hivyo ni mtu
anaye utesa moyo wake kwa kiasi kikubwa sana.
Mlinzi wa John akaingia na kumtoa bosi wake.
Agnes akaufunga mlango kwa nguvu, na kurudi
kwneye kiti chake. Akaipiga tena namba ya
Erickson kwa bahati nzuri ikaanza kuita kitu kilicho
mfanya kushusha punzi huku akiwa na shauku
kubwa ya kutaka kujua ni kitu gani anacho taka
Erickson. Simu ikapokelewa.
“Halooo”
Agnes alizungumza kwa sauti ya mapenzi, ila sauti
alizo zisikia zikamfanya ake vizuri kwenye kiti
chake.
‘Achia funguo wewe mwana haramu mkubwa’
‘Akileta ujinga mpigeni risasi’
‘Lakini hamna haki ya kunipi……aahaaaaa’
‘Nyamaza Nguruwe wewe’
‘Simu yake ipo hawani hiyo hembu ikate kuna mtu
naona ameipokea’
Simu ikakatwa na kumfanya Agnes mwili mzima
kuishiwa nguvu, akatamani kunyanyuka na kwenda
kumfwata John, aliye mueleza kwamba Erickson
wake ametekwa na mtu anaye itwa Eddy ila
akajikuta akishindwa kabisa, woga na wasiwasi
mwingi vikaujaa mwili waka, hata simu aliyo ishika
mkononi mwake akaiweka mezani taratibu akahisi
ni nzito sana kwake.
‘Akilite ujinga mpigeni risasi’
Sauti hiyo ikajirudia kwa haraka kwenye kichwa
cha Agnes, na kujikuta akishusha pumzi na
kujikaza kupoteza wasiwasi unao ufanya mwili
kuishiwa na nguvu kwa haraka akaichukua simu
yake na kuipiga tena namba ya Erickson, ikaita
kidogo ikakatwa, akarudia kwa mara ya pili ikaita
na kukatwa. Akapiga kwa mara ya tatu akakuta
haipo hewani ikiashiria kwamba imezimwa na watu
hao.
‘Lakini hamna haki ya kunipi…….aahaaaaa’
Sauti hiyo ya Erickson ikamfanya Agnes
kumwagikwa na machozi, akifikiria mateso anayo
yapata Erickson mwanaume aliye mpenda kupita
kitu cha aina yoyote.
***
Eddy akawa yupo radhi kufa ila si kuachia funguo
aliyo ishika, anayo minyana na askari wawili wanao
hitaji kuichukua ili kufungua gari lake. Tukio lake
likawafanya askari na wanajeshi wote kuelekezea
mitutu yao ya bunduki eneo la tukio. Simu ya Eddy
ikaita, akaipokea ila askari mmoja akampiga teke
na simu yake kuangukia pembeni ikiwa hewani
“Achia funguo wewe mwana haramu mkubwa”
Askari mmoja alizungumza huku akizidi
kuung’amg’ania mkono wa kulia wa Eddy ulio
shikilia funguo ya gari.
“Akilete ujinga mpigeni risasi’
Mkubwa wao alizungumza huku akiangalia vijana
wake wanavyo minyana na Eddy aliye lala kwenye
lami, huku mkono wenye funguo akiwa ameulalia.
“Lakini hamna haki ya kunipi……aahaaaaa”
Mkuu wao huyo akamshindilia Eddy teke la mbavu
lililo mfanya akatishe sentensi yake na kuugulia na
maumivu makali sana.
“Nyamaza Nguruwe wewe”
Mkuu huyo aliye mrefu na mweusi, alizungumza na
kumtandika Eddy teke jengine la mbavu na kuzidi
kumfanya Eddy kutoa ukelele wa maumivu.
“Simu yake ipo hawani hiyo hembu ikate kuna mtu
naona ameipokea”
Askari mmoja alizungumza na kumfanya askari
mwengine kuiokota simu ya Eddy na kuikata, kisha
akaiweka mfukoni mwake. Foleni ya magari ikazidi
kuongezeka na kuwafanya watu kuchukizwa na
zoezi hilo, kwa maana askari wameacha ukaguzi
na kushindana na mtu mmoja anaye leta ubishi
katika kuitoa funguo ya gari lake, wanalo hisi
limebeba vitu ambavvyo ni haramu.
“Mbona wanachukua muda mrefu?”
Manka alimuuliza dereva wake, wakiwa ni
miongoni mwa magari yaliyo simama foleni
yakitokea Bagamoyo, kuelekea Dar es Salaam.
“Sijui kwa nini?”
“Hembu shuka nenda kaangalie ni kitu gani
wanacho kifanya kwa maana hakuna gari linalo
ruhusiwa”
“Sawa madam”
Dereva huyo akashuka na kuyapita magari saba
yaliyopo mbele yao, ndipo alipo weza kushuhudia
tukio la askari wakiminyana na mmoja wa watu
aliye lala chini, wakimtandika virungu, akionekana
kuwa ni mbishi kutii amri aliyo pewa. Dereva
akarudi kwenye gari.
“Kuna nini?”
“Ahaaa kuna mtu naona anapigwa virungu na
askari sijua amewagomea kitu”
“Daaaa ni mwanaume au mwanamke”
“Ni mwanaume”
“Sasa hawa nao wanaleta mambo yakiseng*
inakuwaje mtu mmoja afanye watu tukae zaidi ya
robo saa kwenye foleni. Wamshike na kumuweka
kando waruhusu magari mengine.”
Manka alizungumza huku akishuka kwenye gari,
akionekana kuchukizwa, kwa mwendo wa haraka
akazipita gari zilizopo mbele yao hadi sehemu ya
geti, askri walipo mtazama wakaweza kumtambua.
“Kuna nini hapa?”
“Ahaa ni yule kijana pale anakataa kutoa funguo ya
gari lake, likaguliwe”
Mwanajeshi mmoja alizungumza huku
akimuonyesha Manka sehemu tukio linapo
endelea. Manka kwa hasira akazidi kupiga hatua
kuelekea eneo hilo la tukio, kila askari na
mawanajeshi aliye muona akampigia saluti.
“Kama ni mbishi si mumtupi………”
Manka hakumalizia sentensi yake ya mwisho,
baada ya kuona mtu anye leta ubishi huo ni
Erickson, mwanaume anaye jaribu kuhakikisha
anamuingiza kwenye imaya yake ya mapenzi.
“Acheni, acheni, acheni”
Manka alizungumza huku akiwasogeza askari
wanao mpiga Eddy kwa virungu. Kwa haraka
akapiga magoti chini kila askari akabaki
akishangaa, kumuona bosi wao akimnyenyekea
mtu waliye mshushia kipigo kizoto.
“Erickson nini tena baba yangu?”
Manka alizungumza huku akimnyanyua Erickson
anaye mwagikwa na damu za mdomo na puani,
kwa kipigo alicho kipata, Eddy hata hakumuona
Manka vizuri, kwani ukungu mwingi ulitawala
kwenye macho yake.
“Kwa nini munapiga pipiga tu watu nyingi mbwa”
Manka alizungumza kwa hasira, hapakuwa na
askari aliye jibu chochote wote wakaka kimya.
Manka akajitahidi kumyanyua Erickson aliye ishiwa
nguvu kabisa hadi akasimama.
“Nani ametoa amri apigwe”
Askari wengine wanye vyeo vya chini,
wakamtazama bosi wao. Manka akamtazama mkuu
huyo wa polisi kwa macho makali yaliyo jaa hasira.
“Si….iimu yangu”
Erickson(Eddy) alizungumza huku akimnyooshea
mkono taratibu kwa askari aliye idumbukiza simu
mfukoni. Kwa haraka askari huyo akaitoa simu
hiyo mfukoni mwake na kumkabidhi haraka Manka
aliye mkata jicho kali baada ya kunyooshewa
mkono na Erickson.
“Wewe kabla ya siku haijaisha nikuone ofisini
kwangu”
Manka alizungumza huku akimkazia macho mkuu
wa polisi, ambaye amenywea kama mwanaume
aliye achia hewa chafu mbele ya mama mke wake.
“Gari yangu”
Eddy alizungumza huku akikabidhi funguo Manka,
aliye ichukua kwa haraka haraka.
“Njooni mumshike mumuingize kwenye gari,
munamtoke nini mimacho”
Askari wawili wakamshika Eddy, Manka akafungua
mlango wa upande wa dereva, kisha akaingia
askari hao wakamzungusha Eddy hadi upande wa
pili, wakamuingiza kwenye siti ya mbele,
wakamfunga na mkanda. Manka taratibu akageuza
gari na safari ya kuelekea Dar es Salaam ikaanza
huku kwa upande mmoja moyoni mwake akiwa
amejawa na furaha kwa kuweza kumpata Erickson.
“Hii kweli ni bonge la movie”
Jamaa mmoja alizungumza, huku akisogeza gari
lake katika sehemu lilipokuwa gari la Eddy.
Akaitazama video aliyo irekodi ya tukio zima la
Eddy kushushushiwa kipogo na polisi. Bila ya
kujiuliza mara mbilimbili akairushia kwenye
mtandao wa kijamii wa Facebok kwenye akaunti
yake huku akiandika maandhishi yaliyo someka
‘Hawa ndio askari wetu wa Tanzania’. Ndani ya
dadika moja watu zaidi ya elfu moja wakawa
wameitazama video hiyo, huku kila mmoja akitoa
maoni yake juu ya tukio hilo.
***
“Jamani njooni muone”
Sa Yoo alizungumza huku akiwa ameshika ‘tablet’
ya madam Mery aliye muomba ili kuperuzi peruzi
kwneye mtandao.
“Tuone nini?”
Shamsa aliuliza huku akiwa ameshika kisu pmoja
na kiazi mkononi mwake anacho kimenya
wakiandaa chakula cha mchana. Sa Yoo hakujibu
kitu zaidi ya kukaa kimya akiitolea macho video
iliyo rushwa mtandanoni inayo onyesha Eddy
akipigwa na askari. Madam Mery aliye kaa pembeni
ya Sa Yoo, akajisogeza na kuangalia ni kitu gani
ambacho Sa Yoo anakitazama.
“Huyo si Eddy?”
Madam Mery aliuliza na kuwafanya Phidaya,
Shamsa na Rahab kunyanyuka walipo kaa na
kusogea sehemu walipo Sa Yoo na madam Mery.
Phidaya akajikuta akimpokonya Sa Yoo tablet hiyo
na kuishika vizuri kumuangalia jinsi mumewe
anavyo shushiwa virungu na polisi hao. Phidaya
akahisi kuchanganyikiwa kwa mana hakujua ni kitu
gani ambacho kimekuta mume wake.
“Watakuwa wamemstukia kwamba ndio Eddy nini?”
Sa Yoo aliuliza huku akimtazama Madam Mery
usoni aliye tingisha kichwa kukataa alicho kisema
Sa Yoo.
“Manka”
Shamsa alizungumza huku akiwa amesimama
pemeni ya Phidaya anaye tazama video hiyo mwili
mzima ukimtetemeka.
“Manka”
Madam Mery akasogea na kutazama video hiyo,
akamuona jinsi Manka akimsaidia Eddy na
kuondoka naye. Phidaya akaiachia tablet hiyo, ila
Shamsa akaiwahi kuidata kabla haijafika chini.
“Phidaya kaa chini utulie”
Rahab alizungumza huku akimshika Phidaya na
kumkalisha chini, dumbuwazi lililo mpata Phidya
likamfannya kukaa kimya asizungumze chochote,
ila macho yake yanaonyesha ni jinsi gani alivyo
jawa na hasira pamoja na uchungu wa kushuhudia
mumewe akipokea kipigo hicho kama mwizi.
“Kuna hatari ya Eddy kugunduliwa”
“Kwa nini unazungumza hivyo madam Mery?”
“Manka ni dada yake Eddy, baba mmoja ila mama
tofauti”
“Sasa hapo atajulikana vipi wakati sura yake
haionyeshi kabisa kama ni yabandia?”
“Hata kama ni ya bandia ila tunatakiwa kuingia
kazini kuhakikisha tunamrudisha Eddy hapa la
sivyo kila kitu kinakwenda kuharibika”
Madam Mery alizungumza kwa msisitizo,
wakaacha kila walicho kuwa wakikifanya.
Wakaingia katika vyumba vyoa kila mtu
akabadilisha nguo alizo kuwa amevaa, kwa maana
walishinda na nguo za kufanyia kazi za jikoni
ikiwemo kanga. Wote watano wakaingia kwenye
gari jengine la Rahab aina ya Prado, safari ya
kuelekea Dar es Salaam ikaanza
“Ila namba ya Eddy madam Mery si unayo?”
Sa Yoo alizungumza huku akimgeukia madam
Mery aliye kaa siti ya nyuma.
“Hapana”
“Mimi nimeishika kwa kichwa”
Rahab alizungumza huku akiongoza mwendo kasi
wa gari. Rahab akamtajia Sa Yoo namba ya Eddy.
Sa Yoo akaipiga namba hiyo ambayo haipo
hewani.
“Vipi?”
Shamsa alizungumza huku wasiwasi ukiwa
umemjaa sana,
“Hapatikani”
***
“Naku..fa, naku…fa”
Eddy alizungumza kwa tabu, na kumfanya Manka
kustuka na kumtazama jinsi alivyo jilaza kwenye
siti hiyo.
“Erickson usife nipo pamoja na wewe”
Manka alizungumza huku akizidi kuongeza
mwendo kasi wa gari lake. Eddy hakujibu kitu cha
aina yoyote, taratibu akaanza kukoroma kama mtu
anaye kata roho, jambo lililo zidi kumuogopesha
sana Manka.
“Erick, Erickson”
Manka aliita huku mkono mmoja akimtingisha
Eddy anaye zidi kukoroma, huku damu zikimtoka
puani. Machozi yakaanza kumlenga lenga, Manka
furaha ya kuwa na Erickson maishani mwake,
akaanza kuona inaingia doa. Manka njia nzima
akawa anapiga honi kuomba kupishwa, hakutamani
kuweza kuona kifo cha Erickson kinatokea mbele
ya macho yake. Majiara ya saa kumi jioni tayari
akawa amefika kwenye foleni ya Mwenge.
Kila alipo mtazama Erickson aliye lala kimya,
kwenye siti akatamani alipaishe gari lake hili kupita
na kumuwahisha hospitalini, ila haikuwa hivyo ni
lazima kufwata foleni hiyo. Jasho jingi likazidi
kumwagika Manka japo ndnai ya gari kuna A/C ya
kutosha ila haikufanya kazi.
Gari zilipo ruhusiwa, Manka, akajitahidi kuongeza
mwendo, akili yake yote inamtuma kumpeleka
Erickson katika hospitalli ya Aghakan.
Hadi anafika hospitalini tayari ilisha timu saa kumi
na moja jioni, kwa haraka kitanda cha matairi
kikatolewa, Erickson akapandishwa kwenye kitanda
na moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba
cha matibabu.
“Muheshimiwa tunakuomba usubiri nje”
Daktari mmoja alimzuia Manka baada ya kumuona
akiitaka kuingia ndani ya chumba hicho. Kwa
haraka mwili wa Erickson ukapigwa X-ray
kuangalia ni sehemu gani ina tatizo. Damu nyingi,
ikaonekana imevilia kwenye mbavu za upande
wake wa kulia, unao onekana kujeruhiwa kwa
kupigwa mara kadhaa.
“Group la damu yake ni nini?”
Daktari alimuuliza nesi, aliye mpa zoezi la kuipima
damu ya Erickson.
“Ni group O plus”
“Mungu wangu, hiyo damu dokta imetuishia katika
benki yatu ya damu”
Nesi mwengine alizungumza huku akimatazama
daktari huyo. Daktari akaka kimya huku
akimtazama Erickson waliye muwekea mshine za
hewa ya oksijeni, inayo msadia kuhema. Daktari
akatoka katika chumba hicho na kumkuta Manka
akiwa amesimama nje ya chumba hicho.
“Daktari vipi, mgonjwa anaendeleaje?”
“Mgonjwa wako, anaupungufu wa damu nyingi.
Kundi la damu ambalo analo sisi imetuishia hapa
hospitalini”
“Ni group gani la damu?”
“Ni O plus”
“Naomba muniangalie mimi kana ninaweza
kumchangia damu”
Hapakuwa na muda wa kupoteza Manka
akaingizwa kwenye chumba cha kupimia damu,
kwa bahati nzuri group la damu yake linaendena
kabisa na group la damu ya Erickson hadi daktari
akshangaa.
“Huyu mgonjwa ni nani yako?”
“Ni mpenzi wangu”
Wakamruhusu Manka kutoka nje ya chumba cha
kutolea damu. Daktari akawaomba manesi wake
kuitanguliza dumu katika chumba cha upasuaji
kisha, yeye akaipima DNA kati ya Manka na
Erickson. Kisha akaelekea katika chumba cha
upasuaji na kuwakuta madaktari wezake
wakiendelea na kazi ya kumshuhulikia Erickson
aliye anza kupasuliwa upande wa mbavu za kulia
sehemu damu ilipo vilia.
Hadi inafika saa mbili usiku tayari wakawa
wamefanikiwa kuta madonge ya damu yaliyo vilia
kwenye mbavu za Erickson. Dokata Nelson akarudi
katika chumba cha kupimia damu, akatazama
vipimo vya DNA, akabaki akitoa macho kwani
Manka na Erickson vipimo vinaonyesha ni damu
moja, ikimaanisha ni ndugu.
“BINGO”
Dokta Nelson alizungumza huku akiachia
tabasamu pana, akiamini utajiri upo mbele ya
maisha yake endapo ataifichua siri hii mbele ya
wahusika.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 87 YA SIMUHILI HII.
 
SORRY MADAM (87)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
INGHIA GOOFLE PLAYSTORE NA DOWNLOAD
APPLICATION(APP) YA STREAM NATION UWEZA
KUSOMA STORI ZA WAANSHI MAHIRI EDDAZARIA
G.MSULWA NA GIFT KIPAPA KWA VIFURUSHI VYA
MWEZI KWA SH 5000 NA KIFURUSHI CHA WIKI
MBILI KWA SH 3000.
ILIPOISHIA
Hadi inafika saa mbili usiku tayari wakawa
wamefanikiwa kuta madonge ya damu yaliyo vilia
kwenye mbavu za Erickson. Dokata Nelson akarudi
katika chumba cha kupimia damu, akatazama
vipimo vya DNA, akabaki akitoa macho kwani
Manka na Erickson vipimo vinaonyesha ni damu
moja, ikimaanisha ni ndugu.
“BINGO”
Dokta Nelson alizungumza huku akiachia
tabasamu pana, akiamini utajiri upo mbele ya
maisha yake endapo ataifichua siri hii mbele ya
wahusika.
ENDELEA
Dokta Nelson akaanza kuaandika majibu hayo
kwenye karatasi sahihi ya kuandikia majibu hayo,
alipo hakikisha ameyamaliza, akayaweka kwenye
bahasha kubwa na kutoka katika ofisi yake kwa ajili
ya kuelekea nyumbani kwake
***
“Hii video inaonyesha Eddy amaondoka na Manka
kutumia gari lako madam”
Sa Yoo alizungumza huku akirudia kuitazama
video hiyo ambayo imerushwa katika mtandao wa
Facebook.
“Ndio”
“Nitajie namba za gari?”
“Za nini?”
“Nahitaji kulitafuta kwa satelait”
Rahab akamtajia Sa Yoo namba za gari lake, kwa
utaalamu mkubwa ambao Sa Yoo anao kwenye
maswala ya ‘IT’, akaanza kuisika gari hiyo,
hazikupita dakika nyingi tayari alama ya gari hilo
ikawa inaonyesha kwamba lipo katika hospitali ya
Agakhan.
“Hapa ndipo lilipo”
Sa Yoo alimuonyesha Rahab ambaye anaendelea
kukanyagia mafuta ya gari lake, safari ikazidi
kusonga, kitu kilicho mchukiza Rahab ni foleni
aliyo ikuta maeneo ya Mbezi Beach kueleka
Mwenge. Hapakuwa na jinsi zaidi ya kukaa kwenye
foleni hiyo inayo kwenda kwa mwendo wa taratibu.
Masaa yakazidi kusonga mbele huku foleni
ikisogea taratibu hadi ikafika zamu ya wao
kuruhusiwa, wakaendelea na safari yao. Hadi
wanafika hospitali ya Agakhan ni majira ya saa nne
kasoro usiku. Kweli wakalikuta gari la Eddy likiwa
sehemu ya maegesho, wakalikagua na kulikuta lipo
salama.
“Sasa watakuwa wapo wapi?”
Phidaya laliuliza huku akionekana kujawa na
wasiwasi mwingi usoni mwake.
“Tujigaweni inabidi kwenda kuuliza kila sehemu”
“Sawa”
Wakajigawa kila watu wakaelekea kwenye upande
wake lengo ni kuhakikisha kwamba wanampata
Eddy katika wakati huo.
***
Kitendo cha Eddy kutolewa katika chumba cha
upasuaji kikafufua matumaini mapya ya Manka
aliye kaa nje ya chumba cha upasuajia kwa masaa
kadhaa akisubiri Eddy kufanyiwa huduma hiyo.
Moja kwa moja Eddy akapelekwa katika chumba
cha wagonjwa mahututi ambacho kipo gorofa ya
chini kabisa. Huku muda wote Manka akiwa nyuma
ya kitanda hicho kinacho sukumwa na manesi
wawili mmoja akiwa mbele huku mwengine akiwa
nyuma.
Kabla Manka hajaingia kwenye chumba hicho, simu
yake ya mkononi ikaita na kumfanuya asimame,
akakuta ni jina la baba yake kipenzi Mzee Godwin,
taratibu akaipokea na kuiweka sikioni
“Upo wapi mwanangu?”
“Baba nipo hospitali?”
“Hospitali?”
“Ndio baba Erickson amepigwa na maaskari”
“U…u…upo hospitali gani?”
“Nipo Agakhan”
“Nakuja sasa hivi”
Mzee Godwin alizungumza akionekana kupaniki
kwa hasira kali, akionyesha dhahiri kukasirishwa
na tukio hilo, Manka akairudisha simu yake
mfukoni na kuingia katika chumba hicho cha
wagonjwa mahututi.
“Ila muheshimiwa utakiwa kukaa humu kwa muda
mrefu hichi ni chumba cha wagonjwa mahututi”
“Siwezi kuondoka na kumuacha mpenzi wangu
katika eneo hili sawa nesi”
“Nimekuelewa muheshimiwa”
Nesi huyo hakuwa hakuwa na kitu cha
kuzungumza zaidi ya kukubaliana na matakwa ya
Manka yote ni kutokana na Manka kuwa ni
kiongozi serikalini. Hazikupita dakika nyingi
ving’ora vya polisi vikasikika nje ya eneo la
hospitali na kuwafanya watu wengie walipo eneo la
nje ya hospitali kushangaa ujio huo wa raisi ambao
ni wa gafla sana.
“Yes nakwenda kufichua bomu”
Phidaya aalisikia sauti hiyo ya kiume ikitokea
kwenye moja ya ofisi.
“Bomu?”
Phidaya akaiuliza mara mbili mbili na kujikuta
akifungua mlango wa ofisi hiyo pasipo kubisha
hodi kwa maana ni siku chache zimepita tangu
mlipuko wa bomu ulio pelekea kuyaangamiza
maisha ya raisi Godwin ulipotokea. Daktari huyo
akaonekana kustuka baada ya kumuona Phidaya
akiwa amesiamama mbele ya meza yake huku
mlango akiwa ameufunga.
“Phidaya?”
Daktari huyo akajikuta akiita jina la Phidyaa huku
mwili mzima ukimtetemeka sana. Phidaya akabaki
akishangaa kila alipo jaribu kuzivuta kumbukumbu
zake juu ya ni wapi aliwahi kumuona daktari huyu
hakuweza kukumbuka kabisa, Phiday akapiga hatua
mbili mbele huku akiwa amemkazia macho daktari
huyo aliye tamani hata kujirusha dirishani kutoka
gorofani ili afe ila si Phidaya kumsogelea.
“Nisamehe Phidaya”
Daktari alizungumza huku mwili mzima
ukimtetemeka hadi haja ndogo akahisi ikimwagika.
Bahasha yenye majibu ya DNA ikamdondoka
mkononi mwake na kuzidi kurudi nyuma hadi
akafika ukutani na pemeni yake kuna dirisha la
vioo lililo wazi.
“Sio mimi niliye kuua ni Ranjiti aliye panga
mpango wa ku…ku…fany…a wewe ufe”
Phidaya akatingisha kichwa, na kuanza kujua ni
kitu gani ambacho kinamfanya daktari huyo kuwa
muoga kwa kiasi hicho.
“Kwa hiyo ukaona ni utu kunitenganisha na mume
wangu si ndio?”
Phidaya alizungumza sasa kwa kujiamini huku
taratibu akizidi kupiga hatua za kumfwata daktari
huyo anaye onekana kuzidi kuweweseka kwa
woga.
“Haa….aahaa panaa”
“Nyionyeshe ni bomu gani ulitaka kwenda
kulifichua”
Dokta Nelson mimacho ikamtoka, sasa muda huu
mkojo ukaanza kushuka kwenye mapaja yake hadi
ukatokeza kwenye suruali yake na kumfanya
Phidaya kuona kabisa dokta huyo amejikojolea
“Niambiee nionyeshe hilo bomu”
Kwa ishara dokata Nelson akamuonyesha Phidaya
baasha iliyo anguka chni, Phidaya akaitazama
bahasha hiyo kisha akatabasamu kwa dharau kwa
maana kitu ambacho dokta Nelson anamuonyesha
akihendani kabisa na kitu ambacho amemuuliza
kwa muda huu.
“Unautani na mimi eheee?”
“Si….siiku tanii”
“Nionyeshe sasa hilo bumu”
“Li….liipo ndani y….a hiyo bahasha”
Dokta Nelson alizungumza huku taratibu
akijisogeza hadi sehemu ya dirisha, Phidaya
akamtazama kwa macho makali ya kujiamini kisha
akapiga hatua kubwa mbili za vishindo kumtisha
dokta Nelson ambaye anautumia udhaifu wa
makosa aliyo yafanya kwa miaka kadhaa
kumtingisha, gafla dokta Nelson akapanda dirishani
na kujirusha nje na kumfanya Phidaya kukimbilia
hadi dirishani, kitu alicho kishuhudia chini
kikamfanya Phidaya kufumba macho kwa sekunda
kadhaa kisha akatazama tena. Kichwa cha dokta
Nelson, kimetua kwenye kiwe kubwa na kupasuka
hapo hapo, hadi ubongo ukatoka.
“Pumzika salama”
Phidaya alizungumza huku akiondoka hapo
dirishani, akafika mlangoni akasimama kwa
sekunde kadhaa, akatazama nyuma, chini ilipo
anguka bahasha aliyo kuwa anaonyeshwa na dokta
Nelson. Akarudi taratibu hadi sheenu ilipo,
akachuchumaa na kuitazama vizururi, akapeleka
kidole taratibu akiamini ni bomu japo hana ukweli
nalo.
Taratibu akainyanyua bahasha hiyo, ila wepesi wa
bahasha hiyo ukamfanya aitazama vizuri kwa
kuifungua ndani, akaona karatasi mbili nyeupe.
Vilio vinavyo tokea chini lilipo dirisha la ofisi ya
dokta Nelson kukamstua Phidaya na kujikuta
akiikunja bahasha hiyo na kuishika mkononi na
kuanza kutoka ofisini humu.
Kundi la watu walio valia suti nyeusi huku mmoja
wao akiwa amevalia suki ya kaki, ukamfanya
Phidaya kusimama akiwa hapo hapo mlangoni na
kuwatizama watu hao. Mmoja wao akamtambua
kwa haraka sana kwamba ni baba yake mkwe Mzee
Godwin ambaye naye pia akapunguza mwendo
kasi na kumkazia macho Phidya aliye simama
katika mlango wa kutokea katika ofisi ya dokta
Nelson.
‘Phiday kimbia’
Ndio sauti ya pekee aliyo isikia akilini mwake, bila
hata ya kujiuliza mara mbili mbili, akaanza kutimua
mbio na kuwafanya walinzi wawili wa raisi Godwin
kuanza kumfukuza Phidaya wakimuhisi kuna
jambo amelifanya pasipo kujua uhasama ulipo kati
ya Phidya na kiongozi wao wanaye mlinda.
Mzee Godwin akaanza kuembea kwa mwendo wa
kujiuliza maswali mengi kichwani mwake huku
akijiuliza ni kwanini Phidaya yupo katika eneo la
hapo hospitalini.
***
Raisi Godwin akiwa ndani ya gari akielekea katika
hospitali ya Agakhan, meseji ikaingi kwenye simua
yake ya mkononi, akaufunua ujumbe huo wa
maneno ulio tumwa na dokta Nelson.
{MUHESHIMIWA NINA BAHASHA YAKO INA UKWELI
WA KILA KITU JUU YA EDDY UNAYE MTAFUTA}
Kwa haraka Mzee Godwin akampigia dokta Nelson
aliye mtumia ujumbe huo.
“Ukweli gani bwana mdogo?”
“Ni juu ya huyo Eddy unaye mtafuta, yaani ni
panya mdogo sana muheshimiwa”
Raisi Godwin akawatazama walinzi wake alio nao
ndani ya gari kisha akazungumza.
“Nipo njiani ninakuja hapo hospitalini kwako
usitoke”
“Sawa mkuu”
Raisi Godwin akakata simu, hawakuchukua muda
mrefu wakawa tayari wamesha fika kwenye
hospitali ya Agakhan, walinzi wake wakashuka
kwenye gari, mmoja akamfungulia mlango naye
akashuka, akaitoa simu yake mfukoni na kumpigia
Manka kumuuliza yupo wapi.
“Nipo ICU baba nimekaa na mgonjwa”
“Ok nakuja”
Mlinzi mmoja akamuuliza nesi juu ya wapi vilipo
vyumba vya ICU, nesi huyo kwa bahati nzuri ni
miongoni mwa manesi wali shuhulika katika
upasuaji wa Erickson. Moja kwa moja nesi huyo
akawaongoza hadi kilipo chumba alicho lazwa
Erickson.
“Nisubirini hapa”
Raisi Godwin akaingia peke yake katika chumba
hicho na kumkuta Manka akiwa amekaa pembeni
ya kitanda alicho lazwa Erickson aliye wekewa
mashine za kupumulia na mashine za kuhesabu
mapigo ya moyo.
“Ilikuwaje?”
Raisi Godwin alizungumza huku akimtazama
Manka usoni aliye anza kulengwa lengwa na
machozi usoni mwake.
“Askari walimpiga”
“Askari gani?”
“Nitawashuhulikia baba mmoja baada ya
mwengine.”
Manka alizungumza kwa kujiamini huku
akimtazama baba yake usoni. Mzee Godwin
taratibu akapiga hatua hadi kitanda alicho lala
Erickson aliye fumnikwa na shuka jeupe. Mzee
Godwin akautazama uzuri wa kijana huyo akajikuta
akitingisha kichwa, kisha akamtazama Manka jinsi
alivyo jawa na uchungutaratibu akamfwata Manka
alipo simama.
“Atapona, hakikisha askari hao wote walio husika
na hili swala unawashuhulikia”
“Sawa dady”
“Kuna daktari ninakwenda kumuangalia mara moja
hapo juu nitarudi”
“Sawa”
Mzee Godwin akatoka katika chumba hicho
akawacha walinzi wake wawili mlangoni hapo kisha
yeye akaondokana na walinzi wengine sita.
Wakaingia kwenye lifti moja kwa moja wakaelekea
gorofa ya tatu ya hospitali hiyo. Wakakiwa
wanatoka kwenye lifti hiyo wakitembea kwenye
kordo ndefu ya gorofa hilo, Mzee Godwin
akamuona Phidaya akitoka katika chumba cha ofisi
ya dokta Nelson. Mkononi mwa Phidaya ameshika
bahasha, ambayo Mzee Godwin hakuitilia maanani
sana.
Kitendo cha Phidya kuanza kukimbia, kikamfanya
raisi Godwin na walinzi wake kuanza kuhisi kuna
tatizo, kwa haraka mzee Godwin akaongeza
mwendo na kuingia katika ofisi ya dokta Nelson,
hawakukuta mtu yoyote zaidi ya kusikia kelele
zikitoke chini ya gorofa kupitia dirisha hilo. Mlinzi
mmoja kwa haraka akakimbilia dirishani na kuona
kundi la manesi pamoja nawatu wengine
wakitazama mwili wa dokta Nelson ulio vunjika
kichwa.
“Muheshimiwa njoo uone”
Raisi Godwin akapiga hatua hadi dirishani,
hakuamini kumuona dokta Nelson akiwa amekufa
kifo cha kikatili hasira ikampanda na kuwageukia
walinzi wake.
“Hakikisheni munamshika yule msichana muliye
muona haraka iwezekavavyo.”
“Sawa mkuu”
Walinzi watatu wakatoka kasi na kumuacha mzee
Godwin akiwa na mlinzi mmoja, anaye muamini
kupita walinzi wote.
“Turudi chini”
Raisi Godwin alizungumza kwa msisitizo huku
akitangulia mbele na mlinzi wake akimfwata kwa
nyuma.
***
Agnes akiwa njia ndani ya gari lake akirudu
nyumbani kwake, meseji ikangia kwenye simu yake
kupitia mtandao wa Whatsapp. Taratibu akaichuku
simu yake aliyo kuwa ameitupia upande wa pili wa
siti. Akaufungua ujumbe huo ambao umetumwa na
namba ngeni. Video aliyo tumiwa ikamfanya
asimamishe gari lake pembeni na kuitazama kwa
umakini.
Macho yakamtoka baada ya kumuona Ericskon
wake akipokea kichapo kitakatifu kutoka kwa
askari, virungu ambavyo askari hao wanamtandika
Erickson vikamfanya Agnes kujikuta akilengwa
lengwa na machozi ya uchungu. Ila alipo muona
Manka akimsaidia Erickson kidogo wasiwasi
ukampungua, kwa haraka akaitafuta namba ya
Manka kwenye orodha ya namba zake kwenye
simu na kumpigia. Simu ya Manka ikaita kwa mara
kadhaa ila haikupokelewa.
Akarudia zaidi ya mara kumi ila Manka hakupokea
simu na muda mwengine alikatiwa simu. Akatuma
meseji kwa Manka na kumuuliza yupo hospitali
gani, ila meseji zilisomwa na hakurudishiwa
majibu.
“Ohhhh Mungu wangu, au Erickson wangu amekufa
nini?”
Agnes alizungumza mwenyewe huku machozi
yakimwagika usoni mwake, akajitahidi hivyo hivyo
kuendesha gari lake hadi nyumbani kwake, huku
mawazo mengi yakitawala kichwani mwake. Kwa
haraka akaingia bafuni na kuoga, kabadilisha nguo
na kuvalia nguo ambazo si rahisi kwa mtu kuweza
kumgundua kwamba yeye ni waziri, kwani amevalia
suruali ya jinzi, tisheti kubwa kidogo pamoja kikoti
juu yake. Akapigilia na kofia iliyo ificha sura yake,
akatoka haraka hadi kwenye gari lake ambalo mara
nyingi halitumii, aina ya BMW X5. Alipo hakikisha
amefunga mkanda wa gari lake, akampigia simu
Fetty.
“Ehee shoga upo wapi?”
“Nipo nyumbani. Vipi mbona unazungumza
kiunyonge?”
“Nahitaji msaada wako”
“Zungumza”
Agnes akamuelezea Fetty kila kitu kuhusiana na
kitu alicho fanyiwa Erickson kisha akamuelezea
jinsi Manka anavyo mkatia katia simu.
“Hembu ngoja nimpigie na mimi nimuulize yupo
wapi?”
“Sawa, mimi nipo ndani ya gari ukiniambia tu mimi
naelekea huko huko asiniletee ujinga wake”
“Tulia nimpigie”
Agnes akaka ndani y a gari lake hadi simu yake
ilivyo ita tena na kupigiwa na Fety.
“Ndio dada”
“Best yako yupo Agakgan, anadai Erickson yupo
ICU”
“Mungu wangu asante”
“Ok kuwa makini si unajua tena mtoto wa
mkubwa”
“Sawa”
Agnes akawasha gari lake na kuondoka nyumbani
kwake, kwa ujuzi wa kulijua jiji la Dar es Salaam,
akakatiza kwenye vichochoro kuzikwepa foleni
majira haya ya usiku. Hadi anafika hospitalini
tayari imesha timu saa nne usiku. Akasimamisha
gari lake kwenye maegesho ya eneo hilo, kabla
hajafungua mlango akashangaa mlango wa nyuma
akifungua mtu kwa haraka na kuingia na kulala
kwenye siti na kumfanya Agnes kugeuka kwa
haraka na kumtazama mtu huyo ni nani.
***
Phidaya akageuka nyuma na kuwaona askari
wawili walio valia suti wakimfwata kwa kasi kitendo
kilicho mfanya kuzidi kukimbia kwa uwezo wake
wote. Rahab akiwa kwa mbali akamuona Phidaya
akikatiza kwa kasi, mara hajakaa sawa akawaona
askari wawili wakimfwata kwa kasi wakitoka katika
majengo wakielekea kwenye maegesho ya magari.
Rahab akafwata kwa nyuma ili kuwazuia askari hao,
huku naye akiwa katika mwendo kasi.
Phidaya katika kutizama tizama kwake kwenye
maegesho ya magari, akaona gari moja likisimama
kwenye maegesho ya hapo hospitalini. Kwa haraka
pasipo hata kuuliza Phidaya akafungua mlango wa
nyuma wa gari hilo na kuingia na kumfanya
muendeshaji aliyopo humo ndani kugeuka kwa
kasi na kumuangalia.
“WEWE NI NANI?”
Muendeshaji ambaye ni mwanamke mwenzake,
alimuuliza kwa sauti ya ukali huku akiwasha taa ya
ndani ya gari lake kuiona sura ya Phidaya vizuri.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 88 YA SIMULI HII. JIUNGE
 
SORRY MADAM (88)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
INGHIA GOOFLE PLAYSTORE NA DOWNLOAD
APPLICATION(APP) YA STREAM NATION UWEZA
KUSOMA STORI ZA WAANSHI MAHIRI EDDAZARIA
G.MSULWA NA GIFT KIPAPA KWA VIFURUSHI VYA
MWEZI KWA SH 5000 NA KIFURUSHI CHA WIKI
MBILI KWA SH 3000.
ILIPOISHIA
Phidaya akageuka nyuma na kuwaona askari
wawili walio valia suti wakimfwata kwa kasi kitendo
kilicho mfanya kuzidi kukimbia kwa uwezo wake
wote. Rahab akiwa kwa mbali akamuona Phidaya
akikatiza kwa kasi, mara hajakaa sawa akawaona
askari wawili wakimfwata kwa kasi wakitoka katika
majengo wakielekea kwenye maegesho ya magari.
Rahab akafwata kwa nyuma ili kuwazuia askari hao,
huku naye akiwa katika mwendo kasi.
Phidaya katika kutizama tizama kwake kwenye
maegesho ya magari, akaona gari moja likisimama
kwenye maegesho ya hapo hospitalini. Kwa haraka
pasipo hata kuuliza Phidaya akafungua mlango wa
nyuma wa gari hilo na kuingia na kumfanya
muendeshaji aliyopo humo ndani kugeuka kwa
kasi na kumuangalia.
“WEWE NI NANI?”
Muendeshaji ambaye ni mwanamke mwenzake,
alimuuliza kwa sauti ya ukali huku akiwasha taa ya
ndani ya gari lake kuiona sura ya Phidaya vizuri.
ENDELEA
Macho ya Agnes yakabaki yakimshangaa
mwanamke huyo ambaye leo ndio mara yake ya
kwanza kumuona. Kabla hajazumgumza kitu Agnes
akashuhudia wanaume wawili mbele ya gari lake
wakipokea kipigo kwa msichana ambaye
anamfahamu fika. Wanaume hao wanao onekana
kuwa ni walinzi wa kiongozi wa nchi, walijikuta
makonde yao hayafui dafu mbele ya makonde ya
Rahab anaye shusha kipigo kikali juu yao.
“Rahab”
Agnes alizungumza huku akiwasha taa za mbele
za gari yake kushuhudia jinsi kifinyo hicho kinavyo
tembea kwa wanaume hao. Ndani ya dakika tano
wanaume hao wakawa wamevunjwa vujnwa viongo
na Rahab aliye simama kwa kijiamini mbele ya gari
la Agnes. Kwa haraka Agnes akashuka kwenye gari
hukku akiwa na tabasamu usoni mwake.
“Rahab”
Agnes aliita huku akianza kumfwata Rahab sehemu
aliyo simama, kabla hajamfikia walinzi wengine
watatu wenye mitutu ya bunduki wakanza
kuzifnyatua risasi zao sehemu alipo simama
Rahab, ambaye hakuwa mzembe kwa kiasi hicho
kwani hata kabla risasi hizo hazijamfikia akaanza
kuruka sarakasi kuelekea naapo tokea Agnes
ambaye kwa haraka akarudi kwenye gari na
kujitosa kama alivyo ingia Phidaya.
Kwa haraka Rahab akaingia kwenye gari la Agnes.
“Go go goo”(Nenda ndenda nendaaa)
Rahab alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya
Agnes kuwasha gari lake kwa haraka, akalirudisha
nyuma kwa mwnedo wa kasi, akakata kona moja
kali, alipo hakikisha amelilenga geti la kutokea,
hakufanya kosa zaidi ya kukanyaga mafuta na
kuondoka eneo la hospitali na kuwaacha walinzi
hao wakifyatua fyatua risasi pasipo mafanikio
yoyote. Mlinzi mmoja akarudi sehemu walipo acha
magari yao akaingia kwenye gari moja na
kuliendesha kwa kasi hadi sehemu walipo simama
wezake, wakaingia ndnai ya gari na kuanza
kuwafukuzia Phidaya na wezake.
***
Milio ya risasi inayo endelea nje ikawafanya watu
kadhaa ndani ya hospitali waliyo isikia
kuchanganyikiwa, mtu aliye toka katika chumba
cha wagonjwa mahututi, akamfanya Shamsa
kumtazama kwa muda, huku akiwa amemkazia
macho.
“Huyu si Manka aliye mchukua Eddy”
Shamsa alizungumza huku akianza kupiga hatua
za haraka kuelekea katika mlango alio simama
Manka pamoja na walinzi wa wawili wa mzee
Godwin.
“Huruhusiwi kuingia hapa binyti”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akimzuia Shamsa
kwa mkono, Manka akamta jicho la dharua
Shamsa, kisha akaendeleak usikilizia milio hiyo ya
bunduki ni wapi inapo tokea. Kwa kasi ya ajabu
Shamsa mguu wake mmoja akaukanyaga kwenye
paja la mlinzi huyo, akajirusha kwajuu na kumkalia
mabegani, bila hata ya huruma akamvuja shingo
na kuanguka naye chini na kumfanya Manka na
mlinzi aliye baki kubaki wameduwaa. Mlinzi
akataka kuchomoa bastola yake, ila tayari amesha
chelewa kwani Shamsa alisha mfikia na kumpiga
mtama ulio muangusha chini, hata kabla
hajajinyanyua tayari shingo yake ilisha vunjwa.
Shamsa akanyanyuka huku akimkazia macho
Manka aliye anza kurudi nyuma na kuingia
chumbani huku Shamsa akimfwata kwa mbele.
Shamsa alipo muona Eddy akiwa amelala kwenye
kitanda akabaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa,
jambo lililo kuwa ni kosa kubwa sana kwake kwa
maana Manka, alimshushia teka zito la tumbo lililo
muangusha chini. Maumivu ya tumbo aliyo yapata
Shamsa yakamfanya ajinyanyua chini taratibu huku
akimtazama Manka aliye jiweka tayari kwa
mashambulizi.
Sa Yoo na madam Merry wakakutana kwneye
kordo inayo elekea kwenye vyumba vya wagonjwa
mahututi. Wakashuhudia walinzi wawili wakiwa
wamelala chini ya sakafu nje ya chumba kimoja.
Kwa haraka wakaanza kukimbia hadi kwenye
mlango wa chumba hicho na kumshuhudia
Shamsa anavyo pokea kichapo kutoka kwa Manka.
Wote wawili wakaingia ndani na kuanza
kumshambulia Manka, kila mmoja aliweza
kumshambulia jinsi alivyo weza, aliye rusha kofi
sawa, aliye vua kiatu na kumtandika sawa, ilimradi
walihitaji kumuokoa Eddy aliye muona amelala
kitandani.
“Mchukueni Eddy muondoke naye mimi
ninamshuhulikia huyu”
Shamsa alizungumza huku akinyanyuka, Madam
Merya na Sa Yoo hawakupoteza muda baada ya
kumuona Manka amelala chini akiwa yupo hoi
taabani. Kutokana kitanda alicho lalia Eddy kina
matairi, walicho kifanya ni kuchomoa waya wa
umeme wa mashinye ya kuhesabu mapigo ya
moyo iliyopo pembeni ya kitanda hicho, na kuanza
kukisukuma kutoka nje.
“Tupite njia hii”
Madam Mery alizungumza, Sa Yoo akatii wakaanza
kukisukuma kitanda hicho hadi nje kwenye
maegesho ya magari cha kushukuru Mungu
hapakuwa na mtu hata mmoja, kutokana milio ya
risasi hiyo ilisikika katika eneo hilo na raisi wote
walikimbia japo ni usiku.
“Kwenye gari hili hawezi kuingia”
“Itakuwaje sasa?”
Sa Yoo akaitazama gari la wagonjwa lililopo
kwenye maegesho hayo kwa haraka akalikimbilia,
akajaribu kufungua mlango wa upende wa dereva
kwa habati nzuri akaukuta upo wazi, kwnai ni
muda mchache gari hilo limeleta mgonjwa hapo
hospitalini, kingine cha kumshukuru Mungu hata
dereva aliweza kusahau fungua kwneye mskani wa
gari hilo. Kwa haraka Sa Yoo akaingia na
kuliwasha gari hilo akalirudisha taratibu hadi
sehemu kilipo kitanda, akshuka kwa haraka,
akazunguka nyuma wakasaidiana na Madan Mery
kumuingia Eddya kaiwa na kitanda chake kisha
madam Mery akaingia nyuma na kufunga mlango
na Sa Yoo akarudi mbele, akakanyaga mafuta na
kuondoka eneo hilop la hospitali.
***
Shamsa akaanza kummalizia hasira Manka kwa
kumbamiza ngumi mfululizo za uso. Kisha
akamnayanyua na kumkalisha kitako na kutaka
kumvunja shingo, ila kabla hajafanya hivyo raisi
Godwin na mlinzi wake wakawa wameingia kwenye
chumba hicho wakiwa na silaha mikononi mwao
baada ya kuwakuta walinzi walio nje ya chumba
hicho wakiwa wamekufa.
“Mikono juu”
Mlinzi huyo alizungumza kwa sauti kali huku
bastola yake akiwa amemuelekezea Shamsa, aliye
tii amri hiyo. Raisi Godwin macho yakamtoka kwa
hasira huku akimtazama mwanaye Manka akiwa
amelala chini huku damu zikimtoka puani na
mdomoni.
Mzee Godwin wala hakuwa na haja ya kumtazama
Shamsa, macho na akili yake vyote akavitupia kwa
Manka wake, taratibu akapiga magoti chini huku
machozi ya hasira yakimtoka usoni mwake,
msichana wake muri na mrembo haswahaswa,
amegeuzwa kuwa mbaya ndani ya muda machache
alio muacha.
“Manka, Manka”
Mzee Godwin aliita huku kichwa cha Manka
akikiweka kwenye mapaja yake.
“Ni nani aliye fanya hivi mwanangu eheee”
Manka taratibu akayageuzia macho yake kwa
Shamsa aliye nyoosha mikono juu, na kumfanya
Mzee Godwin na yeye kuyageuza macho yake na
kumtazama Shamsa, kwa jicho lililo kolea wekundu
wa hasira. Mzee Godwin kwa haraka akaikoki
bastola yake kuruhusu riasi zake kukaa tayari kwa
kutoka pale tu atakapo vuta traiga ya bastola hiyo
na riassi zote zimalizikie mwilini mwa Shamsa.
“Usimu….ue baba”
Manka alizungumza huku akiushika mkono wa
Mzee Godwin uliyo shika bastola huku ukitetemeka
kwa hasira kali.
“Huyu si ndio amekufanya hivi?”
Cha kushangaza Manka akatingisha kichwa, hadi
Shamsa akabaki ameduwaa, kwani tayari kimoyo
moyo alisha anza kusali sala yake ya mwisho
kwani tayari kifo kimesha simama mbele yake.
“Wawili wamemchukua, Erickson wang…….”
Manka hakumalizia sentensi yake akawa
amepoteza fahamu na kumfanya Mzee Godwin
mimacho kumtoka, akaanza kumtingisha Manka
huku akimuita kwa sauti ya juu iliyo jaa hasira.
“Muheshimiwa ngoje nimbebe nimuwahishe kwa
madaktari”
Mlizni wake alizungumza huku akimsogeza
pembeni mzee Godwin anaye lia sasa kwa
uchungu. Mlinzi wake akamnyanyua Manka kwa
mikomo miwili na kutoka na Manka kwa kasi na
kumpeleka mapokezi, ili aanze kupewa huduma ya
kwanza.
Mzee Godwin kwa hasira akanyanyuka na kuanza
kufnyatua risasi juu zilizo toboa toboa sing’bodi
iliyopo hapo hospitalini. Shamsa kuona mzee
amechanganyikiwa akaanza kupiga hatua kabla
hajafika mlangoni akasikia sauti nzito nyuma yake
ikizungumza
“Simama wewe binti, utanionyesha ni nani aliye
mchukua Erickson”
Shamsa akasimama na kugeuka nyuma, akamkuta
raisi Godwin akiwa amemuelekezea bastola, huku
anamsogelea taratibu.
‘Siwezi kukamatika kijinga hivi’
Shamsa alizungumza huku akizitazama hatua za
raisi Godwin zinavyo msogelea, Mzee Godwin hadi
akamkaribia akastukia teke zito likitua kifuani
mwake, ila kutokana na mazoezi mazito anayo
yafanya, teke hilo lilimyumbisha kidogo na
kumrudisha nyuma, Sa Yoo akafungua mlango na
kutoka kasi, Mzee Godwin akafungua mlango na
yeye akatoka huku bastola yake akiwa
amemuelekezea Shamsa anaye karibia kukata
kona. Akafyatua risasi moja iliyo mpata Shamsa
nyuma kwenye bega la mkono wa kulia na
kumuangusha chini.
Shamsa akajikanza hivyo hivyo na kunyanyuka
kwa haraka huku akisikilizia maumivu makali aliyo
yapata, na kuendelea kukimbia. Kabla mzee
Godwin hajachukua maamuzi ya kumkimbiza
mlinzi wake aliye kuwa amempeleka Manka
mapokezi akarudi eneo hilo huku akiwa anakimbia
kwa mwendo wa kasi.
“Muheshimiwa hali ya Manka sio nzuri”
Mzee Godwin kusikia hivyo akachomoka kasi
kuelekea sehemu alipo pelekwa Manka huku mlinzi
wake akiwa nyuma.
Shamsa akafika lilipo gari lao, akafungua mlango
na kuingia. Huku maumivu ya risasi aliyo pigwa
yakiendelea kumtesa sana huku damu nyingi
zikiendelea kumwagika. Shamsa hakukuta funguo
alicho kifanya ni kukata nyanya mbili za hasi na
chanya akazikutanisha na kulifanya gari hilo
kuwaka. Kwa haraka akaondoka eneo la hospitali
huku akijikaza na maumivu hayo makali.
***
Agnes akazidi kuongeza mwendo kasi wa gari
huku akimtazama Rahab aliye keti siti ya pembeni.
Hapakuwa na mtu aliye zungumza chochote hadi
pale walipo anza kusikia milio ya risasi ikirindima
nyuma yao.
“Wanakuja”
Phidaya alizungumza huku akilala chini. Agnes
kwa kioo cha pemeni akaona gari moja nyeusi aina
ya Aud Q5 ikija kwa kasi, huku watu wawili wakiwa
wamechomoza kwenye vioo wakiwa namitutu ya
bunduki wakilishambulia gari lake.
“Rahab mimi mbona sielewi ni kitu gani ambacho
kinaendelea hapa?”
“Wewe enesha gari utajua mbele ya safari”
“Sasa tunaelekea wapi?”
“Popote ili mradi tuwakimbie watu hawa”
“Ahaaaa”
Agnes akaonekana kuchukizwa kwa tukio hilo la
hatari kwenye maisha yake kwani hata leongo
ambalo lilimpeleka hospitalini hapo halikuweza
kukamilika. Agmes kiroho upande, akaongeza
mwendo kasi wa gari lake, kutoka na kujua njia
nyingi za vichochoro, akajitahidi kwa uwezo wake
kuwapotea watu wanao wakimbiza, hadi
akafanikiwa. Breki ya kwanza akafika nyumbani
kwake, honi moja aliyo ipiga, ikamfanya mlinzi
kufungua gate kwa haraka kwa maana anatambua
bosi wake hapendi akiwa nje ya geti apige honi
zaidi ya mara moja. Geti lilipo funguliwa Agnes
akaliingiza gari lake kwa kasi hadi sehemu ya
maegesho ya magari na kushuka kwa hasira.
Rahab na Phidaya nao wakashuka, wote macho
yao wakamtazama Agnes aliye kunya sura yake
akilitazama gari lake lilivyo tobolewa tobolewa
baadhi ya maeneo ya risasi.
“Rahab hembu naomba unieleze ni kitu gani
ambacho kinaendelea mimi mbona siwaelewi
nyinyi watu”
“Punguza hasira, kwanza nashukuru kwa msaada
wako ulio weza kutusaidia”
“Hilo mimi haliniusu, hivi bado hujaacha ujambazi
Rahab, umetoka kuwa mama raisi hadi kazi yako
ya zamani si ndio?”
Agnes aliendelea kuzungumza kwa hasira na
kumfanya Rahab kumfwata kwa kasi hadi sehemu
alipo simama na kumsogelea kwa ukaribu zaidi
huku akiwa amemkazia macho ya hasira Agnes,
kitu kilicho muogopesa Phidaya, aliye simama
pasipo kujua ni jinsi gani watu hao wanavyo juana.
***
“Madam sasa tunampeleka wapi Eddy?”
Sa Yoo aliuliza huku akizidi kukimbiza gari hilo la
wagonjwa.
“Njia ile ya bagamoyo imefungwa na askari.
Tumpeleke nyumbani kwake”
“Nyumbani kwake mimi sipajui”
“Wewe twende nitakuelekeza”
Madam Mery alizungumza huku macho yake yote
yakiwa mbele. Akaanza kumuelekeza Sa Yoo njia
za kupita hadi wakafanikiwa kufika nyumabi kwa
Eddy. Madam Mery akashuka na kuingia ndani,
akafungua geti na Sa Yoo akaingiza gari kisha
madam Mery akalifunga geti hilo. Kwa haraka Sa
Yoo akashuka baada ya kulisimamisha gari
akazunguka nyuma alipo kuta madam Mery tayari
amesha fungua milingo iliyopo nyuma ya gari hilo.
Wakasiaidiana kumshusha Eddy na kitanda chake,
moja kwa moja wakampeleka hadi kwenye sebule.
Madam Mery akatafuta sehemu yenye swichi ya
kuwashia taa, hadi akafanikiwa.
“Tumuweke hapa hapa”
Sa Yoo alizungumza na kuanza kukisukuma
kitanda hadi sehemu alipo hitaji kumuweka Eddy.
Walipo hakikisha wamemuweka sehemu sahihi, kila
mmoja akajikuta akishusha pumzi kwa kuchoka.
Sasa Sa Yoo ndio akaanza kupata muda wa
kuanza kuikagua nyumba hiyo ambayo inaonekana
fika kwamba haitumiki kwa muda mrefu kwa
maana kuta zake pmoja na samani zilizopo zote
zimejaa vumbi jingi sana pamoja ma mitando ya
buibui
***
Akili ya Shamsa, haikupafikiria sehemu nyinyinge
yoyote ya kwenda ziaid ya nyumbani kwa Eddy
kwa maana ndipo karibu na sehemu alipo. Kadri
muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nguvu
zilivyo zidi kumuishia mwilini mwake hii ni
kutokana na kumwagikwa na damu nyongi mwilini
mwake. Hadi anafanikiwa kufika nje ya geti la
nyumba ya Eddy alilo kuta limefungwa, nguvu zote
za mwili zilisha muishia. Taratibu akajikuta
akiulalia mskani wa gari hilo na kufanya gari hilo
kupiga honi mfululizo. Honi hizo zikawastua
Madam Mery na Sa Yoo walipo ndani ya nyumba
hiyo. Sa Yoo aliye kuwa gorofani kwa haraka
akashuka hadi sebleni na kumkuta Madam Mery
akiwa amesimama huku akiwa na wasiwasi
mwingi.
“Ni nani huyo?”
Sa Yoo aliuliza huku naye akionyesha dhairi ana
wasiwasi mwingi
“Hata mimi sifahamu kwa maana hakuna mtu
anaye fahamu kama sisi tupo hapa”
“Isije ikawa ni wale walinzi wa raisi?”
“Si dhani kama wanaweza kuja hapa kwa manaa
hakuna anaye fahamu uwepo hapa”
“Hembu zima zima taa”
Madam Mery akakimbilia sehemu yeney swichi,
akazima taa ya sebleni. Kisha kwa haraka akarudi
sehemu alipo Phidaya.
“Twende tukaangalie ni nani”
“Wee mtoto huogopi, wanaweza kuwa majambazi
hao?”
“Hapana Madam hakuna majambazi wanao kuja
kwa kupiga honi kwa kiasi hicho”
“Mmmmm”
“Yaa twende”
Wakatoka kwa tadhari kubwa huku kila mmoja
akiwa makini kwa kutazama kila upande wa eneo
hilo la nyumba. Wakafika getini, Sa Yoo akawa wa
kwanza kuchungulia nje, hapo ndipo akaliona gari
la madam Rahab.
“Ni madam Rahab”
Sa Yoo alizungumza huku akitoka kwenye kageti
kadogo, madam Mery kusikia hivyo naye akatoka
akionekana kutokuwa na wasiwasi wa aina yoyote.
Sa Yoo alipo ona honi hizo zinaendelea kupigwa
kwa haraka akaelekea upande wa dereva, baada ya
kuchungulia dirishani akamuona Shamsa akiwa
amelalia mskani huku kichwa chake kikiwa kwenye
honi ndio maana inapiga kwa mfululizo.
“Madam ni Shamsa”
Sa Yoo alizungumza huku akiufungua mlango wa
upande wa Shamsa, kitu kilicho mstua Shamsa ni
damu zilizo tapakaa kwneye siti aliyo ikalia
Shamsa, hata kabla hajafanya kitu chochote
akastukia gari yenye mwanga mkali aina ya
defender likisimama nyuma ya gari la Shamsa,
wakaruka wanaume wawili walio kuwa nyuma ya
gari hilo huku wakiwa wamevalia nguo za kiaskari
pamoja na makoti makubwa meusi, huku mikononi
mwao wakiwa na bunduki aina ya SMG.
“Munafanya nini hapo”
Mwanaume mmoja alizungumza na kumfanya Sa
Yoo kwa haraka kufunga mlango wa gari na
kusimama huku akimwatizama wanaume hao
ambao ni polisi wa doria, wakimfwata huku
wamemnyooshea mitutu ya bunduki.
 
SORRY MADAM (89)
(Destination of my enemies)
WRITER………………………………………………………………….
………..EDDAZARIA GERSHOM MSULWA(Next level
Author)
WEBSITE……………………………………………………………………..……
www.storizaeddy.blogspot.com
EMAIL……………………………………………………………………..
………..storyzaeddy@yahoo.com
CONTACT……………………………………………………………
…………….0657072588/0768516188
INGHIA GOOFLE PLAYSTORE NA DOWNLOAD
APPLICATION(APP) YA STREAM NATION UWEZA
KUSOMA STORI ZA WAANSHI MAHIRI EDDAZARIA
G.MSULWA NA GIFT KIPAPA KWA VIFURUSHI VYA
MWEZI KWA SH 5000 NA KIFURUSHI CHA WIKI
MBILI KWA SH 3000.
ILIPOISHIA
“Madam ni Shamsa”
Sa Yoo alizungumza huku akiufungua mlango wa
upande wa Shamsa, kitu kilicho mstua Shamsa ni
damu zilizo tapakaa kwneye siti aliyo ikalia
Shamsa, hata kabla hajafanya kitu chochote
akastukia gari yenye mwanga mkali aina ya
defender likisimama nyuma ya gari la Shamsa,
wakaruka wanaume wawili walio kuwa nyuma ya
gari hilo huku wakiwa wamevalia nguo za kiaskari
pamoja na makoti makubwa meusi, huku mikononi
mwao wakiwa na bunduki aina ya SMG.
“Munafanya nini hapo”
Mwanaume mmoja alizungumza na kumfanya Sa
Yoo kwa haraka kufunga mlango wa gari na
kusimama huku akimwatizama wanaume hao
ambao ni polisi wa doria, wakimfwata huku
wamemnyooshea mitutu ya bunduki.
ENDELEA
“Ahaaa tunamfungulia huyu ndugu yetu amerudi
amelewa”
Sa Yoo alizungumza huku akiwa amesimama huku
ameuegemea mlango wa gari hilo.
“Sasa muambieni asipige honi anawasumbua
majirani walio lala”
“Sawa afande nitamnyanyua”
Afande hao baada ya kuwatazama Sa Yoo na
madam Mery wakawaamini kwamba huyo ndugu
yao amelewa sana hadi hajiwezi. Wakarudi kwenye
gari lao, wakapanda na kuondoka zao. Kila mtu
akashusha pumzi, hususani madam Mery ambaye
mwili mzima ulikuwa unamtetemeka, ila Sa Yoo
alijikaza.
“Madam anatokwa na damu”
“Damu?”
“Ndio?”
Sa Yoo alizungumza huku akimtaza Shamsa aliye
poteza fahamu kabisa. Wakajitahidi na kumuweka
siti ya nyuma ya gari huku wakiwa wamemlaza
kifudi fudi kwa maana risasi hiyo ipo begani kwa
nyuma. Madam Mery akaingia na kufungua geti
kisha Sa Yoo akaliingiza gari hilo, akalisimamisha
karibu sana na sehemu ya mlango. Wakamshusha
Shamsa, kwa haraka haraka wakamuingiza ndani
na kumlaza kwenye sofa. Madam Mery akawasha
taa, na kurudi kwenye sofa walipo mlaza Shamsa
“Aiiii risasi amepigwa hapa”
Sa Yoo alizungumza huku akiichana nguo ya
Shamsa sehemu kwenye jereha. Madam Mery alipo
litazama jeraha hilo kwa haraka akaelekea jikoni,
akafungua friji ambalo halijawashwa, kwa muda
mrefu. Akatoa pombe aina ya Vodka kisha akarudi
nayo sebleni.
Akaifungua, pombe hiyo ambayo ni kali sana,
akamwagia Shamsa kwenye jeraha lake. Kwa
maumivu makali Shamsa akajikuta akizinduka.
“Shamsa tulia tulia”
Sa Yoo alizungumza huku akimzuia Shamsa
kunyanyuka, madam Mery kwa vidole gumba vya
viganja vyake vyote viwili, akanza kuliminya jeraha
la Shamsa kwa staili ambayo anaweza kuipandisha
risasi ili kutoka katika kidonda hicho. Shamsa
akazidi kutoa ukelele wa maumivu makali hadi Sa
Yoo akamsokomeza vitambaa kadhaa mdomoni
mwake ili aiweze kuungata ulimi wake.
“Madam jitahidi inatoka inatoka”
Sa Yoo alizungumza huku akiliangalia jeraha hilo
linalo vuja damu nyingi sana. Madam Mery akazidi
kujitahidi hadi akafanikiwa kuitoa risasi hiyo. Sa
Yoo akachukua pombe hiyo na kumwagia kidonda
hicho, kuua bacteria ambao wameweza kuingia.
Walipo maliza zoezi hilo wakamfunga Shamsa
jeraha lake, kwa kipande cha nguo ambacho Sa
Yoo alichana kwenye shati lake, kwa maumivu
makali, Shamsa akajikuta akipitiwa usingizi na
kulala fofofo.
***
Jinsi Rahab alivyo zidi kumkazia macho Agnes
ndivyo jinsi Agnes alivyo zidi kumkazia macho
Rahab. Wakasimama zaidi ya dakika tano, wote
kwa pamoja wakajikuta wakimwagikwa na machozi
kisha wakakumbatia kwa nguvu.
“Ohooo Rahab”
Agnes alizungumza huku akizidi kumkumbatia kwa
nguvu. Wakaachiana kisha wakamgeukia Phidaya
ambaye naye machozi yalikuwa yakimlenga lenga
baada ya kuwaona wezake hao wakimwagikwa na
machozi.
“Phidaya huyu ni Agnes, ni miongoni mwa marafiki
zangu wa kitambo sana. Agnes huyo ni Phidaya ni
rafiki yangu sana”
“Nashukuru kukufahamu Phidaya”
“Hata wewe nashukuru kukufahamu”
Kwa haraka Phidaya kumbukumbu zikamjia na
kugundua kwamba Agnes ndio mwanake ambaye
ana mahusiano na mume wake Eddy, ila
akajikausha kwa maana yupo kwenye mamlaka ya
mtu ambaye ameweza kumuepusha mikononi mwa
mzee Godwin. Agnes akawakaribisha ndani.
“Niwapatie nini?”
“Mimi nina njaa mshikaji wangu. Alafu umejipanga
kishenzi au ndio huo uwaziri?”
“Daa wee acha tu maisha ndugu yangu
nakumbuka enzi zile tunatumia mitutu, pale benki
nakumbuka tulivyo kwapua ile mihela, alafu sijua
ilikwendaga wapi mshikaji wangu”
“Aisee hata mimi sikumbuki zilikwenda wapi kwa
maana kila mtu alitawanyika, kuja kusikia wezangu
mumekamatwa, nikajaribu kuwaokoa ila ndio hivyo
nikashindwa”
“Ahaa nakumbuka ulisha tuelezaga hiyo ishu
kipindi kile cha kampeni tunamlinda huyu mzee”
Rahab na Agnes walizungumza huku wakieleka
jikoni na kumuacha Phidaya sebleni akitazama
tazama mazingira. Phidaya akakumbuka tukio la
dokta Nelson alivyo weza kujirusha dirishani. Kitu
alicho kikumbuka kingine ni bahasha aliyo kuwa
ameiokota chini, kwa haraka akajipapasa na kuitoa
bahasha hiyo na kuifungua. Akatoa karatasi zilizo
kuwemo humo na kuanza kupitia moja baada ya
nyingine. Kabla hata hajazisoma Agnes akarudi
sebleni hapo huku uso wake ukiwa na tabasamu
pana.
“Phidaya tumesha andaa chakula chap chap njoo
tule”
“Sawa”
Phidaya akazirudisha karatasi mbili kwenye
bahasha hiyo na moja akaisahau juu ya sofa kwa
haraka alizo kuwa nazo. Wakaongozana na Agnes
hadi kikonni na kumkuta Rahab akiendelea kula.
“Unatumia kinywaji gani?”
“Ahaa mirinda nyeusi”
“Ngoja nikakuletee, zipo kwenye friji la sebleni”
Agnes akatoka jikoni na kurudi sebleni, akafungua
friji na kutoa soda hiyo, akiwa anakatikaza hapo
sebleni macho yake yakatua kwenye karatasi
ambayo Phidaya alizisahau. Akaona sio vyema
kuiacha karatasi hiyo ikiwa nje ya bahasha hiyo ni
vyema airudishe ndani ya bahasha hiyo. Kabla
hajairudisha macho yake yakatua kwenye
maandishi meusi na yaliyo kulea vizuri yaliyo
andikwa ‘DNA TEST BETWEEN MANKA GODWIN
AND ERICKSON FORRD’(Vipimo vya DNA kati ya
MANKA GODWIN na ERICKSON FORRS)
Kwa haraka Agnes akaanza kuipitia karatasi hiyo
huku akisoma majibu hayo. Mwili mzima kahisi
ukiishiwa nguvu kwa maana majibu yanaonyesha
Erickson na Manka ni mtu na ndugu yake wa damu
moja.
‘Ina maana Manka na Erickson ni ndugu?’
Agnes alijiuliza huku akiirudia kuisoma tena hiyo
karatasi, akashusha pumzi nyingi na kuirudisha
karatasi hiyo sehemu ilipo kuwa na wala hakuhitaji
kuirudisha kwenye bahasha hiyo. Akaondoka
sebleni hapo akiwa katika dibwi la mawazo,
hakuamini kitu ambacho amekiona kitu kikubwa
anacho jiuliza, kuna uhusiano gani katia ya
Erickson na Manka.
“Vipi mbona umechelewa?”
Rahab aliuliza huku akimtazama Agnes machoni,
aliye mtazama Phidaya na kuachia tabasamu la
kujilazimisha na kumpatia soda aliyo muagiza.
“Ahaa nilikuwa sizioni hadi nikaenda kuchukua
chumbani kwangu”
“Ahaa kumbe hata wewe ni mtumiaji wa hizi soda?”
“Sana huwa nazitumia ila ndio hivyo mara nyingi
nakuywaga whyne”
Agnes hakutaka kuuliza kitu cha aina yoyote zaidi
ya kujifanya hajui chochote, alicho hitaji ni kuanza
kufanya upelelezi wake taratibu hadi afanikiwe
kutambua ni mchezo gani upo katikati ya Manka
na Erickson mwanaume anaye mpenda.
***
Alfajiri na mapema Eddy ayakafumbua macho yake,
kila sehemu aliyo itazama ndani humo, hakuweza
kupakumbuka na wala hakujua amefikaje fikaje
eneo hilo kwa maana kumbukumbu zake za
mwisho zinamkumbuhsa kuhusiana na gari lake
alio kuwa amebeba silaha.
‘Nipo wapi hapa?’
Eddy alijiuliza huku akijaribu kutazama tazama kila
sehemu, picha kubwa ya ukutani inayo muonyesha
yeye pamoja na familia yake, ikamfanya taratibu
anze kupachunguza ndani humo kwa umakini na
kugundua kwamba yupo nyumbani kwake,
akatazama kwenye makochi akamuona Sa Yoo
akiwa amelala huku amekaa, akatazama kochi la
pembeni yake akamuona Shamsa akiwa amelala
kifufidi fudi.
Kabla hajazungumza chochote, akamuona Madam
Mery akishuka kwenye ngari za gorofa, huku
mkononi mwake akiwa ameshika kikombe kinacho
onyesha kuna chai.
“Umeamka”
Madam Mery alizungumza huku akipiga hatua hadi
kwenye kitanda cha Eddy.
“Madam kumetokea nini?”
Eddy aliuliza huku akihitaji kukaa, ila madam Mery
akamzuia, ili asiweza kuutibua mshono alio weza
kufanyiwa.
“Ahaa ni maelezo marefu kidgo ila kusema kweli
polisi jana walikupiga?”
“Ahaaaaa!! Sasa mbona nimelazwa hapa nani
kanileta?”
“Aliye kuleta ni mimi na Sa Yoo tulikuuiba
hospitalini baada ya Manka kukuchukua”
“Manka!! Manka alinichukua mimi?”
“Ndio alikuchukua, mikononi mwa polisi, ila sisi
tukakuiba”
“Yupo wapi mke wangu Phidaya?”
Madam Mery akaka kimya asimjibu Eddy swali lake
kwa maana hata yeye hatambua ni wapi alipo
Phidaya na Rahab ambo tangu walipo achana
hospitali jana usiku hapakuwa na mawasiliano ya
aina yoyote.
Gafla Shamsa akakurupuka, kwenye kochi alipo
kuwa amelala, huku mkono mmoja akiuweka
mdomoni mwake, akakaa kitako na kuanza
kutapika kitendo kilicho washangaza Eddy na
madam Mery wanao mtazama.
***
Hadi inafika majira ya saa kumi na mbili alfajiri,
Manka ndio anazinduka kutoka katika usingizi wa
nusu kifo, mtu aliye muona pembeni yake hakuwa
mwengine zaidi ya Mzee Godwin ambaye alipo
muona mwanaye huyo amezinduka, akaachia
tabasamu pan asana.
“Baba”
“Naam mwanangu”
“Umempata Erickson wangu?”
“Ndio walinzi wapo kwenye harakati za kumtafuta,
ninaamini watampata”
Manka machozi yakaanza kumtiririka, usoni
mwake, na kumfanya mzee Godwin kuchukua
kitambaa chake na kuanza kumfuta mwanaye huyo
machozi.
“Usilie mwanangu, nitahakikisha kwamba Erickson
anarudi mikononi mwako”
“Asante baba, ila kwa nini wamchukue Erickson
wangu wakatia anaumwa”
“Hivi unawakumbuka walio mchukua?”
“Ndio ninawakumbuka na ndio walio nipiga mimi”
Mzee Godwin akatoa simu yake mfukoni na
kumpigia mkuu wa usalama wa taifa na kumuagiza
awalete vijana wawili wenye ujuzi wa kuchora sura
za watu pale wanapo elezwa watu hao
wanaonekana vipi. Alipo toa maagizo hayo akakata
simu na kumgeukia Manka aliye kuwa amempa
mgongo kipindi akizungumza na simu hiyo.
“Kuna wataalamu watakuja hapa na utawaelezea
jinsi watu hao wanavyo onekana kisha picha zao
zitatumika katika kuwatafuta kimya kimya hadi
tuwapate”
“Sawa baba”
“Uletewe kifungua kinywa?”
“Ndio”
Mzee Godwin akatoka na kumuita mmoja wa
walinzi wake, akamuagiza akasimamie kifungua
kinywa cha mwanae jinsi kinavyo andaliwa, ili
kusije tokea makosa yoyote kama ya kuwekewa
sumu. Haukupita muda mrefu, vijana wawili wenye
‘brufcase’ zao mikononi wakaruhusiwa kuingia
kwneye chumba alipo mzee Godwin na Manka.
Wakampa salamu mzee Godwin pamoja na
mwanaye kisha wakaandaa vitendea kazi vyao
ikiwemo karatasi nyeupe pamoja na penseli zao za
kuchorea na rangi kadhaa. Manka kwa masaada wa
mzee Godwin, wa kumnyanyua kitandani, akaka
kitako na kuanza kutoa maelezo ya watu hao
wambao waliweza kumvamia.
“Kumbe ni wanawake?”
Mzee Godwin aliuliza kwa mshangao, baada ya
Manka kutamka jinsi nywele zao zilivyo. Manka
akatingisha kichwa na kuendelea kuwaelezea
wachoraji hao jinsi Sa Yoo na madam Mery
walivyo, hadi zinatimu dakika arobaini na tano,
picha ya Madam Mery na Sa Yoo zikawa tayari
zimesha kamilika na akakabidhiwa Mzee Godwin.
Macho yam zee Godwin yakatua kwenye picha ya
madam Mery na kujikuta akimkazia macho,
akamgeukia Manka aliye kaa kitandani, akataka
kuzungumza kitu ila akanyanyamaza na
kuwaruhusu wachoraji hao kuondoka ili
kuzungumza na mwanaye huyo.
“Unataka kusema huyu mwana mama naye
alikuwepo?”
“Ndio alikuwepo kwani baba unamfahamu?”
Mzee Godwin akajikuta akitingisha kichwa cha
kukubali kwamba ana mfahamu madam Mery
ambaye hadi leo anatambua kwamba amefariki
kutokana na siku ya mwisho kuwa naye alipiga
risasi wakiwa nyumbani kwa Eddy katika zoezi la
kumteka Phidaya.
“Unamjuaje juaje baba?”
Mzee Godwin akashusha pumzi huku taratibu
akikaa kitandani, hakujua aanzie wapi katika
kumueleza Manka ni kitu gani kilitokea katia yake
na mwana mama huyo.
“Baba mbona hunijibu?”
“Huyu alikuwa mama yako mdogo na pia alikuwa
ni mwali wake Eddy”
Manka akaishika picha hiyo ya madam Mery na
kuitazam tena vizuri, kumbukumbu zake zikarudi
zaidi ya mika kumi na mbili nyuma. Akamkumbuka
mwanamke huyo kipindi hicho alikuwa kijana
mzuri, alikuja nyumbani kwa mjomba wake
ambaye alidai ni mwalim anaye fundisha naye
shule moja na shule hiyo hiyo ndio shule ambayo
Eddy alisoma.
Kumbukumbu za Manka kwa haraka zikarudi hadi
kwenye tukio lililo tokea jana usiku wake, alipo
msikia binti mmoja ambaye hakuhitaji kumtaja kwa
baba yake, akiwaeleza madma Mery na Sa Yoo
wamchukue Eddy na kuondoka naye.
“Huyo ni mama yako mdogo kabisa, japo sikuhitaji
kuliweka wazi hilo na yeye wala halijui hilo
kwamba nilisha wahi kuzaa na dada yake ambaye
alisha fariki siku nyingi”
“Baba ni kitu gani hicho unanieleza leo?”
Manka aliuliza kwa ukali huku machozi yakimtoka,
kila anacho kisikia mbele ya baba yake leo ni kitu
kipya kwenye maisha yake.
“Usi kasirike mwanagu, kwani hata yeye hafahamu
kwamba dada yeke nilisha wahi kuzaa naye, na pia
hafahamu kwamba wewe ni mtoto wa dada yake”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti ya upole na
unyonge huku kichwa chake akiwa amekiinamisha
chini wala hakuhitaji kumtazama Manka usoni.
“Huyo anaitwa Mery na alisha wahi kuwa mapenzi
wangu hadi siku ninampiga risasi nikiamini
atakuwa amekufa”
“Dady ni roho gani hiyo uliyo kuwa nayo, tazama
sasa, mama yangu mdogo anahitaji kuniua je
utakwenda kumuua kwa mara ya pili kwa hili alilo
nifanyia mimi eheee?”
Swali la Manka kwa mara ya kwanza, likaanza
kuibua hisia za machozi za Mzee Godwin. Ambaye
kwa muda huu kumbukumbu za maisha yake ya
nyuma zinaanza kujirudia kichwani mwake.
“Baba na je Eddy unahitaji kumuua kisa kikiwa ni
nini, ikiwa ni mwanao wa damu moja na pia
umenipandikiza chuku ya kumchukia mdogo
wangu Eddy ili mradi utimize matakwa yako ya
kuendelea kumwaga damu za watu wasio na hatia,
baba kumbuka kuna usemi unao sema, what gose
around, always come aroud”
Manka alizungumza huku akichomoa mrija wa
dripu na kushuka kitandani akiwa na hasira kali ya
kusikia ukweli kwa baba yake huyo.
“Na tambua Eddy nimesha mfahamu, na Eddy huyo
huyo ndio atakaye kuja kuja kukuangamiza, na
kuanzia hivi sasa usinihusishe na mipango yako ya
kikatili”
Manka alizungumza kwa hasira huku akijikongoja
kutoka mlangoni ila kabla hajafika mlangoni huku
nyuma akasikia bastola ikikokiwa, taratibu
akageuka na kumkuta Mzee Godwin akiwa
amemnyooshea bastola ya uso, huku macho yam
zee Godwin yakiwa yametawaliwa na ukungu
mwekundu wa hasira hadi mkono wake ulio shika
bastola ukawa unatetemeka.
ITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU YA 90 YA SIMULI HII.
 
Back
Top Bottom